Putin atia saini amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi wa Urusi
Idadi hiyo, ambayo ni pamoja na ongezeko la 137,000 katika idadi ya wanajeshi hadi milioni 1.15, inaanza kutumika Januari 1
Moja kwa moja
Vita vya Ukraine: Shambulio la Urusi la kituo cha leri lawauwa 25, na kuwajeruhi makumi kadhaa

Chanzo cha picha, Reuters
Maelezo ya picha, Nyumba ya makazi pia liharibiwa katika shambulio la Chaplyne Shambulio la kombora la Urusi kwenye kituo cha leri limewauwa watu 25, imesema Ukrain, katika siku ya maadhimisho ya miezi sita tangu uvamizi wa Ukraine uanze.
Waathiriwa watano wa shambulio katika mji wa mashariki wa Chaplyne walichomwa moto hadi kufa ndani ya gari, walisema maafisa. Wavulana wawili wenye umri wa miaka sit ana 11 pia waliuawa.
Rais Volodymyr Zelensky aliripoti shambulio hilo wakati wa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa . Baba mweney umri wa miaka 31 alijeruhiwa.
Urusi inasema ilipiga ndege ya kijeshi na kuwauwa mamia ya wanajeshi wa Ukraine.
"Kutokana na kupigwa moja kwa moja kwa kombora la masafa aina ya Iskander kwenye treni ya kijeshi iliyokuwa katika kituo cha leri cha Chaplyne katika jimbo la Dnipropetrovsk , zaidi ya wanajeshi 200 wa kikosi cha akiba cha jeshi la Ukraine na vitengo kumi vya vifaa viliharibiwa, vilipokuwa vikielekea katika maeneo yao ya mapigano ya Donbas," wizara yake ya ulinzi ilisema katika taarifa
Ukraine haijataja lolote kuhusiana na vifo vya wanajeshi katika shambulio hilo.
Vita vya Ukraine: Mkimbizi wa Ukraine aliyegeuza dini baada ya kupewa hifadhi msikitini

Chanzo cha picha, Getty Images
Mkimbizi kutoka Ukraine aligeuza sini yake na kuwa Muislamu baada ya kupewa hifadhi msikitini.
Mwanaume huyo, ambaye jina lake ni Voronko Urko, alikimbilia msikitini baada ya shambulio la vikosi vya Urusi kuharibu nyumba yake iliyokuwa katika mji wa Kharkiv nchini Ukraine.
Kabla ya shambulio kuharibu nyumba yake, Voronko, alikuwa anaishi na mke wake na watoto wao wawili.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hatahivyo, kuharibiwa kwa nyumba yake kumemfanya asiendelee kuishi na familia yake.
Alilazimika usiku kulala katika msikiti wa Imam Muhammad Ali, na baada ya muda, alikuwa Muislamu.
Elly Tumwine :Rais Museveni amkumbuka jenerali aliyefariki wa vita vya msituni nchini Uganda

Chanzo cha picha, UPDF
Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametoa risala za rambi rambi kwa Jenerali Elly Tumwine, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 68, akisema "alifyatua risasi ya kwanza" katika mapinduzi yaliyomuingiza madarakani.
Alikuwa akizungumzia uvamizi wa waasi wa National Resistance Army (NRA) kwenye kambi ya kijeshi mwaka wa 1981.
Taarifa ya jeshi iliongeza kuwa Jenerali Tumwine, ambaye alijiunga na upinzani mwaka 1979, pia alipoteza jicho lake katika vita wakati wa vita vya msituni vilivyodumu kwa miaka mitano na kusifu "mchango wake katika mapinduzi". Mara nyingi alipigwa picha akiwa amevaa miwani yarangi nyeusi.
Jenerali huyo, ambaye alikuwa na saratani ya mapafu, alisafirishwa kwa ndege hadi hospitali katika mji mkuu wa Kenya Nairobi wiki mbili zilizopita.
Katika jumbe za Twitter , rais huyo mwenye umri wa miaka 77 alimzungumziajenerali huyo kama "kada aliyejitolea na kufanya kazi kwa bidii".
"Nilimfundisha katika Shule ya Msingi ya Burunga mnamo 1967, baada ya A-level, kama mwalimu mwanafunzi, kabla ya kwenda chuo kikuu, baadaye mwaka huo," alikumbuka.
Jenerali Tumwine alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Makerere na kupata digrii ya sanaa mnamo 1977, kisha akaacha kazi ya ualimu na kujiunga na upinzani na wengine 9,000 walipata mafunzo ya kijeshi katika nchi jirani ya Tanzania. Aliendelea kuongoza jeshi la waasi mwaka 1984 kwa miaka kadhaa.
Ameshika nyadhifa kadhaa za juu serikalini pamoja na kuwa mbunge wa muda mrefu anayewakilisha jeshi. Kwa miaka mingi pia aliongoza kamati iliyoamua ni nani angepokea medali za shujaa wa kitaifa.
Mkongwe huyo wa vita vya msituni pia alikuwa msanii na mwanamuziki aliyependa kutunga nyimbo za Runyankore, lugha yake ya mama.
Lakini alijulikana sana kwa kuwa mzungumzaji wa moja kwa moja - na wakati mwingine alizua utata.
Aliwahi kuliambia jopo la uchunguzi wa bunge kuhusu madai ya kuteswa kwa washukiwa wanaoshikiliwa katika nyumba za ulinzi na vikosi vya usalama: "Kuna maeneo ambayo kwa sababu za kiusalama kamati hii haiwezi kuyatembelea."
Akiwa waziri wa usalama mwaka 2020 baada ya maandamano mabaya ya kampeni za uchaguzi, alisema vikosi vya jeshi "vilikuwa na haki ya kukupiga risasi na kukuua, ikiwa utafikia kiwango fulani cha vurugu".
Hata alipoondolewa kwenye baraza la mawaziri mwaka 2021, alizungumza waziwazi - akimshauri Rais Museveni, ambaye ndio kwanza ameanza muhula wake wa sita madarakani, kujiandaa kuondoka madarakani.
"Ninasalia mpigania uhuru na kumstaajabia na kumshukuru kama mwalimu wangu, mshauri wangu, kiongozi wangu na shujaa wangu. Nitaendelea kumpa msaada na ushauri wangu wa dhati.
"Na kwangu sasa, ushauri bora tunaoweza kumpa ni kujiandaa kwa mpito mzuri ili tuhakikishe utulivu na amani ya muda mrefu kwa siku zijazo."
Alikuwa mmoja wa kizazi kinachopungua cha maveterani wa vita vya msituni ambao vijana wengi wa Uganda wanahisi wameshikilia nchi na kuwakumbusha mara kwa mara juu ya mapambano ya ukombozi.
Juu ya tangazo la kifo chake, wengi kwenye mitandao ya kijamii walijibu kwa maoni ya kikatili.
Uganda yajiandaa kudhibiti Ebola, baada ya kisa kimoja kupatikana DRC

Chanzo cha picha, Getty Images
Uganda imeweka wilaya 21 jirani na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo chini ya hali ya tahadhari na uchunguzi wa kina kwenye vituo vya mpaka baada ya mwanamke mwenye umri wa miaka 46 kufariki kutokana na maradhi ya Ebola katika Kivu Kaskazini.
Kamishna anayehusika na milipuko katika wizara ya afya Dokta Allan Muruta anasema uchunguzi kwa ajili ya homa ya Ebola kwa sasa unafanyika katika mipaka iliyobainishwa lakini utaongezwa iwapo vitisho vya mlipuko vitaongeza.
Pia unaangaliwa uwezekano wa kuwapatia chanjo wahudumu wa afya wa maeneo hayo.
Uganda iliwahi kuwa na idadi ya watu walioambukia virusi vya Ebola tangu mlipuko huo ulipotokea mwaka 2000.
Mlipuko uliokuwa hatari ulikuwa katika mwaka 2000 ambapo watu zaidi ya 400 walisajiriwa kupata maambukizi, na 224 kati yao walifariki.
Mlipuko wa hivi karibuni wa 2019 ulitokea wakati nchi hiyo ilipopokea kisa kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika wilaya ya kaskazini ya Kasese.
Nchi hiyo pia ilikuwa na mlipuko wa virusi vya vinavyofanana na vile vya Marburg na homa ya Crimea.
Hakuna kisa kipya cha ebola kilichopatikana kwa sasa nchini Uganda.
Putin atia saini amri ya kuongeza idadi ya wanajeshi wa Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Rais wa Urusi Vladimir Putin alitia saini amri ya kuongeza ukubwa wa wanajeshi wa Urusi kutoka milioni 1.9 hadi 2.04, shirika la habari la RIA Novosti liliripoti.
Idadi hiyo, ambayo ni pamoja na ongezeko la 137,000 katika idadi ya wanajeshi hadi milioni 1.15, inaanza kutumika Januari 1.
Hatua hiyo inaniri baada ya Wizara ya ulinzi ya Urusi kusema iliwaua wanajeshi wa Ukraine katika shambulio la kituo cha reli katikati mwa Ukraine ambalo Kyiv ilisema lilisababisha vifo vya watu 25 wakiwemo watoto.
"Kutokana na kushambuliwa moja kwa moja na kombora la Iskander kwenye treni ya kijeshi kwenye kituo cha reli cha Chaplyne ... zaidi ya wanajeshi 200 wa hifadhi ya Kikosi cha Wanajeshi wa Ukraine na vitengo 10 vya vifaa vya kijeshi vilivyokuwa njiani kuelekea eneo la mapigano huko Donbas viliharibiwa, ” wizara ilisema katika taarifa yake ya kila siku.
Moscow pia ilisema kuwa imeharibu ndege nane za kivita za Ukraine katika mashambulizi dhidi ya vituo vya anga katika mikoa ya Poltava na Dnipropetrovsk nchini Ukraine. Hiyo itakuwa moja ya hasara kubwa zaidi kwa jeshi la anga la Ukraine katika wiki za hivi karibuni.
Unaweza pia kusoma
Vilabu vya Ligi ya Primia vyavunja rekodi ya matumizi ya fedha ya usajili wa majira ya joto

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Erling Haaland na Darwin Nunez Vilabu vya Ligi ya Primia vimevunja rekodi yao ya matumizi ya fedha katika dirisha la usajili la majira ya kiangazi, kwa mujibu wa uchambuzi kutoka kwa kampuni ya fedha ya Deloitte.
Deloitte ina klabu zimetumia takriban pauni bilioni 1.5 kufikia sasa msimu huu wa joto, kiwango ambacho kinazidi rekodi ya awali ya pauni bilioni 1.4 mwaka 2017.
Imesalia wiki moja kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa 23:00 BST Septemba mosi.
Matumizi ya wakati sawia na huu mwaka 2021 yalikuwa pauni milioni 895 na imeongezeka na kufikia pauni bilioni 1.1.
" Viwango vya rekodi vya matumizi ambavyo tumeona kwenye dirisha hili la usajili wa majira ya joto hadi sasa vinatoa ishara kwamba mifumo ya biashara ya vilabu vya Ligi Kuu inaongezeka tena baada ya Janga la Corona, "alisema Chris Wood, mkurugenzi msaidizi katika Shirika ;a Biashara yaa Michezo ya Deloitte.
Baadhi ya uhamisho mkubwa umeifanya Liverpool kumsajili mshambuliaji wa Uruguay, Darwin Nunez kutoka Benfica kwa dau la awali la pauni milioni 64 katika dili ambalo linaweza kupanda hadi pauni milioni 85, huku Manchester United wakimnunua kiungo wa kati wa Brazil, Casemiro kwa dau la awali la pauni milioni 60 kutoka Real Madrid kwa mkataba wa thamani ya pauni milioni 70 katika uhamisho ambao unatarajiwa kukamilika hivi karibuni.
Tottenham Hotspur ilimsajili mshambuliaji wa Brazil Richarlison kutoka Everton kwa uhamisho unaoaminika kuwa wa thamani ya £60m na Manchester City wakapata kuwasili kwa mshambuliaji wa Norway Erling Haaland kwa £51.2m kutoka Borussia Dortmund.
Mshambulizi wa Uingereza Raheem Sterling alijiunga na Chelsea kwa mkataba wa pauni milioni 50, huku The Blues pia wakamsajili beki wa Uhispania Marc Cucurellafrom Brighton katika uhamisho wa zaidi ya pauni milioni 60.
Wachezaji 14 hadi sasa wamesajiliwa na vilabu vya Ligi ya Primia kwa ada iliyoripotiwa kuwa zaidi ya £30m, ambayo ni sawa na wanane wakati wa dirisha la uhamisho wa majira ya joto 2021.
Soma:
Mgonjwa wa Zimbabwe akemewa kwa kutafuta huduma ya upasuaji Afrika Kusini

Chanzo cha picha, Mamlaka ya Mkoa wa Limpopo
Maelezo ya picha, Phophi Ramathuba anasema wageni wanavamia huduma za afya za Limpopo. Idara ya afya nchini Afrika Kusini imeanzisha uchunguzi kuhusu kauli iliyotolewa na waziri wa afya wa mkoa huo kwa mgonjwa wa Zimbabwe aliyekuwa akipatiwa matibabu.
Katika kanda ya video iliyovuma sana mtandaoni, Dkt Phophi Ramathuba anaonekana akimkemea mgonjwa wa Zimbabwe ambaye hakuwa na vibali vya kufanyiwa upasuaji katika hospitali moja katika mkoa wa Limpopo nchini Afrika Kusini.
Maoni yake yamelenga kuwalaumu raia wa kigeni kwa kuchangia mfumo mbaya wa afya nchini.
Dk Ramathuba alimwambia mgonjwa kwamba Zimbabwe inapaswa kuwajibika kwa masuala yake ya afya na si Afrika Kusini.
Aliongeza kuwa Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa hakuchangia bajeti ya afya ya Afrika Kusini.
Ruka X ujumbeRuhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya njeMkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe
Vyama vya upinzani vinadai kujiuzulu kwa afisa huyo na vilisema anapaswa kukemewa kwa kumdhalilisha mgonjwa.
Hata hivyo, Dk Ramathuba amesema anasimama na maoni yake, akiongeza kuwa jimbo la Limpopo, ambalo liko mpakani na Zimbabwe, lina "mmiminiko wa raia wa kigeni ambao wanazonga mfumo wa afya wa mkoa huo na kusababisha madaktari kufanya kazi chini ya shinikizo".
Pia alisema maoni yake hayapaswi kueleweka vibaya kama chuki dhidi ya wageni.
Mgonjwa huyo, alisema, alimwambia kwamba alihusika katika ajali ya barabarani katika mji mkuu wa Zimbabwe, Harare, na alishauriwa kuvuka mpaka kutafuta matibabu.
Ufaransa yazua ghadhabu kuhusu hatua ya Uingereza kuelekeza maji taka baharini

Chanzo cha picha, Getty Images
Uingereza inatishia afya na viumbe vya baharini katika ufuo wa Ufaransa kwa kuruhusu maji taka katika eneo la Channel na Bahari ya Kaskazini, wanasema wabunge watatu wa Euro.
Tahadhari ya uchafuzi wa mazingira imetolewa kwa karibu fukwe 50 nchini Uingereza na Wales, baada ya mvua kubwa iliyosababisha mafuriko ya maji taka kuelekezwa kwenye mito na baharini.
Wabunge wa Ufaransa wanaishutumu Uingereza kwa kupuuza ahadi za mazingira na kuhatarisha maisha ya baharini na uvuvi.
Kampuni za maji za Uingereza zimesema zinawekeza katika kutatua tatizo hilo.
Tangu kuondoka kwake kutoka Umoja wa Ulaya, Uingereza ilikuwa imepuuza ahadi zake za mazingira, wabunge hao walisema katika barua inayotaka hatua za kisheria au kisiasa kutoka kwa Tume ya Ulaya.
Msemaji wa serikali ya Uingereza alisema madai yao "sio kweli".
Licha ya kutofungwa tena na sheria za EU, Uingereza bado ilikuwa imetia saini mikataba ya Umoja wa Mataifa kuhusu kulinda maji ya pamoja, wabunge hao walidai.
Wabunge hao watatu wote ni wa chama cha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kinachounga mkono EU, En Marche. Mmoja wao, Pierre Karleskind, ni mwenyekiti wa kamati ya uvuvi ya Bunge la Ulaya.
Ethiopia na waasi waTigray wahimizwa kurejesha mapatano

Chanzo cha picha, Getty Images
Maelezo ya picha, Vikosi vya waasi vilikubali kusitisha mapigano mwezi Machi ili kuruhusu utoaji wa misaada Mapigano makali yamezuka kaskazini mwa Ethiopia kati ya vikosi vya serikali na eneo la Tigrayan, na kuvunja makubaliano ya miezi mitano ya kuwezesha usambazi wa huduma za kibinadamu.
Usuluhishi huo ulikubaliwa kuruhusu msaada kuingia katika eneo la Tigray - ambapo maelfu wamekufa katika vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe na mamilioni wanahitaji vifaa vya kimsingi.
Watu katika mji wa karibu waliiambia BBC kuwa wamesikia silaha nzito na kuona vitengo vya jeshi la serikali vikiwasili.
Pande zote mbili zimelaumiana kwa kuzuka upya kwa mapigano.
Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa na Marekani zimewataka wanajeshi wa Ethiopia na vikosi vya eneo la Tigrayan kurejesha mapatano ya kibinadamu baada ya mapigano mapya kuzuka kwa mara ya kwanza katika miezi kadhaa.
Kuna hofu kwamba mapigano mapya yanaweza kuzuia juhudi za kufikia mamilioni ya watu katika eneo la Tigray ambao wanahitaji sana msaada.
Wakati huo huo Shirika la Mpango wa Chakula Duniani limesema vikosi vya Tigray vimepora lita milioni moja za mafuta kutoka kwenye maghala yake katika mji mkuu wa eneo hilo, Mekelle, ambayo yalikusudiwa kutumika kutoa msaada.
Hata hivyo, vikosi vya Tigray havijajibu shutuma hizo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema ameshangazwa na matukio hayo, huku Marekani ikieleza wasiwasi wake kwamba mapigano mapya yanaweza kuhatarisha maendeleo yaliyofikiwa katika kipindi cha miezi mitano iliyopita.
Kwa nchi ambayo tayari imegharamika pakubwa kutokana na vita vya kikatili vya wenyewe kwa wenyewe, duru nyingine ya umwagaji damu inaweza tu kuwa habari mbaya.
Soma zaidi:
Magavana waanza kuapishwa katika kaunti mbalimbali Kenya

Maelezo ya picha, Fatuma Achani gavana mteule kaunti ya Kwale Mahakama imeanza kuwaapisha magavana 45 katika kaunti zao walikochaguliwa kwa mujibu wa masharti ya Sheria ya Kuchukua Ofisi ya Ugavana.
Sheria hiyo inawataka magavana wateule kuapishwa Alhamisi ya kwanza baada ya siku ya kumi kufuatia tamko la matokeo ya mwisho ya Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC).
Na kati ya watakaoapishwa ni magavana saba wanawake waliochaguliwa kwenye uchaguzi wa Agosti 9.
Idadi hii imeongezeka kidogo ikilinganishwa na 2017 ambapo ni wanawake watatu pekee walichaguliwa kama magavana.
Ulikuwa ushindi ulioweka rekodi kwa wanawake kwani uchaguzi huo umeleta wimbi jipya la viongozi wanawake kwenye viti vya kuchaguliwa na wapiga kura.
Jaji Mkuu wa kwanza mwanamke nchini Kenya Martha Koome amewateua majaji 45 watakaosimamia hafla hiyo ya kuapishwa kwa magavana wanaoingia kuhudumu kwa muhula wa miaka mitano.
Kaunti zote zilichagua magavana isipokuwa mbili ambapo uchaguzi uliahirishwa kutokana na mchanganyiko wa makaratasi.
Katika uchaguzi huo, zaidi ya wanawake 20 waligombea nyadhifa za ugavana.
Tangu kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa ugatuzi mwaka 2013, ni wanawake watatu pekee ndio walikuwa wamechaguliwa katika kile kinachochukuliwa kuwa kiti cha pili chenye nguvu za kisiasa nchini baada ya urais.
Licha ya wanawake wanaounda karibu nusu ya wapiga kura waliojiandikisha, ni viongozi wachache sana wa kike wanaoshikilia nyadhifa za kuchaguliwa.
Soma zaidi:
Rubani wa Uingereza-Ubelgiji, 17, anakuwa mdogo zaidi duniani kuendesha ndege peke yake

Chanzo cha picha, REUTERS/STOYAN NENOV
Maelezo ya picha, Mack Rutherford, 17, akisherehekea ndani ya ndege yake ya Shark baada ya kutua karibu na Sofia huko Bulgaria siku ya Jumatano. Rubani kijana amekuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kuendesha ndege peke yake duniani kote kwa kutumia ndege ndogo.
Mack Rutherford, 17, alitua Sofia huko Bulgaria, baada ya safari ya miezi mitano katika nchi 52.
Wakiwa njiani, Mack, ambaye alizaliwa na wazazi Waingereza lakini amekulia nchini Ubelgiji, alikumbana na dhoruba za mchanga huko Sudan na kulala usiku kucha kwenye kisiwa cha Pasifiki kisichokaliwa na watu.
Dada yake mkubwa Zara ndiye mwanamke mdogo zaidi kuendesha ndege peke yake duniani kote.
Alimaliza safari yake mwenyewe Januari mwaka huu na kufichua kwamba ‘’alimpa ushauri juu ya njia’’ alipokuwa akisafiri hadi Sofia kumsalimia Mack alipokuwa akirejea mahali alipoanzia.
Awali, rubani aliyekuwa na rekodi ya kuendesha ndege peke yake alikuwa rubani Muingereza Travis Ludlow, ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 na siku 150 alipomaliza safari yake mwaka jana.

Chanzo cha picha, REUTERS/STOYAN NENOV
Mjane wa Kobe Bryant alipwa fidia kutokana na kuvuja kwa picha za ajali ya mumewe na binti yake

Chanzo cha picha, Getty Images
Mjane wa Kobe Bryant amelipwa fidia ya $16m (£13.6m) kama kutokana na kuvuja kwa picha za ajali ya helikopta iliyoua nyota huyo wa mpira wa kikapu wa Marekani na bintiye mwaka wa 2020.
Vanessa Bryant, 40, alisema alipatwa na hofu baada ya kubaini picha zilizopigwa na polisi wa Kaunti ya Los Angeles na maafisa wa zima moto zimesambazwa.
Mahakama ilisema kuwa kaunti lazima imlipe Bi Bryant kwa usumbufu iliyompatia.
Mshtaki mwenza Christopher Chester atalipwa $15m. Mume wa Bi Bryant Kobe Bryant, 41, binti Gianna, 13, na marafiki sita wa familia walikufa wakati helikopta yao ilipoanguka California mnamo Januari 2020.
Bw Chester alipoteza mkewe Sarah na binti Payton katika ajali hiyo.
Ripoti ya Los Angeles Times inayodai wafanyakazi wa kaunti walipiga picha kwenye eneo la ajali na kuwasambazi picha watu wengine imewakasirisha wanafamilia wa waathiriwa.
Mkuu wa Polisi aliyeshutumiwa kutochukua hatua stahiki kwa tukio la kuuawa kwa wanafunzi 19 afutwa kazi Marekani

Chanzo cha picha, Reuters
Mkuu wa polisi anayeshutumiwa kutochukua hatua stahiki kwa mauaji ya watoto 19 wa shule na walimu wawili huko Uvalde, Texas, amefutwa kazi.
Bodi ya shule ya eneo hilo ilipiga kura kwa kauli moja kumfuta kazi Pete Arredondo, ambaye alikuwa likizo tangu Juni.Mawakili wake walisema katika taarifa yao iliyoandikwa kwamba alikuwa hajui mtu yeyote alikuwa ndani ya madarasa na mfyatuaji risasi.
Ufyatuaji risasi huo ulikuja miezi mitatu kabla ya shambulio hilo na wiki mbili kabla ya muhula mpya wa shule kuanza.
Shambulizi katika Shule ya Msingi ya Robb mnamo tarehe 24 Mei lilikuwa tukio baya zaidi la ufyatuaji risasi katika shule nchini Marekani katika kipindi cha takribani muongo mmoja.
Wazazi na jamaa wengi wameonesha kukerwa sana na mwitikio wa polisi na kumekuwa na shinikizo la kutaka vyombo vya sheria kuwajibishwa.
Bw Arredondo alikosolewa vikali kwa kuchelewa kwa maafisa kwa dakika 77 kumkabili kijana huyo mwenye bunduki, na ndiye afisa wa kwanza kufutwa kazi.Shangwe zilisikika katika ukumbi huku bodi ya wadhamini wa shule ya Uvalde ikiwasilisha hoja ya kumwondoa kwenye wadhifa wake mara moja.
