Maafisa wa Marekani watoa picha ya mshukiwa Rahmanullah Lakanwal
Rais Donald Trump, ambaye alikuwa Florida wakati huo, alisema mtu aliyefanya shambulizi kwa kutumia bunduki alikuwa raia wa Afghanistan ambaye aliingia Marekani mnamo Septemba 2021.
Maafisa wa Marekani watoa picha ya mshukiwa Rahmanullah Lakanwal
Chanzo cha picha, Reuters
Maafisa wa Marekani walionyesha picha ya mshukiwa. Jina lake ni Rahmanullah Lakanwal, Mwafghanistan aliyeishi katika jimbo la Washington, na ambaye hapo awali alifanya kazi na Marekani nchini Afghanistan.
Mkurugenzi wa CIA John Ratcliffe, aliiambia CBS, mshirika wa BBC nchini Marekani, kwamba mshukiwa wa ufyatuaji risasi aliruhusiwa kuingia Marekani "kutokana na kazi yake ya awali na serikali ya Marekani".
"Kufuatia kujiondoa kwa Biden kutoka Afghanistan, utawala wa Biden ulihalalisha kumleta mshukiwa huyo nchini Marekani mnamo Septemba 2021 kutokana na kazi yake ya awali na serikali ya Marekani, ikiwa ni pamoja na CIA, kama afisa wa kikosi mshirika huko Kandahar, ambacho kilimalizika muda mfupi baada ya kuondolewa," Ratcliffe anasema.
Venezuela yapiga marufuku mashirika sita makubwa ya ndege baada ya mvutano na Marekani kuongezeka
Chanzo cha picha, RONALD PENA R/EPA/Shutterstock
Venezuela imepiga marufuku mashirika sita makubwa ya ndege ya kimataifa kutua nchini humo baada ya kushindwa kufikia tarehe ya mwisho ya saa 48 ya kuanza tena safari za ndege huko.
Mashirika hayo ya ndege yalikuwa yamesitisha kwa muda njia zao kuingia katika mji mkuu, Caracas, baada ya Marekani kuonya kuhusu "shughuli za kijeshi zilizoongezeka" katika eneo hilo.
Ikiwa imekasirishwa na hili, serikali ya Venezuela ilitoa amri ya mwisho ambayo iliisha Jumatano.
Huku mashirika kadhaa madogo ya ndege yakiendelea kuruka hadi Venezuela, maelfu ya abiria wameathiriwa. Marekani imetuma kikosi kikubwa kuisaidia Venezuela, ambayo inasema ni kupambana na biashara ya dawa za kulevya lakini ambayo kiongozi wa Venezuela ameishutumu kama jaribio la kumpindua.
Watu wasiopungua 55 wamefariki na mamia hawajulikani walipo baada ya moto kuteketeza majengo Hong Kong
Chanzo cha picha, Reuters
Watu wasiopungua 55 wamepoteza maisha katika moto mkubwa ulioteketeza majengo mengi marefu huko Hong Kong, moto mbaya zaidi jijini kuwahi kutokea katika zaidi ya miaka 70.
Baadhi ya wakazi bado wamekwama ndani ya majengo hayo, huku zaidi ya watu 270 wakiwa hawajulikani waliko.
Mamia ya maafisa zima moto wamekuwa wakikabiliana na moto huo, ambao sasa unadhibitiwa kwa kiasi kikubwa katika majengo yote yaliyoathiriwa .
Jengo la makazi lilikuwa likifanyiwa ukarabati mkubwa wakati moto ulipoanza. Chanzo halisi hakijulikani lakini polisi wanasema vifaa vilivyo nje ya majengo hayo vinaweza kuwa viliwezesha kuenea kwake.
Watendaji watatu wa kampuni ya ujenzi wamekamatwa kwa tuhuma za mauaji bila kukusudia na uzembe mkubwa.
Moto huo ulianza saa 14:51 saa za huko (06:51 GMT) siku ya Jumatano, huku miali ya moto na mawingu mazito ya moshi wa kijivu yakionekana kutoka kwenye minara, yakitawala anga ya jiji.
Watu hamsini na mmoja walifariki katika eneo la tukio, huku wengine wanne wakifariki hospitalini. Afisa wa zimamoto Ho Wai-ho, mwenye umri wa miaka 37, alikuwa miongoni mwa waliopoteza maisha katika moto huo.
Alipatikana ameanguka katika eneo la tukio kama dakika 30 baada ya kupotea kwa mawasiliano naye.
"Nimehuzunika sana," Jason Kong mwenye umri wa miaka 65 aliliambia shirika la habari la Reuters. "Sijui kinachoendelea tena. Tazama, vyumba vyote vinaungua tu. Sijui la kufanya."
Alisema jirani alikuwa amempigia simu na kusema bado alikuwa amenaswa ndani ya moja ya majengo ya mnara. Joto kali la moto huo, pamoja na uchafu hatari unayotokana na kuanguka kwa mnara, imezuia juhudi za uokoaji, lakini idara ya zimamoto ilisema haikuwa ikizuia kupata watu zaidi waliojeruhiwa ndani.
"Joto ndani ya majengo husika ni kali sana, kwa hivyo ni vigumu sana kwetu kuingia... na kupanda ghorofani kufanya operesheni ya kuzima moto na uokoaji," alisema Derek Armstrong Chan, naibu mkurugenzi wa huduma za zimamoto.
Marekani yasitisha maombi ya uhamiaji kwa Waafghanistan baada ya wanajeshi wake kupigwa risasi
Marekani imesitisha kushughulikia maombi yote ya uhamiaji kutoka kwa Waafghanistan, baada ya mwanaume mmoja wa Afghanistan kutambuliwa kuwa mshukiwa wa tukio la kuwapiga risasi wanajeshi wawili wa Walinzi wa Taifa karibu na Ikulu ya White House.
Huduma ya Uraia na Uhamiaji ya Marekani ilisema uamuzi huo ulifanywa ikisubiri mapitio ya "itifaki za usalama na uchunguzi".
Mshukiwa wa ufyatuaji risasi siku ya Jumatano, ambao uliwaacha maafisa wawili wakiwa wamejeruhiwa vibaya, inasemekana aliwasili Marekani kutoka Afghanistan mnamo Septemba 2021.
Rais wa Marekani Donald Trump alisema shambulio hilo lilikuwa "kitendo cha ugaidi", akiongeza kuwa atachukua hatua za kuwaondoa wageni "kutoka nchi yoyote ambayo haistahili kuwa hapa".
Makumi ya maelfu ya Waafghanistan waliingia Marekani chini ya ulinzi maalum wa uhamiaji kufuatia kujiondoa kwa Marekani nchini Afghanistan mwaka 2021 chini ya Rais wa zamani Joe Biden.
Polisi wachunguza wizi wa mbwa wanne kutoka ikulu ya rais Malawi
Chanzo cha picha, Getty Images
Polisi nchini Malawi wanachunguza jinsi mbwa wanne wa polisi walivyopotea kutoka ikulu ya rais katika mji mkuu, Lilongwe, wakati wa mpito wa kisiasa mwezi Septemba.
Godfrey Arthur Jalale, ambaye alihudumu kama naibu mkuu wa wafanyakazi wa Ikulu chini ya Rais wa zamani Lazarus Chakwera, amekamatwa kuhusiana na wizi wa mbwa wanne wa German Shepherds.
Anakana shtaka hilo. Chakwera alihama ikulu baada ya kushindwa katika uchaguzi na Rais Peter Mutharika, ambaye alirejea kwa njia ya kushangaza.
Jumatano jioni, polisi walikana ripoti kwamba Chakwera alikuwa amekamatwa lakini walithibitisha kupata kibali cha upekuzi wa makazi yake baada ya taarifa kueleza mbwa walioibwa walikuwa wakiwekwa hapo.
Vyombo vya habari vya ndani vimeripoti wizi wa mali ya serikali kutoka kwenye makazi mawili ya rais, Jumba la Kamuzu, na Jumba la Sanjika, huko Blantyre, jiji la pili kwa ukubwa nchini.
Mbwa hao wanne, wenye thamani ya $2,300 (£1,700), walitolewa nje ya jumba hilo kati ya Septemba 19 na Oktoba 4, kulingana na waendesha mashtaka wa serikali.
Katika taarifa siku ya Jumatano, polisi walisema "wameongeza uchunguzi kufuatia ripoti za uporaji wa mali" kutoka Jumba la Kamuzu.
"Huduma ya Polisi ya Malawi inawahakikishia umma kwamba uchunguzi unaendelea vizuri," iliongeza. Wabunge wa MCP walisusia vikao vya bunge Jumatano na kupiga kambi katika makazi ya Chakwera huko Lilongwe.
Aliyekuwa rais wa Peru ahukumiwa kifungo cha miaka 14 jela
Chanzo cha picha, Reuters
Mahakama ya
Peru Jumatano imemhukumu Rais wa zamani Martin Vizcarra kifungo cha miaka 14
jela baada ya kumpata na hatia ya kuchukua hongo miaka kadhaa kabla ya kuchukua
madaraka, na kuongeza orodha ya viongozi wa zamani waliofungwa jela kwa
ufisadi.
Kulingana na
uamuzi huo, Vizcarra alipokea hongo sawa na $676,000 kutoka kwa makampuni ya
ujenzi badala ya kandarasi za kazi za umma alipokuwa gavana wa eneo la kusini
la Moquegua kuanzia 2011 hadi 2014.
Wakati wote
wa kesi hiyo iliyoanza Oktoba iliyopita, Vizcarra alikanusha mashtaka hayo,
akidai alikuwa mwathirika wa mateso ya kisiasa. Aliingia madarakani mwaka wa
2018 baada ya mtangulizi wake kujiuzulu na akafukuzwa miaka miwili baadaye na Bunge
huku kukiwa na uchunguzi wa ufisadi.
"Hii
sio haki, ni kulipiza kisasi," Vizcarra alisema katika chapisho kwenye X
baada ya hukumu yake. "Lakini hawatanimaliza."
Timu yake ya
wanasheria ilithibitisha kuwa imekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, ambayo pia
ilimpiga marufuku Vizcarra kushikilia ofisi ya umma kwa miaka tisa.
Kaka yake
mkubwa, Mario Vizcarra, anapanga kugombea katika uchaguzi wa rais wa Aprili
2026 kwa chama cha "Peru Kwanza", ambapo rais huyo wa zamani amewahi
kuwa mshauri mkuu.
Timu yake ya
wanasheria ilithibitisha kuwa imekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo, ambayo pia
ilimpiga marufuku Vizcarra kushikilia ofisi ya umma kwa miaka tisa.
Kaka yake
mkubwa, Mario Vizcarra, anapanga kugombea katika uchaguzi wa rais wa Aprili
2026 kwa chama cha "Peru First", ambapo rais huyo wa zamani amewahi
kuwa mshauri mkuu.
Kundi la Marekani laishtaki Apple juu ya mzozo wa madini ya Congo
Chanzo cha picha, Reuters
Kundi la
mawakili lenye makao yake makuu nchini Marekani limefungua kesi mjini
Washington likiishutumu kampuni ya Apple kwa kutumia madini yanayohusishwa
na migogoro na ukiukaji wa haki za binadamu katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo
na Rwanda licha ya kampuni ya kutengeneza iPhone kukanusha madai hayo.
Mawakili wa
Kimataifa wa haki za binadamu (IRAdvocates) awali, waliwahi kufungua kesi dhidi
ya makampuni ya teknolojia ikiwa ni pamoja na Tesla, Apple na makampuni mengine
kuhusu upatikanaji wa madini ya cobalti, lakini mahakama za Marekani zilitupilia
mbali kesi hiyo mwaka jana.
Waendesha
mashtaka wa Ufaransa pia walitupilia mbali kesi ya Congo dhidi ya
kampuni tanzu za Apple mnamo mwezi Desemba kuhusu madini yanayokumbwa na mzozo,
kwa sababu ya ukosefu wa ushahidi.
Malalamiko ya
jinai yanayohusiana na hayo nchini Ubelgiji bado yanachunguzwa.
Apple ilikanusha kufanya
makosa yoyote katika kujibu mashtaka ya Congo, ikisema iliwaagiza wanaowauzia kusitisha
utafutaji wa nyenzo kutoka Congo na nchi jirani ya Rwanda.
Apple
ilisema Jumatano "inapinga vikali" madai ya hivi punde kwamba kampuni
hiyo inanufaika kutokana na kazi ya kulazimishwa na uchimbaji madini usio
salama barani Afrika, na kuyataja madai hayo kuwa "hayana msingi."
Wakenya 125 matajiri zaidi wanamiliki mali nyingi zaidi ya watu milioni 42.6 - Oxfam
Chanzo cha picha, Getty Images
Takriban
nusu ya wakazi wa Kenya wanaishi katika umaskini uliokithiri -
kwa chini ya Ksh.130 kwa siku - ripoti mpya ya Oxfam Kenya inafichua.
Ripoti hiyo
pia inaonyesha kuwa watu 125 matajiri zaidi nchini Kenya wanamiliki mali nyingi
zaidi ya watu milioni 42.6, huku kukiwa na ongezeko la viwango vya umaskini.
Ripoti
iliyopewa jina la ‘Mgogoro wa Kukosekana kwa Usawa wa Kenya: Mgawanyiko Mkubwa
wa Kiuchumi’ ilitolewa Jumatano, Novemba 11, 2025,
kuonyesha kwamba idadi ya watu wanaoishi katika umaskini uliokithiri
imeongezeka kwa milioni 7 (37%) tangu 2015.
Matokeo hayo
pia yanaonyesha kuwa ukosefu wa ufadhili wa kutosha wa elimu, afya na kilimo
kwa ajili ya kutoa kipaumbele kwa ulipaji wa madeni umechangia kuongeza pengo
kati ya matajiri wakubwa na wale wanaoishi katika umaskini uliokithiri.
Mnamo mwaka 2024,
kati ya kila Ksh.100 zilizochukuliwa kama kodi, Ksh.68 zilitumika kulipa deni
- mara mbili ya bajeti ya elimu na karibu mara 15 ya bajeti ya afya
ya kitaifa.
Waangalizi wa uchaguzi wa AU na ECOWAS wasikitishwa na tangazo la mapinduzi Guinea-Bissau
Chanzo cha picha, Getty Images
Viongozi wa
Umoja wa Afrika na wa ECOWAS wa ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi nchini
Guinea-Bissau wameelezea "wasiwasi mkubwa juu ya tangazo la mapinduzi ya
serikali na vikosi vya jeshi".
Katika
taarifa ya pamoja ambayo pia ilijumuisha mkuu wa Mkutano wa Wazee wa Afrika
Magharibi, maafisa hao walisema nchi ilikuwa tayari kwa tangazo la matokeo ya
uchaguzi baada ya kile kilichoelezwa kama mchakato wa "taratibu na
amani".
"Ni
jambo la kusikitisha kwamba tangazo hili lilikuja wakati ambapo ujumbe ulikuwa
umemaliza mkutano na wagombea wawili wa urais, ambao walituhakikishia utayari
wao wa kukubali mapenzi ya raia", walisema.
Waangalizi
wa kikanda pia walikosoa kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa ngazi ya juu nchini
humo ikiwa ni pamoja na maafisa wa uchaguzi, wakidai waachiliwe huru mara moja.
Walielezea
mapinduzi ya kijeshi ya Jumatano kama "jaribio la wazi" la kuvuruga
maendeleo ya demokrasia ya nchi.
Wakati wakishtumu
hatua hiyo, viongozi hao pia walihimiza Umoja wa Afrika na ECOWAS kuhakikisha
kwamba utaratibu wa kikatiba unarejeshwa katika taifa hilo la Afrika Magharibi
lenye watu zaidi ya milioni mbili.
Wakati huo
huo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ambaye anafuatilia kwa
karibu hali hiyo, amewahimiza wale wanaohusika katika hali ya nchini
Guinea-Bissau "kuonyesha kujizuia" na "kuheshimu utawala wa
sheria".
Canada pia
ilitoa ushauri wa kusafiri kwa wananchi wake muda mfupi baada ya utawala wa
kijeshi wa Guinea-Bissau.
Rais wa Nigeria atangaza hali ya dharura ya usalama
Chanzo cha picha, Presidency
Rais wa
Nigeria Bola Ahmed Tinubu ametangaza hali ya dharura ya usalama wa kitaifa
katikati ya ongezeko kubwa la mashambulizi ya mauaji na utekaji nyara wa watu
wengi katika majimbo kadhaa nchini humo.
Katika agizo
lenye maneno makali lililotolewa Jumatano, aliamuru kuongezwa haraka kwa vikosi
vya usalama wa nchi na hatua kali kuchukuliwa kukabiliana na kile alichokiita
"mawakala wa uovu" wanaodhoofisha taifa.
Kwa mujibu
wa amri mpya, Jeshi la Polisi la Nigeria lazima liongeze maafisa wengine 20,000
- na kuongeza jumla ya idadi iliyopangwa hadi 50,000.
Rais pia
aliidhinisha matumizi ya kambi za National Youth Service Corps (NYSC) kama
vituo vya mafunzo vya muda ili kuharakisha kupelekwa kwao kuanza majukumu.
Pia alitoa
maagizo kwamba maafisa wa polisi walioondolewa katika kazi za ulinzi wa watu mashuhuri
wapate mafunzo ya dharura kabla ya kupelekwa katika maeneo hatari.
"Idara ya Huduma za Jimbo pia ina mamlaka yangu kupeleka
mara moja walinzi wote wa misitu ambao tayari wamepata mafunzo kukabiliana na
magaidi na majambazi wanaokaa kwenye misitu yetu na kuajiri wengine zaidi kulinda
misitu.
Hakutakuwa na mahali pa kujificha zaidi kwa mawakala wa
uovu," Rais Tinubu alisema.
Rais alisisitiza kwamba shughuli za kuwaokoa wanafunzi
waliotekwa nyara kutoka shule ya Katoliki ya St. Mary katika Jimbo la Niger -
na Wanigeria wengine ambao bado wanashikiliwa na vikundi vyenye silaha - zitaendelea
"bila kukoma".
Pia
alihimiza bunge kuanza kupitia sheria za Nigeria kuruhusu majimbo ambayo
yanataka jeshi la polisi "kikanda" kufanya hivyo kisheria - mahitaji
ya muda mrefu wakati ukosefu wa usalama unaoendelea kuzorota.
Bwana Tinubu
alionya serikali dhidi ya kuanzisha shule za bweni katika wilaya zilizotengwa
bila ulinzi wa kutosha, na kutoa wito kwa makanisa na misikiti katika jamii
zilizo hatarini kudumisha uratibu wa usalama wa karibu.
Idadi ya vifo katika mkasa wa moto Hong Kong inaongezeka mamlaka zinasema
Chanzo cha picha, Getty Images
Zaidi ya
watu arobaini wamethibitishwa kufariki katika moto mkubwa ulioteketeza majengo
kadhaa ya ghorofa huko Hong Kong.
Watu wengine
45 wako hospitalini katika hali mbaya huku wengine 279 wakiwa bado hawajulikani
walipo.
Watu watatu wamekamatwa kwa
tuhuma za mauaji - wawili ni wakurugenzi wa kampuni ya ujenzi na mmoja ni
mshauri wa uhandisi.
Wakati
chanzo cha moto huo kikiendelea kuchunguzwa, polisi wanasema wavu na makaratasi
ya plastiki yalipatikana kwenye madirisha ya majengo hayo yaliyokuwa
yakifanyiwa ukarabati. Polisi wanasema huenda vifaa hivi zilisababisha moto huo
kuenea kwa haraka zaidi.
Asubuhi ya
leo, moshi bado unafuka kutoka kwa baadhi ya majengo ya ghorofa -
lakini moto huo umedhibitiwa katika majengo manne kati ya nane.
Idara ya
zima moto inatarajia kuchukua siku nzima kudhibiti moto huo.
Mamia ya
wakaazi wamehamishwa hadi kwenye makazi ya muda na nyumba za dharura
zinatengewa watu wanaohitaji kuhamishwa.
Idara ya
zimamoto ya Hong Kong imeainisha moto huo kama wa kiwango cha tano – ikimaanisha
ni mkubwa zaidi.
Imepita
miaka 17 tangu moto wa kiwango cha tano ulipoikumba Hong Kong mara ya mwisho.
Wanajeshi wa Marekani wapigwa risasi karibu na Ikulu ya White House
Chanzo cha picha, Reuters
Wanajeshi
wawili wa Ulinzi wa Kitaifa wamejeruhiwa vibaya baada ya kupigwa risasi huko
Washington DC karibu na Ikulu ya White House, katika kile meya wa jiji hilo amekiita
"shambulio la kulengwa".
Polisi
walisema mshukiwa mmoja aliwafyatulia risasi walinzi wawili siku ya Jumatano
alasiri, kabla ya kuzingirwa na kukamatwa na Walinzi wengine wa Kitaifa
waliokuwa karibu ambao walikuwa wamesikia milio ya risasi.
Rais Donald
Trump, ambaye alikuwa Florida wakati huo, alisema mtu aliyefanya shambulizi kwa
kutumia bunduki alikuwa raia wa Afghanistan ambaye aliingia Marekani mnamo
Septemba 2021.
Aliapa
kwamba utawala wake utahakikisha mshukiwa "analipa gharama kubwa
zaidi" kwa "kitendo cha ugaidi".
Vyanzo vingi
vya utekelezaji wa sheria hapo awali vilimtaja mtu anayedaiwa kuwa na bunduki
kwa mshirika wa BBC wa Marekani CBS kuwa ni Rahmanullah Lakanwal, raia wa
Afghanistan mwenye umri wa miaka 29.
"Lazima
sasa tuchunguze upya kila raia wa kigeni ambaye ameingia nchini mwetu kutoka
Afghanistan chini ya [Rais wa zamani Joe] Biden," Trump alisema katika
hotuba ya moja kwa moja Jumatano usiku.
Mshukiwa
alipigwa risasi nne, vyanzo vya utekelezaji sheria viliiambia CBS.
Haijulikani
ni silaha gani ilitumika katika shambulio hilo wala nia haikubainika wazi mara
moja.
Mshukiwa
hakuwa akishirikiana na mamlaka, vyanzo vya kutekeleza sheria viliiambia CBS
Jumatano usiku.
Hujambo. Karibu katika matangazo ya leo ikiwa ni tarehe 27/11/2025.