Vita vya Afghanistan: Taliban yarejelea ukatili wanapofanya mashambulio ya kurudi madarakani

Wapiganaji wa Taliban mjini Balkh
Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Taliban huko Balkh na meneo mengine wameimarisha mashambulio yao katika wiki za hivi karibuni

Wapiganaji wa Taliban tuliokutana nao wako nje kidogo ya miji mikuu ya Mazar-i-Sharif.

"Ghanimat" au nyara za vita wanazojigamba nazo ni pamoja na magari mawili aina ya pick up na shehena ya bunduki za nguvu.

Ainuddin, mwanafunzi wa zamani wa madrassa (shule ya dini) ambaye sasa ni kamanda wa jeshi, anasimama katikati ya umati uliojihami kwa silaha nzito.

Wanamgambo wamekuwa wakiteka maeneo mapya karibu kila siku baada ya majeshi ya kimataifa kuondoka nchini. Raia wa wameachwa na hofu ya kushambuliwa.

Mamia kati ya maelfu ya raia wa Afghanistan waliotoroka mwakwao- wameuawa na wengine kujeruhiwa katika wiki za hivi karibuni.

Ninamuuliza Ainuddin anawezaje kuhalalisha vurugu, kutokana na maumivu yanayowapata watu anaodai anapigania kwa niaba yao?

"Wanapigana, kwa hivyo watu wanafariki," anajibu kwa madaha, akiongeza kuwa kundi hilo linajaribu kadri ya uwezo wake "lisiwaumize raia".

Taliban fighters in Balkh, with captured Humvee
Maelezo ya picha, Wapiganaji wa Taliban wakionesha magari mawili waliyochukua

Niliwaambia kuwa Taliban ndio walioanza mapigano.

"La hasha," alisema. "Tulikuwa na serikali ambayo ilipinduliwa. Wao [Wamarekani] walianza mapigano."

Ainuddin na Wataliban wote wanahisi ushindi ni wao, na wanaelekea kurejea tena madarakani baada ya kuondolewa katika uvamizi wa kijeshi ulioongozwa na Marekani mwaka 2001.

"wasipoacha mtindo wa maisha ya magharibi … tutalazimika kuwaua," alisema kuhusu "serikali ya kikaragosi" iliyopo mjini Kabul.

Muda mfupi baada ya kumaliza kuongea nao tunasikia sauti ya ndege aina ya helikopta juu yetu.

Magari ya Humvee na wapiganaji wa Taliban walitawanyika haraka. Hii ni ishara kwamba vikosi vya angani vya Afghanistan bado ni tishio kwa wanamgambo hao, na kwamba vita hivyo havijakiribia kumalizika.

Afghanistan map
1px transparent line

Tuko Balkh, mji wenye mizizi ya kale, unaoaminiwa kuwa eneo alilozaliwa mshairi maarufu wa Kiislamu, Jalaluddin Rumi.

Tulipitia hapa mapema mwaka huu, wakati tulipokuwa tukiongozwa na serikali, lakini vijiji vilivyompakana na mji huu vilikuwa vikishikiliwa na wanamgambo wa Taliban.

Lakini sasa ni moja ya karibu wilaya 200 zilizotekwa na wanamgambo katika shambulio lisilokuwa la kawaida.

Taliban special forces (fighter kneeling bottom left) in Balkh district
Maelezo ya picha, Moja wa afisa wa vikosi maalum vya Taliba (aliyepiga goti) akiwa na Wataliban wengine mjini Balkh

Mmoja wa maafisa wa ngazi ya juu wa Taliban amesema hatua ya kulenga eneo la kaskazini ni la kimkakati- sio tu kwa sababu umekuwa mpinzani mkuu wa Taliban bali pia kuna masuala mengine muhimu yaliyozingatiwa.

Licha ya uongozi wake wa kimsingi kutawaliwa sana na jamii ya Wapashtun, afisa huyo alisema Taliban walitaka kusisitiza wanajumuisha makabila mengine pia.

Haji Hekmat, kiongozi wa Taliban wa eneo hilo na mwenyeji wetu huko Balkh, anataka kutuonyesha jinsi maisha ya kila siku bado yanaendelea.

Balkh bazaar

Tumeambiwa na vyanzo vya ndani kwamba wanawake waliruhusiwa kwenda kununua bidhaa wakiandamana na jamaa wa kiume lakini tulipofika hapo hali ilikuwa tofauti.

Kila mahali makamando wa taliban wameripotiwa kuweka vikwazo vikali

Wanawake wote tuliowaona walikuwa wamevalia mavazi ya kidini (burka) kufunika mwili mzima hadi uso.

Haji Hekmat inasistiza hakuna mtu "aliyelazimishwa" kuvalia hivyo na kwamba Taliban "inahubiri" hivyo ndivyo wanawake wanatakiwa kuvalia.

Lakini nimeambiwa na madereva wa texi kwamba wameamrishwa wasiwapeleke wanawake mjini ikiwa hawajavalia inavyotakikana.

Siku tuliyoondoka, ripoti ziliibuka kwamba mwanamke mmoja aliuawa kwasababu ya kuvalia visivyo. Ijapokuwa Haji Hekmat,amepinga madai hayo inasemekana wanamgambo wa Taliban walihusika na kifo chake.