Mzozo kuhusu shamba la Osama Pakistan

Bin Laden aliuawa kwenye shambulio lililotekelezwa na wanajeshi wa Marekani katika shamba hilo Mei 2011.

Maafisa wa jiji wanataka kugeuza shamba hilo kuwa uwanja wa kuchezea watoto.

Hata hivyo, jeshi linataka kipande hicho cha ardhi kigeuzwe na kuwa makaburi.
Kuna baadhi ya wakazi wanaotaka shamba hilo litumiwe kujenga shule ya wasichana huku baadhi ya wanajeshi nao wakitaka ligeuzwe kuwa bustani ya burudani na kutumiwa kuzalisha mapato kwa serikali.
- <link type="page"><caption> Kanda za sauti ya Osama zasikika</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/medianuai/2015/08/150817_osama_kanda" platform="highweb"/></link>
- <link type="page"><caption> Mkwewe Bin Laden maisha jela</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2014/09/140924_binladen_mkwe" platform="highweb"/></link>
- <link type="page"><caption> Osama aliacha dola milioni 29 kufadhili Jihad</caption><url href="http://www.bbc.com/swahili/habari/2016/03/160301_osama_inheritance_to_fund_al_qaeda" platform="highweb"/></link>
Huku mzozo kuhusu pande hizo mbili ukiendelea, jeshi mnamo Jumatano lilifika na kujenga ua, jambo lililoshangaza maafisa wa baraza la jiji.
Bin Laden aliishi kwenye jumba la ghorofa tatu lililo kwenye shamba hilo bila kujulikana kwa miaka kadha. Jumba hilo lilikuwa limezungushwa ua mrefu.

Chanzo cha picha, Reuters
Shamba hilo, lenye ukubwa wa mita 3,530 mraba na linalokadiriwa kuwa na thamani ya $285,000 (£218,000), limekuwa wazi tangu wakati huo.
Baada ya kifo cha Bin Laden, shamba hilo lilikabidhiwa serikali ya jimbo la Khyber Pakhtunkhwa (KP) pambayo ilibomoa jumba hilo pamoja na ua ili kuzuia eneo hilo lisigeuzwe na wapiganaji wa kijihadi kuwa eneo 'takatifu'.












