Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Ukraine yadai kudhibiti mji wa Kharkiv baada ya shambulizi la Urusi
Mji wa Kharkiv warejea chini ya udhibiti wa Ukraine asema gavana
Moja kwa moja
Tazama:Wapiganaji wa Ukraine wapambana na wanajeshi wa Urusi huko Kharkiv
Wanajeshi wa Urusi sasa wako ndani ya mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Kharkiv, ambapo wanapambana na wanajeshi wa Ukraine mitaani.
Wanajeshi hao wa Ukraine wanaonekana wakirusha maguruneti ya kurushwa kwa roketi kwenye kona za barabara.
Papa Francis asema anavunjwa moyo na yanayojiri Ukraine
Papa Francis ametoa wito wa kukomeshwa kwa mzozo nchini Ukraine.
Akizungumza na hadhara katika uwanja wa St Peter's, alisema: "Silaha zinyamaze.
Mungu yuko pamoja na wale wanaotafuta amani, sio wale wanaofanya vurugu."
Pia ametoa wito kwa mashirikia ya kibinadamu kusaidia wakimbizi kutoka Ukraine.
Na amewashutumu wale ambao "wanaamini katika uouvu wa silaha".
Habari za hivi punde, Mji wa Kharkiv warejea chini ya udhibiti wa Ukraine asema gavana
Vikosi vya Ukraine vimedhibiti tena mji muhimu wa Kharkiv, gavana wa eneo hilo amesema.
Katika chapisho kwenye Telegraph, Oleh Synyehubov alisema: "Udhibiti wa Kharkiv ni wetu kabisa!
"Vikosi vya jeshi, polisi, na vikosi vya ulinzi vinafanya kazi, na jiji linasafishwa kabisa na adui."
Wanajeshi wa Urusi waliweza kuingia katika mji huo, wa pili kwa ukubwa wa Ukrainia, usiku mmoja.
Picha zilizosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha mapigano ya mitaani kati ya wanajeshi wa Ukraine na Urusi.
Hali bado ni tete na madai ya udhibiti ni vigumu kuthibitisha - lakini raia walioko chini pia wameiambia BBC kwamba Kharkiv imerejea chini ya udhibiti wa Ukraine na kwamba migogoro mitaani ni rahisi.
'Hali ya Ukraine ni ya kutisha' - Chelsea FC
Chelsea FC imeelezea hali nchini Ukraine kuwa ya kutisha na ya kuhuzunisha.
Katika taarifa fupi klabu hiyo ilisema: "Mawazo ya Chelsea yapo kwa kila mtu nchini Ukraine. Kila mtu kwenye klabu anaombea amani."
Mapema wiki hii mmiliki wa Chelsea Mrusi Roman Abramovich alitangaza "kuwapa wadhamini wa taasisi ya hisani ya Chelsea usimamizi na utunzaji" wa klabu hiyo.
Abramovich ni mmoja wa watu tajiri zaidi nchini Urusi na anaaminika kuwa karibu na Rais wa Urusi Vladimir Putin.
Wanasiasa wa Uingereza wametaka awekewe vikwazo - ingawa hapo awali alisafiri hadi Uingereza bila visa kwa pasipoti ya Israeli.
Habari za hivi punde, Ukraine inadai vifo 4,300 vya Warusi kufikia sasa
Naibu waziri wa ulinzi wa Ukraine ametoa makadirio ya hasara anayosema kuwa majeshi ya nchi hiyo yameisababishia Urusi hadi sasa.
Hanna Malyar wa Kyiv alisema katika chapisho la Facebook kwamba takwimu za siku tatu za kwanza za mzozo huo zilikuwa za awali na zinaweza kubadilika.
Ukraine inakadiria hasara za kijeshi za Urusi kufikia sasa kuwa pamoja na:
• vifo 4,300
• Ndege 27
• Helikopta 26
• Vifaru 146
• Magari 706 ya kivita
• Mizinga 49
• Mfumo 1 wa ulinzi wa anga wa Buk
• Mifumo 4 ya kurusha roketi nyingi za Grad
• Magari 30
• Meli 60 za mafuta
• Droni 2
• Boti 2
Zaidi ya raia 200 waliuawa - afisa wa Ukraine
Ofisi ya Haki ya serikali ya Ukraine ikiongozwa na afisa wake mkuu Lyudmyla Denysova inasema zaidi ya raia 210 wa Ukraine wameuawa na zaidi ya 1,100 kujeruhiwa katika uvamizi wa Urusi.
"Kwa ukatili usioonekana, adui anaharibu majengo ya makazi, hospitali, shule za chekechea na shule, akichukua haki ya kuishi kutoka kwa watoto wa kiume na wa kike wa ardhi ya Ukraine, wakiwemo watoto," alisema katika chapisho la mtandao wa kijamii.
Denysova alitoa mifano ya baadhi ya vifo vya raia, ikiwa ni pamoja na mtoto aliyeuawa katika mashambulizi ya makombora katika hospitali huko Kyiv, na mwanamke aliyeuawa baada ya kombora kupiga jengo la makazi huko Kharkiv.
Alitoa wito kwa Urusi "kuadhibiwa vikali kwa uhalifu huu".
"Ukraine inabainisha ukweli huu wote na itauwasilisha kwa mahakama ya kijeshi huko The Hague," alisema.
Idadi ya watu waliokimbia Ukraine sasa ni 368,000
Idadi ya watu wanaokimbia Ukraine sasa imefikia 368,000, kulingana na UNHCR.
Zaidi ya watu 150,000 wameingia Poland tangu kuanza kwa mzozo - huku zaidi ya Waukraine 43,000 wakikimbilia Romania katika siku tatu baada ya Urusi kuivamia.
Mashirika ya Umoja wa Mataifa kusimamisha shughuli nchini Ukraine
Mashirika ya Umoja wa Mataifa na washirika wa kibinadamu wanasitisha shughuli zao nchini Ukraine "kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama".
Umoja wa Mataifa na washirika wake watadumisha uwepo wao kote nchini na kuanza tena kazi "mara tu hali itakaporuhusu", Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu ilisema.
Vita vinaweza kuwa mwanzo wa mwisho kwa Putin-Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza
Shambulio la kijeshi la Urusi dhidi ya Ukraine "linaweza kuwa mwanzo wa mwisho" kwa Rais Vladimir Putin, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Lizz Truss amesema.
Akizungumza na kipindi cha Trevor Phillips kwenye Sky News, Truss alisema "tunaona upinzani mkali na ushujaa wa Ukraine" na Uingereza "itaendelea kuwapa silaha na msaada wa kiuchumi".
Alisema anaamini kuwa Putin "anafanya makosa ya kimkakati" kutokana na uharibifu ambao vikwazo vya magharibi vitafanya kwa uchumi wa Urusi.
Lakini alipendekeza kwamba vita vinaweza kuendelea kwa "miaka kadhaa", na kuongeza: "Hii haitatokea - ninaogopa - haraka."
"Ninahofia mzozo huu unaweza kuwa wa umwagaji damu sana," alisema.
Alipoulizwa kuhusu vikwazo vya Uingereza, Truss alisema "amekusanya orodha ya watu wengine" na kupendekeza kutakuwa na "mpango wa vikwazo zaidi ".
Vita nchini Ukraine vitasababisha "gharama ya kiuchumi" kwa Uingereza, alisema. Lakini, alisema, watu wa Uingereza wataelewa bei ambayo tutalipa ikiwa hatutasimama dhidi ya Putin sasa.
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza - tutamuunga mkono raia wa Uingereza wanaotaka kuelekea kupigana Ukraine
Hapo awali, tulimsikia Rais wa Ukrainia Zelensky akiwahimiza wapiganaji kutoka ng'ambo kujiunga na "jeshi la kigeni" lililoundwa hivi karibuni kuisaidia Ukraine katika vita .
Na asubuhi ya leo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Liz Truss, alisema ikiwa Waingereza watachagua kibinafsi kuelekea Ukraine kujiunga na vita, atawaunga mkono "kabisa ikiwa ndivyo wanataka kufanya".
Hapo awali Uingereza iliwashtaki watu waliosafiri kwenda Mashariki ya Kati kupigania au dhidi ya IS.
Putin asimamishwa kuwa mwanachama wa shirikisho la judo
Shirikisho la Kimataifa la Judo limemsimamisha Vladimir Putin kama rais wa heshima na balozi.
Rais wa Urusi ana mkanda mweusi wa judo.
Uamuzi huo ni mojawapo ya "vikwazo" vya michezo vilivyotangazwa katika siku za hivi karibuni.
Mashindano ya Formula 1 Grand Prix ya Urusi, yaliyotarajiwa kufanyika mjini Sochi mwezi Septemba, yameghairiwa.
Na mapema ilitangazwa kuwa fainali ya Ligi ya Mabingwa ya 2022 itachezwa Paris badala ya St Petersburg.
Hampiti hapa!Raia wa ukraine washirikiana kukirejesha nyuma kifaru cha Urusi
Hii hapa video inayoonyesha wakaazi wa Ukraine wakisimamisha kifaru cha Urusi kwa kukitembeza wakikirudisha nyuma .
Inaeleweka kuwa tukio lilirekodiwa huko Koryukivka, katika mkoa wa Chernihiv.
Uingereza: Mapigano makali huko Kharkiv, Urusi yakabiliwa na upinzani mkali kote nchini
Hii hapa ni taarifa ya hivi punde ya kijasusi ya ulinzi kutoka Wizara ya Ulinzi ya Uingereza - ikisema Urusi inasonga mbele kwa Ukraine "kutoka pande nyingi", huku ikikutana na "upinzani mkali" kutoka kwa jeshi la Ukraine.
Ukraine inawaambia raia: Tengenezeni mabomu, ondoeni alama za barabarani, fanyeni kazi usiku
Jeshi la Ukraine limetoa mwongozo kwa watu wa kawaida katika harakati za kiraia kupinga uvamizi wa Urusi ..
"Bila kujali kama una silaha au risasi au huna, tumia njia zote za kupigana," ilisema.
Watu wameulizwa:
• Kuondoa alama za barabarani
• Kukata miti ili kufanya harakati zisiwezekane
• Tumia kikamilifu vifaa vya kuwashia moto vilivyotengenezwa nyumbani
• Kuharibu vituo muhimu vya usafiri
• Kuwa na shughuli zaidi nyakati za usiku au jioni
Mengi zaidi:
Tazama : Bohari la mafuta Ukraine lashambuliwa na kuteketezwa karibu na Kyiv
Moto huo ulizua hofu ya moshi wenye sumu na wakaazi walionywa kufunga madirisha na kusalia majumbani.
Milipuko hata hivyo ilisikika karibu na mji huo na ghala la mafuta huko Vasylkiv kusini mwa mji mkuu lilishambuliwa na kuchomwa moto.
Unaweza pia kusoma :
Zelensky: Hatutazungumza na Urusi huko Belarus
Urusi inasema wajumbe wamewasili Belarus - kwa mazungumzo na Ukraine.
Lakini Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy amekataa ombi hilo, akisema mazungumzo ya Minsk yangewezekana ikiwa Urusi isingeishambulia Ukraine kutoka eneo la Belarus.
Hata hivyo, anaacha mlango wazi kwa mazungumzo katika maeneo mengine.
Alisema: "Kama hakungekuwa na hatua kali kutoka kwa eneo lenu, tungeweza kuzungumza Minsk... miji mingine inaweza kutumika kama mahali pa mazungumzo.
"Bila shaka tunataka amani, tunataka kukutana, tunataka vita viishe. Warsaw, Bratislava, Budapest, Istanbul, Baku - tumewapa Warusi.
"Jiji lingine lolote litatufaa, pia - katika nchi, ambayo makombora yake hayarushwi dhidi yetu. Hii ndiyo njia pekee ya mazungumzo yanaweza kuwa ya ukweli na yanaweza kumaliza vita."
Rais wa Ukraine awaalika wageni kupigana na 'wahalifu wa kivita wa Urusi'
Rais Zelensky alitoa mwito kwenye akaunti zake za mitandao ya kijamii akimkaribisha mtu yeyote kuja kupigana "bega kwa bega" na Waukreni.
Chapisho hilo linasema: "Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky anahutubia raia wote wa dunia, marafiki wa Ukraine, amani na demokrasia.
"Yeyote anayetaka kujiunga na ulinzi wa Ukraine, Ulaya na dunia anaweza kuja na kupigana bega kwa bega na Waukraine dhidi ya wahalifu wa vita wa Urusi."
Chapisho la kina zaidi linasema raia wa kigeni wanaruhusiwa kisheria kujiunga na ulinzi wa Ukraine, na kwamba mgawanyiko tofauti wa wapiganaji unaundwa unaoitwa "Jeshi la Kimataifa la Ulinzi wa Eneo la Ukraine".
Kiongozi wa Ukraine hapo awali alisisitiza jinsi nchi hiyo imeachwa kujilinda yenyewe.
Washirika wa Magharibi wametuma silaha na risasi - lakini hawaweki buti ardhini. Ukraine sio sehemu ya muungano wa ulinzi wa Nato.
Unaweza pia kusoma :
Mapigano huko Kharkiv - ripoti
Sasa kuna ripoti za mapigano katika mitaa ya Kharkiv. Wanajeshi wa Urusi waliingia katika jiji hilo katika saa moja iliyopita, maafisa wa eneo hilo wanasema.
Picha za mitandao ya kijamii zinaonekana kuonyesha baadhi ya vitengo vya jeshi la Urusi katika jiji hilo. Pia kuna picha zinazoonyesha angalau magari mawili ya Kirusi "Tiger" yakiwaka moto katika jiji hilo.
BBC bado haijathibitisha picha hizi.
Maafisa wa Kharkiv asubuhi ya leo wamewaonya wenyeji kukaa katika makazi na kutoka mitaani.
Matukio ya hivi punde Kwa Muhatasari
• Licha ya onyo jana usiku kwamba Kyiv ingeshambuliwa na makombora ya Urusi, mlipuko wa angani hauonekani kutokea.
• Milipuko hata hivyo ilisikika karibu na jiji na ghala la mafuta huko Vasylkiv kusini mwa mji mkuu lilipigwa na kuchomwa moto, kulingana na meya wa eneo hilo. Moto huo ulizusha hofu ya moshi wenye sumu na wakaazi walionywa kufunga madirisha na kusalia majumbani
•Mji wa kusini wa Nova Kakhovka umechukuliwa na wanajeshi wa Urusi, meya wa jiji hilo alisema asubuhi ya leo.
• Wakati huo huo, magari ya Urusi yameingia katika jiji la pili kwa ukubwa nchini Ukraine, Kharkiv, wanasema maafisa wa Ukraine. Mlipuko mkubwa pia ulisikika mapema katika mji huo, ambapo bomba la gesi linasemekana kugongwa
• Maeneo ya makazi huko Kharkiv pia yalishambuliwa, kulingana na huduma za dharura. Mwanamke mmoja aliripotiwa kuuawa na makumi kadhaa kuhamishwa kutoka kwa jengo la orofa tisa
• Takriban vifo sita vya raia pia viliripotiwa katika mji wa Okhtyrka, kaskazini-mashariki mwa Ukraine, kulingana na meya wa eneo hilo.
• Katika saa iliyopita Idhaa ya BBC ya Kiukreni iliripoti akaunti mpya za milipuko huko Kharkiv na Kherson kusini-mashariki.
• Katika hatua ya kuiadhibu Urusi, Umoja wa Ulaya, Marekani na washirika wao watakata benki kadhaa za Urusi kutoka kwa mfumo mkuu wa malipo wa kimataifa, Swift. Pia watafungia mali ya benki kuu ya Urusi
• Australia imekuwa nchi ya hivi punde zaidi kutangaza kuwa itafadhili usambazaji wa silaha hatari kwa Ukraine ili kuisaidia kupambana na Urusi. Hatua hiyo imekuja baada ya Ujerumani kuamua Jumamosi kusambaza silaha kwa Ukraine, ikiwakilisha mabadiliko makubwa ya sera
Mengi zaidi kuhusu mzozo wa Ukraine:
Hujambo. Ni siku ya nne ya uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine,mengi yanazidi kufanyika nje na ndani ya taifa hilo Karibu kwa taarifa za moja kwa moja kuhusu kinachoendelea hadi sasa katika uvamizi huo .