Ikiwa ndio mwanzo unajiunga nasi...
Vyombo vya habari vya serikali ya Iran vimethibitisha kwamba Kiongozi Mkuu Ali Khamenei ameuawa, katika mashambulizi ya Israel na Marekani dhidi ya Iran kutoka ambayo yalianza Jumamosi asubuhi (saa za ndani).
Haya hapa yaliyojiri kwa mukhtasari:
- Taarifa ya Baraza Kuu la Usalama la Kitaifa la Iran, iliyosomwa vyombo kadhaa vya habari vya serikali, imethibitisha kuwa Ayatollah Khamenei aliuawa ofisini kwake mapema Jumamosi asubuhi.
- Mtangazaji mmoja, alisema nchi itaanza siku 40 za maombolezo huku akitokwa na machozi, .
- Zaidi ya watu 200 wameuawa wakati wa mashambulizi hayo, kulingana na shirika la Red Crescent, huku CBS News, mshirika wa habari wa BBC ikiripoti kuwa maafisa 40 wa Iran wameuawa.
- Kujibu mashamblizi hayo, Iran ilifanya msururu wa mashambulizi Mashariki ya Kati, hasa dhidi ya mataifa washirika wa Marekani na ambapo Marekani ina kambi za kijeshi, ikiwa ni pamoja na Dubai, Doha, Bahrain, na Kuwait.
- Uingereza inashiriki katika "operesheni zilizoratibiwa za ulinzi wa kikanda" kulinda raia wa Uingereza na washirika wa kikanda, Waziri Mkuu wa Uingereza Sir Keir Starmer amesema.
- Rais Donald Trump hapo awali alisema Khamenei alikuwa "mmoja wa watu waovu zaidi katika historia" na kwamba kifo chake kilikuwa "fursa kubwa zaidi kwa Wairan kurujirudishia nchi yao". Alisema Marekani itaendelea kuishambulia Iran kwa mabomu - huku milipuko ikiendelea kusikika katika mji mkuu wake Tehran.
- Marekani haiwezi kutangaza vita bila idhini ya bunge - na operesheni hii imegawanya wabunge, kwa kiasi kikubwa kulingana na vyama.
- Umoja wa Mataifa pia umesema operesheni hiyo ya kijeshi inadhoofisha amani katika eneo hilo.














