Bei ya mafuta imepanda. Kwa nini OPEC haitapunguza bei?

Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Urusi inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 ya mafuta kwa siku na inasaidia OPEC kuweka bei ya juu

Wazlishaji wakubwa wa mafuta duniani wanakutana Mei 5 May, huku kukiwa na wito kutoka kote duniani kushinikiza bei ya bidhaa hiyo kupunguzwa.

Lakini wanachama wa kundi la wazalishaji wa mafuta la Opec+ - ambalo linajumuisha Urusi - halina haraka ya kufanya hivyo.

Opec+ ni nini?

Opec+ ni kundi la nchi 23 zinazouza nje mafuta ambazo hukutana kila mwezi mjini Vienna, kuamua ni kiasi gani cha mafuta ghafi kinafaa kuweka kwenye soko la dunia.

Kundi hililinajumuisha nchi 13 wanachama wa Opec (Shirika la nchi zinazouza mafuta), ambazo ni pamoja na nchi za Mashariki ya Kati na Afrika. Ilianzishwa mwaka wa 1960 kama chombo maalum, kwa lengo la kudhibiti usambazaji wa mafuta na bei yake kote duniani.

Siku hizi, mataifa ya OPEC yanazalisha 30% ya mafuta ghafi duniani, takriban mapipa milioni 28 kwa siku. Mzalishaji mkubwa wa mafuta ndani ya Opec ni Saudi Arabia - ambayo inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 kwa siku.

Mwaka 2016, wakati bei ya mafuta ilikuwa chini, OPEC iliungana na wazalishaji 10 wa mafuta wasio wa Opec kuunda Opec+.

Miongoni mwao Urusi, ambayo pia inazalisha zaidi ya mapipa milioni 10 kwa siku.

Kwa pamoja , nchi hizi zinazalisha karibu 40% ya mafuta yote ghafi dunia.

"Watengenezaji mafuta wa Opec+ wanasambaza na mahitaji ya kusawazisha soko," anasema Kate Dourian, wa Taasisi ya Nishati. "Wanaweka bei juu kwa kupunguza usambazaji wakati mahitaji ya mafuta yanapungua."

Opec+ cpia inaweza kupunguza bei kwa kuweka mafuta zaidi kwenye soka,jambo ambalo waagizaji wakubwa kama vile Marekani na Uingereza wanataka ifanye.

Bar chart showing daily crude output of leading Opec+ members

Chanzo cha picha, AFP

Je, bei ya mafuta ilipanda vipi hadi kiasi hii?

Mnamo mwaka 2020, Covid ilipoenea kote dunuani nchi ziliweka amri ya kutotoka nje, bei ya mafuta ghafi ilianguka kwa sababu ya ukosefu wa wanunuzi.

"Wazalishaji walikuwa wakiwalipa watu kuchukua mafuta kutoka kwa mikono yao, kwa sababu hawakuwa na nafasi ya kutosha ya kuhifadhi yote," anasema Bi Dourian.

Baada ya hayo, wanachama wa Opec+ walikubali kupunguza uzalishaji kwa mapipa milioni 10 kwa siku, ili kuongeza bei.

Mnamo Juni 2021, huku mahitaji ya mafuta ghafi yakianza kupata nafuu, Opec+ ilianza kuongeza usambazaji polepole, na kuweka mapipa 400,000 zaidi kwa siku kwenye masoko ya dunia. Sasa inasambaza mapipa milioni mbili na nusu ya mafuta kwa siku chini ya msimu wa jotona baridi wa 2020.

Hata hivyo, Urusi ilipovamia Ukraine, bei ya mafuta ghafi ilipanda hadi zaidi ya dola 100 kwa pipa. Hii imesababisha kupanda kwa kiasi kikubwa kwa bei ya petroli katika vituo vy akuuza mafuta.

"Wakati Opec+ ilipopunguza uzalishaji kwa pipa milioni 10 kwa siku mnamo mwezi Mei 2020, walipunguza sana," anasema David Fyfe, Mchumi Mkuu katika taasisi ya Argus Media.

"Sasa wanaongeza usambazaji kwa kasi ndogo ambayo haizingatii athari za mzozo wa Urusi na Ukraine."

Brent crude oil price graph

Kuna wasi wasi miongoni mwa wanunuaji mafuta kwamba Muungano wa Ulaya (EU) utafuata mkondo wa Marekani na na kuweka vikwazo vya kuagiza mafuta kutoka Urusi, anasema Bw Fyfe. Hivi sasa Ulaya inaagiza zaidi ya mapipa milioni mbili na nusu ya mafuta ghafi kwa siku kutoka Urusi.

"Tishio la kuwekewa vikwazo kwa mafuta ya Urusi limetikisa soko," anasema, "kwa sababu linaweza kusababisha kubanwa kwa kiasi kikubwa cha mafuta."

Kwa nini Opec+haiongezi uzalishaji?

Rais wa Marekani Joe Biden kwa mara nyingine amerai Saudi Arabia kuongeza uzalishaji wake wa mafuta, lakini bila mafanikio.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson pia aliomba Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu kuongeza uzalishaji. Ombi lake pia lilikataliwa.

Boris Johnston hakuweza kushawishi Saudi Arabia na wengine kuongeza uzalishaji wao wa mafuta

Chanzo cha picha, Gertty Images

Maelezo ya picha, Boris Johnston hakuweza kushawishi Saudi Arabia na wengine kuongeza uzalishaji wao wa mafuta

"Saudi na UAE wana uwezo wa ziada, lakini hawataki kuongeza uzalishaji wenyewe," Kate Dourian anasema. "Hawataki kuamrishwa na nchi za Magharibi.

"Wanasema pengo kati ya ugavi na mahitaji linapungua, na kwamba bei za juu za leo zinaonyesha tu hofu kwa upande wa wanunuzi wa mafuta."

Mataifa mengine ya OPEC+ yanapata ugumu wa kuongeza uzalishaji wao wa mafuta.

"Wazalishaji kama Nigeria na Angola wamekuwa wakipunguza viwango vyao vya uzalishaji kwa jumla ya mapipa milioni moja kwa siku katika mwaka uliopita," anasema David Fyfe.

"Uwekezaji ulishuka wakati wa janga hili - na uifadhi mafuta, katika baadhi ya matukio, haukufanywa vyema. Sasa, wamegundua kuwa hawawezi kuongeza uzalishaji kikamilifu."

Vladimir Putin wa Urusi na Katibu Mkuu wa Opec Mohammad Barkindo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vladimir Putin wa Urusi na Katibu Mkuu wa Opec Mohammad Barkindo: Opec+ ilipunguza usambazaji wa mafuta mwaka 2020

Msimamo wa Urusi ni upi?

Opec+ pia inapaswa kuheshimu matakwa ya Urusi, kwa kuwa ni mojawapo ya washirika wawili wakubwa katika muungano huo.

"Warusi wanafurahia bei katika kiwango hiki," anasema Carole Nakhle, Mkurugenzi Mtendaji wa Crystol Energy. "Hawatapta faida yoyote bei ikishuka.

"Opec inataka kudumisha uhusiano mzuri na Urusi, kwa hivyo kuna uwezekano mkubwa wa kuendelea na makubaliano ambayo wote walifanya mwaka jana. Hii ina maana wataendelea kuongeza usambazaji wa mafuta ghafi hatua kwa hatua kuanzia sasa hadi Septemba."