Nyota wa TikTok wamaasai Kutoka Tanzania wanaopata umaarufu miongoni mwa mashabiki wa Bollywood

Kili and Neema Paul

Chanzo cha picha, Kili Paul

Muda wa kusoma: Dakika 4

Huku wakivalia vazi lao la kitamaduni la jamii ya Maasai na kuzungukwa na ng'ombe, nyota wapya wa Tanzania katika mtandao wa TikTok ambao ni ndugu Kili na Neema Paul, wanajiandaa kurekodi video yao hivi karibuni.

Simu ya smartphone inawekwa kwenye tripod mita chache mbali kutoka kwenye nyumba yao iliyopo katika Kijiji kidogo cha Mindu Tulieni, mashariki mwa jimbo la Pwani.

Mji uliopo jirani ni Lugoba, uko umbali wa saa moja kwa mwendo wa miguu. Kutokana na ukosefu wa umeme kijijini, Kili hulazimika kutembelea mjini ili kuchaji simu yake.

Wanajipanga vyema mbele ya kamera, Kili mwenye umri wa miaka 26, anasimama nyuma kidogo ya dada yake Neema, mwenye umri wa miaka 23 .

Mara muziki unapoanza, ndugu hawa hugeuza midomo yao kuwa sawa kabisa na ile inayoonekana katika baadhi ya nyimbo na densi maarufu Bollywood.

Kwa kipindi cha miezi michache iliyopita, video za uimbaji wao wa nyimbo za Kihindi kwa namna iliyo sawa kabisa na waimbaji halisi zimekuwa zikisambaa sana kote nchini India na kuibua gumzo kwenye mitandao ya kijamii.

Video yao maarufu, iliyochezwa na Rataan Lambiyan kutoka filamu ya mwaka huu ya Bollywood Shershaah, ilitazamwa na watu zaidi ya milioni moja katika kipindi cha siku chache.

Ruka Instagram ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe, 1

Wacheza filamu wakuu Kiara Advani na Sidharth Malhotra waliisambaza kwenye mtandao.

Muimbaji asilia wa wimbo huo, Jubin Nautiyal, aliwashitukiza ndugu hao kwa video hiyo wakati waliposhiriki katika mahojiano katika moja ya vituo vya redio vya India.

"Kila mtu anawafahamu nyinyi nchini India ,"Nautiyal aliwaambia.'' Nyie watu ni maarufu!"

'Jambo la kushangaza'

Kutangaza kutoka Mindu Tulieni, ambako wengi wa wanakijiji hawana simu za smartphones, Kili na Neema hawakuwahi kufikiria kuwa video zao zitawafikia mamilioni ya watu nchini India na maeneo mengine ya dunia.

"Mwanzoni ilikuwa tu ni kujifurahisha, hatukudhani tutajulikana sana ," anasema Kili. "Kwahiyo nilipoanza kuona kiasi cha watazamaji wa video na maoni kutoka kwa watu nchini India, nilishtuka. Haikuniingia akilini nilishangaa.

Kutengeneza video hizo kulitokana na mapenzi yao kwa filamu za Bollywood, ambazo Kili alizitazama kwa mara ya kwanza wakati alipokwenda kusoma katika mji mkuu, Dodoma.

Ingawa hakujua lugha ya Kihindi, yeye na dada yake wamejifunza kuimba kwa Kihindi.

"Tangu nilipokuwa mdogo, nimekuwa nikitazama filamu za Bollywood katika majumba ya sinema nchini Tanzania na nilizipenda nyimbo pamoja na filamu. Wakati unapopenda kitu inakuwa rahisi kujifunza ," anasema Kili.

"Hunichukua siku chache tu kujifunza maneno na wimbo. Huwa ninapata maana ya maneno ya wimbo kwa kiingereza kwahiyo ninaweza kuongeza hisia halisi," anasema.

"Hata kabla nielewe wimbo una maanisha nini, huwa ninaupenda muziki ."

Awali alicheza video hizo peke yake, lakini baadaye akamshirikisha dada yake Neema ambaye pia ni mpenzi wa Bollywood.

"Waati kaka yangu aliponiomba kufanya video naye, nilikataa kwanza kwasababu nilikuwa mwenye aibu sana ya kusimama mbele ya kamera ," anasema Neema.

"Lakini nikaanza kuizowea. Ni ajabu kile kilichotokea-hatukudhani siku kama hii itakuja."

Mkanganyiko kijijini

Wawili hao, ambao awali walitumia siku zao kuwachunga mifugo na kulima, sasa hutumia baadhi ya muda wao kufanya mahojiano kwa ajili ya vituo vikubwa vya televisheni na redio vya India.

Nyumbani pia wanajulikana kama nyota maarufu wa TikTok.

Akaundi rasmi ya Kili ya TikTok sasa ina wafuasi milioni 1.8.

Alifungua akaunti yake chini ya mwaka mmoja uliopita- wakati aliposikia kutoka kwa rafiki yake kuhusu TikTok.

Neema amefungua akaunti yake ya Instagram, ambayo ina wafuasi karibu 65,000

Ruka Instagram ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa Instagram ujumbe, 3

Lakini huku taarifa ya mafanikio ya ndugu kwenye mitandao ya kijamii yameibua umaarifu wa kimataifa, familia yao na wanakijiji hawaelewi kuhusu umaarufu wao mpya walioupata.

"Watu wengi hawana smartphones na hawajui kuhusu mitandao ya habari ya kijamii. Hata Neema haelewi mengi. Anafurahia tu nyimbo, lakini hajui athari," Kili anasema.

"Kila mtu alikuwa amekanganyikiwa wakati waandishi wa habari walipoanza kuja katika kijiji chetu na vifaa vya televisheni.

"Mara ya kwanza, familia ilishangaa, ni kwanini nilikuwa ninaimba na kudensi badala ya kuchunga ng'ombe.

"Sasa wameanza kuelewa kwamba ninafanya kitu fulani kizuri ."

'Ndoto iliyotimia'

Wawili hao bado hawajapata pesa yoyote kutokana na ubunifu wao, lakini hivi karibuni wanaweza kubadilisha maisha katika kijiji chao kwa nafasi yao katika skrini kubwa za televisheni.

Vyombo vya habari nchini India vinaripoti kwamba ofa kutoka Bollywood zimeanza kumwagika.

Ni ndoto iliyotimia kwa Kili na Neema, ambao wanasema wamekuwa kila mara wakitaka kuwa katika sekta ya burudani, lakini hawakuwa na imini kuwa itawezekana.

"Tunatoka katika Kijiji kidogo nje ya jiji, kwahiyo sikuwahi kufikiria ndoto zangu za kuwa mcheza filamu na kuwa mbele ya kamera zitawahi kamwe kutokea. Nilitunza ndoto zangu moyoni mwangu tu ," anasema Neema, ambaye tofauti na kaka yake hajawahi kuishi mbali na kijiji cha Mindu Tulieni.

" Kupata fursa ya kusafiri kwenda India litakuwa ni jambo la kufurahisha."

Huku dunia ikitazama, ndugu hawa wanasema wako tayari kuanza kufanya kazi katika bara jipya kwa ajili ya wafuasi wao.

"Tunataka tu watu wawe wanafurahia video, ndio maana tulianza kuzifanya," anasema Kili.

"Vitu vikubwa vinakuja, kwahiyo mashabiki wetu muendelee kutufuatilia."

Unaweza pia kutazama:

Maelezo ya video, Khaby Lame: Siri ya mafaniko ya nyota huyu wa TikTok kutoka Senegal ni gani?