Kituo cha kwanza cha mwanadamu cha safari za anga za mbali

Chanzo cha picha, Vegitel
Kituo cha kwanza duniani chenye usiri mkubwa cha anga za mbali, Baikonur Cosmodrome, kiko kati kati mwa jangwa kubwa la Asia ya Kati kilomita 2600 kusini mashariki mwa Moscow na kilomita 1,300 kutoka miji mikuu ya Kazakhstan ya Nur-Sultan na Almaty.
Ni kutoka eneo hili la mbali ambapo mwaka 1957 Muunganoa wa Usovieti ulizindua kwa mara ya kwanza setilaiti ya Sputnik 1 kwenda orbit.
Miaka minne baadaye mwaka 1961, Yuri Gagarin alipaa kutoka hapa na kuwa mwanadamu wa kwanza kusafri kwenda anga za mbali akiabiri chombo cha Vostok 1. Na mwaka 1963, Valentina Tereshkova alipaa kutoka Baikonur kama mwanamke wa kwanza kusafiri kwenda anga za mbali.
Baanda ya kusitishwa kwa program ya safari za anga za mbali ya Nasa mwaka 2011, Baikonur kikawa ndicho kituo pekee duniani kilichokuwa kinadumia kituo cha anga za mbali ISS. Sasa miaka 60 baada ya safari ya kihistoria ya Gagarin, kimekuwa kituo kikuu cha safari za anga za mbali duniani.
Lakini ilikuwaje kituo hicho chenye vumbi na kilicho misitu ya Kazakhstan kilikuja kuwa kama mlango wa mwanadamua kufanyaa safari za anga za mbali?
Kusafiri kwenda anga za mbali kunahitaji vitu viwili; kuwa mbali na maeneo wanamoishi watu na kuwa karibu na ikweta kwa kuwa dunia inazunguka kwa kasi zaidi katika ikweta. Upande kwa programu ya safari za anga za mbali ya Marekani kituo kama hicho kipo pwani ya Texas ambapo kumejengwa kituo cha Johnson Space Center.

Chanzo cha picha, Vegitel
Muungano wa Usovieti ukaelekea Jamhuri ya Kazakhstan kutafuta eneo ambalo laweza kutumiwa kwa majaribio ya makombora ya masafa marefu na roketi.
Muungano wa Usovieti ulikua ukifanya majaribio ya roketi tangu mwaka 1920 na baada ya vita vya pili vya dunia, walipata teknolojia ya roketi ya Ujerumani ya V-2 iliyosaidia sana kuboreka programua yake.
Usovieti ilitambua eneo kubwa lenye vichaka kusini kwa Kazakhstan kando la mto Syr Darya. Tayari eneo hili lilikuwa na kituo kilichojenjwa kwa wanajiolojia na watu waliokuwa wanatafuta mafuta.
Ilikuwa nchi tambarare yenye hali mbaya ya mazingira ambapo viwangi vya joto vinaweza kufika nyuzi joto 50 msimu wa joto na hadi nyuzi -30 msimu wa baridi.
Wakitumia reli, usovieti iliwasafirisha maelfu ya wafanyakazi kujenga kituo likiwemo shimo kubwa la kuzima moto utakanao na kurushwa roketi lenye urefu wa mita 250, upana wa mita 100 na kina cha mita 45.
Mji wa Tyuratam ukakua kando ya mto, kilimita 30 kusini mwa kituo cha cha kuzindua roketi. Usovieti ikabadilisha jina la Tyuratam kwa kuazima jina la mji mwingine uliokuwa umbali wa kilomita kadhaa na kukipa kituo hicho na mji ulio karibu, Ndipo kituo hicho kikapewa jina Baikonur.
Eneo hilo lililotengwa ndilo la mwisho wana anga huishi kabla ya kuondoka duniani na la kwanza wanaloliona wakati wanarejea nyumbani.

Chanzo cha picha, Vegitel
Katika makala kuhusu rekodi yake ya kuishi kituo cha anga za mbali ISS ya 'mwaka mmoja angani', Mwana anga Scott Kelly alikieleza kituo cha Baikonur kama aina fulani ya nyumba kwenda anani.
Kwa njia nyingine ina maana kwangu kuja eneo kama hili kwanza ambalo tayari limetengwa kutoka kile nimekizoea, kwa sabubu kinaonekana kama jiwe la kuvuka kwenda eneo ambalo limetengwa zaidi. Unajua eneo lililotengwa kwenda lile lililotengwa zaidi.
Warusi walikuwa wanalinda kituo hicho na teknolojia yao. Kambora la R7 ambalo Gagarin alilitumia kusafiri lilikuwa kombora kubwa zaidi la masafa marefu duniani wakati huo. Na siri zake zilistahili kulindwa. Watu walikuwa na hofu kuwa Marekani ingapata teknolojia hiyo ambayo kwa kweli waliipata.
Kufuatia kuporomoka kwa muungano wa usovieti mwaka 1991, Kazakhstan ikapata uhuru na ghafla kituo muhumu zaidi cha safari za anga za mbali kilikuwa kwenye ardhi ya nchi ya kigeni. Mwaka 1994 Warusi walifikia makubaliano na Kazalhstan ya kukodi kituo cha Baikanur kwa pauni milioni 82.5 kwa mwaka.
Idadi ya watalii inayozidi kuongezeka sasa wanazuru Baikonur kutazama uzinduzi wa roketi hususan safari za kwenda kituo cha ISS, lakini usiri umebaki hadi eleo.
Kwa mfano mji huo umejaa warusi ukiwa unazungukwa na Kazakhstan na eneo hilo linalindwa na shirika la safari za anga za za mbali la urusi Roscosmos.
Watalii wanaofika eneo hilo hushiriki kwenye tamasha zikiwemo kutazama kusafirishwa roketi za Soyuz wakati ikitolewa kwa hangar kwenda eneo la uzinduzi na kuhudhuria shere za kuwaaga wana anga wanapo abiri basi kwenda kuabiri roketi.
Kwa Robert mtalii kutoka Swansea, Wales, aliyetembelea Baikonur mwaka 2019, kuona roketi ikisafirishwa ilikua kilele cha ziara yake. "Unasimama kando na roketi na kuifuata hadi kituo cha uzinduzi."
Joy anasema safari yake huko Baikonur ilikuwa ndoto yake ya muda mrefu. "Nilitaka kuzuru Baikonur tangu nikiwa mtoto mdogo."

Chanzo cha picha, Vegitel
Novemba mwaka 2020, kampuni ya kimarekani SpaceX, inayomilikiwa na Elon musk ilifanya safari yake ya kwanza na kusafirisha wana anga kwenda kituo cha ISS kutoka kituo cha Kennedy Space Center huko Florida.
Ilikuwa ndio mara ya kwanza wana anga kufanya safari yao kutoka Marekani tangu safari ya mwisho iliyofanywa na chombo cha Discovery mwaka 2010.
Huajalishi siku zake za usoni zitakuwaje lakini thamani ya Baikonur ni historia inayoishi London, Paris, Beijing na Washington zaweza kuwa himaya za zamani na sasa, lakini ni kutoka kituo chenye vumbi cha reli huko Kazakhstan ndippo mwanadamu wa kwanza aliweza kufanya safari ya anga za mbali.














