IEBC yaagizwa kumruhusu Raila Odinga kutazama sava za matokeo ya Uchaguzi
Mahakama ya Juu imeamuru tume ya uchaguzi IEBC kumpa mgombea urais wa Muungano wa Azimio Raila Odinga idhini ya kutazama sava za tume ya Uchaguzi katika Kituo cha Kitaifa cha Kujumlisha kura ambazo huenda zilitumika kuhifadhi na kusambaza taarifa za upigaji kura.
Moja kwa moja
Makamishna wanne wa IEBC wapata pigo
Maelezo ya picha, Makamishna wanne wa IEBC waliojitenga na uamuzi wa IEBC
Mahakama ya Juu imetupilia mbali majibu
yaliyowasilishwa kwa niaba ya shirika la uchaguzi na makamishna wanne
wakiongozwa na naibu mwenyekiti Juliana Cherera, na kutoa ushindi wa mapema kwa
mwenyekiti Wafula Chebukati.
Akizungumza Jumanne wakati wa kikao cha
pili cha malalamishi ya kesi ya uchaguzi wa urais ya 2022 katika
Mahakama ya Milimani, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu alisema mahakama imemuamuru
Mwanasheria Mkuu Prof Githu Muigai, ambaye anawakilisha kundi la Chebukati kuwa
wakili anayewakilisha Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) katika suala hilo.
Mrengo unaoongozwa na Juliana Cherera
ulikuwa umemwasilisha mbele ya mahakama
hiyo Wakili Paul Muite kama wakili wa IEBC.
Lakini mwendo wa alasiri, mahakama iliwapatia
pigo makamishna wanne -- Bi Cherera, Bi Irene Masit, Bw Justus Nyang'aya na Bw
Francis Wanderi -- huku ikifafanua kuwa wako huru kuhifadhi huduma za Bw Muite
na Issa Mansu kwa muda wa kesi hiyo.
Katika kikao cha asubuhi, mawakili wote
wawili walikuwa wamesisitiza kuwa wanawakilisha IEBC katika ombi la kupinga
uchaguzi wa urais lililowasilishwa na kiongozi wa Azimio Raila Odinga.
Mrengo unaoongozwa
na Cherera ulikuwa umewasilisha jibu kwa niaba ya IEBC iliyotaka kubatilishwa
kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyomtangaza William Ruto kuwa Rais mteule.
Katika usomaji wa
awali wa uamuzi wa mahakama, Jaji Mwilu alikuwa amewataka makamishna wanaogombana
wa shirika la IEBC kutatua mizozo yao ya ndani nje ya mahakama. Bi Mwilu
alikuwa amesema mahakama haitajiingiza katika suala la kuamua ni wakili gani
atawakilisha IEBC.
Na kufikia hapo ndio tunakamilisha matangazo yetu kwa hii leo.
Wanajeshi wa Ukraine:Tunaipiga Urusi kwa mashambulio ya usahihi wa hali ya juu
Utawala wa kijeshi wa Ukraine unasema
kuwa wanajeshi wake wanaoshambulia wanajeshi wa Urusi wanaoshikilia mji wa Kherson
wamefanikiwa "kuharibu maghala, mengi ya silaha na sehemu za udhibiti wa
adui kwa mashambulizi ya usahihi wa hali ya juu"
Wanajeshi hao pia wameweza kusababisha
uharibifu wa "madaraja kuvuka Dnipro", maafisa walisema katika ujumbe
uliotumwa kwa Telegram, na kuifanya "kuweza kukata mawasiliano ya jeshi la
Urusi kutoka kwa usambazaji wa silaha na wanajeshi wake kutoka Crimea".
Shirika la habari la serikali ya Urusi
Tass limeripoti kuwa Urusi inatumia mifumo ya ulinzi wa anga katika jaribio la
kukabiliana na mashambulizi ya Ukraine katika eneo hilo.
Maelezo ya picha, Gari la kurusha makomboramengi ya roketi kwa wakati mmoja
Majeshi ya umoja wa Sudan Kusini hatimaye yafuzu
Zaidi ya
wanajeshi 21,000 wamefuzu nchini Sudan Kusini, kama sehemu ya kikosi cha pamoja
kitakachosimamia usalama wa nchi hiyo.
Hii
inafuatia kuongezwa kwa makataa kadhaa baada ya makubaliano ya amani ya mwaka
2018, ambayo yanahitaji kwamba pande zote zinazopigana ziweke silaha zao chini
na kuunda jeshi la pamoja la serikali.
Wanajeshi
wengi katika hafla hiyo, hapo awali walikuwa wa vikundi tofauti vya mapigano.
Lakini leo,
waliahidi utii kwa nchi yao.
Vikosi vya umoja ni pamoja na jeshi, polisi na maafisa wa
huduma ya magereza.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Waziri wa Ulinzi Angelina Teny aliambia vyombo vya habari
vya ndani siku ya Jumatatu kwamba idara yake sasa itaanza kupeleka vikosi vya
usalama kwao na kwamba kundi lingine litahitimu katika kipindi cha takriban
miezi sita.
Viongozi wa kanda, ambao ni wadhamini wa mkataba huo wa
amani, walishuhudia sherehe za kuhitimu.
Mnamo mwaka wa 2013, vita vilizuka nchini Sudan Kusini
kati ya vikosi vinavyomuunga mkono Rais Salva Kiir na makamu wake wa wakati huo
Riek Machar.
Maelfu ya raia waliuawa, na wengine kuyahama makazi yao.
Mkataba wa amani uliotiwa saini mnamo mwaka 2018
ulimaliza mapigano mengi, na ilikubaliwa kuwa takriban wanajeshi 80,000
wafunzwe kwa ajili ya kikosi cha usalama kilichoungana.
Serikali ya pamoja ya mpito iliundwa mwaka 2020, ikiwa na
mipango ya kufanya uchaguzi mwezi Desemba, lakini uchaguzi huo umeahirishwa
hadi 2024.
Sudan Kusini
inakabiliwa na hali tete ya amani na makundi yenye silaha bado yanafanya kazi
katika baadhi ya maeneo.
Tanzania imezindua sensa ya majengo,
Chanzo cha picha, get
Tanzania
leo imezindua sensa ya majengo kwa siku nne ili kujua idadi ya majengo,
umiliki, gharama na upatikanaji wa miundombinu muhimu katika makazi yote nchini
humo.
Aidha
Kamishina wa Sensa,Anna Makinda amesema
kufikia jana Jumatatu, zaidi ya asilimia 93 ya kaya nchini humo tayari zilikuwa
zimehesabiwa.
Makinda
alisema zoezi la kuhesabu kaya linaendelea vyema na sasa wanaendelea na
usimamizi wa sensa ya majengo itakayosaidia kutambua umiliku wa makazi, ubora
wa nyumba lakini pia kurahisisha upatikanaji wa maji, umeme, barabara na
kadhalika.
Pia
kwa mujibu wa mamlaka nchini humo, takwimu hizo za sensa ya majengo na mali
zisizohamishika zitasaidia katika kuboresha sera ya makazi.
Katika
sensa ya watu ya mwaka 2012, ilibainika kuwa kati ya nyumba milioni 9.3
zilizokuwepo nchini Tanzania, nyumba milioni 6.3 ziliezekwa kwa mabati na
milioni tatu ziliezekwa kwa udongo.
IEBC yaagizwa kumruhusu Raila Odinga kutazama sava za matokeo ya Uchaguzi
Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Raila Odinga
Mahakama ya Juu imeamuru tume ya uchaguzi
IEBC kumpa mgombea urais wa Muungano wa Azimio
Raila Odinga idhini ya kutazama sava za tume ya Uchaguzi katika Kituo cha Kitaifa cha Kujumlisha kura
ambazo huenda zilitumika kuhifadhi na kusambaza taarifa za upigaji kura.
Mahakama pia iliagiza tume hiyo kumpa
masanduku ya kura ya vituo mbalimbali vya kupigia kura kwa lengo la ukaguzi, ili
kuchunguzwa na kuhesabiwa upya.
Vituo hivyo ni pamoja na Shule ya Msingi
ya Nandi Hills na Sinendeti huko Nandi, Belgut, Kapsuser na Shule ya Msingi ya
Chepkutum katika Kaunti ya Kericho; Vituo vya Kupigia Kura vya Jomvi, Mikindani
na Wizara ya Maji katika Kaunti ya Mombasa; Shule za Msingi ya Mvita, na Majengo
katika Kaunti ya Mombasa; Tinderet CONMO, katika Kaunti ya Nandi; Jarok,
Gathanji na Shule ya Msingi ya Kiheo katika Kaunti ya Nyandarua.
Matokeo ya hesabu hiyo yanahitajika kuwasilishwa mbele ya mahakama hiyo hapo siku ya Alhamisi saa nane.
Maagizo hayo yatamwezesha Bw Odinga na
walalamishi wengine wa uchaguzi wa Rais kuthibitisha madai kwamba kura
ziliibiwa.
Kulingana na agizo hilo, Tume Huru ya
Uchaguzi na Mipaka (IEBC) inahitajika kumpa Bw Odinga ufikiaji unaosimamiwa na
seva zozote ambazo zinaweza kuhifadhi habari za kitaalamu zinazotumiwa kunasa
nakala ya Fomu 34C ambayo ni jumla ya kura zilizopigwa.
Walalamishi wengine watakaopewa fursa ya
kutazama sava hizo ni pamoja na mgombea mwenza wa Bw Odinga Martha Karua, Youth
Advocacy for Africa (YAA), Peter Kirika, Khelef Khalifa, George Osewe, Ruth
Mumbi na Grace Kamau.
IEBC pia iliamriwa kuwapa nakala za sera
yake ya usalama ya mfumo wa teknolojia inayojumuisha sio tu sera ya neno la siri,
matrix ya neno la siri na wamiliki wa nywila za usimamizi wa mfumo.
Pia watapewa Habari zozote kuhusu
utumiaji wa mfumo huo wa teknolojiana viwango
vyake vya kuutumia , mazungumzo yaliofanyika ndani yake kwa utambulisho ,
ujumlishaji wa kura, upperushaji matokeo na uchapishaji matokeo hayo.
Tukisalia katika masuala ya Teknolojia ,
IEBC itatoa sera yake ya usalama kuhusu utumiaji wa mfumo huo na idadi ya watu
walioingia .
Matokeo ya Uchaguzi Kenya 2022: Kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi nchini Kenya yaanza kusikilizwa
Chanzo cha picha, Judiciary
Majaji saba wameanza
kusikiliza maombi ya kutaka kubatilishwa kwa uchaguzi wa William Ruto kuwa rais
mteule wa Kenya.
Wakiongozwa
na Jaji Mkuu Martha Koome, majaji hao walifutilia mbali maombi mawili na
kuunganisha mengine saba kwa sababu yaliibua masuala sawa na kutaka maagizo
sawa.
Mahakama pia
ilitupilia mbali maombi matatu likiwemo ombi la Bw Ruto, ambaye alitaka
kukizuia Chama cha Wanasheria nchini Kenya kushiriki katika kesi hiyo.
Mahakama
imeweka masuala tisa ambayo yatachagiza uamuzi wa mwisho utakaotolewa tarehe 5
Septemba.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje
Mwisho wa X ujumbe
Kiongozi
mkongwe wa upinzani Raila Odinga alikataa matokeo ya uchaguzi akisema tangazo
hilo lilikuwa kinyume cha sheria.
Alitaja
mgawanyiko kati ya makamishna saba wa uchaguzi na mwenyekiti wa tume hiyo
Wafula Chebukati kukosa kueleza jinsi alivyofika kwenye mchujo wa mwisho.
Bw Chebukati
alimtangaza Bw Ruto kuwa rais mteule wa Kenya akisema alipata kura 7.1m dhidi
ya Bw Odinga kura 6.9m.
Mahakama
hiyo ambayo ilifanya kikao cha awali Jumanne asubuhi, imeahirisha kikao hicho na
itaendelea tena alasiri ili kutafakari masuala kadhaa yaliyotolewa na mawakili.
Kesi hiyo
itaendelea kusikilizwa kikamilifu kuanzia Jumatano.
Habari za hivi punde, Bournemouth yampiga kalamu kocha wake baada ya kipigo cha 9-0 na Liverpool
Chanzo cha picha, PA Media
Maelezo ya picha, Mkufunzi Parker
Bournemouth imemfuta kazi kocha wake
Scott Parker baada ya kufungwa magoli 9-0 na Liverpool Jumamosi, mechi nne tu
baada ya msimu kuanza.
Baada ya kupoteza, Parker, 41, alisema
"hakushangazwa" na akasema timu "haikuwa katika kiwango cha
kuikabili liverpool".
"Ili tuendelee kusonga mbele kama
timu na klabu kwa ujumla, ni lazima tuwe sawa katika mkakati wetu wa kuendesha
klabu kwa uendelevu," alisema mmiliki wa klabu hiyo Maxim Demin.
"Lazima pia
tuonyeshe imani na kuheshimiana."
Demin aliongeza:
"Hiyo ndiyo njia ambayo imeiletea klabu hii mafanikio makubwa katika
historia ya hivi karibuni, na ambayo hatutakengeuka kuanzia sasa. Utafutaji
wetu wa kocha mkuu mpya utaanza mara moja."
Kipigo cha
Liverpool kilikuwa kipigo cha tatu mfululizo kwa Bournemouth kwenye ligi, baada
ya kushinda mechi yao ya ufunguzi.
Gary O'Neil
atachukua usukani wa timu kwa muda na atasaidiwa na Shaun Cooper na Tommy
Elphick.
Umoja wa Ulaya unatayarisha kituo cha mafunzo ya kijeshi nchini Ukraine
Chanzo cha picha, Reuters
Mawaziri
wakuu wa Umoja wa Ulaya, wanakutana katika Jamhuri ya Czech, huku mawaziri wa
ulinzi wakienda kujadili jinsi ya kuanzisha kituo kikuu cha mafunzo kwa jeshi
la Ukraine nchini humo.
Wataalamu
maalum wamekuwa wakitoa mafunzo kwa jeshi la Ukraine kwa muda, wengi wao
wakifanya kazi na silaha mpya.
Lakini mkuu
wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Josep Borrell, alisema anatumai ‘’mafunzo
ya hali ya juu’’ yatatolewa kwa vikosi vya Ukraine.
Aliongeza
kuwa mfumo wa kati wa mafunzo utaruhusu wataalam wa EU kutabiri vita, wakati
huo huo kutoa msaada mkubwa kwa Waukraine.
Kwa upande
mwingine, mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya pia wamepangwa kukutana
wiki hii, na matokeo ya mkutano wao kuwasilishwa kwa majadiliano kuhusiana na
vikwazo vya visa kwa raia wa Urusi.
Wanachama wa
Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuendelea na majadiliano katika mji mkuu wa Czech
wa Prague hadi Jumatano.
Wagombea wa Muungano wa Azimio washinda ugavana Mombasa na Kakamega
Chanzo cha picha, fernandes baraza /facebook
Maelezo ya picha, Fernandes Barasa
Mgombea wa chama cha ODM Fernandes
Odinga Barasa ameshinda kinyang’anyiro cha kuwania kiti cha Ugavana katika
kaunti ya Kakamega nchini Kenya baada ya kumshinda mpinzani wake wa chama cha
Amani National Congress ANC Cleophas Malala.
Bwana Baraza alitangazwa mshindi baada
ya kujipatia kura 192,929 ikilinganishwa na Bwana Malala aliyepata kura
159,508.
Baada ya kutangazwa mshindi , bwana Barasa
aliambatana na mkewena wafuasi wake
katika kituo kikuu cha kujumlisha kura cha Kakamega ili kuchukua cheti chake
cha ushindi.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa cheti
hicho, Baraza alikishukuru chama cha ODM , mtangulizi wake Wycliffe Oparanya na
mgombea wa urais wa Muungano wa Azimio Raila Odinga kwa kumuunga mkono.
Wakati huohuo Abdulswamad Nassir wa chama cha Orange Democratic Movement ndiye gavana mteule wa Mombasa baada ya kupata kura 119,083 dhidi ya mpinzani wake wa karibu wa UDA Hassan Omar aliyepata kura 98,108.
Mapema Jumanne asubuhi, matokeo yaliyojumlishwa kutoka takriban maeneo bunge yote ya Mombasa yalionyesha mgombeaji wa ODM akiwa anaongoza katika kinyang'anyiro cha ugavana. Matokeo kutoka eneo bunge la Likoni ndiyo yaliyokuwa yakisubiriwa.
Hatahivyo ushindi wa Barasa unajiri kama pigo
kwa kambi ya Muungano wa Kenya Kwanza unaoongozwa na rais mteule William Ruto na
kiongozi wa ANC Musalia Mudavadi ambao ulijaribu kila njia kukinyakua kiti
hicho kutoka kwa Muungano wa Azimio la Umoja.
Uchaguzi huo ulikumbwa na tatizo la
idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokezasiku ya Jumatatu na ushindi huo wa Barasa umeongeza nguvu kwa Muungano
wa Azimio na mgombea wake wa urais Raila Odinga katika mkoa wa Magharibi.
Kulikuwa na wagombea saba waliokuwa
wakigombea kiti cha ugavana. Walijumuisha aliyekuwa Mbunge wa Lugari Cyrus
Jirongo (UDP) aliyepata kura 5,974, Bw Suleiman Sumba (Kanu) kura 178, Samuel Omukoko
(MDP) kura 761, wakili Michael Osundwa (Independent) alipata kura 1,146 naye
Austin Opitso Otieno (Huru) alipata kura 761.
Uchaguzi wa kaunti za Kakamega na Mombasa uliahirishwa baada ya makaratasi ya kupigia kura kuchanganyika na yale ya kaunti nyengine.
Katika kinyang'anyiro cha ubunge wa Pokot Kusini, David Pkosing aliyemaliza muda wake alimshinda Simon Kalekem wa United Democratic Alliance (UDA) baada ya kupata kura 28,225. Mgombea
wa UDA alipata kura 15, 295.
Kwengineko,
Titus Lotee amembwaga mbunge wa zamani Mark Lomunokol kunyakua kiti cha Eneobunge
la Kacheliba. Lomunokol was vying on a UDA party ticket.
Totee alipata kura 20,073 naye Lomunokol akapata kura 17, 963.
Kati uchaguzi wa ubunge wa Kitui vijijini, David Mwalika wa chama cha Wiper alimpiku mpinzani wake wa karibu Charles
Nyamai wa UDA baada ya kujizolea kura 19,745. Nyamai alipata kura 10,178.
Hata hivyo chama cha UDA kilishinda
kiti cha eneo bunge la Rongai kupitia mgombea wake Paul Chebor ambaye alimbwaga
Raymond Moi wa chama KANU.
Cheboi alipata jumla ya kura 27,021
huku mwana wa rais wa zamani wa Kenya hayati Daniel Moi akipata kura 14,725.
Chaguzi katika maeneo bunge hayo
manne uliahirishwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Ukaguzi wa Mipaka (IEBC)
kufuatia mkanganyinyiko uliotokea wakati wa kuchapisha makaratasi ya kupigia kura
.
Kufuatia
matokeo ya uchaguzi huo wa hivi punde, Azimio sasa ina wanachama 165 huku Kenya
Kwanza ikipanda hadi 160 kutoka 159.
Chanzo cha picha, Abdulswamad Sharrif Nassir /facebook
Maelezo ya picha, Abdulswamad Sharrif Nassir
Nasa inasema hii ndio sauti inayosikika katika shimo jeusi kwenye anga za mbali
Maelezo ya video, Nasa inasema hii ndio sauti inayosikika katika shimo jeusi kwenye anga za mbali
Katika ombwe la anga za mbali, hakuna mengi unayoweza kusikia. Lakini angaza mbali unaweza kusikia kelele katika eneo linalozingira Shimo Jeusi.
Shirika la anga za mbali la Marekani Nasa limetoa sauti zinazotoka kwenye moja ya mahimo ambalo liko katikati ya uzio wa nyota wa Perseus galaxy.
Ilisema Nasa: ‘Uzio wa nyota una kiasi kikubwa cha gesi nyingi ambacho kimekuwa na sauti inayosikika.
Hii ni sauti yake iliyokuzwa na kuchanganywa na data nyingine, ili kuisikia sauti ya Shimo Jeusi!.'
Mashimo Meusi yanadhaniwa kuwa yametokana na kuporomoka kwa nyota nyingi sana.
Warusi lazima watoroke ikiwa wanataka kunusurika- Zelensky
Chanzo cha picha, Huduma ya Vyombo vya Habari vya Rais wa Ukraine/Reuters
Maelezo ya picha, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky
Ikiwa wanataka kunusurika, ihuu ndio wakati wa wanajeshi wa Urusi kutoroka, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alidai katika hotuba yake ya kila siku kwa taifa jana usiku wakati alipokuwa akijadili matukio ya hivi punde dhidi ya vikosi vya Urusi upande wa kusini maeneo ya Kherson.
Mpaka kati ya nchi hizo mbili haujabadilika, alisema, akiongeza kuwa “wavamizi wanajua hilo” na Ukraine itawafurusha nchini humo.
“Ukraine inarejelea hali yake ya kawaida,” Zelensky aliwaambia watu wa Ukraine. “Na itakomboa maeneo ya Kharkiv, Luhansk, Donetsk, Zaporizhzhia, Kherson, Crimea, na kwa ujumla maeneo yote yanayozunguka Bahari Nyeusi na Bahari ya Azov - kutoka Kisiwa cha Zmiinyi hadi Kerch Strait.
“Hili litafanyika. Haya ni maeneo yetu. Na kama jamii yetu inavyoelewa. Hauna eneo lao katika ardhi ya Ukraine.”
Alisema tangu kuanza kwa vita mwaka 2014 na Urusi kunyakuwa Crimea na kujaribu kuteka eneo la Donbas “lazima ikomee hapo”, baada ya maeneo hayo mawili kukombolewa.
Kikosi cha kwanza cha muungano chahitimu Sudan Kusini
Chanzo cha picha, Af
Maelezo ya picha, Sudan Kusini imekumbwa na vita vibaya vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi
Sudan Kusini iko tayari kwa mahafali ya kundi lake la kwanza la vikosi vya muungano nchini humo - jeshi la taifa na huduma za polisi.
Mahafali yaliyopangwa kufanyika Jumanne asubuhi katika mji mkuu, Juba, yanatarajiwa kushuhudiwa na viongozi watano kutoka eneo hilo - ambao ni wadhamini wa makubaliano ya amani. Sikukuu ya umma imetangazwa ili kuwawezesha wananchi kushuhudia sherehe hizo.
Serikali ya umoja wa Sudan Kusini iliundwa Februari 2020, lakini bado haijaunda jeshi la umoja wa kitaifa. Waziri wa Ulinzi na Masuala ya Wastaafu Angelina Teny aliwaambia waandishi wa habari Jumatatu kwamba angalau wanajeshi 10,000 watahitimu wakati wa sherehe rasmi.
Alisema kundi lijalo la vikosi vya umoja linatarajiwa kuhitimu katika kipindi cha miezi sita ijayo. Nguvu ya umoja ilikuwa nguzo muhimu ya mkataba wa amani ulioimarishwa uliotiwa saini Septemba 2018 ili kumaliza miaka mitano ya mzozo.
Hadi wanajeshi 83,000 awali walitakiwa kujiunga na jeshi la taifa, lakini makubaliano mapya yaliyofikiwa mwezi Aprili mwaka huu yalikubaliwa kuhusu wanajeshi 53,000.
Tangu uhuru, Sudan Kusini imekumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha maelfu ya watu kuuawa, huku makundi yanayopigana yakigawanyika kwa misingi ya kikabila.
Meli ya nafaka ya Ukraine yatia nanga nchini Djibouti
Chanzo cha picha, Getty Images
Meli
iliyobeba nafaka ya Ukraine imetia nanga katika taifa la Afrika Mashariki la
Djibouti.
Ni
shehena ya kwanza ya nafaka kutoka Ukraine hadi Afrika tangu uvamizi wa Urusi.
Usafirishaji
kwenye meli hiyo ‘Brave Commander’ umepangwa na UN ili kufikisha ngano hiyo katika nchi
zilizo hatarini kukumbwa na njaa.
Inapaswa
kuchukua takriban siku nne kushusha na kubeba mizigo kabla ya kusafirishwa kwa
barabara hadi nchi jirani ya Ethiopia, ambako zaidi ya watu milioni 20
wanahitaji msaada wa chakula.
Ethiopia
inakabiliwa na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40,
pamoja na mizozo kadhaa.
Usafirishaji
huo umepungua baharini ikilinganishwa na kile kinachohitajika katika nchi za
Afrika Mashariki - ambako ukame umeenea.
Mafuriko Pakistan: Thuluthi moja ya nchi imesombwa na maji – waziri
Chanzo cha picha, EPA-EFE/REX/Shutterstock
Thuluthi moja ya Pakistan imesombwa
kabisa na maji ya mafuriko, waziri wake wa hali ya hewa anasema.
Mafuriko hayo mabaya yamesomba barabara nyumbana mimea- na kuacha nyuma uharibifu mkubwa
katika maeneo tofauti nchini Pakistan.
"Kwote ni kama bahari kubwa, hakuna ardhi kavu ya kusukuma
maji nje," Sherry Rehman alisema, akiutaja kuwa "mgogoro mkubwa
usiomithilika."
Karibu wa 1,136 wameuawa tangu kuanza kwa msimu wa masika mwezi
Juni, kulingana na maafisa.
Mvua ya kiangazi ndiyo kubwa zaidi kurekodiwa katika muongo
mmoja na serikali inasema imechangiwa na mabadiliko ya tabia nchi.
"Kiuhalisia, theluthi moja ya Pakistan iko chini ya maji, hali
ambayo haujawahi kushuhudia hapo awali," Bi Rehman aliambia shirika la habari la AFP.
"Hatujawahi kuona kitu kama hiki," aliongeza waziri huyo.
Akizungumza na BBC, Waziri wa Mambo ya Nje wa Pakistan Bilawal Bhutto-Zardari alisema thuluthi moja ya waliouawa wanaaminika kuwa watoto. "Bado tunaendelea kutathmini ukubwa wa uharibifu," aliongeza.
Mahakama ya Juu Zaidi Kenya kufanya kikao cha kuweka mikakati ya kesi ya kupinga matokeo ya Urais
Chanzo cha picha, Getty Images
Mahakama ya juu zaidi nchini kenya imepangiwa kufanya kikao cha kutathmini masuala yatakayoibuka kwenye kesi tisa zilizowasilishwa katika kupinga kutangazwa kwa William Ruto kuwa Rais Mteule.
Kwenye tangazo lililotolewa na msajili wa mahakama hiyo, Bi Letizia Wachira, kikao hicho kimepangiwa kuanza leo katika Mahakama ya Milimani.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Idara ya Mahakama, kesi hizo zitaanza kusikilizwa kesho Jumatano na kumalizika Jumapili.
Majaji watapumzika kwa siku moja ili kutathmini masuala yatakayowasilishwa na pande zote. Baadaye, watarejea Jumatatu ili kutoa uamuzi wao.
Wakati wa kikao cha leo Jumanne, mahakama itaeleza kanuni ambazo zitazingatiwa na walalamishi na mawakili wao.
Chanzo cha picha, AFP
Maelezo ya picha, Jaji Mkuu wa Kenya Martha Koome
Huku hayo yakiarifiwa majaji watano kutoka
mataifa ya kigeni wamefika nchini kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya urais
itakayoanza leo saa tano katika Mahakama ya juu
Majaji hao wanachama wa Chama cha Majaji wa
Afrika (AJJF), walitua nchini siku ya Jumatatu wakiongozwa na Jaji Mkuu
(mstaafu) Mohammed Chande Othman wa Tanzania.
Majaji wengine katika ujumbe huo ni Lillian
Tibatemwa-Ekirikubinza wa Mahakama ya Upeo Uganda, Ivy Kamanga wa Mahakama ya
ya Upeo Malawi, Moses Chinhengo wa Mahakama ya Rufaa Lesotho na Henry Boissie
Mbha ambaye ni Rais wa Mahakama ya Masuala ya Uchaguzi Afrika Kusini.
Urusi kufanya mazoezi makubwa ya kijeshi na China pamoja na mataifa mengine
Chanzo cha picha, AFP
Urusi imesema
itaanzisha mazoezi makubwa ya kijeshi pamoja
na vikosi kutoka China ili kuonyesha uhusiano wa karibu wa ulinzi kati ya
Moscow na Beijing huku kukiwa na vita nchini Ukraine.
Mazoezi ya Vostok
2022 (Mashariki 2022) yatafanyika Septemba 1-7 katika maeneo mbalimbali katika
Mashariki ya Mbali ya Urusi na Bahari ya Japan na kuhusisha zaidi ya askari
50,000 na vitengo vya silaha 5,000, ikiwa ni pamoja na ndege 140 na meli za
kivita 60, kulingana na ulinzi wa Urusi
Wizara ya ulinzi Ilitoa video ya wanajeshi wa China wakiwasili nchini Urusi kwa ajili ya
maandalizi ya zoezi hilo kubwa.
Mazoezi hayo
yatafanyika katika vituo saba vya kurusha risasi mashariki mwa Urusi na
yatashirikisha wanajeshi kutoka mataifa kadhaa ya zamani ya Usovieti, China,
India, Laos, Mongolia, Nicaragua na Syria.
Wizara hiyo
ilisema vitengo vya wanajeshi wa anga vya Urusi,
walipuaji wa masafa marefu, na ndege za kijeshi za shehena zitashiriki katika
mazoezi hayo pamoja na vikosi vingine.
Wakati wa kwanza
kutangaza zoezi hilo mwezi uliopita, jeshi la Urusi lilisisitiza kuwa ni sehemu
ya mafunzo ya mapigano yaliyopangwa ambayo yanaendelea licha ya hatua ya
kijeshi ya Moscow nchini Ukraine. Haijafichua idadi ya wanajeshi waliohusika
katika kile Kremlin inachokiita "operesheni maalum ya kijeshi" huko.