Elon Musk na Twitter: Sababu sita zilizomfanya bilionea huyu kujipata mashakani mtandaoni

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangazo la makubaliano ya ununuzi wa mtandao wa Twitter na Elon Musk lilizua mjadala mkali kuhusu mustakabali wa jukwaa hilo la mawasiliano.
Hata serikali ya Marekani ililichukulia kwa uzito mkubwa, ikieleza "wasiwasi kuhusu nguvu ya mitandao mikubwa ya kijamii."
Lakini makadirio ya kuchukua mtandao huo wa $44bn pia ulidhihirisha "simulizi ya Twitter" yenye utata ya mfanyabiashara bilionea mzaliwa wa Afrika Kusini.

Chanzo cha picha, Getty Images
Tangu ajiunge na jukwaa hilo mwaka 2009, Musk mara nyingi amejipata matatani na zaidi ya mara moja alikabiliwa na hatua za kisheria kwa ujumbe wake alioandika mtandaoni.
Tazama hapa baadhi ya ujumbe kwenye Twitter uliomletea utata zaidi mmiliki mpya wa Twitter hivi karibuni.
1. Uokoaji wa wavulana wa katika pango la Thai

Chanzo cha picha, Getty Images
Mnamo mwaka 2019, Elon Musk alikabiliwa na kesi ya kashfa baada ya kumwita mpiga mbizi wa Uingereza Vernon Unsworth ''mnyanyasaji'' kwenye Twitter.
Ujumbe huo hatimaye ulifutwa mtandaoni.
Unsworth alikuwa amejizolea umaarufu wa kimataifa mwaka mmoja mapema baada ya kuongoza juhudi za kuwaokoa vijana 12 waliponaswa kwenye pango la chini ya ardhi nchini Thailand.
Musk alikuwa akijaribu kusaidia operesheni hiyo na alitaka kuchangia manowari ndogo.
Badala yake, aliingia kwenye vita vya maneno na Unsworth kwenye mtandao wa kijamii baada ya mpiga mbizi huyo kukataa ofa hiyo, akiiita ''kutafuta angalizo kutoka kwa umma.''
Baada ya maoni ya Musk, Unsworth alimshtaki kwa kumkashifu, akidai dola milioni 190, lakini mahakama ya Los Angeles iliamua kumuunga mkono Musk.
Wakati huo, wakili wa Unsworth, Lin Wood, alisema: ''Hukumu hii inatuma ishara ... kwamba unaweza kutoa mashtaka yoyote unayotaka, hata kama ni mabaya na ya uongo, na mtu anaweza kuepuka.''
2. Mwitiko wake kutokana na corona

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati wa maambukizo ya Covid-19 yalipoenea ulimwenguni mnamo Machi 2020 na kidogo kujulikana juu ya ugonjwa huo, Elon Musk alikosoa hatua kama vile kupigwa marufuku ya kutoka nje na kuita hofu ya ugonjwa wa corona ''upumbavu.''
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
Katika moja ya ujumbe kwenye Twitter, uliochapishwa mnamo Juni 30 ya mwaka huo, Musk alihoji vigezo vya kuamua ikiwa mtu amefariki dunia kutokana na virusi vipya vya corona.
Mfanyabiashara huyo, ambaye amepewa chanjo dhidi ya Covid-19, alipinga hadharani wajibu wa kuchanjwa na kukasirisha mashirika ya Kiyahudi kwa kulinganisha Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau na Adolf Hitler wakati wa maandamano ya madereva wa lori wa Canada dhidi ya chanjo ya lazima.
3.Katika kilele cha Putin

Chanzo cha picha, Getty Images
Kulikuwa na hisia nyingi za shauku kutoka kwa umma kwa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, lakini Elon Musk hakika ilikuwa moja ya maajabu zaidi.
Mnamo Machi 14, mfanyabiashara huyo alienda kwenye jukwaa la Twitter na kumpa changamoto Rais wa Urusi Vladimir Putin kwenye pambano.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2
"Ninampa changamoto Vladimir Putin kwa pambano moja. Kilicho hatarini ni Ukraine."
Baadaye, alienda moja kwa moja kwenye akaunti rasmi ya urais wa Urusi, akirudia mwaliko huo wa pambano.
Putin, aliye na mkanda mweusi katika judo, hakujibu.
4. Kosa kwa rais wa Marekani

Chanzo cha picha, Getty Images
Musk hakupenda kutokuwepo kwa Biden katika kampuni ya Tesla kutokana na maoni yake juu ya utengenezaji wa gari la umeme.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 3
Elon Musk alijipatia utajiri wake kutoka kwa makampuni kadhaa ikiwa ni pamoja na kiwanda cha magari ya umeme cha Tesla, ambacho kilikua muhimu katika biashara hiyo.
Januari iliyopita, bilionea huyo alionekana kuchukizwa na maoni ya Rais wa Marekani Joe Biden juu ya utengenezaji wa gari la umeme nchini Marekani, ambapo Tesla haikutajwa na washindani wake wakatajwa.
''Biden ni kikaragosi cha soksi chenye umbo la binadamu,'' aliandika kwenye ujumbe wa Twitter.
5. Uharibifu kwa Tesla na ujumbe wa Twitter

Chanzo cha picha, Getty Images
Ujumbe wa Twitter wa Musk kuhusu Tesla zina athari kwa thamani ya kampuni.
Elon Musk amejipata matatizoni na wanahisa wa Tesla mara nyingi kutokana na maoni yake ya Twitter, ambayo yameigharimu kampuni hiyo pesa.
Novemba mwaka jana, hisa za Tesla zilishuka kwa karibu 5% baada ya mfanyabiashara huyo kufanya kura ya maoni ya Twitter kama anapaswa kuuza sehemu ya hisa zake katika kampuni.
Ukweli ni kwamba, 58% ya milioni 3.5 kwa waliopiga kura walisema inapaswa kuwa hivyo.
Mnamo mwezi Mei 2020, Musk alileta uharibifu zaidi kwa kutuma ujumbe kwenye Twitter kwamba alidhani bei ya hisa ya kampuni ilikuwa ''juu sana.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 4
Maoni hayo yaliondoa dola bilioni 14 kutoka kwa soko la hisa la Tesla.
6. Na hivi karibuni zaidi... ni utani wa Coca-Cola

Chanzo cha picha, Getty Images
Mzozo wa hivi majuzi zaidi wa Elon Musk kwenye Twitter, ambao ulikuja baada ya kutangaza mpango wa kuinunua kampuni hiyo, ulizua taharuki.
Siku ya Jumatano, alitangaza kwa mzaha mipango ya kununua kampuni ya Coca-Cola ili aweze kuongeza kokeini kwenye mchanganyiko wa kinywaji chake maarufu zaidi duniani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 5
Kinywaji cha asili, kilichovumbuliwa mnamo mwaka 1885 na mfamasia wa Marekani John Pemberton, kilikuwa na jani la koka.
Wakati huo, cocaine ilikuwa halali na kiungo cha kawaida katika dawa, kulingana na Taasisi ya Kitaifa ya Marekani ya Matumizi Mabaya ya Madawa ya Kulevya.
Dutu hii baadaye iliondolewa kwenye kinywaji hicho na haijawahi kuwa kiungo tangu mwaka 1929. Wakati baadhi ya wafuasi milioni 87.4 wa Musk waliitikia vyema ujumbe wake, wengine wamekosoa kile walichokiona kama marejeleo ya dawa za kulevya.
Haikuwa mara ya kwanza kwa mfanyabiashara huyo kupata shida kwa vitu haramu.
Katika mahojiano ya video ya maoni na podcaster Joe Rogan mnamo 2018, Elon Musk alivuta bangi.
Walikuwa California wakati huo, ambapo dawa hiyo ni halali, lakini wakosoaji walidai kuwa haikuwa vizuri kwake yeye kufanya hivyo.