Blinken akutana na Netanyahu kushinikiza 'hatua madhubuti' kuwalinda raia wa Gaza

Jeshi la Israel lilisema "limekamilisha kuzunguka mji wa Gaza" na limekuwa likishambulia maeneo yanayotumiwa na Hamas.

Moja kwa moja

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho majaaliwa.

  2. Netanyahu apinga wito wa kusitishwa kwa vita kwa muda

    .

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Netanyahu

    Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, amekataa wito wa kusitishwa kwa muda mapigano katika mzozo na Hamas.

    Akizungumza wakati wa hotuba yake kwa njia ya televisheni, Netanyahu alisema hatakubali hatua hiyo hadi mateka wa Hamas waliotekwa wakati wa shambulio lake dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba waachiliwe.

    Alikuwa akizungumza muda mfupi baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken kusisitiza wito wa "kusitishwa kwa vita " katika mzozo huo ili kuruhusu misaada zaidi katika Gaza. Blinken pia alisema kusitishwa kwa vita hivyo kwa muda kunaweza kuunda "mazingira bora ambayo mateka wanaweza kuachiliwa".

    Blinken alisema maelezo ya jinsi kusitishwa huko kwa vita kungefanya kazi yanaangaziwa na kwamba Israel ilikuwa na "maswali halali" kuhusu jinsi mipango hiyo itafanya kazi

    Lakini Netanyahu alisema: "Israel inakataa usitishaji vita wa muda ambao haujumuishi kurejea kwa mateka wetu."

    Ingawa usitishaji vita rasmi kwa kawaida huwa ni mipango ya muda mrefu unaoruhusu wahusika kushiriki katika mazungumzo, mapumziko ya kibinadamu yanaweza kudumu kwa saa chache.

  3. Blinken anasema mengi yanahitajika kufanywa ili kuwalinda raia wa Palestina

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anasema hatua kadhaa muhimu zinapaswa kuchukuliwa ili kufanikisha ili kuwalinda raia wa Palestina ikiwa ni pamoja na kuzuia mzozo usiendelee na kusambaa katika maeneo mengine ya ukanda huo.

    Antony Blinken ameyasema hayo mjini Tel Aviv Israel ambapo anasema alirejea Israel kushiriki katika "diplomasia kali na washirika wetu" ili kuhakikisha shambulio kama la Hamas mnamo Oktoba 7 halitokei tena.

    Pili, anasema mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kuwalinda raia wa Palestina, na hali ya namna Israel inavyoendesha kampeni yake ya kuishinda Hamas.

    Blinken anasema raia hawapaswi kuteseka kutokana na ukatili wa Hamas.

    Anaongeza kuwa usambazaji endelevu wa misaada ya kibinadamu katika Gaza lazima uongezwe.

  4. Kiongozi wa Hezbollah apongeza mashambulizi ya Hamas dhidi ya Israel lakini anasema yalikuwa 'asilimia 100 ya Wapalestina'

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Kiongozi wa kundi la Kiislamu la Hezbollah, jeshi lenye nguvu zaidi kisiasa na kijeshi nchini Lebanon, amevunja ukimya wake kuhusu vita vya Israel na Gaza.

    Katika hotuba yake kutoka eneo la siri, iliyotazamwa na maelfu ya watu katika mkutano wa hadhara katika mji mkuu wa Lebanon Beirut, Hassan Nasrallah alipoyangeza mashambulizi ya Oktoba 7 nchini Israel ambayo yalisababisha vifo vya watu 1,400.

    Alisema vitendo vya Hamas - ambayo kama vile Hezbollah ni shirika la kigaidi lililopigwa marufuku nchini Uingereza, Marekani na kwingineko - ni "sawa, busara na haki" lakini akayaelezea mashambulizi dhidi ya Israel kama "asilimia 100 ya Wapalestina".

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wafuasi wa Hezbollah walikusanyika katika vitongoji vya kusini mwa Beirut kusikiliza hotuba hiyo

    Katika hotuba yake, alikashifu Marekani, akisema ilihusika na vita vya Gaza.

    Nasrallah pia alishukuru vikosi vinavyoungwa mkono na Iran nchini Yemen na Iraq.

    Waasi wa Houthi nchini Yemen wamekuwa wakifyatua ndege zisizo na rubani dhidi ya Israel, huku wanamgambo wa Shia wa Iraq wakilenga vikosi vya Marekani nchini Iraq na Syria.

    Iran inaunga mkono kile kinachoitwa Axis of Resistance, muungano unaojumuisha Hezbollah - kikosi chake muhimu - pamoja na wanamgambo nchini Iraq, Rais wa Syria Bashar al-Assad, Wahuthi na Hamas.

    Mkuu huyo wa Hezbollah amesema inaonekana kwamba serikali ya Israeli haizingatii masomo ya vita vya awali.

    ‘’Moja ya makosa muhimu ambayo Waisraeli wamefanya na bado wanayafanya ni kuweka malengo ya juu ambayo hawawezi kuyafikia’’, amesema mkuu huyo wa Hezbollah.

    Inafanya makosa kama iliyoyafanya nchini Lebanon mwaka 2006.

    Ni mafanikio gani ambayo jeshi la Israeli limepata hadi sasa Gaza baada ya uharibifu unaoendelea na mauaji ya maelfu ya raia, wengi wao wanawake na watoto, alihoji Sayyed Hassan Nasrallah.

    Nasrallah ameiwajibisha Washington kikamilifu kwa vita dhidi ya Gaza, kwa kuwa Israel ni chombo tu, na Marekani ndio inayozuia usitishaji mapigano, na kutaka iwajibike.

  5. Mafuriko ya ghafla yasababisha maafa katika baadhi ya maeneo ya Kenya

    h

    Chanzo cha picha, Kenya Met Department

    Maelezo ya picha, Watu wanane waliokolewa kutoka kwa lori lililozama kaskazini mwa Kenya siku ya Alhamisi

    Mafuriko makubwa yameyakumba baadhi ya maeneo ya Kenya, na kusababisha uharibifu wa barabara na kuzama kwa magari.

    Katika mji wa pwani wa Mombasa, madereva wa magari walilazimika kuacha magari yao na kutumia pikipiki kufika kwenye uwanja wa ndege na kituo cha treni siku ya Ijumaa, baada ya mafuriko kukata barabara katika sehemu hiyo ya jiji.

    Katika kaunti ya Isiolo kaskazini mwa Kenya, wenyeji wanamsaka kijana aliyesombwa na mafuriko alipokuwa akiendesha pikipiki siku ya Alhamisi.

    Shirika la uuhifadhi wa wanyamapori la Save the Elephants pia liliwaokoa watu wanane waliokuwa katika lori lililozama siku ya Alhamisi, baada ya mafuriko kuwakumba.

    Sio mara ya kwanza kwa kundi la uhifadhi wa wanyamapori nchini Kenya kuwaokoa binadamu walioathiriwa na mafuriko .

    Mapema mwaka huu The Sheldrick Wildlife Trust lilitumia helikopta yao kumuokoa dereva aliyekwama.

    Idara ya hali ya hewa ilikuwa imeonya kuwa mvua ya El Niño inaweza kunyesha Kenya na mataifa mengine ya Afrika Mashariki kuanzia katikati ya mwezi wa Oktoba na kusababisha mafuriko, uharibifu wa miundombinu na vifo.

    Nchi jirani za Tanzania na Somalia pia zimekumbwa na mvua kubwa katika siku za hivi karibuni.

    Lakini tarehe 22 Oktoba, Rais wa Kenya William Ruto alizua mkanganyiko alipodai kuwa nchi haitakumbwa na El Niño, tukio la hali ya hewa ya asili, kama ilivyotabiriwa.

    "Idara ya utabiri wa hali ya hewa kwa sasa imesema hakutakuwa na El Niño. Tutapata tu mvua kubwa lakini hazitafikia kiwango cha uharibifu," Bw Ruto alisema.

    Pamoja na kusababisha mabadiliko ya mvua, halijoto duniani kwa kawaida huongezeka wakati wa kipindi cha El Niño.

  6. Fally Ipupa awataka Wacongo waishio nje ya DRC kutopinga tamasha zake

    g

    Fally Ipupa ni mmoja wa nyota wakubwa wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

    Wimbo wake Un Coup, akimshirikisha mwimbaji mwenye uraia wa Congo na Ufaransa Dadju, kwa mfano, umetazamwa zaidi ya mara milioni 80 kwenye YouTube, na mmatamasha yake ya moja kwa moja yanavutia maelfu ya mashabiki.

    Kwa hakika, watu wengi walitamani sana kumuona akitumbuiza katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwaka jana hivi kwamba Uwanja wa Martyrs wa Kinshasa ulikuwa umejaa kupita kiasi na kukawa na vurugu mwishoni.

    Taarifa za awali kutoka kwa serikali zilisema kuwa watu 11 walipoteza maisha. Kulingana na Ipupa na mwandishi wa BBC Kinshasa, takwimu hii haikuwahi kuthibitishwa kikamilifu.

    Hili si tamasha pekee la Ipupa lililologonga vichwa vya habari. Alipotumbuiza nchini Ufaransa mwaka wa 2020, kulikuwa na ghasia nje ya ukumbi wa Paris huku waandamanaji wakichoma moto mapipa na pikipiki.

    Yote yalihusishwa na siasa. Kwa kipindi cha muongo uliopita Wacongo wanaoishi ugaibuni wamejaribu kuwazuia wanamuziki wa Kongo kufanya matamasha barani Ulaya, ili kuonyesha upinzani wao kwa wanasiasa nyumbani.

    Wamewashutumu nyota wakubwa wa muziki kwa kuwa karibu sana na mamlaka na kushindwa kuzungumza dhidi ya unyanyasaji unaotokea nchini DRC

    h

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Mnamo 2020, waandamanaji waliokuwa wakiandamana kupinga tamasha la Fally Ipupa mjini Paris walichoma moto pikipiki na mapipa.

    Kwa hivyo ni wakati mkubwa kwa Fally Ipupa kwamba kwa mara ya kwanza katika kazi yake hatimaye anastahili kutumbuiza London. Tamasha lake litakuwa mwezi wa Disemba, wakati uchaguzi utakapopangwa kufanyika nyumbani.

    Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 45 na wasimamizi wake wananiambia kwamba makubaliano sasa yamefikiwa na jamii zenye mashaka za Wakongo na anatazamiwa kutumbuiza tena Paris na Brussels.

    "Watu wengi wanajua sasa kwamba sifanyi mambo ya kisiasa, mimi ni mwanamuziki tu na wamegundua kuwa huwezi kumwadhibu mtoto wako maisha yake yote," alisema.

    Ipupa ana huruma kwa wale waliosusia tamasha zake lakini anahisi ni wakati wa kuachana na siasa na kuunga mkono tasnia ya muziki ya Congo.

    "Ninakubali kwamba mambo yalikuwa yakifanyika kisiasa ambayo hayakuwa sawa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na mara zote nimekuwa nikiwaambia kwamba ninakubaliana na baadhi ya waandamanaji ambao walitaka kufikisha ujumbe na kuongeza ufahamu kwa watu.

    “Lakini sasa umefika wakati wa kusema angalieni jamani, tumewaadhibu wasanii, tumepunguza utamaduni wa Congo, ni wakati wa kuionyesha dunia kuwa tuna muziki mkali sana.”

    Anahisi kwamba muziki wa Kongo umeteseka sana, na kupoteza nafasi yake Ulaya dhidi ya muziki kutoka Nigeria, Ghana na Jamaica.

    Wasanii wa Afrobeats wa Nigeria sasa wanajaza kumbi kubwa ambazo wasanii wa Congo walikuwa wakizijaza miaka 10 iliyopita. Lakini ana uhakika kwamba hii inaweza kubadilika.

    “Muziki wa Congo ni miongoni mwa miziki mizuri , tuna wasanii wengi wenye vipaji, hivyo kama ndugu na dada zetu wa Ulaya wanasema hakuna tena kufungia muziki wa Congo huko Ulaya niamini tutachukua nafasi yetu duniani,” alisema.

  7. Habari za hivi punde, Vita vya Gaza: Familia ya Waziri Mkuu wa Uskochi Humza Yousaf yaondoka Gaza

    g

    Chanzo cha picha, PA

    Maelezo ya picha, Wakwe wa Humza Yousaf wamekwama huko Gaza

    Taarifa za hivi punde zinasema famili ya Naibu waziri wa Uskochi Humza Yousaf imeondoka Gaza kuelekea Misri, baada ya kukwama katika eneo hilo tangu yalipotokea mashambulizi ya Hamas ya Oktoba 7 dhidi ya Israel.

    Familia hiyo ni miongoni mwa zaidi ya watu 100 walioorodheshwa katika na Uingereza ya watu wanaoruhusiwa kutoka Gaza leo.

    Taarifa kutoka kwa Yousaf na mkewe Nadia El-Nakla inasema: "Tunafuraha sana kuthibitisha kwamba wazazi wa Nadia waliweza kuondoka Gaza kupitia kivuko cha

    ‘’Wiki hizi nne zilizopita zimekuwa ndoto mbaya kwa familia yetu, tunashukuru sana kwa jumbe zote za faraja na sala ambazo tumepokea kutoka kote ulimwenguni, na kwa kweli kutoka kwa wanasiasa wa pande zoteza Uskochi na Uingereza’’.

  8. Milki za Kiarabu zaonya kuhusu hatari ya vita kuenea hadi eneo lake

    g

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Muungano wa Mataifa ya Kiarabu (UAE) umeonya kuhusu kueneokwa vita vya Gaza hadi kanda nzima ya Mashariki ya Katina umesema kuwa unafanya juhudi ‘’bila kukoma’’ kuhakikisha mapigano yanasitishwa kwa misingi ya kibinadamu.

    UAE ilikuwa moja ya nchi mashuhuri za Kiarabu ambazo zilitia saini Makubaliano ya "Abraham" na Israeli mnamo 2020, kwa upatanishi wa Marekani.

    Israel ilitumai kuwa hilo lingefungua njia ya kuhalalisha uhusiano na Saudi Arabia, taifa kuu la Kiislamu katika eneo hilo, lakini vita vya Gaza vilileta pigo kubwa kwa mpango huo.

    Vita hivyo vilianza kuleta uhasama baada ya kituo cha Mawasiliano cha Kitaifa nchini Bahrain kuthibitisha Alhamisi jioni kurejea kwa balozi wa Bahrain nchini Israel nchini mwake, na kuondoka kwa balozi wa Israel nchini Bahrain.

    Kituo cha serikali pia kilionyesha kuwa safari za ndege za moja kwa moja kati ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Bahrain na Uwanja wa Ndege wa Tel Aviv zimesitishwa kwa wiki kadhaa, na kuongeza kwamba "kipaumbele cha juhudi katika hatua hii lazima kiwekwe katika kulinda maisha ya raia kwa mujibu wa sheria za kimataifa za kibinadamu, na kufanya juhudi ili kupata njia za dharura za kibinadamu ili kupeleka misaada katika Ukanda wa Gaza."

    Haya yanajiri baada ya Bunge la Bahrain kutangaza kusitisha uhusiano wa kiuchumi na Israel.

    Hivi majuzi Jordan ilisitisha uhusiano wake na Israel na kumuondoa balozi wake- Israeli.

    Unaweza pia kusoma

    • China inataka nini katika vita vya Israel na Hamas?
    • 'Sitaki kufa nikiwa na miaka 24' - Mwanamke wa Gaza aliyekwama kwenye kivuko cha Rafah
    • Ezekiel Kitiku: Aieleza BBC namna alivyopotezana na marafiki zake Israel
    • Wakristo wa Gaza: Jinsi waumini hawa wanavyotafuta usalama kati ya makanisa mawili
    • Raia 120,000 wa Israel waomba bunduki kwa mara ya kwanza
    • Kuripoti kuhusu Gaza: 'Wakati mwingine nikiwa nyuma ya kamera mimi husimama tu na kulia'
    • Palestina - Israel: Yahya Sinwar ni nani na kwanini Israel inamsaka?
    • Siri ya Israel kuwafukuza maelfu ya Wapalestina kutoka Gaza mnamo 1971 yafichuliwa
  9. Habari za hivi punde, Israel katika hali ya 'tahadhari ya juu sana' mpakani na Lebanon - IDF

    Tumekuwa tukisikia kutoka kwa msemaji wa jeshi la Israeli Daniel Hagari, ambaye anasema kuwa wako katika hali ya "tahadhari ya juu sana" kwenye mpaka wa kaskazini wa Israeli.

    Kumekuwa na ghasia katika mpaka wa kaskazini mwa Israel na Lebanon katika wiki za hivi karibuni kati ya kundi la Kiislamu la Hezbollah na jeshi la Israel.

    Baadaye leo mkuu wa Hezbollah, shirika la kigaidi lililopigwa marufuku nchini Uingereza, Marekani na mataifa mengine Ulaya wanatazamiwa kutoa hotuba ili kuvunja wa kiki kadhaa.

    "Jana tulifanya shambulio kubwa na kuvipiga vikundi kadhaa vya kigaidi vya Hezbollah ili kukabiliana na shambulio kubwa la Hezbollah ambalo liliwajeruhi raia," Hagari alisema, kulingana na Reuters.

    "Tutaendelea kujibu kwa vikali shambulio lolote dhidi ya raia wa Israel. Tuko kwenye maandalizi ya hali ya juu katika mpaka wa kaskazini, tukiwa katika hali ya tahadhari ya kujibu tukio lolote, leo na katika siku zijazo."

  10. Ndege zisizo na rubani za Marekani zaruka juu ya Gaza kuwatafuta mateka.

    g

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Wanajeshi wa Marekani wakitayarisha ndege isiyo na rubani ya Jeshi la Wanaanga la MQ Reaper kabla ya kuondoka kwenye Uwanja wa Ndege wa Kandahar, Afghanistan, Machi 9, 2016.

    Maafisa wawili wa Marekani walisema Alhamisi, kwa mujibu wa tovuti ya Middle East Eye, kwamba Marekani inarusha ndege zisizo na rubani za upelelezi juu la Gaza, ili kuwapata mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

    Ndege hiyo ya MQ-9 Reaper, inayoendeshwa na Kikosi Maalum cha Operesheni cha Marekani, ilionekana kwenye tovuti ya ufuatiliaji wa safari za ndege za umma -Flightraider24.

    Lakini, maafisa wa Marekani wanasema kwamba ilianza kufanya kazi katika eneo hilo baada ya Oktoba 7, kulingana na jazeti la New York Times.

    Ingawa Israel hufanya safari za upelelezi mara kwa mara juu la Gaza, hii inaweza kuwa mara ya kwanza kwa ndege zisizo na rubani za Marekani kutumika katika vita vya anga vya Gaza," maafisa wa ulinzi wa Marekani walibainisha.

    Unaweza pia kusoma

    • China inataka nini katika vita vya Israel na Hamas?
    • 'Sitaki kufa nikiwa na miaka 24' - Mwanamke wa Gaza aliyekwama kwenye kivuko cha Rafah
    • Ezekiel Kitiku: Aieleza BBC namna alivyopotezana na marafiki zake Israel
    • Wakristo wa Gaza: Jinsi waumini hawa wanavyotafuta usalama kati ya makanisa mawili
    • Raia 120,000 wa Israel waomba bunduki kwa mara ya kwanza
    • Kuripoti kuhusu Gaza: 'Wakati mwingine nikiwa nyuma ya kamera mimi husimama tu na kulia'
    • Palestina - Israel: Yahya Sinwar ni nani na kwanini Israel inamsaka?
    • Siri ya Israel kuwafukuza maelfu ya Wapalestina kutoka Gaza mnamo 1971 yafichuliwa
  11. Urusi inavutiwa na madini ya Equatorial Guinea – Putin

    rg

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Rais Teodoro Obiang Nguema (kushoto) akiwa na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin (kulia) mjini Moscow

    Rais Vladimir Putin anasema kuwa makampuni ya Urusi yana nia "kubwa" katika kuchimba rasilimali za madini nchini Equatorial Guinea.

    Amefanya mazungumzo na Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema siku ya Alhamisi mjini Moscow, ambapo viongozi wote wawili walikubaliana kuimarisha uhusiano baina ya nchi hizo mbili.

    "Uwezo unaowezekana wa uwekezaji ni mkubwa, na uwezo wa nchi yako katika kuendeleza mahusiano haya pia ni mzuri," Bw Putin alisema.

    "Ninamaanisha kuhusu uwezo zaidi unaohusiana na uchimbaji wa rasilimali za madini," aliongeza.

    Equatorial Guinea, nchi ndogo ya Afrika ya kati yenye utajiri wa mafuta, imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi za madini kama vile dhahabu, almasi, urania na gesi.

    Rais Nguema alisema amezikaribisha kampuni za Urusi zinazokuja kuwekeza nchini mwake.

    Pia aliishukuru Urusi kwa kufungua tena ubalozi wake nchini Equatorial Guinea.

  12. Marekani inatumai mikutano ya Blinken itawezesha kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza,

    Antony Blinken amewasili Tel Aviv na ana siku nzima iliyopangwa na viongozi wa Israeli.

    Tofauti na safari nyingi za kimataifa za waziri wa mambo ya nje wa Marekani, ambazo hupangwa kwa uangalifu mapema, inaonekana kana kwamba mpangilio na kile kinachotakiwa kufanyika katika safari hii kimepangwa ndani ya ndege

    Asubuhi yake inaanza na mkutano na Benjamin Netanyahu. Katika ziara ya mwisho ya katibu huyo, mazungumzo yake na waziri mkuu wa Israel yalichukua muda wa saa saba. Leo, ratiba ya Wamarekani ni ngumu zaidi.

    Baada ya saa moja na Netanyahu, Blinken anatembelea baraza la mawaziri la vita la Israeli na Rais wa Israeli Isaac Herzog.

    Baadaye atazungumza nasi waandishi wa habari kupitia vyombo vya habari na, pengine, ataelezea ni nini ameweza kufikia, ikiwa kuna chochote.

    Wamarekani wanatumai mikutano hii italeta mafanikio zaidi katika kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

    Majirani wa Israel Waarabu wanazidi kuwa wazi katika kulaani kampeni ya Israel dhidi ya Hamas.

    Baada ya mikutano ya leo ya Israel, katibu huyo ataelekea Jordan ambako atawasikiliza moja kwa moja baadhi ya viongozi hao wa Kiarabu.

    Upeo wa kuamua ni wapi katibu atafuata kutoka hapa unapimwa kwa masaa - na inategemea kabisa ni wapi Wamarekani wataamua juhudi zake za kidiplomasia zitakuwa na tija zaidi.

    Malengo ya Marekani, hata hivyo, ni kuendelea kuonyesha uungaji mkono kwa Israel, kufanya juhudi zinazoonekana na zinazofaa kupunguza mzozo wa kibinadamu unaoendelea Gaza. Na kuzuia vita vya Israel na Hamas kuingiza eneo zima katika mzozo unaozidi kukua.

  13. Israel inafanya mashambulizi kutoka angani, baharini na nchi kavu

    TH

    Chanzo cha picha, EPA

    Mapigano ya leo asubuhi ni katika maeneo matano tofauti katika mji wa Gaza na kaskazini, ambapo operesheni ya ardhi ya Israel ilikuwa ikizidishwa hapo jana, na magharibi mwa Gaza ndiko kunako uvamizi mkubwa zaidi.

    Jeshi la Israel linajihusisha namashambulizi kutoka angani, baharini na nchi kavu dhidi ya wanamgambo wa Hamas.

    Hamas walitoa taarifa hapo jana kuwa wanapambana na jeshi la Israel kwa kutumia makombora ya vifaru.

    Mashambulizi hayo ya anga yaliendelea usiku kucha hasa karibu na Hospitali ya Al-Quds karibu na Mji wa Gaza ambapo takriban watu 14,000 wamekita kambi katika hospitali hiyo.

    Hospitali hiyo ilisema watu wanane waliunganishwa kwa mashine za kuokoa maisha na haikuwezekana kuzisogeza kwa sababu barabara nyingi karibu na hospitali hiyo zimeharibika, na mapigano makali na Hamas yalikuwa yakitokea umbali wa mita 500 kutoka hospitalini.

    Israel inadhibiti barabara zote mbili - njia kuu za kutokea Gaza kaskazini na barabara ya pwani - kwa hivyo kutoka nje ya Gaza ni vigumu sana, watu wanahatarisha maisha yao kuondoka kuelekea kusini.

    Theluthi mbili ya wakazi wanapata aina fulani ya misaada kutoka Misri kusini - takriban lori 300 na nyingine 100 zinatarajiwa leo - ingawa hali ya kibinadamu ni mbaya zaidi kwa wale walio kaskazini.

    Takriban watu 700,000 huko Gaza hawana umeme, maji au mtandao.

    Unaweza pia kusoma

  14. Mwili wa mwanamke kutoka Kenya aliyetoweka wapatikana katika uwanja wa ndege wa Boston

    th

    Chanzo cha picha, Supplied

    Maelezo ya picha, Margaret Mbitu aliuawa na mpenziwe, ambaye kisha alikimbilia Kenya, polisi wanasema

    Mamlaka za Marekani na Kenya zinamsaka muuaji wa mwanamke Mkenya mwenye aliye pia na urai wa Marekani aliyepatikana amefariki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Boston Logan huko Massachusetts.

    Polisi walisema waliupata mwili uliokuwa na majeraha wa Margaret Mbitu, 31, kwenye kiti cha abiria cha gari lililokuwa limeegeshwa kwenye uwanja wa ndege.

    Mshukiwa mkuu ni mpenzi wa Mbitu, Kevin Kangethe, ambaye inaaminika alikimbilia Kenya baada ya kuuacha mwili wake kwenye uwanja wa ndege.

    Mamake Mbitu aliambia kituo cha Boston 25 News kwamba binti yake amekuwa akijaribu kukatisha uhusiano wake na Kangethe.

    Mbitu alionekana akiwa hai mara ya mwisho alipoondoka kazini Jumatatu usiku.

    • Mzozo wa Israel na Palestina:Matukio ya hivi punde

      Huu hapa muhtasari wa matukio ya hivi punde kutoka eneo Gaza;

      • Waziri wa mambo ya nje wa MarekaniAntony Blinken amewasili Israel, ikiwa ni ziara yake ya pili nchini humo tangu mashambulizi mabaya ya Hamas tarehe 7 Oktoba.Anakutana na Benjamin Netanyahu na ataangazia "hatua madhubuti" ili kupunguza madhara kwa raia katika Ukanda wa Gaza.
      • Jeshi la Israel limetangaza kuwa"limekamilisha kuzingira mji wa Gaza"
      • Kivuko cha Rafah kitafunguliwa kwa mara ya tatu leo ​​tangu Jumatano kwa ajili ya kuwahamisha raia wa nchi mbili.Kuna watu 127 walioorodheshwa katika sehemu ya Uingereza, na karibu 100 wanajulikana kama Waingereza, wengine kama wategemezi wa Palestina au Ireland.
      • Wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas huko Gaza imesema zaidi ya watu 9,000 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu Israel ilipoanzisha mashambulizi yake ya kulipiza kisasi.
      • Maelfu ya watu wa Gaza wanaofanya kazi nchini Israel wanarudishwa Gaza, vibali vyao vya kufanya kazi vimefutiliwa mbali, serikali ya Israel imesema
      • Vyanzo vya kimatibabu vya Palestina viliiambia Reuters kuwa Wapalestina wanane waliuawa katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan usiku kucha
      • Wanawake 242, watoto na wazee wanashikiliwa mateka na Hamas huko Gaza.

      Unaweza pia kusoma

    • 'Hakutakuwa na wafanyikazi wa Kipalestina kutoka Gaza ndani ya Israel'

      th

      Chanzo cha picha, EPA

      Kuna ripoti kwamba maelfu ya wafanyikazi na vibarua wanaovuka mpaka wa Gaza huko Israeli na Ukingo wa Magharibi wamerudishwa Gaza.

      Raia wa Gaza wanaofanya kazi nchini Israel watarejeshwa kwenye eneo lililozingirwa, serikali ya Israel imetangaza.

      Mashahidi waliambia Reuters siku ya Ijumaa kwamba baadhi ya wafanyakazi wa Gaza walikuwa wamerudishwa kupitia kivuko cha Kerem Shalom, kivuko cha bidhaa za kibiashara na Israel kusini mwa Gaza.

      "Israel inakata mawasiliano yote na Gaza.Hakutakuwa na wafanyikazi tena wa Kipalestina kutoka Gaza.Wafanyikazi hao kutoka Gaza waliokuwa Israel siku ya kuzuka kwa vita watarejeshwa Gaza,” ujumbe kutoka ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwenye X, zamani Twitter, ulisomeka.

      Baraza la mawaziri la usalama la Israel pia lilikubali "kukata fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya Ukanda wa Gaza... kutoka kwa fedha za Mamlaka ya Palestina [PA]".PA ina udhibiti wa maeneo ya Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, lakini sio Ukanda wa Gaza unaosimamiwa na Hamas.

      Takriban Wapalestina 18,500 kutoka Gaza walikuwa wamepokea vibali vya kuingia Israel kabla ya shambulio baya la Oktoba 7 lililofanywa na wanamgambo wa Hamas, kulingana na Cogat, chombo cha ulinzi cha Israel kinachohusika na masuala ya kiraia ya Wapalestina.

      Tangu wakati huo, Israel imeanzisha mashambulizi ya kulipiza kisasi katika Ukanda huo.Zaidi ya watu 9,000 wameuawa hapa, kulingana na wizara ya afya inayosimamiwa na Hamas.

      Hayo yakiarifiwa, habari zaidi zimekuwa zikiibuka kutoka Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na Israel kuhusu kile ambacho Reuters inakiita matukio kadhaa tofauti.

      Vyanzo vya matibabu vya Palestina vililiambia shirika hilo la habari siku ya Ijumaa kwamba Wapalestina wanane waliuawa huko usiku kucha.Mmoja wao alikufa kwa majeraha kutokana na tukio la awali, ilisema.

      Ukingo wa Magharibi unaendeshwa na Mamlaka ya Palestina na ni tofauti na Gaza inayosimamiwa na Hamas.

      Marekani inatumai mikutano ya Blinken itaruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza

      Antony Blinken amewasili Tel Aviv na ana siku nzima iliyopangwa kufanya mkutano na viongozi wa Israeli.

      Tofauti na safari nyingi za kimataifa za waziri wa mambo ya nje wa Marekani, ambazo zimetangazwa sana na kupangwa kwa uangalifu mapema, safari hii ina hisia ya timu ya kidiplomasia inayoshughulikia mambo, kihalisi, kwa kasi.

      Asubuhi yake inaanza na mkutano na Benjamin Netanyahu.Katika ziara ya mwisho ya katibu huyo, mazungumzo yake na waziri mkuu wa Israel yalichukua muda wa saa saba.Leo, ratiba ya Wamarekani ni ngumu zaidi.

      Baada ya saa moja na Netanyahu, Blinken anatembelea baraza la mawaziri la vita la Israeli na Rais wa Israeli Isaac Herzog.

      Baadaye atazungumza na sisi kwenye mkutano na vyombo vya habari na, pengine, atasimulia nini - ikiwa ni chochote - amekamilisha.

      Wamarekani wanatumai mikutano hii itafanikisha hatua zaidi katika kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Gaza.

      Majirani wa kiarabu wa Israel wanazidi kuwa wazi katika kulaani kampeni ya Israel dhidi ya Hamas.

      Baada ya mikutano ya leo ya Israel, katibu huyo anaelekea Jordan ambako atasikiliza moja kwa moja kutoka kwa baadhi ya viongozi hao wa Kiarabu.

      Darubini ya kuamua ni wapi katibu huyo ataelekea kutoka hapa itaangaliwa kwa masaa - na inategemea kabisa wapi Wamarekani wataamua juhudi zake za kidiplomasia zitakuwa na tija zaidi.

      Malengo ya Marekani, hata hivyo, ni ya moja kwa moja.Kuendelea kuonyesha uungaji mkono kwa Israel, kufanya juhudi zinazoonekana na zinazofaa kupunguza mzozo wa kibinadamu unaokua huko Gaza Na kuzuia vita vya Israel na Hamas kuingiza eneo zima katika mzozo unaozidi kukua.

      Unaweza pia kusoma

    • Baba ya mchezaji Díaz 'alitekwa nyara na waasi'

      th

      Chanzo cha picha, Getty Images

      Serikali ya Colombia inasema babake mwanasoka wa Liverpool Luis Díaz alitekwa nyara na waasi wa mrengo wa kushoto wa National Liberation Army (ELN).

      Luis Manuel Díaz alikamatwa na watu waliokuwa wamejihami kwa silaha pamoja na mkewe siku ya Jumamosi.

      Mamake mchezaji huyo aliachwa ndani ya gari na watekaji nyara huku polisi walipokaribia lakini watu hao wenye silaha walimburuza baba yake.

      Mamia ya polisi na wanajeshi wametumwa ili kumuokoa .

      Hapo awali polisi walikuwa wamesema kwamba kuna uwezekano mkubwa wa genge la wahalifu kuhusika na kutoweka kwake.

      Lakini siku ya Alhamisi, wajumbe wa serikali ambao kwa sasa wanafanya mazungumzo ya amani na kundi la waasi, walisema kwamba walikuwa na "Ufahamu rasmi" kwamba utekaji nyara huo umefanywa na "kitengo cha ELN".

      Mwakilishi wa kundi hilo ameripotiwa kusema kuwa kundi hilo litamwachilia babake Díaz katika siku zijazo.

      ELN ndilo kundi kuu la waasi nchini Colombia lililosalia.Imekuwa ikipigana na serikali ya taifa hilo tangu 1964 na ina takriban wa wanachama 2,500.

      Linahudumu sana katika eneo la mpaka na Venezuela ambapo Luis Manuel Díaz na mkewe Cilenis Marulanda wanaishi.

    • Blinken kuangazia kupunguza madhara kwa raia

      th

      Chanzo cha picha, Reuters

      Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anafanya ziara yake ya pili nchini Israel tangu Hamas ilipoanzisha mfululizo wa mashambulizi mabaya nchini humo tarehe 7 Oktoba na Israel kuanza kulipiza kisasi huko Gaza.

      Safari yake itazingatia hatua za kupunguza madhara kwa raia katika Ukanda wa Gaza.

      Kabla ya kuondoka kwake, Blinken alisema atatafuta "hatua madhubuti" kutoka kwa Israel ili kuhakikisha kuwa madhara kwa raia wa Palestina yanapungua, kwani Rais wa Marekani Joe Biden pia alitoa wito wa kusitishwa kwa kwa vita kwa muda kwa ajili ya kupeleka misaada ya kibinadamu huko Gaza.

      Blinken pia atafanya mazungumzo nchini Jordan.

      Ziara yake Inakuja wakati Israel iliposema Alhamisi jioni jeshi lake lilikuwa limeuzingira kabisa mji wa Gaza na ilikuwa likishiriki katika mapigano ya ana kwa ana na wapiganaji wa Hamas.

      Unaweza pia kusoma

    • RSF yasema inasonga mbele kuteka Sudan nzima

      th

      Chanzo cha picha, Reuters

      Naibu kamanda wa Kikosi cha (RSF), nchini Sudan Abdel Rahim Hamdan Daglo, anasema kundi lake litaendelea kusonga mbele na kuchukua majimbo yaliyosalia nchini humo kutoka kwa jeshi.

      Tamko la Bw Daglo lilikuja baada ya hivi karibuni RSF kupata mafanikio katika uwanja wa vita katika eneo la magharibi la Darfur, ambako iliteka baadhi ya majimbo na kambi za jeshi.

      Darfur inachukuliwa kuwa ngome ya RSF.

      "Tutaelekea katika majimbo mengine yaliyosalia na makao makuu ya [jeshi], na yatakuwa chini ya udhibiti wetu, Mungu akipenda," Bw Daglo alisema siku ya Alhamisi alipokuwa akiwahutubia wapiganaji wa RSF waliokuwa na furaha katika mji mkuu wa jimbo la Darfur la Kati la Zalingei.

      Hapo awali, wanajeshi walipuuza mafanikio ya uwanja wa vita yaliyopatikana hivi majuzi na kikundi huko Darfur.

      Mazungumzo ya amani kati ya pande hizo mbili yanaendelea katika mji wa bandari wa Saudia wa Jeddah katika jitihada za kumaliza mzozo uliozuka katikati ya mwezi Aprili.

      Unaweza pia kusoma

    • Wanajeshi wanne zaidi wa Israel wauawa katika mashambulizi ya ardhini Gaza