Urusi na Ukraine: Hizi ni njia tano zinazoweza kutumika kumaliza mzozo wa Ukraine

Chanzo cha picha, Getty Images
Katikati ya vita, inaweza kuwa vigumu kuona njia ya kusonga mbele. Habari kutoka uwanja wa vita, kelele za kidiplomasia, hisia za waombolezaji na waliohamishwa; Yote haya yanaweza kuwa makubwa.
Hebu turejee nyuma kidogo kwa muda na kufikiria jinsi mgogoro wa Ukraine unaweza kupelekwa kwenye muelekeo fulani. Ni mambo gani na njia gani ambazo wanasiasa na waratibu wa masuala ya kijeshi wanazifuatilia kwa ukaribu? Wachache wanaweza kutabiri yajayo kwa ujasiri, lakini hizi ni baadhi ya njia zinazoweza kutumika.
Vita fupi
Katika mazingira haya, Urusi inaongeza operesheni zake za kijeshi. Kunafanyika mashambulizi zaidi ya silaha na roketi nchini Ukraine. Malefu ya raia wanakufa. Licha ya kujibu mapigo, Kyiv inaanguka.
Matokeo haya si rahisi kutokea kwa urahisi lakini yatategemea mambo kadhaa kubadilika: Vikosi vya Urusi vinafanya vizuri zaidi, vikosi vingi vikipelekwa uwanja wa vita, huku morali ya juu ya mapigano ya Ukraine inazidi kufifia.
Bwana Putin anaweza kufanikiwa kuleta mabadiliko ya utawala huko Kyiv na kuhitimisha ushirikiano wa magharibi na Ukraine. Serekali mpya ya vibaraka wa urusi itaundwa. Rais Zelensky ama atauawa ama atakimbilia magharibi mwa Ukraine au ughaibuni, kujiokoa. Rais Putin atatangaza ushindi na kuondoa baadhi ya vikosi vyake, na kuacha wanajeshi kadhaa kuendelea kudhibiti nchi hiyo. Maelfu ya wakimbizi wataendelea kukimbilia magharibi. Ukraine itaungana na Belarus kuwa 'vibaraka' wa Moscow.
Lakini serikali yoyote inayoiunga mkono Urusi itakuwa haina uhalali itakuwa kwenye hatari ya mkukutana na uasi. Matokeo kama hayo yanaonekana si imara na uwezekano wa kuzuka kwa migogoro mingine tena ni mkubwa.
Vita ndefu
Pengine uwezekano zaidi ni kwamba hii inaweza kuwa vita vya muda mrefu. Pengine vikosi vya Urusi vikapunguzwa, vikizuiwa na morali yao ya chini, vifaa duni na uongozi usio na uwezo.
Labda inaweza kuchukua muda mrefu kwa vikosi vya Urusi kuudhibiti miji kama Kyiv ambao wanaoutettea wanapigana kutoka kila mtaa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Na hata kama vikosi vya Urusi vikifanikiwa kujisambaza katika miji ya Ukraine, labda watapata tabu kudumisha udhibiti. Pengine Urusi itashindwa kusambaza majeshi yake katika kila pembe ya Ukraine. Vikosi vya Ukraine vitageuka kuwa waasi vikisaidiwa na wananchi. Nchi za Magharibi zitaendelea kusaidia kuwapa silaha. Hapo baadaye, pengine baada ya miaka mingi, Urusi inapata uongozi mpya, vikosi vya Urusi vinaondoka Ukraine baada ya umwagaji damu, kama vile walivyofanya watangulizi wao waliondoka Afghanistan mwaka 1989.
Vita ya Ulaya
Inawezekana vita hii ikasambaa zaidi na kuvuka mipaka? Rais Putin anaweza kutafuta kurejesha sehemu zaidi za himaya ya zamani ya Urusi kwa kutuma majeshi katika jamhuri za zamani za Soviet kama Moldova na Georgia, ambazo sio sehemu ya NATO. Au kunaweza tu kuwa na kuongezeka kwaathari zaidi. Bwana Putin anaweza kutangaza kuwa silaha za mataifa ya magharibi kwa vikosi vya Ukraine ni kitendo cha uchokozi ambacho kinasababisha kulipiza kisasi.
Anaweza kutishia kutuma vikosi katika mataifa ya Baltic - ambayo ni wanachama wa NATO - kama vile Lithuania, kuanzisha ukanda wa ardhi na eneo la pwani ya Urusi la Kaliningrad. Hilo linaweza kuzusha hatari kubwa ya mgogoro dhidi ya NATO. Lakini Putin anaweza kuchukua njia hiyo ya hatari kama atadhani hiyo ndiyo njia pekee ya kunusuru mamlaka yake.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJAUrusi na Ukraine: Mlipuko wakumba Kyiv huku Urusi ikiendeleza mashambulizi
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine
Suluhisho la kidiplomasia
Licha ya yote yanayotokea, je kuna uwezekano wa suluhisho la kidiplomasia?
"Bunduki zinazungumza sasa, lakini njia ya mazungumzo wakati wote iko wazi," alisema Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres. Kwa hakika mazungumzo yanaendelea. Rais Macron wa Ufaransa amezungumza na Rais Putin kwa njia ya simu.
Cha kushangaza, maafisa wa Urusi na Ukraine wamekutana kwa mazungumzo katika mpaka wa Belarus. Huenda hawajapiga hatua kubwa. Lakini, kwa kukubaliana na mazungumzo hayo, Putin anaonekana kukubali angalau uwezekano wa kusitisha mapigano.
Lakini fikiria mazingira haya: Urusi inashindwa vita, vikwazo vinaanza kuiathiri Urusi. Upizani unakuwa wakati miili ya waliokufa inarejeshwa nyumbani. China inaisukuma Urusi kukubaliana na hali kama haitafana hivyo itasusa kununua mafuta. Kwa hivyo Putin anaanza kutafuta namna ya kutoroka.
Wanadiplomasia wanaingilia mzozo na labda Ukraine inakubaliana na Urusi kuichukua Crimea na sehemu za Donbas. Huku Putini askikubali uhuru wa Ukraine na ushirikiano wake na Ulaya. Hili kama haliwezekani lakini si jambo lisilowezekana, linaweza kuibuka katikati ya mapigano makali ya vita.

Chanzo cha picha, Getty Images
Putin kuondolewa madarakani
Vladimir Putin mwenyewe alipoanzisha uvamizi wake, alisema: "Tuko tayari kwa matokeo yoyote."
Lakini vipi kama matokeo hayo yatakuwa ni kwa yeye kupoteza mamlaka? Inaweza kuonekana kuwa haiwezekani. Hata hivyo, dunia imebadilika katika siku za hivi karibuni na mambo kama hayo sasa yanafikiriwa. Profesa Sir Lawrence Freedman, Profesa wa Mafunzo ya Vita katika Chuo cha Kings, London, aliandika wiki hii: "Sasa kuna uwezekano kwamba kunaweza kutokea mabadiliko ya serikali huko Moscow kama ilivyo Kyiv."
Kwa nini mtaalamu huyu kasema hivyo? Naam, pengine Putin anakutana na vita mbaya. Maelfu ya wanajeshi wa Urusi wanariki. Vikwazo vya kiuchumi vinaiathiri Urusi. Bwana Putin anapoteza uungwaji mkono mkubwa. Pengine kunazuka tishio la mapinduzi ya watu wengi. Anatumia vikosi vya usalama vya ndani vya Urusi kukandamiza upinzani huo. Lakini hii inageuka kuwa mwiba mchungu kwake ambapo wanajeshi wengi wa jeshi la Urusi, wanasiasa na wachumi wanamsaliti na kummgeuka.
Ulaya inatangaza Putin kuondolewa na amerithiwa na kiongozi mwingine mwenye msimamo wa kawaida, na kurejeshwa ka uhusiano wa kidiplomasia. Inawezekana kwa sasa hili likawa jambo gumu kutokea. Lakini Inaweza ikawa ikiwa watu ambao wananufaika na uwepo wa Putin hawataamini tena kwamba anaweza kutetea maslahi yao.
Matukio haya si ya kipekee sio mapya- baadhi yanaweza kwenda sambamba kuleta matokeo tofauti.
Urusi yaishambulia Ukraine:Mengi zaidi
- MOJA KWA MOJAUrusi na Ukraine: Mlipuko wakumba Kyiv huku Urusi ikiendeleza mashambuliziShambulio la Urusi katika mtambo wa nishati wa Ukraine lasababisha moto mkubwa
- YA MSINGI:Mzozo wa Ukraine: Kwanini Urusi inaivamia Ukraine na Putin anataka nini?
- UFAFANUZI:Mzozo wa Ukraine: Swift ni nini na kwa nini kuipiga marufuku Urusi ni muhimu sana?
- UCHAMBUZI:Mzozo wa Ukraine: Putin humsikiliza nani?
- KWENYE RAMANI:Uvamizi wa Ukraine: Shambulio la Urusi kwenye ramani
- ZELENSKY:Volodymyr Zelensky: Mfahamu rais wa Ukraine aliyeacha umaarufu wake wa TV na kuingia kwenye siasa
- PUTIN:Vladimir Putin: Rais wa Urusi aliyeagiza shambulio Ukraine












