Watanzania wamepokeaje agizo la kupeleka 10% ya kodi ya upangaji TRA ?

Maelezo ya video, Tanzania: Agizo la wapangaji kupeleka 10% ya pango TRA imepokelewaje?
Watanzania wamepokeaje agizo la kupeleka 10% ya kodi ya upangaji TRA ?

Baadhi ya wananchi jijini Dar es salaam wameonesha hisia zao juu ya kodi ya zuio ya ambayo iko chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Euginia Mkumbo , Afisa Mkuu Usimamizi wa Kodi (Principal Tax Management Officer) Ambaye pia ni Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi kanda ya Kaskazini amefafanua..

Kwa mujibu wa TRA, kila mpangaji anapaswa kukata asilimia kumi ya kodi yake ya pango na kuwasilisha TRA.

Mwandishi wa BBC @frankmavura amefanya mazungumzo na baadhi ya wananchi hao jijini Dar es Salaam.