Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.

Bofya kuelekea tovuti kuu

Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data

Moja kwa moja, Israel yafanya mashambulizi mapya dhidi ya Iran huku Marekani ikiwatambua wanajeshi wake waliouawa

Wanajeshi wanne wa akiba wa Marekani waliuawa Jumapili katika shambulizi la ndege zisizo na rubani nchini Kuwait siku ya moja baada ya Marekani na Israel kuanza mashambulizi dhidi ya Iran.

Moja kwa moja

Na Ambia Hirsi

  1. Wanajeshi wa Marekani waliuuawa katika mzozo wa Iran watambuliwa

    Jeshi la Marekani limewataja wanajeshi wake wa kwanza kuuawa katika mzozo kati ya Marekani na Iran.

    Wanajeshi sita walikufa wakati "mfumo wa ndege isio na rubani" ulipokwepa ulinzi wa anga na kugonga kituo cha amri katika bandari ya Shuaiba, nchini Kuwait, Jumapili.

    Kamandi Kuu ya Marekani hapo awali ilisema wanajeshi watatu walifariki katika shambulio hilo, lakini maafisa walithibitisha Jumatatu kwamba idadi ya waliofariki iliongezeka maradufu, baada ya mtu mmoja kufariki dunia kutokana na majeraha na miili miwili zaidi kupatikana kwenye vifusi.

    Wanajeshi hao wa Akiba wa Jeshi la Marekani ni wa Kamandi ya 103 ya Ulinzi ya Des Moines, Iowa, ambao ni:

    • Kapteni Cody A. Khork, 35, wa Winter Haven, Florida
    • Sajenti Daraja la kwanza Noah L. Tietjens, 42, wa Bellevue, Nebraska
    • Sajenti wa Daraja la kwanza Nicole M. Amor, 39, wa White Bear Lake, Minnesota
    • Sajenti Declan J. Coady, 20, wa West Des Moines, Iowa

    Siku ya Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kwamba ngome ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait ilipigwa wakati shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran.

    Vifo hivyo sita pekee ndivyo vilivyothibitishwa na jeshi la Marekani tangu lilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa ushikiano na Israel.

    Unaweza kusoma:

  2. Mataifa ya Ghuba yanatathmini jinsi ya majibu mashambulizi ya Iran

    Mataifa ya Ghuba yamejikuta katikati ya katika vita vipya vya Mashariki ya Kati, na yameghadhabishwa na hali hiyo.

    Iran imelipiza kisasi mashambulizi ya anga ya Marekani na Israel kwa kurusha mamia ya makombora na ndege zisizo na rubani kuelekea majirani zake wa Kiarabu - kulenga kambi za kijeshi vya Marekani zilizopo kwenye himaya yao, lakini pia miundombinu ya kiraia na nishati.

    Hatua hiyo ya Irana inabadili taswira ya Ghuba kuwa eneo salama, linalovutia wa wasafiri, utalii na fedha, na kuvuruga sekta ya mafuta na gesi katika msingi wake.

    Hii ni vita ambayo serikali za Kiarabu hazikutaka na zilijaribu kuzuia. Swali ni kama watavutwa ndani yake na kile walichokiita mashambulizi ya "haini" ya Irani.

    "Mipaka yote ya kisheria imevukwa," msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al Ansari alisema katika mkutano na waandishi wa habari siku ya Jumanne.

    "Mashambulizi dhidi ya uhuru wetu yamefanyika mara kwa mara," aliwaambia waandishi wa habari.

    "Miundombinu imeshambuliwa. Kuna mashambulizi yamefanywa maeneo ya makazi yetu. Na athari ya mashambulizi haya yako wazi. Inapokuja suala la kulipiza kisasi, uamuzi uko mikononi mwa uongozi wetu. Lakini tunapaswa kuweka wazi kwamba mashambulizi kama haya hayatafumbiwa macho."

    Makombora mengi ya Iran yanazuiliwa katika eneo la Ghuba, lakini vifusi vinavyoanguka vimeanzisha moto na kuua watu

    Ndege zisizo na rubani ambazo zinaweza kupenya kwa urahisi ulinzi wa anga mara nyingi husababisha uharibifu mdogo lakini huzua machafuko ambayo yavuruga biashara na usafiri.

  3. Wanafunzi na wafanyakazi waliouawa katika shambulo dhidi ya shule ya Iran wazikwa

    Wanafunzi na wafanyakazi waliuawa katika kile mamlaka ya Iran imedai kuwa shambulio la Marekani na Israel katika shule moja kusini mwa Iran wamezikwa.

    Maafisa wa Iran walisema zaidi ya watu 160 waliuawa wakati shule ya wasichana iliposhambuliwa katika mji wa Minab siku ya Jumamosi, wakati Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi makubwa yakilenga kambi za kijeshi na uongozi wa Iran.

    BBC haijafanikiwa kuthibitisha idadi ya vifo vilivyotolewa na mamlaka ya Iran.

    Shule hiyo ilikuwa karibu na kambi ya Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC).

    Jeshi la Marekani lilisema linachunguza ripoti za tukio hilo, huku jeshi la Israel likisema "halina habari" kuhusu operesheni zozote katika eneo hilo.

    Mamia ya waombolezaji walimiminika barabarani kutoa heshima zao za mwisho wakati wa mazishi hayo ambayo yalirushwa moja kwa moja kwenye televisheni ya taifa ya Iran.

    Majeneza yaliyokuwa yamefunikwa bendera ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalibebwa katika umati wa watu, huku sauti ya kina mama walioshindwa kuhimili majonzi ya kina mama na baba waliopoteza mabinti zao zikisikika hewani.

    Maafisa wa Iran wanasema shule hiyo ilishambuliwa kwa makombora matatu Jumamosi asubuhi. Ilikuwa takribani mita 600 (1970ft) kutoka kambi ya Walinzi wa Mapinduzi wa Iran,IRGC.

    Soma pia:

  4. Habari za hivi punde, Saudi Arabia yadungua makombora mawili ya kulipua meli

    Wizara ya ulinzi ya Saudi Arabia imesema kuwa imezuia makombora mawili kusini mwa mji mkuu wake, Riyadh, mashirika ya habari ya Reuters na AFP yanaripoti.

    Wakati huo huo Shirika rasmi la Habari la Saudia linaripoti kuwa ndege tisa zisizo na rubani zimeangushwa nchini humo.

    Maafisa wa Saudia hawajasema makombora na ndege hizo zisizo na rubani zilirushwa kutoka wapi.

  5. Uingereza na Uhispania zakataa ombi la Marekani kutumia kambi zake za kijeshi kuishambulia Iran

    Uingereza imeripotiwa kukataa ombi la Rais wa Marekani Donald Trump la kutumia kambi za kijeshi za Uingereza, ikiwa ni pamoja na kambi ya Jeshi la Wanahewa la Diego Garcia katika Visiwa vya Chagos vinavyodhibitiwa na Uingereza katika Bahari ya Hindi, kwa ajili ya mashambulizi yanayoweza kutokea dhidi ya Iran.

    Wakati huo huo serikali ya mrengo wa kushoto mjini Madrid Jumatatu ilisema kuwa imekanusha matumizi ya kambi zake za kijeshi kwa vikosi vya Marekani vilivyohusika katika shambulizi dhidi ya Iran, ikiwa ni pamoja na ndege kuu za kujaza mafuta ambazo ziliondoka Uhispania kuelekea nchi nyingine siku ya Jumapili.

  6. Korea Kusini yasitisha biashara kwa muda baada ya bei ya hisa kuporomoka

    Masoko ya hisa kote barani Asia yameathiriwa na mzozo unaoendelea kati ya Marekani, Israel na Iran, lakini Korea Kusini ina ndio iliyoathiriwa vibaya zaidi.

    Korea Kusini Ililazimika kusitisha biasha kwa dakika 20 Jumatano as baada ya hisa bei ya kushuka kwa zaidi ya 8% kutokana na kushuka thamani kwa sarafu yake ya Kospi.

    Biashara imeanza tena lakini thamani ya Kospi iko chini zaidi ya 10%.

    Kusitishwa kwa biashara ni sehemu ya utaratibu unaofahamika kama circuit breaker au kikatiza mzunguko wa mauzo, iliyoundwa ili kuzuia kuyumba kwa soko ikiwa bei za hisa zitashuka kwa kiasi kikubwa.

    Hii ni mara ya kwanza hali hiyo imeshuhudiwa nchini tangu Agosti 2024.

    Biashara itasitishwa tena ikiwa bei za hisa zitashuka kwa 15%.

    Seoul ni muagizaji mkubwa wa mafuta ya Mashariki ya Kati na uchumi wake unaotegemea mauzo ya nje uko katika hatari kubwa yakuathiriwa na mzozo wa kikanda ambao unaweza kulemaza shughuki za usafirishaji.

    Soma pia:

  7. Uingereza yakodi ndege kuwaondoa raia wake nchini Oman

    Taarifa tulizopokea muda mfupi uliopita zinasema kuwa serikali ya Uingereza imekodisha ndege ya kibiashara kutoka Oman kuwasaidia raia wa Uingereza wanaotaka kuondoka Mashariki ya Kati.

    Ndege inatarajiwa kuondoka mjini Muscat leotarehe 4 Machi saa tano usiku saa za ndani (19:00 GMT), na itawapa kipaumbele watu walio hatarini zaidi.

    Raia wa Uingereza na wenzi wao na watoto wao walio chini ya umri wa miaka 18, wataruhusiwa kutumia ndege hiyo.

    Ofisi ya Mambo ya Nje inasema raia wa Uingereza ambao wamejiandikisha kuwa wapo UAE na kwa sasa wako Oman wanapaswa kujaza fomu maalumu haraka iwezekanavyo, ikiwa wangependa kuabiri ndege hiyo.

    Ofisi hiyo aidha imeomba watu kutofika uwanja wa ndege hadi watakapofahamishwa na Ofisi ya Mambo ya nje.

    Inaongeza kuwa itaendelea kushirikiana na mashirika ya ndege kutafuta njia zaidi za kurejea watu nyumbani Uingereza.

    Usafiri wa anga katika Mashariki ya Kati umetatizika sana tangu Jumamosi, wakati Marekani na Israel zilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran na kumuua Kiongozi Mkuu Ayatollah Ali Khamenei.

    Iran tangu imelipiza kisasi kwa kufanya mashambulizi katika kanda nzima, yakilenga kambi za kijeshi vya Marekani zilizopo katika mataifa Kiarabu, lakini pia miundombinu ya kiraia na nishati.

    Maelfu ya safari za ndege zimesitishwa, raia wengi wa Uingereza ambao wangependa kuondoka wamekwama katika eneo hilo.

  8. Qatar yawakamata watu 10 wanaoshukiwa kuwa majasusi wa Iran

    Shirika la habari la serikali ya Qatar linasema kuwa vikosi vya usalama vya Qatar " vilifanikiwa kukamata seli mbili" zinazofanya kazi katika Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) mapema Jumatano.

    Saba kati ya washukiwa hao "walipewa jukumu la kijasusi kukusanya taarifa za kijasusi kuhusu miundombinu muhimu ya taifa na kijeshi," shirika la habari linasema.

    Wengine watatu pia waliotumiwa kwa ujasusi "wana uzoefu wa kutumia ndege zisizo na rubani", inaongeza.

    "Wakati wa uchunguzi, washukiwa walikiri uhusiano wao na Walinzi wa Mapinduzi ya Irani na kusema kwamba walikuwa wamepewa jukumu la kufanya ujasusi na uasi," shirika la habari la serikali linasema.

    Maelezo zaidi:

  9. Israel yaanzisha wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran, IDF inasema

    Jeshi la Ulinzi la Israel linasema kuwa limeanza wimbi jipya la mashambulizi dhidi ya Iran.

    "IDF imeanza mashambulizi yanayolenga maeneo ya kufyatulia makombora ya utawala wa kigaidi wa Iran, mifumo ya ulinzi wa anga na miundombinu ya ziada," Jeshi la Ulinzi la Israeli liliandika kwenye mtandao wa wa kijamii wa Telegram.

    Huku hayo yakijiri Jeshi la Marekani limewatambua wanajeshi wanne wa kwanza wa Kimarekani waliouawa katika mashambulizi ya Iran.

    Wanajeshi hao wa Akiba wa Jeshi la Marekani, kutoka Kamandi ya 103 ya Ulinzi ya Des Moines, Iowa, ni pamajo na:

    • Kapteni Cody A. Khork, 35, wa Winter Haven, Florida
    • Sajenti Daraja la kwanza Noah L. Tietjens, 42, wa Bellevue, Nebraska
    • Sajenti wa Daraja la kwanza Nicole M. Amor, 39, wa White Bear Lake, Minnesota
    • Sajenti Declan J. Coady, 20, wa West Des Moines, Iowa

    Wengine wawili waliuawa katika shambulizi la Iran dhidi ya kituo cha kijeshi huko Kuwait siku ya Jumapili, lakini bado hawajatambuliwa.

    Siku ya Jumatatu Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth alisema kwamba ngome ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait ilipigwa wakati shambulio la kulipiza kisasi lililofanywa na Iran.

    Vifo hivyo sita pekee ndivyo vilivyothibitishwa na jeshi la Marekani tangu lilipoanzisha mashambulizi dhidi ya Iran kwa ushikiano na Israel.

    Unaweza kusoma:

  10. Natumai hujambo.