Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Mboga za majani peke yake haziwezi kuzuia hatari ya magonjwa ya moyo, utafiti
Mboga za majani zinaweza kuwa nzuri kwako, lakini zinaweza zisikusaidie kupunguza hatari ya mshtuko wa moyo au kiharusi endapo utazila nyingi, uchunguzi mkubwa wa Uingereza unapendekeza.
Chakula gani kingine tunachokula, kiasi gani cha mazoezi tunafanya , maeneo tunayoishi na jinsi tunavyoishi kunaweza kuwa na athari zaidi, watafiti wanasema.
Lakini wanasisitiza kuwa lishe bora husaidia kupunguza hatari ya magonjwa mengi, pamoja na saratani.
Kula angalau matunda na mboga za majani kiasi kila siku wataalamu wa afya wanashauri.
Utafiti huo, kutoka chuo kikuu cha Oxford na Bristol na Chuo Kikuu cha China cha Hong Kong, uliwataka karibu watu 400,000 wanaoshiriki katika utafiti wa Biobank ya Uingereza kujaza dodoso kuhusu mlo wao, ikiwa ni pamoja na wingi wa mboga zilizopikwa na mbichi walizokula. kila siku.
Kwa wastani, watu walisema walikula vijiko viwili vya mboga mbichi, mboga tatu zilizopikwa na aina tano za mboga kila siku.
Afya yao, na matatizo yoyote ya moyo ambayo yalisababisha matibabu au kifo hospitalini, yalifuatiliwa kwa muda wa miaka 12 iliyofuata.
Utajiri wa virutubisho
Ingawa hatari ya kufa kutokana na ugonjwa wa moyo na mishipa ilikuwa karibu 15% chini kwa wale wanaokula mboga nyingi - haswa wale wanaokula mboga mbichi nyingi - ikilinganishwa na wale wanaokula kidogo, watafiti walisema hii yote inaweza kuelezewa na sababu zingine.
Hizi ni pamoja na mitindo ya maisha ya watu - kwa mfano, kama walivuta sigara na kiasi cha pombe walichokunywa - pamoja na kazi zao, mapato na lishe kwa ujumla.
Matokeo yake, walisema utafiti wao haukupata ushahidi wa "athari ya ulinzi wa ulaji wa mboga" kuwa mara ngapi matatizo ya moyo na mzunguko wa damu ulitokea.
Dkt. Ben Lacey, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, alisema: "Huu ni utafiti muhimu wenye athari za kuelewa sababu za chakula za ugonjwa wa moyo na mishipa (CVD)."
Lakini Prof Naveed Sattar, profesa wa dawa za kimetaboliki katika Chuo Kikuu cha Glasgow, alisema kuna "ushahidi mzuri wa majaribio" kwamba kula vyakula vyenye virutubishi vingi kama vile mboga, "kunaweza kusaidia kupunguza uzito na kuboresha viwango vya hatari binavyoweza kusababisha ugonjwa wa moyo." .
Alisema hitimisho la utafiti linaweza kujadiliwa na haipaswi kubadili ushauri ulioenea wa kula angalau sehemu tano za matunda na mboga kwa siku.
"Wengi wanaoishi nchini Uingereza wanapungukiwa na hili, cha kusikitisha, na mengi zaidi yanahitajika kufanywa ili kuhimiza ulaji bora wa mboga za majani," alisema.
"Kwa kweli, ninashuku kuwa tunaweza kuwa tumepuuza umuhimu wa lishe bora kwa afya na magonjwa kwa jumla," akaongeza.
Wataalamu wengine walisema kupima kiwango cha chakula na ni aina ya vyakula ambacho watu hula kwa miaka mingi ili kujua athari ya kupata magonjwa aina fulani ni makosa.
"Kwa bahati mbaya wasiwasi inabidi ielekezwe juu ya kutegemewa kwa matokeo kutoka kwa matumizi ya maswali rahisi yanayotarajia watumiaji kueleza thamani ya wastani ya ulaji," alisema Prof Janet Cade, kutoka Chuo Kikuu cha Leeds.
Utafiti huo uliochapishwa katika jarida la Frontiers in Nutrition, unasema watu wanaokula mboga za majani mbichi kwa wingi wanaweza kupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa moyo kwa sababu kupika mboga za majani huondoa virutubisho muhimu, kama vile vitamini C.
Mafuta yanayotumika katika kupikia yanaweza pia kuongeza ulaji wa vyakula vya mafuta, ambayo ni sababu zinazojulikana kuwa hatari kwa matatizo ya moyo.
Watu wanaokula vyakula vya mboga nyingi za majani wanaweza kula mafuta kidogo, huku wakitumia vitamini na kuweza kuzuia uharibifu wa seli.