Tuzo ya amani ya Nobel 2021:Maria Ressa na Dmitry Muratov washinda Tuzo ya amani ya Nobel 2021

Chanzo cha picha, Getty Images
Waandishi wa habari Maria Ressa na Dmitry Muratov wameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel kwa "mapambano yao ya ujasiri" kutetea uhuru wa kujieleza huko Ufilipino na Urusi.
Kamati ya Nobel iliwataja wawili hao kuwa "wawakilishi wa waandishi wote wanaotetea msimamo huu".
Washindi wa tuzo hiyo ya kifahari, yenye thamani ya 10m krona za Uswidi (£ 836,000; $ 1.1m), walitangazwa katika Taasisi ya Nobel ya Norway huko Oslo.
Walichaguliwa kati ya wagombea 329.
Wengine waliokuwa wakizingatiwa kwa tuzo hiyo mwaka huu ni pamoja na mwanaharakati wa wa mabadiliko ya tabia nchi Greta Thunberg, kikundi cha haki za vyombo vya habari Reporters Without Borders (RSF) na shirika la afya ulimwenguni (WHO).
Tuzo hiyo hutunukiwa mtu au shirika ambalo "limefanya kazi kubwa zaidi au bora kwa undugu kati ya mataifa".
Mshindi wa mwaka jana alikuwa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu chakula (WFP), ambalo lilituzwa kwa juhudi zake za kupambana na njaa na kuboresha hali ya amani.
Je ni kipi tunachojua kuhusu washindi hawa?
Maria Ressa ndio mwanzilishi mwenza wa kituo cha habari cha Rappler mwaka 2012.
Mtandao huo una wafuasi milioni 4.5 katika facebook , na umejulikana kwa tathmini za kiwango cha juu na uchunguzi.
Ni mojawapo ya mashirika ya habari ya Ufilipino ambayo yamekuwa yakikosoa kwa uwazi sera za rais Rodrigo Durtete.
Rappler amechapisha habari za rais huyo kuhusu vita vyake vikali dhidi ya dawa za kulevya pamoja kuangazia suala la unyanysaji ,ukiukwaji wa haki za kibinadamu na ufisadi.
Bi Resa yeye binafsi ameripoti kuhusu kuenea kwa propaganda za serikali katika mitandao ya kijami.
Bi Ressa amekabiliwa na kesi ambazo anasema zimechochewa kisiasa. Hatahivyo serikali imesisitiza kuhusu uhalali wake.
Mwandishi Ellen Tordesillas aliambia BBC mwaka uliopita kwamba Bi Ressa alikuwa miongoni mwa wale waliopinga baadhi ya sera za Durtete.
Dmitry Muratov ni mwanzilishi mwenza wa gazeti la co- Novaya mwaka 1993 na amefanya kazi kama muhariri wake.
Novaya Gazeta ni mojawapo ya magazeti machache yaliosalia nchini Urusi ambayo yamekuwa yakiukosoa utawala wa taifa hilo hususan rais Vladmir Putin.
Likichapishwa mara tatu kwa wiki, ni gazeti ambalo limekuwa likifanya uchunguzi kuhusu ufisadi na maovu mengine ya viongozi walio madarakani na kuangazia matatizo ya wakazi wanaodaiwa kuathiriwa na unyanyasaji.
Waandishi wake sita , ikiwemo Anna Politkovskaya , wameuawa kutokana na kazi zao za uandishi , kulingana na kamati ya kuwalinda waandishi.
Gazeti hilo pia limekuwa likitishiwa na kunyanyaswa ikiwemo ripoti zake kuhusu unyanyasaji wa haki za kibinidamu katika eneo la Chechnya.














