Uzazi: 'Uwongo' unaoenezwa na filamu za Hollywood kuhusu kujifungua mtoto

Katherine Heigl wakati wa tukio la kujifungua katika sinema ya 2007 Knocked Up

Chanzo cha picha, Universal Studios/BBC Mundo

Maelezo ya picha, Filamu ya Knocked Up ya mwka 2007, iliyoigizwa na nyota Katherine Heigl, ni moja wapo ya maonyesho mengi ya Hollywood iliyo na picha za kuzaa ambazo hutofautiana sana na kile kinachotokea katika maisha halisi.

Filamu za Marekani zimeangazia matukio mengi yanayoigiza mwanamke akijifungua, lakini matukio hayoa hayakaribiani na kile kinachofanyika kiuhalisia.

Ni mara ngapi tumeona wanawake wachangamfu, maji yao yakivunjika ghafla? Je na wenza wao ambao wanaonekana kutojua la kufanya na kubabaika hadi wanaishia kuzimia katika chumba cha kujifungulia?

Kisha baada ya yote hayo anatokea mtoto mzuri kutoka chini ya shuka akiangalia juu ya dari au upande wa kamera.

Daktari wa Uingereza Adam Key anaelezea kwa kina kile kinachotokea katika vyumba vya kujifungulia - pamoja na uchambuzi wa wataalam watatu - unaofichua dhana sita za kuzaa ambazo zimeendelezwa na filamu za Hollywood.

Sinema zaa Hollywood juu ya kuzaa mara nyingi hutofautiana sana ha hali halisi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Sinema zaa Hollywood juu ya kuzaa mara nyingi hutofautiana sana ha hali halisi

1. Hatuzaliwi tukiangalia juu

Kwa kawaida wakati mwanamke akijifungua kitu cha kwanza kutoka kupiti anjia ya uzazi ni kichwa cha mtoto.

Hili pia hufanyika katika filamu.

Lakini, katika runinga mtoto mchanga huonekana akiangalia juu, kwa hivyo unaweza kuona uso wa mtoto mara baada ya kuzaliwa. Kiuhalisia hili halifanyiki.

Zaidi ya asilimia 90 ya watoto huwa wameangalia chini kabla ya kuzaliwa - kichwa kinaangalia chini, kidevu kimeegemea kifua mikono iko karibu pamoja na huo mwili umejikunyata.

Hii inamaanisha uso umeelekea upande wa mgongo wa mama na kile ambacho kamera inaweza kuona ni kichwa cha mtoto,

Hatuzaliwi tukijua kuangalia kamera jamani!

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hatuzaliwi tukijua kuangalia kamera jamani!

"Nafasi ya asili wakati wa kuzaa ni kwa watoto kujielekeza wakitazama chini, au angalau kidogo kwa upande," anasema daktari wa wanawake na mtaalamu wa uzazi Damián Dexeus, kutoka Barcelona, ​​Uhispania.

"Na sababu ya mwelekeo huo ni kwamba inatoa nafasi nzuri kwa mtoto: ikiwa wanaangalia chini, wanaweza kutumia vyema nafasi ya kupita katika njia ya uzazi ya mama," anasema.

"Mara nyingi watoto wanaozaliwa katika filamu huonekana wakiangalia juu, macho yao yamefunguka - na hata kutabasamu wakati mwingine! Hilibila shaka sio jambo la kawaida," anaongeza daktari.

Pia watoto hawazaliwa wakiwa wasafi kama tunavyooneshwa katika sinema hizo.

"Watoto kamwe hawazaliwi wakiwa wasafi kabisa. Sijui ikiwa hili ni suala la urembo katika sinema au dhana," anasema Dkt Dexeus.

Mwanamke ameshikilia mtoto mchanga ambaye ana safu ya vernix kwenye ngozi yake

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ni nadra sana kuona sinema ikionesha vernix, dutu nyeupe ambayo inahufunika mwili wa mtoto wakati wa kuzaliwa

Anaelezea kuwa zamani hospitali zilikuwa zinaosha watoto punde wanapozaliwa na kisha kuwapatia mama zao wakiwa wasafi.

Hilo siku hizi halifanyiki, anaeleza daktari bingwa wa uzazi .

Hii ni kwa sababu dutu nyeupe inayofunika mwili wa mtoto wakati wa kuzaliwa ina umuhimu kwa mtoto.

2. Jinsi mfuko wa maji unavyopasuka

Picha zinazoonesha mfuko wa maji ya uzazi unavyopasuka ghafla,huku maji yakitiririka kutoka kwa mama ni jambo la kawaida filamu na vipindi vya Runinga.

Na moja kwa moja,mwanamke mjamzito anaanapata uchungu wa uzazi.

Kwa mfano katika kipindi televisheni cha uhalisia: Sex and the City, mfuko wa maji ya uzazi ya muigizaji Charlotte yalipasuka wakati akigombana mtu mbele ya mgahawa lakini baadae anaonekana akikimbia kwenda kuingia teksi.

Mchakato kati ya kuvunja maji na mtoto kuzaliwa ni mgumu zaidi ya kile kinachooneshwa katika kipindi cha televisheni cha Sex and the City.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchakato kati ya kuvunja maji na mtoto kuzaliwa ni mgumu zaidi ya kile kinachooneshwa katika kipindi cha televisheni cha Sex and the City.

Hii ni kwasababu sio rahisi watu kutofautisha maji ya uzazni na mikojo hasa.

Na ukweli ni kwamba kupasuka kwa maji ya uzazi ndio mwanzo wa mchakato wa kijifungua na ni mchakato ambao unaendelea.

3. Mwanamke anavyolala wakati wa kujifungua

Another common scene in films is for delivery to take place with the soon-to-be mum sitting on a raised birthing table.

Mwanamke akijifungua

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuna namna zaidi ya moja ya kulala wakati wa kijifungua, tofauti na ile tunayoona kawaida kwenye filamu

Kuna namna zaidi ya moja ya kulala wakati wa kijifungu, tofauti na ile tunayoona kawaida kwenye sinema au safu za Runinga.

"Nchini Uingereza na Marekani, ni kawaida kwa wanawake kuketi nusu, miguu yao ikiwa juu ya meza [ya kuzaa]," anasema Dkt Dexeus.

Njia hiyo ya kulala inategemea awmu ya leba y amwanamke mjamzito

Mwanamke pia anaweza kulala vingine ili kurahisisha kujifungua.

Yates anaamini kuwa picha hii ya uwongo juu ya kuzaa husababisha shida katika ulimwengu wa kweli.

"Ni vigumu kwa wanawake kuzaa kwa njia fulani na, kwa bahati mbaya, wengi wao wana matarajio ya kufanya kile wanachoona katika sinema."

Mchoro wa mwanamke akijaribu kuchuchumaa wakati wa kujifungua akiwa amejishikilia kwenye matofali

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mchoro wa mwanamke akijaribu kuchuchumaa wakati wa kujifungua akiwa amejishikilia kwenye matofali

4. Nini hufachofanyika baada ya mamam kujifungua?

Postpartum ni neno linalotumiwa kuelezea hali anayopitia mwanamke wiki ya kwanza baada ya kujifungua.

"Postpartum ni kitu kikubwa kinachosahaulika katika filamu nyingi", anasema Dkt Dexeus.

Mambo kadhaa yanayofanyika baada ya kujifungua ni nadra sana kuangaziwa katika filamu za Hollywood.

Vitu kama vile kushuka kwa nyumba ya uzazi (plasenta) - na majeraha anayopata mwanamke wakati wa kujifungua hayaangaziwi.

Saa 4 za kwanza punde baada ya plasenta kutoka huwa muhimu.

Baadhi ya wataalam wamekipa kipindi hiki jina awamu ya nne ya leba. Mwanamke anaweza kuvuja damu kwa wingi baada ya plasenta kutoka.

Nasio hayo tu kuna mengine mengi.

Hollywood inatuhumiwa kupuuza maswala kama unyogovu baada ya kuzaa, wakati nyota za filamu kama Brooke Shields amezipitia katika maisha halisi

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Hollywood inatuhumiwa kupuuza maswala kama unyogovu baada ya kuzaa, wakati nyota za filamu kama Brooke Shields amezipitia katika maisha halisi

Sinema hazionyeshi jinsi ugumu wa kunyonyesha unaweza kuwa, jinsi kuzaa kwa mtoto kunaweza kuathiri kibofu cha mkojo cha mwanamke na hali kadhaa za mabadiliko ya mwili ambayo inaweza kuwa ngumu sana kwa wanawake.

"Pia hawaoneshi changamoto anazopitia mama aliyejifungua kupitia njia ya upasuaji kabla ya kupona," anasema Dkt Dexeus.

"dhana hizi zinapelekea watu kufikiria kujifungua mtoto ni tukio hatari sana - kwa sababu kwa sababu sio kila wakati huwa hivyo "anaongeza.

5. Kupiga kelele kwa maumivu

Hali nyingine ya kawaida katika filamu za Hollywood ni wakati mama anapiga kelele kwa maumivu wakati wa kujifungua.

"Zamani wanawake walikuwa wakijifungua bila kudungwa singano ya kufisha ganzi ", anaelezea daktari wa Cuba Josefina López.

"Ni kweli uchungu wa uzazi ni mkali usiomithilika hasa ukichukua mudu mrefu wakati mama amechoka. Lakini sio uchungu ambao utamfanya kupiga kelele, ijapokuwa watu hutofautiana na kila mmoja ana namna yake ya kukabiliana na uchungu."

Wataalam wanasema kiuhalisia ni wanawake wachache hupiga kelele wakati wa kujifungua

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wataalam wanasema kiuhalisia ni wanawake wachache hupiga kelele wakati wa kujifungua

Yates Anadhani kuwa sinema wakati mwingine huwafanya wanawake waonekane dhaifu katika matukio ya kuzaa.

"Wanawake ni wajasiri. Hili ni jambo linalojulikana kote ulimwenguna," anasema mkunga huyo .

"Na wana uwezo wa kuhimili uchungu wa uzazi- bila kupiga mayowe."

"Ni ukweli, wakati mwingine wanapiga mayowe lakini ni wanawake wachache hupiga kelele wakati wa kujifungua ukilinganisha na kile kinachoigizwa katika filamu" Yates aliongeza kusema.