Vita ya Ukraine : Ukraine Urusi na Putin, Ni kwanini Donbass inamuhutaji Putin?

Chanzo cha picha, Getty Images
Urusi, ambayo bado haijauteka mji mkuu wa Ukraine, Kiev, sasa inaelekeza umakini wake kwa Donbass. Imefanya mashambulio makubwa dhidi ya jimbo hilo lililojitenga la Ukraine. Marekani tayari ina hofu kubwa juu ya mwelekeo huu mpya wa vikosi vya Urusi . Kulingana na Washington,hii inaweza kuashiria muendelezo wa mzozo wa Ukraine. Lakini je ni kwanini Donbass inamuhitaji Putin?
Vikosi vya Urusi tayari vimekwisha sababisha janga la kibinadamu katika maeneo ya mashariki mwa Ukraine, vikiuangamiza mji wa Mariupol, lakini vimeshindwa kulishinda jeshi la Ukraine. Onyo la mashambulio mapya katika mashariki, limetolewa na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliahidi, "Tutapigana kwa ajili ya kila inchi ya ardhi yetu."
Ukraine tayari imekwisha wapeleka wanajeshi wake wenye mafunzo bora zaidi katika eneo la mashariki baada ya miaka minane ya mapigano na wapiganaji waliojitenga wanaoungwa mkono na Urusi. Wamepata majeruhi wengi, lakini wakebakia kuwa tatizo kuu kwa uvamizi wa wa jeshi la uvamizi la Urusi.
Donbas ya Ukraine ni nini?
Wakati Rais Putin anapozungumzia kuhusu Donbass, anamaanisha jimbo la zamani la Ukraine la makaa ya mawe na chuma. Hatahivyo, anamaanisha majimbo mawili makubwa zaidi ya mashariki yaani Luhansk na Donetsk, yanayotoka kuanzia kusini mwa Mauripol hadi kwenye mpaka wa kaskazini.
"Swala kuu ni kwamba Kremlin inafahamu kuwa ina sehemu ya wazungumzaji wa lugha ya Kirusi na inaiangalia kuwa ni sehemu ya Urusi zaidi kuliko Ukraine," alisema Sam Cranney-Evans wa taasisi ya Royal United Services.
Maeneo haya kwa kawaida watu wake huzungumza Lugha ya Kirusi, lakini haiwaiungi tena mkono Urusi . "Mariupol wakati mmoja ulikuwa mmoja ya miji inayounga mkono sana Urusi katika Ukraine, na nivigumu kuelewa ni kwa jinsi gani inaweza kuwekwa katika hali kama hii na Urusi," alisema Konrad Muzika, mtaalamu wa masuala ya ulinzi na mkuu wa kampuni ya ushauri wa masuala ya ulinzi ya Rochan.

Urusi ilisema juma lililopita kwamba imechukua udhibiti wa asilimia 93 ya majimbo ya Luhansk Luhansk na asilimia 54 Donetsk .
Vikosi vya Urusi vinajaribu kuzingira jeshi la Ukraine upande wa mashariki. Waichukua udhibiti wa Kyiv, mji wa pili kwa ukubwa wa Ukraine , na Izyum, mji wa mkakati uliopo kwenye barabara iliyopo katikati ya majimbo yaliyojitenga- miji ambayo kwa sasa inatafutwa na Urusi imenusurika na miaka kadhaa ya vita tangu mwaka 2014, na hakuna siku inayopita bila kupigwa na shambulio la mauaji.
Raia sasa wanaondolewa kabla Urusi haijasonga mbele. Kiongozi wa kieneo Sergei Gaidai alisema kuwa Watoto 20 wamekwishaondolewa kutoka shule ya chekechea katika eneo la Lisichansk siku ya Alhamisi , huku raia 200 wakiwa tayari wameondolewa kwa basi katika Severodonetsk. Waliondoka kwenda magharibi mwa Ukraine mikono mitupu, Bw Gaidai alisema, lakini walikuwa hai.

Chanzo cha picha, Getty Images
Marina Agafonova, 27, aliitoroka nyumba ya familia yake katika Lisichansk mapema wiki hii.
Kulingana na yeye, mwanzoni mwa vita, vikosi vya Urusi vilivamia viungani mwa mji, lakini hivi karibuni vilipiga makombora katikati mwa mji. "Walishambulia hospitali na nyumba za watu. Hakuna umeme. Wazazi wango bado wako kule ."
Vikosi vya Ukraine bado viko kule, aliambia BBC : "Hawataruhusu Warusi kuchukua miji ."
Lengo linalofuatia la Urusi ni kuuzingira mji wa kusini wa Slovyansk, mji wenye wakazi 125,000 tambao ulitekwa na kukombolewa na vikosi vinavyoungwa mkono na Urusi katika mwaka 2014n na kukombolewa tena.
Ni kwanini Putin anataka kuiteka Donbass?
-Kiongozi wa Urusi amekuwa akirudia mara kwa mara madai yasiyo na msingi kwamba mauaji ya halaiki (genocide) yanafanyika mashariki mwa Ukraine.
Wakati vita vilipoibuka, theluthi mbili ya majimbo ya mashariki ilikuw amikononi mwa Waukraine. Yaliyosalia yaliongozwa na ikosi vya kieneo vinavyotaka kujitenga vinavyoungwa mkono na Urusi katikati ya vita ambavyo vilianza miaka minane iliyopita.
Iwapo Urusi inataka kunyakua majimbo yote makubwa, hatua inayofuatia inaweza kuwa ni kuyatenga, kama ilivyokuwa kwa Crimea mwaka 2014.
Kabla ya uvamini wa Ukraine, Rais wa Urusi Vradimir Putin alikuwa ameyatambua majimbo hayo mawili ya mashariki kama yaliyo huru kutoka kwa Ukraine. Kiongozi aliyewekwa na Urusi katika jimbo la Luhansk alikuwa tayari amekwisha zungumza kuhusu kuitisha kura ya maoni " katika siku chache zijazo," na hata kutumia kura bandia katika eneo la vita.
Hali ni ''mbaya sana'' katika Luhansk
Ingawa viongozi wanaotaka kujitenga wamevishutumu vikosi vya Waukraine kwa kufyatua makombora kwenye nyumba za raia, maisha ni ya amani zaidi katika eneo hilo. Maafisa wa utawala katika Donetsk wanasema raia 72 wameuawa tangu katikati ya mwezi Februari.

Chanzo cha picha, Getty Images
Mwanamke katika Luhansk aliiambia BBC kuwa amekuwa akiona magari mengi ya wanajeshi wa Urusi katika mji huo na sasa anaishi katika hali ya hofu na wasiwasi
"Ninaogopa sana- inatisha sana ," alisema.
Je vikosi vya Ukraine vinaweza kumudu?
Katika mwanzo wa vita, brigadia 10 za vikosi vya pamoja (UNF) mashariki kulikuwa na jeshi bora na kuwafunza wanajeshi wa Ukraine.
"Hatujui vikosi vya Ukraine ni imara kiasi gani kwa sasa ," Crane-Evans alisema.
Baada ya zaidi ya wiki tano za mapigano, vikosi vya Urusi vimekuwa vikipatwa na idadi kubwa ya majeruhi na wamewa katika hali chini kiakili.
Wanajumuisha wanaume kutoka maeneo ya wanaotaka kujitenga na wanaume kutoka katika jeshi zima la Warusi.
Hatahivyo, wamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya kusini mashariki na tumaini la kudhibiti eneo lote la mwambao kutoka Crimea hadi kwenye mpaka wa Urusi.
"Lengo kuu la Waukraine ni kusababisha majeruhi wengi iwezekanavyo upande wa Warusi. Wanatumia mikakati," alisema Konrad Muzika.
Mwanamke anayeitwa Nikita, ambaye alifanikiwa kutoroka mabomu Warusi ya mauripol, anasema anaamini jeshi la Ukraine litaweza kujibu mapigano.
"Siku moja watachukua tena miji yetu, na bataliani ya Azov haitaiachilia Mariupol," aliiambia BBC.












