Je ni kweli nyani wamewaua watoto 200 wa mbwa India 'kulipiza kisasi'?

Chanzo cha picha, Getty Images
Kijiji cha Lavul katika eneo la Maharashtra nchini India kimegonga vichwa vya habari kitaifa na kimataifa kwa wiki moja. Kilichozua gumzo hilo ni mzozo kati ya nyani na mbwa.
Kila aina ya madai yametolewa katika vyombo vya habari kuhusiana na mzozo huo. Ripoti kadhaa za vyombo vya habari zinadai kuwa nyani waliwaua watoto 200 wa mbwa. Hata hivyo BBC ilipozuru eneo hilo kuchunguza madai hayo taswira nyingine imejitokeza.
Nyani waliwachukua watoto wa mbwa...
Ijapokuwa suala hilo liligongwa vichwa vya habari nchini na kimataifa wiki iliyopita, wakazi wa kijiji cha Lavul, wanasema mzozo kati ya wanyama hao ulianza mwezi Septemba,wakati nyani wawili walipokuja katika kijiji cha Lavul.
Mmoja wa wakazi hao Panchayat Samiti anasema, "Hakuna nyani wengi katika jijiji hicho na waliokuweko hawakuwa wakisumbua watu.
Lakini mara hii baada ya kuwasili kwa nyani hao wawili , visa vya kushangaza vimekuwa vikishuhudiwa."
Nyani hawa wamekuwa wakiwachukua watoto wa mbwa na kwenda nao juu ya miti mirefu au juu ya paa za nyumba za watu. Mwanzoni wanakijiji hawakutilia maanani kwani hawakufanya hivyo mara kwa mara. Lakini kadri muda ulivyosonga ndivyo nyani hao waliendelea kuchukua watoto wa mbwa na kwenda nao.

Chanzo cha picha, Nitin Sultane
Nini kilifanyika baada ya hapo...
Baadhi ya watoto wa mbwa waliochukuliwa na nyani na kupandishwa juu ya miti mirefu au paa la nyumba walianguka na kufa. Kutoka hapo uvumi ulianza kuennezwa kuwa nyani wanawaua watoto wa mbwa.
Baada ya matukio hayo, uvumi wa kila aina ulianza kuenezwa, kama vile nyani kumfukuza mtu ao nyani alipita kari na mtu mara ghafla akaanguka na kuumia.
Kisa kama hicho kilimkumbwa Sitaram Naibal ambaye alipanda juu yap aa la nyumba kuwatetemsha watoto wa mbwa mara ghafla alipoona nyani, akaruka kwa kuhofia kushambuliwa na nyani hao na kujeruhiwa.
Naybal alivunjika visigino vya miguu yate miwili. Anasema alitumia karibu rupee laki moja na nusu kupata matibabu. Inaelekea karibu miezi mitatu na mpaka sasa hajaweza kutembea japo anajaribu kujivuta pole pole.
Kumekripotiwa visa kadhaa vya watoto kufukuzwa na nyani hao. Baada ya hapo watu walianza kujifungia majumbani, hali iliyofanya mamlaka ya eneo hilo kuchukua hatua.

Chanzo cha picha, Nitin Sultane
Awali idara ya misitu ilipuuza
Kulikuwa na hali ya taharuki katika Kijiji hicho. Hali iliyofanya mamlaka ya Gram Panchayat kuwasilisha malalamishi ya wakazi kwa idara ya misitu.
Afisa wa maendeleo katika kijiji hicho Nanasaheb Shelke alisema, " Niliandikia barua idara ya misitu tangu Septemba 12-13, kuhusu suala hili lakini sijapata majibu."
Wanakijiji waliamua kutafuta usaidizi kupitia vyombo vya habari na haikuchukua muda suala hilo lilianza kuangaziwa.
Baada ya mjadala wa muda mrefu katika vyobo vya habari, hatimaye idara ya misitu ya Dharur iliwasiliana na maafisa wake wa Nagpur na kuagiza nyani hao wakamatwe.
Baada ya hapo, ilipofika Disemba 19, maafisa kutoka Nagpur walianza kuwawekea mitego nyani hao. Baadhi yao waliwekewa watoto wa mbwa kwenye mtego na walipojaribu kuwachukua walikamatwa.
'Baadhi ya watoto waokolewa'
Laxman Bhagat alisema, "Watoto wanaogopa kwenda shule. Wanaume hawawezi kwenda mashambani na wanawake hawawezi kutoka majumbani kwenda kufanya kazi."
Nyani hao walikaa juu yap aa la nyumba ya Laxman Bhagat kwa siku kadhaa. Wakati huo walikuwa wameleta watoto wa mbwa kati ya nane na kumi kwenye ngazi ya kushuka.
Lakshman Bhagat alisema, "Tulisumbuliwa na kelele za watoto hao wa mbwa na nyani wakati wa usiku. Watoto wangu walijawa ha hofu. Lakini nadhani walikuwa wakilia kutokana na njaa. Kwania siku ya pili tuliwawekea maziwa na mkate kwenye ngazi. Ili kuwatuliza."
Hatua hiyo iliwaokoa watoto wa mbwa na leo wanaonekana mbele ya nyumba ya Bhagat.

Chanzo cha picha, Nitin Sultane
Kwa nini nyani walifanya hivi?
Afisa wa misitu wa DS More pia alieleza kwa nini nyani walikuwa wakiwachukua watoto wa mbwa. Kulingana naye, 'Kuna chawa wadogo, viroboto kwenye nywele za mbwa na nyani wanawala na wanawachukua watoto wa mbwa ili kuwala tu.'
DS More alisema, "Mbwa wakubwa hawawezi kubebeka kwa urahisi wakiwa mikononi nyani.
Ndio maana watoto wa mbwa wanaochukuliwa na nyani hawawezi kujiokoa. Baada ya kula chawa, nzi, nyani hao huwaacha juu ya miti au kwenye paa la nyumba ambako watoto hao wa mbwa wanakufa kwa kukosa chaku na maji kwa kati ya siku mbili hadi nne. Watoto wa mbwa hawawezi kushuka kutoka urefu kama huo na wengine huenda wamekufa walipokuwa wakijaribu kushuka.
Wataalamu wanasemaje?
Hifadhi ya Wanyama ya Siddharth Udyan katika eneo Aurangabad ina wanyama aina tofauti. Dr BS Naikwade amefanya kazi hapo kwa muda mrefu. Wao pia wanajaribu kuelewa mienendo ya nyani hao.
Naikwade alisema, "Ni kweli nyani wanaweza kudhuru wanapokuwa na hasira. Wanaweza kufanya kitendo cha kulipiza kisasai. Hata hivyo inasemekana kile kilichofanyika katika Kijiji cha Lavul ni kutia chumvi."
Dhanraj Shinde, rais wa Life Care Animal Association, ana maoni tofauti. Kulingana na yeye, "Tumbili ni mnyama anayependa kudadisi sana. Labda alifanya hivyo kwa lengo la udadisi.
Afisa wa misitu DS More alisema, "nyani hawakushambulia mtu yeyote kijijini. Kulikuwa na baadhi ya ajali kutokana na hofu ya nyani lakini hawakuwahi kumshambulia mtu yeyote.












