Hatari ya kuosha kuku: Fahamu namna ya kuzuia sumu kwenye chakula

Chanzo cha picha, Getty Images
Watu wengi wanaweza kufikiria kuwa kuosha kuku ni jambo zuri. Hakuna kitu zaidi ya ukweli.
Kuosha kuku mbichi huongeza hatari ya kupata sumu kwenye chakula.
Shirika la Viwango vya Chakula la Uingereza (FSA) limeonya kwa muda mrefu kuwa kuosha kuku kabla ya kupika huongeza hatari ya kueneza bakteria ya 'campylobacter' kwenye mikono, sehemu za kazi, nguo na vyombo vya kupikia na hata jikoni kwa kumwaga matone ya maji.
Hata hivyo, watu wengi wanaendelea kufanya makosa hayo hayo. Unapoweka kuku chini ya bomba na kua, ni rahisi maji kuruka na kusambaa kwenye vitu vilivyoko karibu.
Kwa njia hii, bakteria wanaweza kuishia kupita ndani ya mwili wako, kwa mfano, kisu ambacho tulikuwa nacho karibu na karo au sinki jikoni.
Sio kila mtu anafikiria juu ya hili.
Kulingana na FSA, 44% ya watu nchini Uingereza huosha kuku kabla ya kupika.
Sababu zilizotajwa zaidi za kufanya hivyo zilikuwa ni kuondoa uchafu au vijidudu, au kwa sababu walikuwa wakifanya hivyo kila mara.
Campylobacter enteritis ni moja ya bakteria wanaosababisha sumu ya chakula na hatimae mtu kupata maambukizi ya matumbo.
Hasa wakati wa kusafiri, ambayo pia imejulikana kusababisha kuhara kwa wasafiri.
Maambukizi mara nyingi husababishwa na ulaji wa kuku mbichi, mboga ambazo hazijaiva vizuri au maziwa ambayo hayajaondolewa vijidudu.

Bakteria hii huenezwa kwa kula au kunywa chakula kilichoambukizwa na, kulingana na tovuti ya MedlinePlus, inaweza kusababisha kuhara, maumivu ya tumbo, homa, kichefuchefu na kutapika.
Matokeo ya maambukizi
Watu wengi ni wagonjwa kwa siku chache tu, lakini inaweza kusababisha matatizo ya muda mrefu ya afya. Ugonjwa wa utumbo kutatiza kweli ambao hushambulia mfumo wa neva wa pembeni, unaweza kutokana na kuambukizwa na bakteria hii.
Inaweza pia kusababisha kifo.
Watu walio hatarini zaidi ni watoto na watu wazima.
Kwa kawaida matibabu ya maambukizi na bakteria hii ni pamoja na kunywa maji mengi. Kula sehemu ndogo za chakula siku nzima, badala ya kiasi kikubwa wakati wa kifungua kinywa, chakula cha mchana, na chakula cha jioni.
Kula chakula chenye wingi wa potasiamu, pamoja na kula vyakula vya chumvi.
Hata hivyo, kila hali ya ugonjwa huu inaweza kutofautiana, hivyo daima inashauriwa kutembelea daktari.














