Mwaka mpya: Hivi ndivyo dunia ilivyoupokea mwaka 2022, huku ikikabiliwa na maambukizi ya omicron

Chanzo cha picha, Getty Images
Mamilioni ya watu walishuhudia fataki za mwaka mpya katika miji tofauti duniani,huku dunia ikishuhudia wimbi jipya la maambukizi ya aina mpya ya virusi vya corona katika linaloyakumba baadhi ya maeneo yake.

Chanzo cha picha, Getty Images

Chanzo cha picha, Getty Images
Sherehe hatahivyo ziliendelea, kuwa tofauti katika naadhi ya maeneo kutokana na janga la Covid-19, ambalo tangu mwaka 2020 limezilazimisha serikali kuweka sheria na masharti ili kuepuka mikusanyiko ya umati wa watu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Moja ya nchi za kwanza dunaini kuukaribisha mwaka 2022 ilikuwa ni Australia , ambako fataki zilitawa anga juu ya bandari ya Sydney ya Jackson Bay.

Chanzo cha picha, Getty Images
Licha a janga, tabasamu za watu ziliweza kushuhudiwa katika picha za tukio.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kinyume na Australia, New Zealand iliukaribisha mwaka mpya kwa mataa na kuepuka fataki, tukio hilo lilifanyika Auckland, kutoka kwenye mnara wa Skytower.

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika Taiwan kulikuwa na onyesho la fataki katika wilaya ya Xinyi Taipei. Sawa na Australia, watu pia waliruhusiwa kukusanyika kushuhudia tukio hilo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati huo huo katika mji wa Tokyo, furaha ilitawala mitaa. Watu walikusanyika kuukaribisha mwaka pya, hususan katika mji wa Shibuya, huku wakiwa wamevalia mavazi ya rangi za kuvutia, wakitabasamu na kulikuwa na polisi wengi.
Mwaka mpya ulikaribishwa huku kukiwa na wimbi la wasi wasi, huku kukiwa na watu waliopatikana na aina moya ya kirusi cha omicron , ambacho kinasambaa kwa kasi kubwa zaidi kote duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kufikia Alhamisi visa vipya, 1,944,392 vya virus viliripotiwa duniani

Chanzo cha picha, Yuichi Yamazaki
Serikali nyingi zinahofia kwamba kuongezeka kwa maambukizi kunaweza kuzidi uwezo wa hospitali, ingawa matokeo ya tafiti za awali yanaonyesha kirusi cha Omicron kina adhari ndogo kuliko vilivyotangulia.
Wakati mwamka 2022 ulipoingia, eneo maarufu la Red Square mjini Moscow lilikuwa pweke, kinyume na kawaida yake.
Kutokana na janga la corona, sherehe zilizozoweleka katika medani hiyo maarufu zilifutwa, lakini halikupungukiwa fataki.

Chanzo cha picha, EPA/MAXIM SHIPENKOV
Eneo la the Big Apple liliukaribishwa mwaka kwa miziki ya aina mbali mbali , mataa, na itifaki ya usalama kwa wale waliofika kwenye sherehe maarufu katika eneo la Times Square: wakiwa wamepata chanjo kamili na wamevalia barakoa.

Chanzo cha picha, REUTERS/Dieu-Nalio Chery
Iingawa kulikuwa na watu wachache , kutokana na kuogezeka kwa maambukizi ya COVID-19 katika mji wa New York, sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya ilijumuisha onyesho la muziki.

Chanzo cha picha, REUTERS/Hannah Beier
Pia Rio de Janeiro iliukaribisha mwaka mpya kwa fataki katika ufukwe wa Copacabana, licha ya kwamba watu walikuwa ni wachache kutoka na janga la Corona.

Chanzo cha picha, REUTERS/Ricardo Moraes












