Urusi yaushambulia mji wa Aleppo huku waasi wakichukua udhibiti
Vikosi vya waasi nchini Syria vimechukua udhibiti wa "nusu" ya mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Aleppo, kwa mujibu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu wa Syria lenye makao yake nchini Uingereza
Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo haya ya moja kwa moja, shukran kwa kuwa nasi lakini kumbuka unaweza kufuata taarifa zetu zaidi kwenye Chaneli yetu ya WhatsApp:
Chanzo cha picha, Getty
Bofya hapa ili kujiunga na
chaneli yetu ya WhatsApp ikiwa unatumia simu yako ya mkononi au Wavuti ya
WhatsApp.
Je, kundi la Hayat Tahrir al-Sham llinaloongoza mashambulizi ya Syria ni nini?
Chanzo cha picha, Reuters
Kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Hayat Tahrir al-Sham (HTS) lina historia ndefu na inayohusika katika mzozo wa Syria.
HTS lilianzishwa chini ya jina tofauti, Jabhat al-Nusra , mwaka wa 2011 kama mshirika wa moja kwa moja wa Al Qaeda.
Kiongozi wa kundi la IS, Abu Bakr al-Baghdadi , pia alihusika katika uundaji wake.
Iilionekana kuwa mojawapo ya makundi yenye ufanisi zaidi na hatari kwa mauaji kati ya makundi yaliyolengwa dhidi ya Rais Assad.
Lakini itikadi yake ya kijihadi ilionekana kuwa nguvu yake ya kuendesha badala ya bidii ya mapinduzi - na lilionekana wakati huo kama halikubaliani na muungano mkuu wa waasi chini ya bendera ya Free Syria.
Lakini mnamo 2016, kiongozi wa kundi hilo, Abu Mohammed al-Jawlani, alivunja uhusiano hadharani na Al Qaeda, akavunja Jabhat al-Nusra na kuanzisha shirika jipya , ambalo lilichukua jina la Hayat Tahrir al-Sham lilipounganishwa na vikundi vingine kadhaa sawa. mwaka mmoja baadaye.
Ruto achaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Rais wa Kenya William Ruto
Rais wa Kenya William Ruto amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akichukua nafasi ya mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir. Ruto atashikilia wadhifa huo kwa mwaka mmoja ujao.
Aliteuliwa kushika wadhifa huo wakati wa mkutano wa 24 wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Arusha, Tanzania.
Mkutano wa 24 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki unawaleta pamoja viongozi wa kanda hiyo ili kujadili masuala muhimu yanayochagiza mustakabali wa Afrika Mashariki.
Mkutano huo wa hadhi ya juu, uliofanyika chini ya kaulimbiu kuu ya Maadhimisho ya Miaka 25 ya EAC, unatumika kama jukwaa la kutathmini mafanikio ya miaka 25 iliyopita huku ukielekeza njia ya kusonga mbele kwa utangamano wa kina.
Zelensky asema vita vinaweza kumalizika iwapo Ukraine ambayo haijavamiwa itakuwa chini ya Nato
Chanzo cha picha, EPA
Rais Volodymyr Zelensky wa Urusi amesema kwamba sehemu za Ukraine ambazo bado zipo chini ya udhibiti wake zichukuliwe "chini ya mwavuli wa Nato" ili kujaribu kuzuia "awamu ya moto" wa vita.
Katika mahojiano marefu na mapana na Sky News, rais wa Ukraine aliulizwa kama angekubali uanachama wa Nato, lakini tu katika eneo ambalo Kyiv inashikilia kwa sasa.
Zelensky alisema atafanya hivyo, lakini ikiwa tu uanachama wa Nato utatolewa kwa Ukraine nzima, ndani ya mipaka yake inayotambulika kimataifa, kwanza.
Ukraine inaweza basi kujaribu kujadili kurejeshwa kwa eneo lililo chini ya udhibiti wa Urusi "kwa njia ya kidiplomasia", alisema.
Lakini pendekezo hilo ni la kinadharia sana. Kama Zelensky alivyosema, hakuna mtu ambaye bado ametoa pendekezo kama hilo.
Iwapo Nato inaweza kufikiria hatua kama hiyo inatia shaka sana.
"Ukraine haijawahi kuzingatia pendekezo kama hilo, kwa sababu hakuna mtu ambaye amelitoa rasmi kwetu," Zelensky alisema.
Nato itahitaji kutoa uanachama kwa nchi nzima, ikiwa ni pamoja na sehemu hizo ambazo kwa sasa zinadhibitiwa na Urusi, alisema.
Tazama:Waasi wa Syria walivyoteka sehemu za jiji la Aleppo
Maelezo ya video, Waasi wa Syria wateka sehemu za Aleppo - ripoti
Vikosi vya waasi nchini Syria vimedhibiti vitongoji kadhaa mjini Aleppo, kwa mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za bidamu nchini Zyria- Syrian Observatory for Human Rights (SOHR) lenye makao yake nchini Uingereza.
Video inaonyesha vikosi vya waasi vikiwa katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria kama sehemu ya mashambulizi makubwa dhidi ya serikali.
Hii ni mara ya kwanza kwa waasi wanaopigana na majeshi ya Rais Bashar al-Assad kufika Aleppo tangu walazimishwe kuondoka na jeshi mwaka 2016.
Mwanamuziki wa Mali azuiliwa nchini Ubelgiji kutokana na mzozo wa malezi ya mtoto
Chanzo cha picha, Reuters
Mmoja wa wanamuziki mashuhuri
barani Afrika wa Mali Rokia Traoré ameripotiwa kufungwa nchini Ubelgiji kama
sehemu ya mzozo unaoendelea wa malezi ya mtoto.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 50 amezuiliwa baada
ya kurejeshwa kutoka Italia, kwa ajili ya kifungo cha miaka miwili jela,
kulingana na shirika la habari la AFP.
Sakata hiyo ya muda mrefu ilianza 2020 wakati Traoré
aliwekwa kizuizini nchini Ufaransa kutokana na hati ya kukamatwa ya Ubelgiji
baada ya kushindwa kutii amri ya mahakama ya kumkabidhi binti yake kwa baba wa
msichana huyo kutoka Ubelgiji.
Miezi kadhaa baada ya kuachiliwa kwa masharti , Traoré
alisafiri hadi Mali kwa ndege ya kibinafsi, akikaidi marufuku ya kuondoka
Ufaransa hadi aliporejeshwa Ubelgiji.
Oktoba
mwaka jana, Traoré alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela bila kuwepo
mahakamani na mahakama nchini Ubelgiji kwa tuhuma za utekaji nyara wa mzizi kwa
"kukosa kumkabidhi mtoto kwa mtu anayestahili kumlea"
'Nilitazama ponografia asubuhi, mchana na usiku'
Maelezo ya picha, Shaun Flores anashirikisha umma hadithi yake katika mfululizo mpya wa BBC iPlayer
Shaun Flores alikuwa na umri wa miaka 11 alipoanza kutazama ponografia,
baada ya kutambulishwa aina hizo za
video na rafiki yake.
"Nilivutiwa mara moja," kijana huyo mwenye umri wa miaka 30
sasa anasema.
"Nilihisi, msisimo nikasema wow, ni kitu gani hiki ambacho watu wakifanya wanaonekana kama wana wakati wa mzuri wa maisha yao."
Udadisi wa Shaun haraka ukabadilika na kuwa kitu ambacho alikiona ni
vigumu kukiacha.
Anaeleza kuwa alitazama ponografia asubuhi, mchana na usiku, akisema ikawa "kawaida kama
kupiga mswaki".
Ingawa sio kila mtu
anayetazama ponografia ataendeleza uhusiano usiofaa nayo, Shaun hayuko peke
yake katika tabia hii ya kutazama ponografia.
Ripoti ya shirika la Ofcom ya
Online Nation 2024 inasema 29% ya watu wazima wa Uingereza walitazama ponografia
mtandaoni Mei 2024.
Zaidi ya hayo,
utafiti mpya kutoka kituo cha matibabu ya watu walioathiriwa, UKAT, unaonyesha kuwa mamilioni ya Waingereza wanatazama
ponografia mara kwa mara, huku milioni
1.8 wakitazama kila siku, au mara kadhaa kwa siku.
Kulingana na wanaotibu uraibu huo,
watu wengi zaidi wanatafuta usaidizi kwa utumiaji wa ponografia wenye shida.
'Mara tu unapoanza ni ngumu sana kuacha'
Lee Fernandes, mtaalamu wa tiba katika Kundi la UKAT, pia anasema idadi ya watu wanaowatibu kwa matumizi mabaya ya ponografia imeongezeka "kwa kiasi kikubwa" katika miaka ya hivi karibuni.
Sasa wanapokea maswali mengi kwa usaidizi kutoka kwa watu wanaopambana na utumiaji wao wa ponografia kila siku. Kabla ya 2020, ilikuwa ni swali moja au mbili kwa wiki
Fernandes anaeleza kuwa maendeleo ya teknolojia na upatikanaji rahisi wa ponografia unarahisisha watu wa rika zote kufikia maudhui ya ngono mtandaoni. Anaamini yake inachangia ongezeko la watu wanaotafuta msaada ambao amepata.
Urusi yaushambulia mji wa Aleppo huku waasi wakichukua udhibiti
Chanzo cha picha, Getty Images
Vikosi vya waasi nchini Syria vimechukua
udhibiti wa "nusu" ya mji wa pili kwa ukubwa nchini humo, Aleppo, kwa
mujibu wa shirika la waangalizi wa haki za binadamu wa Syria -Syrian Observatory for Human Rights
(SOHR) lenye makao yake nchini Uingereza.
Urusi ilianzisha mashambulizi ya anga katika sehemu za Aleppo usiku wa kuamkia Jumamosi kwa mara ya kwanza tangu 2016, waangalizi hao waliongeza.
SOHR ilisema zaidi ya watu 300 ikiwa ni pamoja na zaidi ya raia 20 wameuawa tangu mashambulizi kuanza siku ya Jumatano.
Mashambulizi hayo ni makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Syria kwa miaka mingi na ni mara ya kwanza kwa waasi wanaopigana na vikosi vya Rais Bashar al-Assad kufika Aleppo tangu kulazimishwa kuondoka na jeshi mwaka 2016.
SOHR
ilisema watu 277 ikiwa ni pamoja na
zaidi ya raia 20 wameuawa tangu
mashambulizi kuanza siku ya Jumatano.
Safu ya makundi yenye silaha yanayoipinga serikali ya Assad ikiwa ni pamoja na wafuasi wa jihad - walichukua fursa ya ghasia na kunyakua maeneo mengi.
Serikali ya Syria kwa usaidizi wa Urusi na washirika wengine, baadaye ilichukua tena maeneo mengi iliyokuwa imepoteza.
Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Waasi wanaendesha gari kwenye barabara kuu ya kimataifa ya M5, njia ya kuelekea Aleppo, Syria
Mashambulizi hayo ni makubwa zaidi dhidi ya serikali ya Syria kuwahi kushuhudiwa kwa miaka mingi na ni mara ya kwanza kwa waasi wanaopigana na vikosi vya Rais Bashar al-Assad kufika Aleppo tangu kulazimishwa kuondoka mjini humo na jeshi mwaka 2016.
Uwanja wa ndege wa Aleppo na barabara zote zinazoingia mjini zimefungwa, vyanzo vya kijeshi vililiambia shirika la habari la Reuters.
Karibu kwa matangazo haya ya mubashara ya leo Jumamosi ya mwisho wa mwezi wa Novemba, tukikuletea habari za kikanda na kimataifa, shukrani kwa kujiunga nasi.