Tiba binafsi : Je ni vyema kutafuta taarifa kwenye mtandao na kutumia dawa bila ushauri wa daktari?

Chanzo cha picha, iStock
Maria (jina lake limebadilishwa) ana umri wa miaka 48 . Amekuwa akiugua kipandauso kwa miaka 20. Yeye pia ni daktari wa meno.
Hatahivyo, humuona daktari na mara moja au mara mbili kwa ajili ya kupata matibabu ya kipandauso. Alifikiri anafahamu dawa kwasababu alikuwa ni daktari.
Alikuwa akimeza dawa za kuzuwia maumivu wakati wote alipohisi ana maumivu ya kichwa na kupata nafuu ya muda. Kila mara nilipokuwa nikienda kwa daktarin nilikuwa napewa dawa hiyo hiyo.
Suala hilo lilikuwa la kawaida na wala halikuwahi kujadiliwa nyumbani kwake. Alichukulia ugonjwa wa maumivu ya kichwa cha kipandauso kama tatizo dogo. Lakini tatizo lile dogo liligeuka kuwa baya siku moja.
Alipogundua, vipimo vya matibabu vilionyesha kuwa utendaji kazi wa figo yake umepungua kwa asilimia 5.
Dkt Kanneganti Chandra, ambaye anafanya kazi kama daktarin nchini Uingereza, aliiambia BBC kuwa sasa ameshauriwa kupata matibabu ya figo.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni yapi madhara ya tiba binafsi ?
Watu wengi kama vile, Maria, hutumia madawa kwa ajili ya matatizo ya kiafya kama vile maumivu ya kichwa, homa, maumivu ya mgongo na maumivu ya miguu bila kupata ushauri wa daktari.
Utafiti wa mwaka 2015 wa timu ya madaktari katika hospitali ya Safdarjung katika New Delhi ulibaini kuwa 37% ya watu katika miji na 17% katika maeneo ya vijijini hawkautaka kwenda kwa datary kwa matatizo madogo ya kiafya.
Watu walioelemika wana uwezekano mkubwa wa tiba ya kibinafsi.
Utafiti ulibaini kwamba watu wengi hujitibu binafsi iwe kupitia uzoefu wa kibinafsi au kwa kuzingatia dawa walizoandikiwa na daktari awali.
Pia inafahamika kwamba wat umara nyinyi pia hutumia dawa zao wenyewe kama vile kutibu homa na mafua. Pia iligundulika kuwa baadhi ya watu wanaotumia dawa hizi za tiba ya kibinafsi hawakumeza dozi nzima ya dawa za kutibu maambukizi(Antibiotics).
Madaktari walionya kwamba kumeza antibiotics na dawa nyingine za homoni(steroids) bila wiushauri wa daktari ni jambo linaloweza kuhatarisha maisha.

Chanzo cha picha, CHANDRA KANNEGANTI/FACEBOOK
Akitoa mfano wa Maria, Dkt . Chandra salisema kuwa tiba-binafsi wakati mwingine huhatarisha maisha saw ana inavyokuwa tatizo dogo wakati ugonjwa unapojitokeza.
Madaktari wamebaini kuwa kutumia dawa za maumivu bila kushauriwa na daktarin kwa miaka 20 ndio tatizo la kuugua kwa figo yake . Alifanyiwa upandikizwaji wa figo baada ya mume wake kumpatia msaada wa figo.
Hatahivyo, Dkt. Chandra aliuliza, "Ni figo watoaji wangapi wa figo waliopo? Na ni watu wangapi wanaweza kupona baada ya kupoteza kiungo kingine cha mwili kama mafigo?"

Chanzo cha picha, Getty Images
Katika eneo la Kerala nchini India , msichana mwenye umri wa miaka 17 alitazama video ya YouTube wiki iliyopita na akajifungua mtoto bila msaada wowote. Watu wa familia yake walimkimbiza hospitali baada ya kuvuja damu nyingi.
Dokta Dakshyaini Purini, ambaye ni daktarin bingwa wa wanawake katika hospitali ya seikali ya Bibinagar, alisema ni hatari sana kujifungua ukiwa peke yako.
Katika mwaka 2018, mwanamke alifariki wakati alipokuwa akijifungua katika nyumba yake katika jimbo la Tamil Nadu.

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati wa utoaji wa mimba, kutokana na tiba binafsi bila uangalizi wakat iwa kijifungua inaweza kusababisha:
- Osteoporosis (ukosefu wa homoni za jinsia estrogen, ukosefu wa madini ya calcium katika mifupa, na kusababisha kuvunjika kwa urahisi ).
- Kuondolewa kwa mfuko wa uzazi
- Kuendelea kupotea kwa mifupa
Alionya kuwa hali kama hizo huwafanya watoto washindwe kujifanyia kazi katika miaka yao ya kwanza ya maisha.

Chanzo cha picha, DR DAKSHAYANI PURINI
Je vipimo vya matibabu vinakuzuwia kumuona daktari?
Dokta Chandra Kanneganti anasema sio sahihi kumwambia mgonjwa afanyiwe vipimo vya kila kitu bila kuangalia hali yake ya afya kwa siku chache.
"Kwa bahati mbaya kuna propaganda nyingi zinazoendelea kwamba ni muhimu kwenda katika hospitali zenye madaktari bingwa zaidi kwa kila tatizo dogo la kiafya ," alilalamika.
Dokta Chandra alisema kuwa watu wanaogopa kwenda hospitali kutokana na madaktari kuwataka wagonjwa kufanyiwa 'uchunguzi wa mwili mzima' katika hospitali za kibinafsi na hilo huwafanya watu kuepuka hospitali kwa kuogopa garama kubwa za vipimo na matibabu.
Anasema garama ya tiba imekuwa mzigo mkubwa kwa mtu wa kawaida.
" Nyenzo kama Intaneti na Google zimewarahisishia watu kupata taarifa, lakini madhara ya tiba binafsi yanatisha ," alisema Dkt Chandra.
PICHA
Ni yapi madhara ya tiba binafsi ?
Dkt . Chandra anaonya kuwa tiba binafsi inaweza kukupa nafuu ya muda mfupi lakini hmadhara yake ni ya muda mrefu na ya kiwango cha juu
Nchi kama Uingereza, tiba binafsi ni marufuku.
Anasema kwamba katika nchi zilizoendelea madawa huwa hayatolewi dukani bila karatasi ya maelezo ya daktari na ukosefu wa sera hiyo kwa mataifa mengi duniani ni chanzo cha matatizo mengi ya kiafya.
Amewaonya watu kuacha kwenda katika maduka ya dawa na kununua dawa zao, kama njia ya kujitibu wenyewe, na kuongeza kuwa tiba hiyo inaweza kupelekea mtu kupata mshituko wa moyo, kuharibika kwa figo na viungo vingine vya mwili.
Anashauri usitumie dawa za kumaliza maumivu bila ushauri wa daktari. "Zinaleta uharibifu usioweza kukarabatiwa kabla haujagundua kosa ," alisema.












