Christine Mboma: Mwanariadha wa Namibia aliyeshinda medali ya fedha mita 200

Maelezo ya video, Christine Mboma: Mwanariadha wa Namibia

"Mbio bora katika maisha yangu " - hivyo ndivyo Christine Mboma alivyoelezea ushindi wake jijini Tokyo Japan 2020 baada ya kuwa mwanamke wa kwanza nchini Namibia kusimama katika jukwaa la medali la Olimpiki. Baada ya kulishindia taifa lake medali miaka 25 baadaye, kijana huyo alijishindia medali ya fedha katika mbio fupi za mita 200, akimaliza nyuma ya bingwa mara tano wa michezo ya Olimpiki kutoka Jamaica Elaine Thompson Herah. Muda wake wa dakika 21 na sekunde 81 ndio uliokuwa bora zaidi kuwahi kushindwa na mwanamke chini ya umri wa miaka 20.

Baadaye aliibuka mshindi katika mbio za Diamond league mita 200 mwezi Septemba mjini Zurich, ambapo muda wake wa dakika 21 .sekunde 78 ulivunja rekodi nyengine ya dunia na rekodi mpya ya Afrika. Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 18 alianza kulenga mbio za mita 200 mapema mwaka huu, baada ya kuzuiliwa kushiriki katika mbio za mita 400 na shirika la riadha duniani kutokana na kumiliki homoni nyingi za kiume.