Vita vya Jamhuri ya Afrika ya Kati: Maeneo usiyoweza kuyafikia na uingiliaji wa Urusi

Chanzo cha picha, Getty Images
Wakati vikosi vinavyoungwa mkono na Urusi vikisonga mbele, tishio linaendelea kuongezeka kuhusu milipuko ya mabomu ya kutegwa ardhini na vilipuzi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (CAR), ambavyo sasa vinaonekana kuwa mkakati mpya na wa hatari huku vita vya msituni vikiendelea.
Mapema mwezi huu, msafara uliokuwa ukisafiri kaskazini magharibi mwa nchi upipigwa na kilipuzi kilichomuua mfanyakazi wa misaada kutoka Baraza la Wakimbizi la Denmark.
Hata katika moja ya nchi hatari zaidi kwa wafanyakazi wa misaada, ambao kwa kawaida hukabiliwa na vitisho, tukio hilo la kutisha lilitangazwa sana -na kuonyesha kuongezeka kwa tisho la vita vya miaka mingi.
Vifaa hivi ambavyo vinaua na kusababisha majeruha ya kutisha, vimewafanya wapelelezi wa haki za binadamu na wasambazaji wa misaada kuyaepuka maeneo yaliyokumbwa na vita zaidi-na kuziacha jamii bila msaada.
'Kumbukumbu ya Maasi'
Huku CAR ikikumbwa na machafuko kwa miongo kadhaa, asili ya ukurasa huu mpya katika mzozo ni mwaka 2013 wakati muungano wa waasi ulipochukua mamlaka , na kusababisha kisasi kutoka kwa wanamgambo walioung'oa madarakani utawala huku nchi hiyo ikikumbwa na vita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Chanzo cha picha, AFP
Huku pande zinazohasimiana zikiwa zimegawanyika, Urusi iliingia nchini humo 2017 katika juhudi za kupanua ushawishi wake kote barani Afrika- ikiunga mkono serikali iliyoshindwa katika mji mkuu, Bangui, na kuipatia silaha, risasi na wakufunzi wa kijeshi 175.
Ushahidi unaonesha hawa wanaoitwa wakufunzi au waalimu, wanajumuisha mamluki wa Urusi kutoka Wagner Group, kampuni ya kibinafsi ya kijeshi yenye uzoefu wa kupigana katika Ukraine, Syria na Libya - ingawa serikali za nchi hizo zote zilipinga hili.
Makundi ya waasi wa CAR -yanayojumuisha wale waliorejea, wanaotaka kuikomboa nchi, na ukarabati (al maarufu 3R) - kwa kiasi kikubwa wanatoka katika jamii ya Waislamu walio wachache, ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiachwa nyuma katika maendeleo ya nchi.
Kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Disemba mwaka jana, makundi haya ya waasi yalijiunga na muungano wa waasi ambao haukuwa imara na kusababisha kuvunjika kwa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwaka 2019.
Soko jeusi la mabomu ya ardhini
Kwa usaidizi wa Warusi, vikosi vyenye silaha vimeweza kuwarudisha nyuma, na kuchukua miji na vijiji vilivyokuwa vimechukuliwa na waasi.
Hofu ya mabomu ya kutegwa ardhini na vilipuzi vya kutengenezwa inalozingira mzozo huu wa ghasia ambao unaenea katika kanda hiyo, hususan kaskazini mwa Nigeria, bonde la mto Chad na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Matumizi ya kwanza ya mabomu ya ardhini na vilipuzi katika CAR yalianza katika mwezi wa Juni 2020, wakati wa mapambano yaliyoungwa mkono na Umoja wa Mataifa dhidi ya makundi ya waasi ambayo yalitumia silaha hizi katika jaribio katili la kuyanyakua maeneo

Chanzo cha picha, AFP
Miongoni mwa aina za vilipuzi vilikuwa ni pamoja na mabomu ya kulipua magari yanayofahamika kama PRB-M3, yenye nguvu, vilipuzi vilivyotengenezwa Ubelgiji kuanzia miaka ya 1970 na 1980.
Wataalamu wa silaha wanasema huenda silaha hizi zinasafirishwa kutoka kwenye gala la Libya au zinachimbuliwa kutoka kwa kwenye kiwanja chenye mabomu ya ardhini cha Chad na Sudan kabla ya kuingia katika soko jeusi.

Chanzo cha picha, AFP
Athari kwa raia ni msiba. Yakiwa yamewekwa kwenye barabara na hata karibu na shule, vilipuzi hivyo vimetenganisha vijiji na walinda amani pamoja na usaidizi wa kibinadamu, na kuwalazimisha watu kuzikimbia nyumba zao.
Zaidi ya watu milioni 1.4 hadi sasa ni wakimbizi wa ndani -idadi ambayo ni ya juu kuwahi kushuhudiwa katika kipindi cha miaka mitano.
Kwa mfano, takriban watu 1,000 walitoroka vijiji katika jimbo Nana-Mambéré baada ya kilipuzi kulipuka May; vijiji viliendelea kutofikiwa kwasababu ya vitisho vya mashambulizi.

Chanzo cha picha, Minusca
Kampeni za kupaka matope
Kikosi imara cha walinda amani 15,000 wa Umoja wa Mataifa (Minusca) ambacho kilikumbwa na madai kadhaa ya unyanyasaji wa kingono , pia kiliathiriwa.
Vikosi vilivyoshindwa pia vimekuwa vikilengwa na kampeni za kupakwa matope kutoka pande zote, huku kazi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa ikivurugwa na uwepo wa vilipuzi na uwepo wa wanajeshi na mamluki wa Urusi katika nchi hiyo.
"Minusca hakijawahi kutumia mabomu ya kutegwa ardhini," alisema msemaji wa vikosi vya Umoja wa mataifa Maj Ibrahim Atikou Amadou, na kuongeza kuwa shuguli za kutegua mabomu ya ardhini bado haijatekelezwa kwasababu ya shutuma.
Hatahivyo inaonekana jukumu la kutega mabomu ya ardhini huenda sio la waasi pekee. Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa mwezi Juni ilifichua kuwa vikosi vya serikali vilikuwa vimezionya jamii katika maeneo mawili tofauti kwamba wanajeshi wa Urusi walikuwa wameweka mabomu ardhini kwenye barabara na kando ya daraja.
Hata kama uwepo wa bomu ni wa nia njema, ukweli ni kwamba, hofu liyosababishwa ni kubwa, kwani imewazuwia watu kufanya shuguli za kilimo, na watoto kwenda shuleni, ilisema ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Chanzo cha picha, Getty Images
CAR na Urusi kwa pamoja zinakana kwamba vikosi vyao vilitekeleza ukiukaji wa wahi za binadamu au vilitumia mabomu ya ardhini au vifaa vya vilipuzi vya mabomu.
Huku waasi wa 3R wamekuwa wakilaumiwa kwa kiasi kikubwa kwa kutega mabomu , waasi hao wanakana tuhuma hizi, waliwalaumu Warusi kwa kufanya .
Miaka zaidi ya 20 iliyopita, mkataba wa dunia ulipiga marufuku matumizi ya mabomu ya kutegwa ardhini kuwalenga watu binafsi, ingawa Urusi haikusaini mkataba huo na mabomu ya ardhini yenye lengo la kulipua magari hayamo chini ya makubaliano hayo .
'Hakuna suluhu la kijeshi'
Wataamu wanaonya kwamba, licha ya kusonga mbele katika mapigano, vikosi vya serikali havijawamaliza waasi, bali wamewarudisha nyuma tu katika maeneo machache na kuwalazimisha kutumia mbinu za vita vya msituni.

Hawajatatua uhasama wa kina ambao ulichochea uwepo wao-hali ya muda mrefu ya ghasia na kubaguliwa kwa rais Waislamu.
."Wiki hii, rais wa CAR Faustin-Archange Touadéra alipuuzilia mbali ukosoaji juu ya ushirika wake na Urusi, na akasisitiza yuko tayari kwa mazungumzo na waasi, akisema : "Sikuchagua vita hii."
Huku nchi ikidumbukia katika kina cha mkasa, raia ambao ndio wanaokabiliwa na athari za mapigano watakuwa na matumaini kwamba anachukua mweleko mwingine wa kuwaondoa katika limbo la mzozo.








