Sudan Kusini: Mambo matano usiyoyajua kuhusu Sudan Kusini

Maelezo ya video, Sudan Kusini: Mambo matano usiyoyajua kuhusu Sudan Kusini

Ni miaka 10 tangu Sudan Kusini ilipokuwa taifa changa duniani, baada ya watu wake kupiga kura ya kujitenga na Sudan kufuatia miongo miwili ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, vilivyomalizika mwaka 2005.

Miaka miwili baada ya uhuru, vita vipya vya wenyewe kwa wenyewe vilizuka mwaka 2013, kabla ya pande zote mbili kutia saini makubaliano ya amani mwaka 2018.

Nchi hiyo kwa sasa inakabiliwa tisho la mzozo wa kibinadamu na kuna hofu huenda mzozo kamili ukaibuka kwa mara nyingine tena. Lakini kama wanavyosema baadhi ya raia wa Sudan Kusini, kuna mengi zaidi ya kujivunia nchini mwao zaidi ya vita.