Christine Mboma: Jinsi mwanariadha alivyoepuka vikwazo na kushindia Namibia medali

Christine Mboma akisherehekea ushindi wa medali ya fedha katika Olimpiki ya Tokyo

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mafanikio ya Christine Mboma mjini Tokyo yalikuja baada ya kulazimika kuacha kukimbia katika mbio za mita 400, tukio alilopendelea zaidi.
    • Author, Piers Edwards
    • Nafasi, BBC Sport Africa

Alipokuwa na umri wa miaka 13, marafiki walianza kuachana na Christine Mboma - kwa sababu za ukatili - lakini sasa malkia huyo kutoka Namibia asiyepingika michezoni ni mtu maarufu wa taifa hilo.

Aliporejea kutoka Tokyo, ambako alikua mwanamke wa kwanza wa Namibia kushinda medali ya Olimpiki, safari yake kutoka uwanja wa ndege hadi mji mkuu Windhoek iliangazia hadhi yake mpya.

Safari ya kilomita 45 ilichukua masaa matatu kutokana na idadi kubwa ya watu walivyojitokeza kumpokea.

"Watu walikuwa wakiita jina langu kwa sauti huku wakikimbiza gari nililokuwa ndani- ilikuwa raha sana'',Mboma, 18, aliiambia BBC Sport Africa.

Lakini miaka mitano iliyopita, maisha yake yalikuwa tofauti katika eneo la vijijini kaskazini mwa Namibia, ambako alikuwa akiishi na familia yake katika mazinfira ya umasikini.

"Nililelewa na mama pekee," alisema mteule wa mwanamichezo wa Kiafrika wa mwka wa BBBC. "Nikiwa na umri wa miaka 13, mama yangu aliaga dunia na ilibidi nibaki na mjomba na nyanya yangu.

"Kila kitu kilibadilika na nilipoteza marafiki wengi. Wengine hawakunipenda kwa sababu nilikuwa yatima."

Kuwa yatima kunaweza kuwa changamoto kubwa barani Afrika kutokana na unyanyapaa unaohusishwa mara nyingi na hali hiyo, huku wengine wakiwaona kama mzigo wa kifedha, wengine wakiwahusisha na ushirikina wakiamini kuwa wana bahati mbaya.

Baba yake yuko hai lakini alimtelekeza mama yake ambaye alikuwa mlemavu, wakati, Mboma alipokuwa na miaka sita.

Mboma, ambaye alijitose katika ulingo wa riadha mwaka huu, alikuwa haraka sana kwani alikuwa na jukumu la kuwatunza ndugu zake wawili.

"Sasa ni watoto wangu. maisha niliyokuwa nikiishi yalikuwa magumu - msongo wa mawazo, na kufikiria kuhusu mama yangu," anasema. "Nilikuwa na msongo wa mawazo, kndipo nikajiingiza kwenye michezo ili kujituliza."

Uwezo wake katika mchezo wa riadha umebadilisha maisha yake, sio tu kiuchumi bali pia kijiografia, ikwa kuwa sasa anaishi karibu kilomita 500 kutoka nyumbani na kocha wake Henk Botha na familia yake.

"Christine alikulia katik amazingira magumu alafu mama yake akafariki wakati akijifungu amtaoto ambaye pia hakuponea kifo," alisema Botha, nahodha wa zamani wa timu ya raga ya Namibia.

"Alilazimika awe mtu mzima haraka kwasababu mazingira hayakumruhusu kukua kama watototo wengine. Matotokeo yake ndio haya unayoona katika tabia yake ."

Na ni tabia iliyomsaidia - kushinda medali ya fedha ya Olimpiki, kijana huyo mpole alishinda marufuku ambayo haikutarajiwa, kuingiliwa na vyombo vya habari na mabadiliko ya tukio, chini ya mwezi mmoja kabla ya Michezo kuanza.

Masaibu katika safari yake

Maelezo ya video, Christine Mboma: Mwanariadha wa Namibia

Chini ya wiki moja, taaluma ya Mboma ilienda mrama.

Mnamo Juni 30, alivunja rejodi ya ya dunia ya wanariadha waliyo chini ya miaka -20 katika mbio za mita 400, nchini Polanda- "Nilishtuka, lakini furaha".

Siku mbili baadaye, aligundua kwamba hangeweza tena kushindana zaidi ya mita 400 kwa sababu ya viwango vyake vya juu vya homoni ya testosterone - "Nilishtuka, na kuhuzunika."

"Zilikuwa habari mbaya," anakumbuka.

Sheria za Shirikisho la Riadha Duniani zinasema kwamba wanariadha wa kike walio na viwango vya juu vya testosterone hawawezi kushindana katika mbio zozote kati ya mita 400 na maili moja hadi wapunguze viwango vyao homoni hiyo.

"Nilijiambia nina nafasi moja - mita 200," Mboma anakumbuka. "Laiti ningefikiria juu ya mbio za mita 400 na ​​mambo hayo yote, ningepoteza mwelekeo na nisingefanya vyema kwenye Olimpiki."

Ndani ya miezi miwili, Mboma alikuwa amevunja rekodi ya Afrika na Dunia ya wanarisdha walio na chini ya miaka-20 katika mbio za mita 200 mara nne, huku zote zikitokea Tokyo.

"Nilipofika fainali ya Olimpiki, nilikuwa na hofu sana. Nilijifanya niko sawa, nikitabasamu na kuwapungia mkono watu, kamera na mambo hayo yote."

Lakini aliweka kando hofu aliyokuwa nayo kwani hakustahili kuwa hivyo.

Ulimwengu ulishuhudia, msichana huiyo mdogo akipokea medali yake ya kwanza ambayo ilikuwa imeshindwa na mashujaa wake wa utotoni Shelly-Ann Fraser Pryce wa Jamaica na Marie-Josee Ta Lou wa Ivory Coast, akiandikisha rekodi bora ya kibinafsi kwa kumaliza nyuma ya Mjamaica Elaine Thompson-Herah.

"Sikuwa nikifikiria kuhusu mbio hizo - Nilikuw anikikimbia tu - na [ nilipovuka] utepe, walisema nilikuwa wa pili. Niligusa uso wangu, [nikijiuliza] 'hivi ni kweli ama naota?'"

Haikuwa ndoto bali ni ukweli kwamba Namibia, nchi ndogo yenye watu milioni 2.5, imerejea kwenye jedwali la juu la riadha kwa mara ya kwanza tangu 1996, wakati Frankie Fredericks aliposhinda medali yake ya nne na ya mwisho ya Olimpiki.

Siku kumi na nane baadaye, Mboma alishinda taji la Dunia la Vijana wasiozidi umri wa miaka 20 (nchini Kenya) kabla, mnamo Septemba, mara mbili alinyakua uwanja wa hali ya juu katika Diamond League - kushinda fainali yenyewe huko Zurich na kunyakua taji la kila mwaka

Maisha mazuri siku za usoni?

Mboma na mshirika wa mafunzo Beatrice Masilingi walipatikana kuwa na viwango vya juu vya testosterone mwezi Julai

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mboma na mshirika wa mafunzo Beatrice Masilingi walipatikana kuwa na viwango vya juu vya testosterone mwezi Julai

Mboma anasema haelewi kanuni tata za Riadha za Duniani zinazowahusu wanariadha wanaogunduliwa kuwa na 'Tofauti ya maumbile ya Kijinsia' (DSD).

"Kwa kweli sijui," alikiri wazi wazi.

Kocha wake, anasema baada ya Shirikisho la Riadha ya Duniani kumwambia Mboma na mwenzake Beatrice Masilingi hawawezi kushiriki mbio za mita 400 kutokana na sheria za DSD, alikataa mwaliko wa kufanyiwa vipimo zaidi, akisema hana imani na mchakato wa shirika hilo.

Alimradi Shirikisho la Riadha za Dunia haibadilishi kanuni zake zaidi ili kufikia mbio za mita 200, ambazo Botha ana wasiwasi nazo, Mboma hakika inatazamia mustakabali wa kusisimua kwa umbali huo.

"Nilipochukua medali na kuiweka shingoni, machozi yalikuwa yanadondoka machoni mwangu. Sikuwahi kuwa na ndoto ya kuwa Mwana Olimpiki na sasa nilikuwa na medali ya fedha - nilijivunia sana."

Je, alitoa medali kwa mtu yeyote?

"Naam - kwa mama yangu."

Tafadhali Mpigie kura Mwanamichezo Bora wa Afrika wa BBC 2021 ambapo pia utapata sheria na ilani ya faragha. Upigaji kura utafungwa Jumapili Disemba 19 2021 saa 23:59 GMT."