Mgombea wa chama cha ODM Fernandes
Odinga Barasa ameshinda kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha Ugavana katika
kaunti ya Kakamega nchini Kenya baada ya kumshinda mpinzani wake wa chama cha
Amani National Congress ANC Cleophas Malala.
Bwana Baraza alitangazwa mshindi baada
ya kujipatia kura 192,929 ikilinganishwa na Bwana Malala aliyepata kura
159,508.
Baada ya kutangazwa mshindi , bwana Barasa
aliambatana na mkewena wafuasi wake
katika kituo kikuu cha kujumlisha kura cha Kakamega ili kuchukua cheti chake
cha ushindi.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa cheti
hicho, Baraza alikishukuru chama cha ODM , mtangulizi wake Wycliffe Oparanya na
mgombea wa urais wa Muungano wa Azimio Raila Odinga kwa kumuunga mkono.
Wakati huohuo Abdulswamad Nassir wa chama cha Orange Democratic Movement ndiye gavana mteule wa Mombasa baada ya kupata kura 119,083 dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa UDA Hassan Omar aliyepata kura 98,108.
Mapema Jumanne asubuhi, matokeo yaliyojumlishwa kutoka takriban maeneo bunge yote ya Mombasa yalionyesha mgombeaji wa ODM akiwa anaongoza katika kinyang'anyiro cha ugavana. Matokeo kutoka eneo bunge la Likoni ndiyo yaliyokuwa yakisubiriwa.
Hatahivyo ushindi wa Barasa unajiri kama pigo
kwa kambi ya Muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na rais mteule William Ruto na
kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi ambao ulijaribu kila njia kukinyakua kiti
hicho kutoka kwa Muungano wa Azimio la Umoja.
Uchaguzi huo ulikumbwa na tatizo la
idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokezasiku ya Jumatatu na ushindi huo wa Barasa umeongeza nguvu kwa Muungano
wa Azimio na mgombea wake wa urais Raila Odinga katika mkoa wa Magharibi.
Kulikuwa na wagombea saba waliokuwa
wakigombea kiti cha ugavana. Walijumuisha aliyekuwa Mbunge wa Lugari Cyrus
Jirongo (UDP) aliyepata kura 5,974, Bw Suleiman Sumba (Kanu) kura 178, Samuel Omukoko
(MDP) kura 761, wakili Michael Osundwa (Independent) alipata kura 1,146 naye
Austin Opitso Otieno (Huru) alipata kura 761.
Uchaguzi wa kaunti za Kakamega na Mombasa uliahirishwa baada ya makaratasi ya kupigia kura kuchanganyika na yale ya kaunti nyengine.
Katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Pokot Kusini, David Pkosing aliyemaliza muda wake alimshinda Simon Kalekem wa United Democratic Alliance (UDA) baada ya kupata kura 28,225. Mgombea
wa UDA alipata kura 15, 295.
Kwengineko,
Titus Lotee amembwaga mbunge wa zamani Mark Lomunokol kunyakua kiti cha Eneobunge
la Kacheliba. Lomunokol was vying on a UDA party ticket.
Totee alipata kura 20,073 naye Lomunokol akapata kura 17, 963.
Kati uchaguzi wa ubunge wa Kitui vijijini, David Mwalika wa chama cha Wiper alimpiku mpinzani wake wa karibu Charles
Nyamai wa UDA baada ya kujizolea kura 19,745. Nyamai alipata kura 10,178.
Hata hivyo chama cha UDA kilishinda
kiti cha eneo bunge la Rongai kupitia mgombea wake Paul Chebor ambaye alimbwaga
Raymond Moi wa chama KANU.
Cheboi alipata jumla ya kura 27,021
huku mwana wa rais wa zamani wa Kenya hayati Daniel Moi akipata kura 14,725.
Chaguzi katika maeneo bunge hayo
manne uliahirishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Ukaguzi wa Mipaka (IEBC)
kufuatia mkanganyinyiko uliotokea wakati wa kuchapisha makaratasi ya kupigia kura
.
Kufuatia
matokeo ya uchaguzi huo wa hivi punde, Azimio sasa ina wanachama 165 huku Kenya
Kwanza ikipanda hadi 160 kutoka 159.