Uganda yathibitisha mlipuko mpya wa virusi vya Ebola

Mwanaume mwenye umri wa miaka 24 aliyeambukizwa Ebola amefariki dunia katikati mwa Uganda katika mlipuko mpya uliothibitishwa na maafisa wa afya.

Moja kwa moja

  1. Na kufikia hapo tunakamilisha matangazo hayo ya moja kwa moja. Hadi kesho kwaheri.

  2. Vita vya Ukraine: Maeneo yaliyochukuliwa yatoa wito wa kura ya haraka ili kujiunga na Urusi

    Ni vigumu kuona jinsi kura inaweza kufanyika wakati Ukraine bado inadhibiti maeneo mengi ya Donetsk na Zaporizhzhia.

    Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

    Maelezo ya picha, Ni vigumu kubaini jinsi kura ya maoni inaweza kufanyika wakati Ukraine bado inadhibiti maeneo mengi ya Donetsk na Zaporizhzhia.

    Takriban miezi saba baada ya Urusi kuivamia Ukraine, maeneo manne yaliyo chini ya udhibiti wa Moscow yametangaza mipango ya kile kinachoitwa kura ya maoni ya dharura ya kujiunga na Urusi.

    Uvamizi wa Urusi umekwama katika miezi ya hivi karibuni na Ukraine imetwaa tena maeneo mengi ya kaskazini-mashariki.

    Sasa maafisa wanaoungwa mkono na Urusi huko mashariki na kusini wanasema wanataka kura za siku tano kuhusu kuchukuliwa kwa maeneo hayo kuanzia wiki hii. Urusi ilitwaa eneo la Crimea mnamo 2014, baada ya kura iliyolalamikiwa na watu wengi kama udanganyifu.

    Jumuiya ya kimataifa haijawahi kutambua uchukuliwaji wa eneo hilo, lakini imekuwa wazi kwa muda mrefu kuwa Urusi inakusudia kuthibisha uvamizi wake katika maeneo mengine waliyoyachukua kwa njia hiyo hiyo.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Dmytro Kuleba alisema kuwa "kura za maoni za uongo hazitabadilisha chochote."

    Naibu mkuu wa Baraza la Usalama la Urusi, Dmitry Medvedev, alisema mapema Jumanne kwamba kupiga kura katika mikoa ya mashariki ya Donetsk na Luhansk - pia inajulikana kama Donbas - kutarekebisha "haki ya kihistoria" na haitaweza kutenguliwa: "Baada ya marekebisho ya katiba ya serikali yetu, hakuna kiongozi wa baadaye wa Urusi, hakuna afisa, atakayeweza kubadili maamuzi haya.''

    Mamlaka mbili zilizojitenga zinazoungwa mkono na Urusi huko Donetsk na Luhansk zimesema zingepiga kura tarehe 23-27 Septemba.

    Maafisa waliowekwa na Urusi katika eneo la kusini la Kherson walisema pia wangepiga kura, na tamko kama hilo lilitoka katika maeneo yanayokaliwa na Urusi ya Zaporizhzhia.

    • Vita vya Ukraine: Je nani anayeibuka mshindi?
    • Kwa nini Ukraine imekuwa na mafanikio makubwa dhidi ya Urusi na inakabiliwa na changamoto gani?
    • Vita vya Ukraine: Hasara waliopata wanajeshi wa Urusi inamaanisha nini kwa Putin?
  3. Ashtakiwa kwa kumuua mwalimu wa dini kwa 'kukataa kuolewa naye '

    JELA

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Polisi katika kijiji cha Badh Bir wilaya ya Peshawa, Pakistan wanamshikilia mwanaume mmoja kwa kumuua mwalimu wa madrasa baada ya kukataa kuolewa naye Mwalimu huyo hakutaka kuolewa na mwanaume huyo ambaye alikuwa ni kaka wa shemeji yake na wiki moja iliyopita wazazi wake walimtafutia uhusiano mwingine sehemu nyingine , jambo ambalo lilimsikitisha sana shemeji wa mwalimu huyo na ndipo alipomtesa na kumuua.

    Hayo yalisemwa na polisi katika mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo katika kijiji cha Badh Bir wilaya ya Peshawar.

    Kwa mujibu wa polisi wamemkamata shemeji wa mwalimu huyo na kumfikisha mahakamani ambapo mahakama iliamuru mshitakiwa arudishwe rumande kwa siku tatu kwa uchunguzi.

    "Mauaji hayo yalikuwa ya kupangwa na inaonekana mtuhumiwa alikuwa amefanya mipango bora kwa upande wake, lakini polisi kwa msaada wa kamera za CCTV na ushahidi wa papo hapo."

    Mtuhumiwa alikamatwa ndani ya siku chache baada ya tukio hilo. Alisema kuwa baada ya mauaji hayo,

    shemeji wa mwanamke huyo aliongoza katika maandamano ya kupinga kitendo hicho katika eneo la Budh Bir na pia alishiriki kikamilifu katika kutoa kauli mbiu dhidi ya polisi na uongozi wa madrassa, ‘ili mtu yeyote asitie shaka, lakini mshtakiwa aliacha alama za uhalifu wake mahali fulani.'

    Maiti ya mwalimu huyo ilipatikana huko Badh Bir Ijumaa iliyopita asubuhi, ambapo wananchi wa eneo hilo waliandamana na kufunga barabara kuu ya Indus.

  4. Mazishi ya Malkia: Bendera zapandishwa huku kipindi cha maombolezo kikifika mwisho

    Bendera

    Chanzo cha picha, NEIL HALL/EPA-EFE/REX/SHUTTERSTOCK

    Bendera kwenye majengo ya serikali ya Uingereza kote ulimwenguni zimepandishwa tena kutoka nusu mlingoti, huku kipindi cha maombolezo ya kitaifa kufuatia kifo cha Malkia Elizabeth II kikiwa kinakaribia kumalizika.

    Malkia alizikwa katika hafla binafsi huko Windsor Jumatatu jioni, kufuatia mazishi ya serikali huko London na maandamano ya kijeshi kuelekea Windsor Castle.

    Lakini Familia ya Kifalme itaendelea kuadhimisha wiki nyingine ya maombolezo. Washiriki wa familia ya kifalme hawatarajiwi kutekeleza majukumu yoyote ya umma kwa wakati huu.

    Bendera katika makazi ya kifalme zitasalia nusu mlingoti hadi tarehe 27 Septemba siku moja baada ya muda wao wa maombolezo kuisha.

    Kasri ya Buckingham imesema wafanyikazi wa nyumba ya kifalme, wawakilishi kwenye majukumu rasmi na wanajeshi waliojitolea kutekeleza majukumu ya sherehe pia watazingatia maombolezo yaliyoongezwa.

    Operesheni ya kusafisha inaendelea baada ya mamia ya maelfu ya watu kote Uingereza kumiminika London kutazama mazishi ya Malkia.

    Wasafishaji katika Baraza la Southwark kusini mwa London walifanya kazi kwa saa 24 zaidi wakati waombolezaji wakiwa kwenye foleni ya kutembea wakiondoa tani saba za takataka katika mchakato huo.

  5. Maandamano ya Hijabu Iran: Massa Amini afariki baada ya kukamatwa na polisi kwa kutovaa hijab

    .

    Chanzo cha picha, FAMILIA YA MAHSA AMINI

    Maelezo ya picha, Massa Amini

    Kifo cha mwanamke mwenye umri wa miaka 22 aliyekamatwa na polisi wa kitamaduni wa Iran kwa kutofuata kanuni za mavazi ikiwemo kuvaa hijabu kimezusha maandamano makali nchini humo.

    Masa Amini, mwanamke wa Kiirani mwenye umri wa miaka 22, alikamatwa na kundi la polisi lenye msimamo mkali wa Kiislamu.

    Ni jeshi la polisi linalofanya kazi kutekeleza kanuni za kimsingi za Kiislamu nchini Iran.

    Polisi huchukua hatua iwapo kanuni za dini ya Kiislamu zitakiukwa.

    Masa Amini alikamatwa Jumanne, Septemba 13.

    Maafisa wa polisi walisema kwamba alikamatwa kwa maelezo na maoni yake kuhusu hijabu.

    Katika hali hii, Massa alifariki siku ya Ijumaa tarehe 16.

    Alikufa kwa mshtuko wa ghafla wa moyo, polisi wa Tehran walisema.

    Lakini wazazi wa Masa wanakanusha hili.

    Wanaripoti kwamba binti yao alikuwa mzima na hakuwahi na ugonjwa kama huo.

    Akiongea kuhusu hili, babake Massa aliambia vyombo vya habari vinavyounga mkono mageuzi Emthedad, kwamba ‘’Mimi binafsi nakataa maoni yaliyotolewa na polisi kuhusu hali ya binti yangu’’, kulingana na shirika la habari la Reuters.

    Vilevile, aliyeshuhudia alisema polisi walimpiga Masa wakati akikamatwa na kupakiwa kwenye gari.

    Alikamatwa kwa kutovaa hijabu ili kufunika nywele zake kikamilifu na alikuwa katika hali ya kukosa fahamu kabla ya kufariki hospitalini siku ya Ijumaa, kulingana na Reuters.

    Ni katika hali hiyo ambapo wanawake wa Iran wanachapisha video zao wakikata nywele na kuchoma hijabu zao kupinga tukio hilo.

    soma zaidi:

  6. Sherri Papini: Mwanamke wa Marekani aliyeghushi kutoweka kwake ahukumiwa kifungo cha miezi 18

    .

    Chanzo cha picha, SHASTA COUNTY SHERIFF

    Maelezo ya picha, Mama huyo amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela

    Mwanamke wa California ambaye alifeki utekaji nyara wake binafsi amehukumiwa kifungo cha miezi 18 jela kwa kutoa taarifa za uongo kwa FBI.

    Sherri Papini, 39, alipotea Novemba 2016 baada ya kwenda kukimbia.

    Alionekana wiki tatu baadaye ‘Siku ya Shukrani’ akidai kuwa wanawake wawili wa Kihispania walikuwa wamemteka nyara, na hivyo kuzua msako wa mataifa mengi.

    FBI baadaye ilihitimisha kuwa alikuwa akiishi katika nyumba ya mpenzi wake wa zamani na alikuwa amejijeruhi kama sehemu ya mpango huo.

    Katika Mahakama ya Wilaya ya Marekani huko Sacramento siku ya Jumatatu, Papini aliomba msamaha, akisema alikuwa na hatia ya kusema uwongo na ‘’kuvunja heshima’’.

    ‘’Ninasikitika sana kwa watu wengi ambao wameteseka kwa sababu yangu - watu waliojitolea kwa hiari kunisaidia katika wakati ambao nilihitaji sana msaada,’’ alisema.

    ‘’Ninachagua kukubali kwa unyenyekevu wajibu wote.’’

    Chini ya mkataba wa Aprili na waendesha mashtaka, Papini alikiri kosa moja la kudanganya afisa wa serikali na ulaghai wa barua.

    Wakili wa Papini, William Portanova aliomba mteja wake apewe kifungo kidogo cha jela, akiiambia mahakama kwamba kufedheheshwa kwa matendo yake kungekuwa kifungo chake cha maisha.

    Kwa kubadilishana na hatia ya Papini, waendesha mashtaka walitaka hukumu nyepesi - kati ya miezi minane na 14 - chini ya kiwango cha juu cha miaka 25 ambacho angekabiliwa nacho.

    Papini pia alikubali kulipa $300,000 (£231,000), ambayo sehemu yake itagharamia uchunguzi wa polisi.

    Pia atatumia miaka mitatu chini ya ulinzi unaosimamiwa baada ya kuachiliwa kutoka jela.

    Habari za kutoweka kwake ziliibuka kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 2016, wakati mumewe aliripoti kutoweka baada ya kukosa kuwachukua watoto wao kutoka kwa kituo cha kutunza watoto.

    Wiki tatu baadaye, alipatikana akiwa amepigwa na kujeruhiwa kando ya barabara akidai alitekwa nyara kwa mtutu wa bunduki.

    Hata hivyo, shirika la FBI lilihitimisha mwezi Machi kuwa, hili suala zima lilipangwa (feki).

  7. Mazishi ya Malkia Elizabeth II: Mwanamume wa Hong Kong ambaye alihudhuria ibada azuiliwa

    .

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Picha kutoka maktaba ya muombolezaji akiweka shada la maua nje ya Ubalozi Mkuu wa Uingereza

    Mwanaume mmoja wa Hong Kong ambaye alienda katika ubalozi mdogo wa Uingereza Jumatatu usiku kutoa heshima kwa Malkia Elizabeth II, miongoni mwa waombolezaji wengi, amezuiliwa.

    Ripoti za ndani zinasema mwanamume huyo, 43, alicheza nyimbo kadhaa kupitia kinanda chake cha mdomo, ikiwa ni pamoja na iliyohusishwa na maandamano ya 2019, pamoja na wimbo wa taifa wa Uingereza.

    Alizuiliwa chini ya sheria ya uchochezi ya wakati wa ukoloni, polisi waliambia BBC Kichina.

    Sheria hii hadi hivi karibuni ilikuwa haitumiki sana na waendesha mashitaka.

    Lakini miezi michache iliyopita tumeona kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoshtakiwa chini ya sheria hii, ikiwa ni pamoja na waganga watano ambao walipatikana na hatia mapema mwezi huu ya kuchapisha vitabu vya watoto ‘’vya uchochezi’’.

    Kanda zilizosambazwa sana kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha mwanamume huyo akiwa amesimama nje ya ubalozi huo akicheza nyimbo wa ‘’Glory to Hong Kong’’, wimbo usio rasmi wa waandamanaji wakati wa maandamano ya demokrasia ya 2019, kupitia kinanda chake cha mdomo.

    Umati mkubwa, uliokuwa umekusanyika kutazama matangazo ya moja kwa moja mtandaoni ya mazishi ya Malkia wa baadaye nchini Uingereza, wanaonekana wakiimba pamoja na wimbo huo.

    Mashairi ya wimbo huo yanarejelea ‘’machozi kwenye ardhi yetu’’, na pia yanataja ‘’demokrasia na uhuru’’.

    Polisi waliambia BBC mwanamume huyo alizuiliwa kwa tuhuma za kutekeleza ‘’kitendo kwa nia ya uchochezi’’.

    Hong Kongers kwa muda wa wiki moja iliyopita wamekuwa wakipanga foleni kwa masaa mengi ili kutoa heshima zao kwa Malkia, katika kile ambacho kimekuwa onyesho kubwa zaidi la mapenzi kwa Malkia kuonekana nje ya Uingereza.

    Mji huo, ambao zamani ulikuwa koloni la Uingereza, ulirejea katika utawala wa China mwaka 1997.

    Chini ya masharti ya makabidhiano hayo, China ilikubali kuitawala Hong Kong chini ya kanuni ya ‘’nchi moja, mifumo miwili’’, ambapo mji huo utafurahia ‘’kiwango cha juu cha uhuru, isipokuwa katika mambo ya nje na ulinzi’’ kwa miaka 50 ijayo.

    Lakini ukandamizaji dhidi ya wanaofanya maandamano, Beijing kuweka sheria yake ya usalama wa kitaifa na kuruhusu tu ‘’wazalendo’’ kutawala kunaonekana na wengi kama kwenda kinyume na ahadi hiyo.

    Soma zaidi:

  8. Maandamano ya Uganda yalaani sera ya mradi wa mafuta ya Umoja wa Ulaya

    Kikundi kidogo cha waandamanaji waliokuwa wamebeba mabango wamekusanyika nje ya ofisi za Umoja wa Ulaya katika mji mkuu wa Uganda, Kampala, kuelezea kutofurahishwa na wito wake kwa nchi hiyo kusitisha mradi wa kimkakati wa bomba la mafuta na nchi jirani ya Tanzania.

    ‘’EU inaheshimu Waafrika na rasilimali zao,’’ bango moja linasema, ‘’mafuta yetu ni tumaini letu,’’ lingine linasema.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Wiki iliyopita bunge la EU lilipitisha azimio la onyo la ukiukwaji wa haki za binadamu na hatari ya kijamii na kimazingira inayoletwa na mradi huo.

    Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema baadhi ya watu 100,000 wako katika hatari na wamewataka wakandarasi, Kampuni ya Total Energies ya Ufaransa na Shirika la Mafuta la Kitaifa la China, kusitisha mradi wa $10bn (£8bn) hadi wapate njia mbadala.

    Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki utaenea kilomita 1,443 (maili 896) kutoka Ziwa Albert magharibi mwa Uganda hadi bandari ya Tanga ya Tanzania kwenye Bahari ya Hindi.

    Mamlaka nchini Tanzania na Uganda zimekosoa upinzani wa EU kwa mradi huo.

    Rais wa Uganda Yoweri Museveni alisema hakuna kitakachozuia mradi huo.

    “Niliona kwenye magazeti kwamba bunge la EU lilipitisha azimio la kuelekeza Total kutoendelea na Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki.

    Tafadhali, usipoteze muda wako kufikiria hilo.

    Tuna mkataba na Total umeandikwa vizuri sana.

    Mafuta yatatoka mnamo mwaka 2025, kundi la kwanza.

    Mradi wa mafuta utaendelea na hakuna anayeweza kuuzuia,” rais alisema Ijumaa wiki jana.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Mark Frerichs: Mateka wa Marekani aliyebadilishwa na kiongozi wa Afghanistan anayehusishwa na Taliban

    .
    Maelezo ya picha, Mark Frerichs alitekwa nyara na Taliban mnamo 2020

    Kundi la Taliban limemwachilia mhandisi wa Marekani ambaye walikuwa wamemshikilia mateka tangu 2020 ili kubadilishana na kiongozi wa kikabila wa Afghanistan aliyekuwa kizuizini na Marekani tangu 2005.

    Mark Frerichs alikabidhiwa katika uwanja wa ndege wa Kabul siku ya Jumatatu, Taliban walisema.

    Kwa upande wao walimpokea Bashir Noorzai, mshirika wa Taliban anayetumikia kifungo cha maisha jela kwa ulanguzi wa dawa za kulevya.

    Rais wa Marekani Joe Biden alisema kuwa kubadilishana kunahitaji "maamuzi magumu" ambayo hakuyachukulia kirahisi.

    Bw Frerichs, mwenye umri wa miaka 60, alitekwa nyara na kundi la Taliban mwaka mmoja kabla ya kundi hilo kurejea madarakani nchini Afghanistan na serikali yake inayoungwa mkono na nchi za Magharibi kuporomoka.

    Alikuwa akiishi na kufanya kazi huko Kabul kama mhandisi wa ujenzi kwa miaka 10.

    Dadake Bw Frerich, Charlene Cakora, alisema familia haijawahi kukata tamaa ya kumpata tena.

    "Nimefurahi sana kusikia kwamba kaka yangu yuko salama na anaelekea nyumbani kwetu. Familia yetu imesali kwa hili kila siku ya zaidi ya miezi 31 ambayo amekuwa mateka," alisema katika taarifa.

    "Kulikuwa na baadhi ya watu waliokuwa wakibishana dhidi ya mpango huo uliomrudisha Mark nyumbani, lakini Rais Biden alifanya kilichokuwa sawa. Aliokoa maisha ya mkongwe wa Marekani asiye na hatia."

    "Kwa hakika tunajisikia faraja sana. Imekuwa muda mrefu," alisema.

    Kuzuiliwa kwa afisa huyo wa zamani wa jeshi la wanamaji kumekuwa kikwazo kikubwa katika kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Taliban, ambayo serikali yao bado haijatambulika na nchi yoyote duniani.

    Rais Biden alisema mwezi Januari: "Taliban lazima imwachilie mara moja Mark kabla ya kutarajia kuzingatiwa kwa matarajio yake ya uhalali. Hili haliwezi kujadiliwa."

    Hata hivyo, Mmarekani mwingine mmoja amesalia mikononi mwa Taliban.

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Bashir Noorzai aliwaambia waandishi wa habari mjini Kabul kuachiliwa kwake kutaleta amani na Marekani

    Kwa upande mwingine, Bashir Noorzai alikaribishwa kishujaa aliporejea katika mji mkuu wa Afghanistan, na alilakiwa na wapiganaji wa Taliban waliobeba taji za maua.

    "Kuachiliwa kwangu pamoja na Mmarekani kutafanya amani kati ya nchi hizi," aliuambia mkutano wa wanahabari.

    Noorzai alikuwa mshirika wa karibu na rafiki wa mwanzilishi wa Taliban Mullah Omar na alisaidia kufadhili serikali ya kwanza ya Taliban katika miaka ya 1990.

    Soma zaidi:

  10. Serikali ya Tanzania yafuta baadhi ya tozo za miamala,

    Mwanamke akiwa ameshika simu

    Serikali ya Tanzania hatimaye, imepunguza baadhi ya tozo zinazotozwa katika baadhi ya miamala nchini humo. Haya ni kwa mujibu wa Waziri wa Fedha Mwigulu Nchemba ambapo mapema hii leo ametoa kauli ya serikali kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusu tozo yanayoendelea nchini.

    Waziri Nchemba, amesema, kufuatia malalamiko hayo, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Mwenyekiti wake ambae pia ni rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kiliielekeza Serikali kupitia upya tozo za miamala na kuzingatia maoni ya wananchi.

    ”Wizara ya Fedha na Mipango kupitia wataalam wake wa Bajeti na wataalam wa Sera wakiwashirikisha wadau wamefanyia kazi maelekezo ya Chama na Maelekezo ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia upya tozo hizo,” amesema Nchemba, na kuongeza, ”Napenda kuwasilisha taarifa kuwa tumefanya mapitio kama ifuatavyo: Kupunguza mzigo wa tozo kwa jamii, Kuchochea matumizi ya miamala kwa njia ya fedha taslimu (cash); Kurahisisha utozaji, na Kuzuia utozaji wa tozo husika mara mbili kwa kuwa utozaji wake kwa sasa unahusisha pande zote mbili yaani mtoaji na mpokeaji.

    Kwa mujibu wa taarifa yake, marekebisho yatakayofanyika ambayo yataanza rasmi tarehe moja mwezi Oktoba, ni pamoja na kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki kwenda mitandao ya simu (pande zote); kufuta tozo ya kuhamisha fedha ndani ya benki moja (pande zote); kufuta tozo ya kuhamisha fedha kutoka benki moja kwenda benki nyingine (pande zote).

    Aidha, wafanyabiashara (merchants) hawatahusishwa kama ilivyo kwenye kanuni za sasa.

    Msamaha huo pia utahusisha kusamehe tozo ya miamala kwenye utoaji wa fedha taslimu kupitia wakala wa benki na ATM kwa miamala yenye thamani isiyozidi shilingi 30,000; na kupunguza gharama ya miamala kwa asilimia 10 hadi asilimia 50 kufuatana na kundi la miamala.

    Marekebisho haya yataanza kutumika tarehe 1 Oktoba 2022.

    Wakati huo huo, Waziri Nchemba, amekiri kwamba ni dhahiri punguzo hilo litaathiri mapato ya Serikali, lakini ameelekeza fedha hizi zifidiwe kutokana na kubana matumizi mengineyo ndani ya Serikali ambayo hayataathiri utekelezaji wa majukumu ya Msingi ya mafungu husika.

    ”Namwelekeza Mlipaji Mkuu wa Serikali kukaa na Maafisa Masuuli wote kuyaangalia upya mafungu ya matumizi mengineyo ili miradi ya maendeleo yote isiathirike kwa hatua hii. Tukate kwenye chai, vitafunwa, misafara kwenye safari za ndani na nje kwa maafisa wa Wizara zetu kama Mhe Rais alivyoelekeza, tukate Mafunzo, Semina, Matamasha, Warsha, makundi yanayokwenda kukagua mradi uleule kwa nyakati tofauti au makundi yanayokwenda eneo lilelile kila mtu na gari lake,” ameeleza.

  11. Nick Mwendwa arejea tena kama rais wa Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) baada ya tuhuma za utumizi mbaya wa pesa

    .
    Maelezo ya picha, Nicholas Mwendwa

    Rais wa Shirikisho la Soka la Kenya Nick Mwendwa Jumanne aliwaongoza maafisa wengine wa bodi hiyo hadi ofisini, Kandanda House huko Kasarani, zaidi ya miezi 10 baada ya kufukuzwa na Katibu wa Baraza la Mawaziri la Michezo Amina Mohamed.

    Mwendwa aliongoza Makamu wa Rais wa FKF Doris Petra, Katibu Mkuu Barry Otieno, Mkuu wa Uadilifu wa FKF Michael Kamure miongoni mwa wengine hadi Kandanda House kulikokuwa kumefungwa baada ya kuondolewa ofisini.

    Pamoja na Wanachama wengine Mtendaji wa Kitaifa wa FKF, Mwendwa alifukuzwa ofisini mnamo Novemba 11, 2021 na Waziri wa Michezo Amina Mohamed baada ya ukaguzi wa hesabu za shirikisho zinazodaiwa utumizi mbaya wa pesa.

    Akiwa ameshtakiwa mahakamani kwa makosa manne ya ulaghai, Mwendwa - katika barua ya Novemba 29 iliyotumwa kwa NEC ya FKF - alisema alihamisha majukumu yake kwa naibu wake Petra huku akitaka kusafisha jina lake.

    Mohamed aliteua Kamati ya Utunzaji ya FKF kwa kipindi cha awali cha miezi sita kabla ya kubadilika na kuwa Kamati ya Mpito.

    Amina aliongeza muda ya Kamati ya Mpito kwa miezi miwili mnamo Agosti 16. Bado haijabainika hatma ya Kamati hiyo huku FKF ikipanga kurejea ofisini.

    Mwendwa alikamatwa mara kadhaa na kushtakiwa kwa ulaghai, lakini kesi hiyo ilifutwa chini ya Kifungu cha 87 cha Kanuni ya Adhabu mnamo Julai 6.

    Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma akamshtaki Mwendwa upya katika Mahakama za Kiambu siku moja baadaye, lakini bosi wa FKF akapata amri ya mahakama kutoka kwa Mahakama Kuu ya kusitisha mashtaka yoyote mapya dhidi yake.

    Mwendwa mnamo Septemba 9 alimwandikia Rais wa Fifa Gianni Infantino akimjulisha kuwa yuko tayari kurejea ofisini baada ya kujiondoa kushughulikia kesi zake.

    Jaji Esther Maina alitangaza Septemba 21 kuwa siku ya kutoa uamuzi iwapo mashtaka mapya yaliyowasilishwa dhidi ya Mwendwa ni ya kisheria na kikatiba.

    Soma zaidi:

  12. Miili zaidi yaopolewa kutoka mto Yala Magharibi mwa Kenya

    .

    Chanzo cha picha, TWITTER

    Maelezo ya picha, Chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya Yala

    Miili saba zaidi imeopelewa kutoka mto Yala Magharibi mwa Kenya karibu na mahali ambapo makumi ya wengine zaidi wamegunduliwa katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

    Ripoti ya polisi iliyoonekana na maafisa katika hifadhi ya maiti ya kaunti ndogo ya Yala, miili ambayo haikudaiwa na yeyote ilitolewa mtoni katika muda wa miezi miwili iliyopita.

    Miili hiyo haijatambuliwa huku ikisubiri kufanyiwa uchunguzi.

    Maafisa wa chumba cha kuhifadhi maiti wanasema miili mitatu ilitolewa na wapiga mbizi mwezi Septemba na mingine minne iligunduliwa na wakazi kando ya mto huo.

    Ugunduzi wa hivi punde unaongeza idadi ya miili iliyochukuliwa kutoka mtoni hadi zaidi ya 30 tangu Januari mwaka huu.

    Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wanasema wakaazi katika eneo hilo wanaishi kwa hofu kutokana na kupatikana kwa miili isiyojulikana kutoka kwenye mto huo.

    Polisi bado hawajatoa maoni yao kuhusu suala hilo.

    Maelezo ya uchunguzi wa kitaalamu uliofanywa mapema mwaka huu kutaka kubaini ni nani alihusika na sababu za mauaji hayo bado hazijawekwa wazi.

    Kumekuwa na wasi wasi kuhusu visa vya utupaji miili katika mito ya Kenya siku za hivi karibuni.

    Septemba iliyopita, miili 11 iligunduliwa katika Mto Tana katika Kaunti ya Garissa kaskazini-mashariki mwa Kenya.

    Soma zaidi kuhusu suala hili:

  13. Nigeria yanasa kiasi kikubwa zaidi cha dawa za kokeini kuwahi kutokea

    .

    Chanzo cha picha, NDLEA NIGERIA

    Maelezo ya picha, Wanaume watano walikamatwa katika operesheni hiyo

    Shirika la Kitaifa la Kusimamia Sheria ya Dawa za Kulevya nchini Nigeria linasema kuwa limefanya kile kinachoonekana kuwa kunasa kiasi kikubwa zaidi cha dawa za kulevya aina ya kokeini katika historia ya nchi hiyo.

    Tani 1.8 za kokeini zinazokadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya $278m (£243m) ziligunduliwa katika ghala katika eneo la Ikorodu, kaskazini-mashariki mwa kitovu cha kibiashara, Lagos.

    Dawa hizo zilihifadhiwa katika mifuko 10 ya kusafiria na mapipa 13, lilisema Shirika la Kitaifa la Kusimamia Sheria ya Dawa za Kulevya (NDLEA).

    Wanaume wanne wa Nigeria wenye umri wa miaka 69, 65, na wawili wenye umri wa miaka 53 walikamatwa katika maeneo tofauti ya Lagos.

    Raia wa kigeni pia alifafanuliwa kwa kina, katika kile ambacho shirika hilo lilisema ni ‘’operesheni iliyoratibiwa vyema na iliyoongozwa na ujasusi’’ iliyofanywa kwa siku mbili.

    NDLEA inasema wanaume hao walikuwa wakipanga kuuza dawa hizo kwa wanunuzi wa Ulaya, Asia na sehemu nyingine za dunia.

    Mkuu wa shirika hilo, Brigedia Jenerali Mohamed Buba Marwa (Mstaafu), aliwasifu maafisa wake walioshirikiana na wenzao wa Marekani katika operesheni hiyo.

    ‘’Msako huo ni pigo la kihistoria kwa mashirika ya dawa za kulevya na onyo kali kwamba wote watakamatwa ikiwa watashindwa kutambua kuwa mchezo umebadilika,’’ taarifa kutoka kwa shirika hilo ilimnukuu akisema.

    Soma zaidi:

  14. Habari za hivi punde, Uganda yathibitisha mlipuko mpya wa virusi vya Ebola

    Mwanaume mwenye umri wa miaka 24 aliyeambukizwa Ebola amefariki dunia katikati mwa Uganda katika mlipuko mpya uliothibitishwa na maafisa wa afya.

    Waziri wa afya amewaambia waandishi wa habari kwamba mwathiriwa alikuwa ameonyesha dalili kabla ya kuugua ugonjwa huo.

    Alikuwa mkazi wa kijiji cha Ngabano katika wilaya ya Mubende, yapata kilomita 147 (maili 91) kutoka mji mkuu, Kampala.

    Ruka X ujumbe
    Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

    Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

    Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

    Mwisho wa X ujumbe

    Kisa cha aina hiyo ambacho ni nadra kilithibitishwa na Taasisi ya Utafiti wa Virusi vya Uganda, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilisema katika taarifa.

    “Shukrani kwa utaalamu wake [Uganda], hatua imechukuliwa ili kubaini virusi hivyo haraka na tunaweza kutumia ujuzi huu ili kukomesha kuenea kwa maambukizi,’’ alisema Dk. Matshidiso Moeti - Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika.

    Shirika la Afya Ulimwenguni linasema kuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha takriban muongo mmoja kwa kesi ya Ebola kuthibitishwa nchini humo.

    Takriban watu wanane walio na dalili zinazoshukiwa wanapokea huduma ya matibabu, na WHO sasa inatuma wafanyikazi katika eneo lililoathiriwa.

    Visa vingi vya virusi hivyo vimeripotiwa katika nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, hivi karibuni zaidi ikiwa mwezi uliopita.

    Sampuli zilizokusanywa kutoka kwa mwanamume huyo ambaye aliwasilishwa hospitalini akiwa na dalili za maambukizi ya virusi vilipatikana na virusi vya ugonjwa wa Ebola aina ya Sudan.

    Kijana huyo alikuwa mgonjwa kwa takriban siku nne, na amekufa.

    Baada ya uchunguzi wa maafisa wa afya, vifo vingine sita katika familia moja vimethibitishwa kuwa Ebola.

    Wizara ya afya nchini Uganda imedhibitisha watu sita wamefariki wilayani Mubende wakiwa na dalili za ugonjwa wa Ebola.

    Watu wazima watatu na watoto watatu walikufa katika hali isiyoeleweka ndani ya wiki mbili zilizopita.

    Marehemu ni pamoja ni pamoja na mtoto wa kike wa miezi 10 ambaye alifariki tarehe 11 Septemba 2022.

    Inasemekana kuwa walionyesha dalili za Ebola.

    Timu za afya ya jamii sasa zinafuatilia watu wowote ambao wanafamilia wanaweza kuwa wamewasiliana nao.

    Familia hizi zitatengwa na kuwekwa chini ya karantini.

    Wizara ya afya ya Uganda ilisema kuwa chanjo pekee zinazopatikana nchini humo ni zile zilizokusudiwa kwa aina ya Ebola ya Congo.

    Lakini mamlaka imewahakikishia umma kuwa wana uwezo na ujuzi wa kudhibiti Ebola, kulingana na uzoefu wa awali wa milipuko ya virusi.

    Shirika la Afya Ulimwenguni pia linatuma wafanyikazi wa ziada kwenye eneo lililoathiriwa.

    Hii ni mara ya tano Uganda kupata mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, mara ya kwanza ulikuwa mbaya zaidi mwaka 2000 na kuua watu 224, na mlipuko wa mwisho nchini ilikuwa mwaka 2018. Milipuko mingine ilitokea 2014 na 2017.

    Soma zaidi:

  15. Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa inaishutumu Ethiopia kwa ukatili wa Tigray

    .

    Chanzo cha picha, AFP

    Maelezo ya picha, Ripoti hiyo inasema ukiukaji wa haki za binadamu umefanywa na pande zote

    Ripoti hiyo inasema ukiukaji wa haki za binadamu umefanywa na pande zote

    Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema wanaamini kuwa serikali ya Ethiopia ndiyo inayohusika na uhalifu dhidi ya binadamu unaoendelea katika eneo la Tigray kaskazini mwa nchi hiyo.

    Katika ripoti yake, Tume ya Wataalamu wa Haki za Kibinadamu nchini Ethiopia iliangazia kile ilichokiita taarifa za kuaminika za mauaji makubwa yaliyofanywa na jeshi la ulinzi la taifa la Ethiopia, ambayo yaliwalenga wanaume na wavulana wa Tigray walio katika umri wa kupigana.

    Hata hivyo, serikali haijajibu tuhuma hizo.

    Wachunguzi wanasema pia kuna ushahidi kwamba njaa inatumiwa kama silaha ya vita.

    Ripoti hiyo inasema ukiukaji wa haki za binadamu umefanywa na pande zote tangu mapigano yalipozuka karibu miaka miwili iliyopita.

    Inaelezea mzozo wa kibinadamu huko Tigray kama wa kushtua.

    Msemaji wa Tigray ameliambia shirika la habari la AFP kwamba "daima wameshikilia" kwamba serikali ya Ethiopia inawajibika kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu katika eneo hilo.

    Wadadisi wanaonya kuwa kuanza tena kwa mzozo huo hivi majuzi baada ya kusitishwa kwa miezi mitano kunaongeza hatari ya ukatili zaidi.

    Pia unaweza kusoma zaidi:

  16. Mataifa ya Kiafrika yatakiwa kuwa makini na sera ya 'kibeberu' ya Urusi

    .

    Chanzo cha picha, EPA

    Maelezo ya picha, Urusi itakuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele kati ya Urusi na Afrika mwezi ujao nchini Ethiopia

    Rais wa Poland Andrzej Duda ameonya mataifa ya Afrika kuwa makini na kile alichokiita 'sera ya kibeberu ya Urusi kwa bara hilo.

    Katika mahojiano na BBC, Bw Duda alisema kuongezeka kwa ushawishi wa Urusi barani Afrika katika masuala ya usalama na nishati ni "jaribio jipya la ukoloni".

    Alidai kuwa Urusi ilikuwa ikitumia kundi la Wagner - kampuni ya usalama ya kibinafsi - kama "chombo chake cha kijeshi" barani Afrika na matokeo ya"kikatili".

    Rais wa Poland hivi majuzi alizitembelea nchi tatu za Afrika - Nigeria, Senegal na Ivory Coast - katika jaribio la kuimarisha uhusiano na bara hilo na kutafuta njia mbadala za mafuta na gesi ya Urusi kutokana na mzozo wa nishati duniani.

    Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi Sergei Lavrov mwezi Julai alionyesha nguvu ya kidiplomasia ya nchi hiyo barani Afrika wakati wa ziara yake ya mataifa manne nchini Misri, Ethiopia, Uganda na Congo-Brazzaville.

    Mkutano wa pili wa kilele kati ya Urusi na Afrika unatarajiwa kufanyika nchini Ethiopia mwezi Oktoba, ambapo mikataba ya kibiashara na ulinzi inaweza kusainiwa ili kuimarisha uhusiano.

    Soma zaidi:

  17. Biden: Janga la corona limeisha Marekani

    gg

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Rais Joe Biden ametangaza janga hilo kuwa limekwisha nchini Marekani, hata kama idadi ya Wamarekani ambao wamekufa kutokana na Covid inaendelea kuongezeka.

    Bw Biden alisema ingawa "bado tuna tatizo", hali inaimarika kwa kasi.

    Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya Wamarekani 400 kwa wastani wanakufa kutokana na virusi kila siku.

    Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) alisema wiki iliyopita kwamba mwisho wa janga hilo "unaonekana".

    Katika mahojiano na kipindi cha CBS cha 60 Minutes kilichopeperushwa Jumapili, Bw Biden alisema kuwa Marekani bado inafanya "kazi nyingi" kudhibiti virusi.

    "Ukigundua, hakuna mtu aliyevaa barakoa," alisema. "Kila mtu anaonekana kuwa katika hali nzuri ... Nadhani inabadilika."

    Lakini maafisa wa utawala waliambia vyombo vya habari vya Marekani Jumatatu kwamba maoni hayo hayaashiria mabadiliko ya sera na hakukuwa na mipango ya kuondoa dharura inayoendelea ya afya ya umma ya Covid-19.

    Mnamo Agosti, maafisa wa Wamerekani waliongeza dharura ya afya ya umma, ambayo imekuwa tangu Januari 2020, hadi 13 Oktoba.

    Kufikia sasa, zaidi ya Wamarekani milioni moja wamekufa na ugonjwa wa Corona.

    Takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins zinaonyesha kuwa wastani wa siku saba wa vifo kwa sasa unasimama zaidi ya 400, na zaidi ya 3,000 wamekufa katika wiki iliyopita.

    Mnamo Januari 2021, kwa kulinganisha, zaidi ya watu 23,000 waliripotiwa kufa na virusi kwa muda wa wiki moja. Takriban 65% ya watu wote wa Marekani wanachukuliwa kuwa wamechanjwa kikamilifu.

    Wanachama wakuu wa Republican walikosoa matamshi ya rais, huku Katibu wa zamani wa Jimbo la Mike Pompeo akakituma kupitia ukurasa wake wa Twitter "Biden sasa anasema 'gonjwa limekwisha' kwanini anawafukuza makumi ya maelfu ya askari wenye afya njema kutoka jeshini kwa agizo lake la chanjo ya COVID."

    Maafisa wa afya ya umma wameelezea matumaini ya tahadhari katika wiki za hivi karibuni kwamba ulimwengu unaelekea kupona kwa janga, lakini wanaendelea kuwasihi watu kuwa waangalifu.

    Siku ya Jumatatu, Dk Anthony Fauci, mkuu wa Taasisi ya Kitaifa ya Ugonjwa wa Mzio na Magonjwa ya Kuambukiza, alikiri hali ilikuwa nzuri.

  18. Ukraine yaishutumu Urusi kwa kushambulia kinu cha nyuklia cha Ukraine Kusini

    w

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mamlaka ya Ukraine imesema kuwa jeshi la Urusi lilifyatua risasi kwenye kinu cha nyuklia cha Ukrain Kusini katika eneo la Nikolaev.

    "Usiku, roketi iliruka mita 300 kutoka kwa kinu cha nyuklia cha Ukraine Kusini. Kulikuwa na hitilafu ya muda mfupi ya umeme. Madirisha yaliharibiwa katika majengo kwenye eneo la kinu cha nyuklia. Wavamizi walitaka kupiga tena, lakini walisahau. mtambo wa nyuklia ni nini. Urusi inahatarisha dunia nzima. Tunahitaji kuizuia kabla haijachelewa," alisema Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

    Kituo rasmi cha Telegraph cha Zelensky pia kilichapisha picha zinazoonyesha matokeo ya shambulio hilo.

    Hapo awali, kampuni ya nishati ya Kiukreni ya Energoatom pia ilitangaza shambulio hilo.

    "Mlipuko mkubwa ulitokea mita 300 tu kutoka kwa vinu vya nguvu za nyuklia. Jengo la kituo cha nguvu za nyuklia liliharibiwa na wimbi la mshtuko, madirisha zaidi ya 100 yalivunjika. Moja ya vitengo vya umeme vya maji vya kituo cha kuzalisha umeme cha Aleksandrovskaya, ambacho ni sehemu ya eneo la ujenzi wa nishati ya Ukraine Kusini, ilizimwa. Njia tatu za umeme zenye nguvu ya juu pia zilizimwa," Energoatom alisema.

    Katika hali ya vita, BBC haiwezi kuthibitisha habari mara moja kutoka kwa wawakilishi wa pande zinazozozana.

    Hapo awali, Urusi na Ukraine zilishutumu kila mmoja kwa kushambulia kinu cha nyuklia cha Zaporozhye. Wiki iliyopita, IAEA ilipitisha azimio la kutaka Urusi iachilie ZNPP.

    Azimio hilo, ambalo lilijadiliwa kwa siri, liliitaka Urusi "kusitisha mara moja shughuli zote ndani na karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporozhye, pamoja na kituo kingine chochote cha nyuklia nchini Ukraine." Kazi ya kituo hicho, inasema, "inaongeza kwa kiasi kikubwa hatari ya ajali ya nyuklia." Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 26 "kwa" na mbili "dhidi" (hii ni Urusi yenyewe na China).