Wanajeshi wa Uingereza wachunguzwa kuhusu operesheni ya Libya

Macron alisema kuwa viongozi wa mataifa ya Afrika katika eneo la Sahel "walisahau" kuishukuru Ufaransa kwa kuyasaidia mataifa yao kukabiliana na wanamgambo wa kijihadi.

Muhtasari

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi, Mariam Mjahid na Rashid Abdalla

  1. Kwaheri hadi kesho

    Na hapa ndio mwisho wa taarifa zetu za moja kwa moja, tukutane kesho.

  2. Wanajeshi wa Uingereza wachunguzwa kuhusu operesheni ya Libya

    edc

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Wanajeshi wa kikosi maalumu cha jeshi la wanamaji la Uingereza wanachunguzwa kuhusu operesheni zake nchini Libya miaka miwili iliyopita, BBC imearifiwa.

    Gazeti la Daily Mail, ambalo liliripoti uchunguzi huo kwa mara ya kwanza, linasema takribani wanajeshi watano wa kikosi cha maalumu cha SBS, wanachunguzwa kuhusu tukio lililohusisha kuifukuza gari ambapo risasi zilifyatuliwa.

    Maelezo ya nini hasa kilitokea na ni wanajeshi wangapi wa SBS wanaochunguzwa hayajathibitishwa.

    BBC inaelewa kuwa uchunguzi umekuwa ukiendelea kwa miezi kadhaa. Hadi sasa, hakuna chochote ambacho kimekabidhiwa kwa huduma ya kuendesha mashtaka ya kijeshi (SPA).

    Inaaminika kuwa wanajeshi wa kikosi hicho cha Uingereza walikuwa nchini Libya tangu NATO ilipozindua mashambulizi yake ya anga kulenga vikosi vya Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.

    Fauka ya hilo, wiki iliyopita, kuliibuka taarifa kuwa wanajeshi tisa wa kikosi maalumu cha jeshi la Uingereza wanaweza kushtakiwa kwa tuhuma za uhalifu wa kivita katika matukio mawili tofauti nchini Syria.

  3. Kijiji kimoja Italia chapiga marufuku wakaazi wake kuwa 'wagonjwa'

    ds

    Chanzo cha picha, Comune di Belcastro/Facebook

    Maelezo ya picha, Belcastro, kusini mwa Italia, ni nyumbani kwa karibu watu 1,200

    Watu wanaoishi katika kijiji cha Belcastro "wameamriwa kujizuia kuambukizwa ugonjwa wowote ambao unaweza kuhitaji usaidizi wa dharura wa matibabu," amri kutoka kwa Meya wa eneo hilo Antonio Torchia.

    Kijiji cha Belcastro kiko katika eneo la kusini la Calabria – ni mojawapo ya vijiji maskini zaidi ya Italia.

    Torchia amesema hatua hiyo "ni wazi inachekesha," lakini ina athari zaidi kuliko notisi za dharura alizotuma kwa mamlaka za mkoa ili kuangazia mapungufu ya mfumo wa afya wa eneo hilo.

    Takribani nusu ya wakazi 1,200 wa Belcastro wana umri wa zaidi ya miaka 65 na idara ya karibu ya Ajali na Dharura (A&E) iko umbali wa zaidi ya kilomita 45 (maili 28), amesema meya.

    Aliongeza kuwa unaweza kuifikia idara hiyo kwa kusafiri kwenye barabara yenye kikomo cha mwendo kwa kilomita 30 kwa saa.

    Na operesheni za upasuaji katika kijiji hupatikana kwa kipindi fulani, na hakuna bima wakati wa wikendi, likizo au baada ya saa za kazi.

    Kama sehemu ya agizo hilo, wakaazi pia wameamriwa "kutojihusisha na tabia ambazo zinaweza kudhuru afya na kuepuka ajali za nyumbani," na "kutotoka nyumbani mara kwa mara, kusafiri au kufanya mazoezi ya michezo, na badala yake wapumzike wakati mwingi."

    Utawala mbovu na makundi ya kimafia - vimeharibu mfumo wa huduma za afya katika eneo hilo, ambao uliwekwa chini ya usimamizi maalumu kutoka serikali kuu karibu miaka 15 iliyopita.

    Makamishna walioteuliwa na Roma wanapata changamoto kushughulikia viwango vikubwa vya deni vinavyokabili hospitali, ikimaanisha kwamba watu wa Calabrians wana ukosefu mkubwa wa wafanyakazi wa matibabu na vitanda.

    Hospitali kumi na nane za mkoa huo zimefungwa tangu 2009. Matokeo yake, karibu nusu ya wakazi milioni mbili wa Calabria wanatafuta usaidizi wa kimatibabu nje ya eneo hilo.

    Mwaka 2022, ilitangazwa kuwa Cuba itatuma madaktari 497 katika mkoa huo kufanya kazi kwa miaka mitatu katika vituo mbali mbali vya matibabu. Gavana wa mkoa Roberto Occhiuto alisema mwaka jana madaktari hawa "wameokoa" hospitali za Calabria.

    Wakaazi wa Belcastro wameviambia vyombo vya habari kuwa Meya Torchia "amefanya jambo sahihi katika kuangazia suala hilo", na uamuzi huo "utatoa mwamko."

  4. Waliofariki katika tetemeko la ardhi Tibet wafikia 126

    er

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mitetemeko pia ilisikika nchini Nepal, lakini haijaripoti majeruhi

    Takribani watu 126 wamefariki, na wengine 188 wamejeruhiwa, baada ya tetemeko la ardhi kupiga vilima vya Himalaya siku ya Jumanne, kulingana na vyombo vya habari vya serikali ya China.

    Wafanyakazi wa uokoaji wanafukua vifusi kutafuta manusura baada ya tetemeko hilo lililoharibu zaid ya majengo 1,000 katika eneo la Tibet, karibu na mlima wa Everest.

    Operesheni kubwa ya uokoaji inaendelea, huku walionusurika wakiwa chini ya shinikizo la ziada kwani halijoto inatabiriwa kushuka hadi nyuzijoto 16C (3.2F).

    Matetemeko ya ardhi ni ya kawaida katika eneo hilo, kutokana na jiografia yake, lakini tetemeko hilo limeacha vifo vya watu wengi zaidi nchini China katika miaka ya hivi karibuni.

    Tetemeko hilo la ukubwa wa 7.1, ambalo lilipiga kwa kina cha kilomita 10 (maili sita), kulingana na data kutoka Geological Survey ya Marekani, pia lilisikika nchini Nepal na nsehemu za India, ambazo ni jirani na Tibet.

  5. Iran yawanyonga watu 901 mwaka 2024 - UN

    d

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Idadi hiyo ni ya juu zaidi kurekodiwa katika miaka tisa

    Takribani watu 901 wamenyongwa nchini Iran mwaka jana, wakiwemo 40 ndani ya wiki moja mwezi Disemba, kulingana na mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa.

    "Inasikitisha sana bado tunaona idadi kubwa ya watu wanaokabiliwa na hukumu ya kifo nchini Iran mwaka hadi mwaka," amesema Volker Türk. "Ni wakati muafaka Iran kukomesha wimbi hili la kunyonga."

    Ni kiwango kubwa zaidi kurekodiwa katika miaka tisa iliyopita na ongezeko la 6% kutoka 2023, mwaka ambao watu 853 waliuawa.

    Wengi wa walionyongwa yalikuwa ya makosa yanayohusiana na dawa za kulevya, pia wapinzani na watu waliohusishwa na maandamano ya 2022 walinyongwa, kulingana na UN. Vilevile kulikuwa na ongezeko la idadi ya wanawake walionyongwa, wakifikia 31.

    Türk ameitaka Iran kusitisha unyongaji na kusitisha matumizi ya hukumu ya kifo kwa nia ya kukomesha kabisa hukumu hiyo.

    Msemaji wa ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa aliwaambia waandishi wa habari kwamba takwimu hizo zimetoka kutoka mashirika kadhaa ambayo inaamini yako huru, likiwemo Shirika la Habari la Wanaharakati wa Haki za Kibinadamu la Iran (HRANA), Shirika la Haki za Binadamu la Iran (IHR) na Hengaw.

    Pia unaweza kusoma:

  6. Rais mpya wa Ghana John Mahama aapishwa

    John Dramani Mahama

    Chanzo cha picha, myjoy

    Rais John Dramani Mahama, ameapishwa kushika wadhifa huo katika hafla iliyofanyika kwenye ukumbi wa Black Star Square katika mji mkuu wa Ghana, Accra.

    Ni kufuatia ushindi mkubwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita. Na kwa mara ya kwanza, nchi hiyo pia ina Makamu wa Rais mwanamke, Profesa Jane Naana Opoku Agyemang.

    Mapema leo, Wabunge na spika wapya waliapishwa. Mahama amewahi kuwa Rais wa Ghana kuanzia 2012 hadi 2017.

    Viongozi 21 wa nchi akiwemo Rais wa Nigeria na Mwenyekiti wa ECOWAS Bola Tinubu walikuwepo kushuhudia tukio hilo.

    Mahama anachukua wadhifa huo wakati ambapo Ghana inapata nafuu kutokana na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi kuwahi kutokea. Matarajio ni makubwa, na Mahama ameahidi kuletea mageuzi ya uchumi.

  7. Jarida la Charlie Hebdo laadhimisha miaka kumi tangu shambulio la 2015

    df

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Miaka 10 imepita tangu shambulio la bunduki la wanajihadi katika ofisi za jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa ambalo liliua wafanyakazi wake wengi na wahariri.

    Tarehe 7 Januari 2015, ndugu wawili Saïd Kouachi na Chérif Kouachi walivamia mkutano katika ofisi ya Paris ya jarida la kila wiki la katuni, na kuwaua wachora katuni wake nyota Cabu, Wolinski, Charb na Tignous.

    Kwa ujumla, watu 12 waliuawa, akiwemo polisi Mwislamu aliyekuwa zamu nje. Siku mbili baadaye walizungukwa na kuuawa kwa kupigwa risasi na polisi karibu na uwanja wa ndege wa Charles-de-Gaulle.

    Siku hiyo hiyo Amedy Coulibaly – rafiki wa mmoja kati ya ndugu wawili - aliwaua Wayahudi wanne katika utekaji nyara katika duka kubwa mashariki mwa Paris.

    Coulibaly aliyeuawa kwa kupigwa risasi na polisi - alikuwa amemuua polisi mwanamke siku moja kabla.

    Muongo mmoja baadaye, Charlie Hebdo inaendelea kutoa nakala mtandaoni na nakala ngumu katika ofisi ambayo ilipo ni siri, na wafanyakazi ambao wanalindwa na walinzi.

    Maandamano ya watu milioni mbili yalifanyika katikati jiji la Paris na wakuu wa nchi na serikali kutoka nchi mbalimbali duniani wakahudhuria kwa mwaliko wa Rais wa wakati huo François Hollande.

    Pia unaweza kusoma:

  8. Jeshi la Uganda lakanusha wanajeshi wake kuuawa na wanamgambo wenye uhusiano na IS

    c

    Chanzo cha picha, The Independent

    Maelezo ya picha, Msemaji wa jeshi Meja Charles Kabona.

    Jeshi la Uganda limekanusha madai kuwa wanajeshi wake 10 wameuawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio la wanamgambo wa kundi la Islamic State Allied Democratic Forces (ADF), katika wilaya ya kati ya Kayunga.

    Tovuti binafsi ya Chimp Reports iliripoti tarehe 6 Januari kuwa shambulio hilo lilitokea katika eneo la Misanga wilayani Kayunga, bila kutaja lini lilitokea.

    "Hizi ni propaganda mbovu na zisizo na msingi zilizobuniwa na watu wabaya ili kutia hofu umma. Hakuna mauaji ya askari wetu huko Kayunga," amesema msemaji wa jeshi Meja Charles Kabona.

    "Eneo hilo ni la amani na wakazi wanaendelea na shughuli zao za kila siku katika mazingira tulivu."

    IS ilidai tarehe 5 Januari kupitia Telegram kwamba wanamgambo wake walipambana na wanajeshi wa Uganda huko Misanga tarehe 3 Januari wakati vikosi vya kijeshi "vilipojaribu kusonga mbele" kwenye maeneo ya kundi hilo katika eneo hilo.

    ADF lililoundwa nchini Uganda lakini sasa lina makao yake makuu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, inaaminika kuwa limejiunga na kundi la IS.

    Majeshi ya DR Congo na Uganda yamekuwa yakiendesha operesheni za pamoja dhidi ya ADF tangu 2021.

    Pia unaweza kusoma:

  9. Marekani yawapeleka wafungwa 11 wa Guantanamo Bay nchini Oman

    Ghu

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wafungwa 11 kutoka Yemen katika jela ya kijeshi ya Marekani huko Guantanamo Bay yamepelekwa Oman.

    Hatua hiyo imewaacha wafungwa 15 katika gereza hilo - ikiwa ni idadi ndogo zaidi katika wakati wowote katika historia ya jela hiyo.

    Katika taarifa ya Idara ya Ulinzi iliishukuru Oman kwa kuunga mkono juhudi za Marekani "zinazolenga kupunguza idadi ya wafungwa na hatimaye kulifunga" gereza hilo.

    Hakuna hata mmoja kati ya wanaume waliokamatwa baada ya shambulio la kigaidi la 9/11 aliyeshtakiwa kwa uhalifu wowote katika zaidi ya miongo miwili kizuizini.

    Uhamisho huo, ambao inasemekana ulifanyika mapema siku ya Jumatatu, unakuja siku chache kabla ya mtuhumiwa mkuu wa mashambulizi ya Septemba 11, 2001 dhidi ya Marekani, Khalid Sheikh Mohammed, atakapokiri makosa, kufuatia makubaliano na maafisa wa shirikisho ili kuepuka hukumu ya kifo.

    Jela hiyo ya kijeshi ni sehemu ya kambi ya jeshi la wanamaji la Marekani kusini mashariki mwa Cuba. Ilianzishwa na utawala wa Bush mwaka 2002, kufuatia mashambulizi ya 9/11, ili kuwashikilia washukiwa waliokamatwa katika operesheni za kukabiliana na ugaidi. Katika kilele chake, ilishikilia wafungwa wapatao 800.

    Pia unaweza kusoma:

  10. Idadi ya watu waliofariki katika tetemeko la ardhi Tibet yafikia 95

    Hh

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Zaidi ya majengo 1,000 yameharibiwa na tetemeko hilo la ardhi

    Takriban watu 95 wamethibitishwa kufariki na wengine 130 kujeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kupiga eneo la milima la Tibet Jumanne asubuhi, vyombo vya habari vya serikali ya China vinasema.

    Tetemeko la ardhi lililokumba mji mtakatifu wa Tibet wa Shigatse lilikuwa na ukubwa wa 7.1 na kina cha kilomita 10 (maili sita), kulingana na data kutoka Geological Survey ya Marekani. Mitetemeko pia ilisikika katika nchi jirani ya Nepal na sehemu za India.

    Shigatse unachukuliwa kuwa moja ya miji mitakatifu zaidi ya Tibet. Ni eneo la jadi la Panchen Lama, mtu mkuu katika Ubuddha huko Tibet ambaye mamlaka yake ya kiroho ni ya pili baada ya Dalai Lama.

    Pia unweza kusoma:

  11. Kwa picha: Wakristo wa Orthodox leo wanasherehekea Krismasi

    Wakristo wa Orthodox duniani kote wamekuwa wakiadhimisha Krismasi kwa kuhudhuria ibada za kanisani.

    Wakati Wakristo wengine duniani huadhimisha Sikukuu ya Krismasi tarehe 25 Desemba, kwa Wakristo milioni 200 wa Orthodox duniani, kuzaliwa kwa Yesu Kristo kunaadhimishwa tarehe 7 Januari.

    Hii inatokana na kwamba wanatumia kalenda ya Julian, tofauti na madhehebu ya Wakristo yanayotumia kalenda ya papa Gregory.

    Mwanamke katika mji mkuu wa Syria Damascus akipokea Ushirika Mtakatifu katika Kanisa la Kitume la Armenia la Mar Sarkis. Hii ni Krismasi ya kwanza Wasyria wanasherehekea tangu kuanguka kwa mtawala wao wa muda mrefu - Rais wa zamani Bashar al-Assad.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mwanamke katika mji mkuu wa Syria Damascus akipokea Ushirika Mtakatifu katika Kanisa la Kitume la Armenia la Mar Sarkis. Hii ni Krismasi ya kwanza Wasyria wanasherehekea tangu kuanguka kwa mtawala wao wa muda mrefu - Rais wa zamani Bashar al-Assad.
    Nchini Misri, kasisi anayewakilisha Kanisa la Kiorthodoksi la Coptic - jumuiya kubwa zaidi ya Kikristo ya Mashariki ya Kati - anawabariki waabudu katika Kanisa la Kiorthodoksi la Malaika Mkuu Michael Coptic huko Cairo.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Nchini Misri, kasisi anayewakilisha Kanisa la Kiorthodoksi la Coptic - jumuiya kubwa zaidi ya Kikristo ya Mashariki ya Kati - anawabariki waabudu katika Kanisa la Kiorthodoksi la Malaika Mkuu Michael Coptic huko Cairo.
    Kijana anayeabudu akiwasha mshumaa wakati wa sherehe za mkesha wa Krismasi wa Kiorthodoksi huko Sharjah, Falme za Kiarabu

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Kijana huyu anaonekana akiwasha mshumaa wakati wa sherehe za mkesha wa Krismasi wa Kiorthodoksi huko Sharjah, Falme za Kiarabu
    Hapo awali, waumini na viongozi wa kidini walikusanyika katika Kanisa la Nativity huko Bethlehem, katika Ukingo wa Magharibi unaotawaliwa na Israel, ambao unasemekana kuwa ndiko alikozaliwa Yesu.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Hapo awali, waumini na viongozi wa kidini walikusanyika katika Kanisa la Nativity huko Bethlehem, katika Ukingo wa Magharibi unaotawaliwa na Israel, ambao unasemekana kuwa ndiko alikozaliwa Yesu.
    Waumini wa Ethiopia wamekuwa wakishikilia mishumaa na kuimba nyimbo za nyimbo katika kanisa la Bole Medhanialem mjini Addis Ababa.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Waumini wa Ethiopia wamekuwa wakishikilia mishumaa na kuimba nyimbo za nyimbo katika kanisa la Bole Medhanialem mjini Addis Ababa.
    Mamilioni ya Warusi wanasherehekea Krismasi na Rais Vladimir Putin (kushoto) aliadhimisha msimu wa sherehe katika Kanisa la St George's la Moscow.

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Maelezo ya picha, Mamilioni ya Warusi wanasherehekea Krismasi na Rais Vladimir Putin (kushoto) aliadhimisha msimu wa sherehe katika Kanisa la St George's la Moscow.
  12. Chad na Senegal zakerwa na kauli ya Macron dhidi ya viongozi wa Afrika

    Chad imetamaushwa na kauli iliyotolewa na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron dhidi ya viongozi wa Afrika.

    Macron alisema kwamba viongozi wa mataifa ya Sahel ''hawana shukurani licha ya kusaidiwa kupambana na makundi ya kijihadi'' huku wanajeshi wake wakindelea kuondoka za Afrika Magharibi.

    Akimjibu Rais Macron, Waziri wa Mambo ya Nje wa Chad, Abderaman Koulamallah alisema "Afrika, ikiwemo Chad, iliisaidia Ufaransa kwa kiwango kikubwa wakati wa vita viwili vya dunia, jambo ambalo Ufaransa haijawahi kukubali," tovuti ya habari ya Alwhida Info iliripoti.

    Koulamallah alisema "viongozi wa Ufaransa wanastahili kuheshimu watu wa Afrika na kutambua thamani ya kujitolea kwao".

    Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko amepuuza jukumu la Ufaransa katika kuhakikisha nchi za Afrika zina uhuru, akiishutumu Paris kwa kufanya kinyume na hilo.

    "Macron anajigamba kwamba "hakuna nchi ya Kiafrika ambayo leo ingekuwa huru kama haingesaidiwa na Ufaransa," Sonko aliandika kwenye kwenye mtandao wake wa Facebook.

    "Tutambue kwamba Ufaransa haina uwezo wala uhalali wa kuzihakikishia usalama na mataifa ya Afrika," aliongeza, akiituhumu kwa kuchangia machafuko ya Libya na kuilaumu kwa kuchochea hali tete ya usalama katika Sahel.

    Sonko alisema tangazo la Novemba 2024 kwamba Ufaransa itafunga kambi zake za kijeshi nchini Senegal lilitokana na " juhudi za taifa hilo wa la Kiafrika kama nchi huru, inayojitawala".

  13. Bobi Wine amjibu mkuu wa jeshi Uganda kwa kutishia kumkata kichwa

    Bobi Wine

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Vita vya mitandaoni vimeendelea kutokota kati ya Mkuu wa jeshi la Uganda Generali Muhoozi Kainerugaba na mwanasiasa mashuhuri wa Uganda Bobi Wine.

    Hii ni baada ya mtoto wa Rais wa muda mrefu Yoweri Museveni, kusema kuwa anataka kumkata kichwa kiongozi mashuhuri wa upinzani nchini humo Bobi Wine.

    Katika chapisho kwenye X Jumapili jioni, Kainerugaba alisema babake aliyeitawala Uganda tangu 1986, ndiye mtu pekee anayemlinda kiongozi wa upinzani Bobi Wine dhidi yake.

    Bobi wine ambaye aliibuka wa pili katika uchaguzi wa urais 2021 ulioshindwa na Yoweri Museveni, amejibu vitisho vya mtoto wa rais akisema kuwa kauli hizo anazichukulia kwa uzito kutokana na vitisho vya kuuawa.

    Naye Kainerugaba ambaye ni mtoto wa rais akamjibu: “Nimekuamsha? Kabla nikumalize kwanza tulipe mkopo tuliokupa,” akionekana kudai kuwa serikali ilikuwa imelipa Bobi Wine apunguze joto la upinzani nchini humo.

    Hata hivyo msemaji wa serikali ya Uganda pamoja na Kainerugaba hawakupatikana kuzungumzia kauli hizi za mitandaoni.

    Naye msemaji wa wanajeshi nchini Uganda alikataa kuzungumzia mtafaruku uliopo.

    Awali msemaji wa serikali alisema kauli za Kainerugaba mitandaoni zinapaswa kuchukuliwa kama “stihizai” na hazipaswi kuchukuliwa kwa uzito au kupima sera za serikali ya Uganda.

    Bobi Wine amepinga vikali madai kuwa alihongwa na serikali ya Uganda katika shughuli zake za kuwania urais mwaka 2021. “Iwapo walinifadhili kwanini wananifuata kila mahali na kuua wafuasi wangu?” Bobi Wine anasema.

    Bobi wine ambaye jinalake halisi ni Robert Kyagulanyi alikuwa mwanamiziki na kugeukia siasa amekuwa kigogo wa kupinga utawala wa rais Yoweri Museveni.

    Katika chaguzi za 2021 Bobi Wine alipinga matokeo ya uchaguzi akidai uchaguzi uliingia dosari kwa wizi na wapiga kura kutishiwa maisha.

    Kainerugaba mara kwa mara hutoa machapisho yenye utata kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni pamoja na tishio la 2022 la kutaka kuivamia nchi jirani ya Kenya.

  14. Afrika Kusini: Wachimbaji madini waliokataa kutoka kwenye shimo ‘wanakula nyama ya binadamu’ na mende

    Mgodi

    Chanzo cha picha, Reuters

    Wachimba madini watatu waliotoka kwenye shimo zilizozibwa na polisi katika mgodi wa Buffelsfontein huko Stilfontein Afrika Kusini wanasema kwamba hali imekuwa mbaya sana kiasi kwamba wale walio chini ya ardhi wameamua kula nyama ya binadamu na mende.

    Maelezo yao yamenakiliwa kwenye nyaraka zilizowasilishwa kwa Mahakama ya Kikatiba.

    Tangu Agosti mwaka jana, polisi wamezuia chakula na bidhaa nyingine kuwafikia wachimbaji madini wanaodaiwa kuingia kwenye migodi ya Buffelsfontein iliyotelekezwa.

    Wanasema wachimbaji hao wanafanya kazi haramu na wanajua jinsi ya kutoka.

    Lakini mashirika ya kutetea haki za binadamu, wanaharakati wa ndani na wachimba migodi ambao wameibuka, wanasema polisi wanafanya unyama.

    Soma pia:

  15. Afisa wa zamani wa gereza afungwa jela kwa kufanya mapenzi na mfungwa

    XX

    Chanzo cha picha, PA Media

    Afisa wa zamani wa gereza la HMP Wandsworth ambaye alionekana kwenye video akifanya mapenzi na mfungwa, amepewa hukumu ya miezi 15 jela.

    Linda De Sousa Abreu alikamatwa na maafisa wa gereza baada ya video hiyo kusambazwa mtandaoni na kutamba haraka.

    Gavana wa gereza la Wandsworth alisema kitendo cha Abreu kilichukua “siku moja” tu kubomoa miaka mingi ya juhudi za kuendeleza mazingira bora kwa wafanyakazi wa kike katika magereza ya kiume.

    Abreu, mwenye umri wa miaka 30, alikamatwa katika uwanja wa ndege wa Heathrow kabla ya kujaribu kuabiri ndege kuelekea Madrid akiwa na baba yake. Aliwahi kukiri kosa la kutenda uhalifu wa kimaadili akiwa kazini.

    Abreu na mfungwa huyo walionekana kwenye video wakifanya mapenzi katika seli kati ya tarehe 26 na 28 mwezi Juni.

    Polisi wa Metropolitan walieleza kuwa uchunguzi unaendelea kuhusu wafungwa wawili waliotambulika kwenye video hiyo.

    Mahakama pia ilielezwa kwamba kuna video nyingine iliyoonekana kwenye kamera aliyovaa Abreu akiwa katika huduma ya gereza, ikionyesha akifanya kitendo cha ngono na mfungwa huyo.

    Jaji Martin Edmunds KC alisema video hiyo iliyosambaa mtandaoni siyo tukio moja tu, bali ni sehemu ya tabia ya kurudia.

    Chama cha Wafanyakazi wa Magereza, kinachowakilisha wafanyakazi wa gereza, kilikubali kuwa kuna idadi ndogo ya wafanyakazi wapotovu wanaoharibu kazi ya wengine.

  16. Makumi wafariki baada ya tetemeko la ardhi lakumba eneo Tibet nchini China

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Takriban watu 53 wamethibitishwa kufariki na wengine 62 kujeruhiwa baada ya tetemeko kubwa la ardhi kukumba eneo la milima la Tibet nchini China Jumanne asubuhi, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya serikali ya China.

    Tetemeko la ardhi lililokumba mji mtakatifu wa Tibet wa Shigatse mwendo wa 09:00 saa za huko (01:00 GMT) lilikuwa na ukubwa wa 7.1 na kina cha kilomita 10 (maili sita), kulingana na data kutoka kwa Utafiti wa Jiolojia wa Marekani, ambao pia ulionyesha mfululizo wa matetemeko ya ardhi katika eneo hilo.

    Mitetemeko pia ilisikika katika nchi jirani ya Nepal na sehemu za India.

    Matetemeko ya ardhi hutokea mara kwa mara katika eneo hilo, ambalo liko kwenye mkondo mkubwa wa hitilafu ya kijiolojia.

  17. Vifo vilivyotokana na dhoruba ya baridi kali vyaongezeka Marekani

    xx

    Chanzo cha picha, Getty Images

    Mwanamume mmoja alipatikana amefariki Jumatatu asubuhi nje ya kituo cha basi katika eneo la Houston, Texas "kutokana na hali ya hewa ya baridi", msemaji wa mfumo wa metro wa jiji hilo alithibitisha kwa BBC.

    "Mwili ulipatikana kwenye eneo la kuegesha mabasi," Lester Gretsch, mkurugenzi wa habari wa Mamlaka ya Usafiri wa jiji katika kaunti ya Harris, alisema.

    Kifo hicho kinaongeza hadi tano idadi ya vifo vinavyoaminika kusababishwa na Dhoruba ya Majira ya Baridi , ambayo imesababisha theluji na baridi kali katika sehemu kubwa ya Marekani.

    Wakati huo huo polisi wanaoshika doria katika barabara kuu ya Jimbo la Missouri waliitikia mwito wa zaidi ya ajali 350 za barabarani.

    Watu wawili wamekufa katika ajali mjini Kansas kutokana na hali mbaya ya hewa, mwingine huko Virginia.

    Polisi wanasema mwanamume mwenye umri wa miaka 32 alifariki usiku wa manane huko Wakefield, Virginia, baada ya lori lake kuteleza kutoka barabarani na kugonga mti.

    Maafisa wanasema alikuwa akiendesha gari kwa kasi sana kwa hali ya barabarani na hakuwa amefunga mkanda, na huenda alikuwa mlevi.

    Maelezo zaidi:

  18. John Mahama kuapishwa leo kuwa rais Ghana

    Rais mteule wa Ghana, John Mahama,

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais mteule wa Ghana, John Mahama,

    Rais mteule wa Ghana, John Mahama, anatarajiwa kuapishwa leo baada ya kushindi uchaguzi wa mwezi uliopita.

    Kwa mara ya kwanza, nchi hiyo pia itakuwa na Makamu wa Rais mwanamke, Profesa Jane Naana Opoku Agyemang.

    Mahama amewahi kuhudumu kama Rais wa Ghana kuanzia 2012 hadi 2017.

    Viongozi 21 wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo katika ukumbi wa Black Star Square mjini Accra.

    Anachukua hatamu ya uongozi wakati Ghana inajikwamua kutokana na mzozo mbaya zaidi wa kiuchumi.

    Ghana kwa sasa inakabiliwa na kuongezeka kwa mfumuko wa bei, ukosefu wa ajira, na iko chini ya mpango wa uokoaji wa IMF wa dola bilioni 3.

    Mahama ameahidi kupunguza ushuru na kusaidia wajasiriamali ili kupunguza hali ngumu ya kiuchumi. Hata hivyo, Rais anayeondoka Nana Akufo Addo anadai uchumi umeimarika, kauli iliyopingwa na wabunge wa upinzani.

    Raia wengi wa Ghana wana matumaini kwamba uzoefu wa Mahama kama rais wa zamani utamsaidia kutatua changamoto za kiuchumi za nchi hiyo.

    Pian unaweza kusoma:

  19. Macron: Viongozi wa Afrika 'walisahau kuishukuru Ufaransa'

    Macron

    Chanzo cha picha, Reuters

    Maelezo ya picha, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron

    Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa mataifa ya Afrika "yalisahau" kuishukuru Ufaransa kwa kunusuru mataifa yao kuwa chini ya udhibiti wa wanamgambo.

    "Nadhani walisahau kutushukuru, lakini ni sawa, itakuja kwa wakati," Macron alisema.

    "Hakuna hata mmoja wao angelikuwa na serikali huru kama Ufaransa halingepeleka jeshi lake katika eneo hili," aliongeza kiongozi huyo wa Ufaransa.

    Maoni yake yalitolewa wakati wa mkutano wa kila mwaka huko Paris kwa mabalozi wa Ufaransa na ulizingatia malengo ya sera ya kigeni ya Ufaransa kwa mwaka wa 2025.

    Maelezo zaidi:

  20. Natumai hujambo.