Olimpiki Tokyo 2020: Fahamu jinsi mashindano Olimpiki ya kale ya Ugiriki yalivyokuwa

Alhamisisi wiki hii, pazia la michuano ya Olimpiki ya Tokyo linafunguliwa na mashindano makubwa zaidi ulimwenguni ya michezo yatatimua vumbi kwa kwa wiki mbili unusu.

Mashindano ya mwaka huu yalitakiwa kufanyika mwaka jana lakini yakaahirishwa kutokana na mlipuko wa janga la virusi vya corona. Mashindano ya Olimpiki ya Tokyo 2020 yanaingia katika rekodi mpya ya kujumuisha michezo 33 itakayohusisha matukio 339, ambayo yatafanyika katika viwanja 42 nchini Japan.

Hata hivyo michuano ya Olimpiki si mipya kama watu wengi wanavyodhani. Michezo hiyo ina asili ya Ugiriki na ilianza zaidi ya miaka 2,700 iliyopita mjini Olympia. Hi yo ni takribani miaka 700 kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo

Kila baada ya miaka minne, karibu watu 50,000 kutoka ulimwengu wa Ugiriki walihudhuria michezo hiyo mikubwa , ambayo pia ilikuwa hafla ya kidini ambapo walisherehekea kwa heshima ya Zeus, mfalme wa miungu.

Hakukuwa na nishani ya dhahabu, fedha au almasi. Wahindi walipokea taji ya mizeituni na kukaribishwa nyumbani kwa shujaa. Wanariadha walishindania utukufu wa jiji lao na washindi walichukuliwa kuwa wameguswa na miungu.

Hebu tafakari kama ungeliweza kuhudhuria?

Naam tunakukaribisha katika michezo ya Olimpinki ya 436 BC (kabla ya Kristu).

Huu hapa muongozo wa utakaokusaidia kuelewa jinsi watu walivyosafiri kwenda kuhudhuria michezo hii ya kale.

Mwafaka wa amani ya Olimpiki inatumika kinadharia kwa muda wa Michezo, vita vinavyoendelea haviwezi kusimamishwa katika maeneo na mikoa fulani.

Hii inamaanisha kuna uwezekano mkubwa wa kujikuta mashakani, kwa hivyo kuwa mwangalifu wakati wa safari.

Kumbuka: Hakuna mwanamke atakayeruhusiwa kuingia Olympia wakati wa michezo hiyo. Ni wanaume na wanawake ambao hawajaoa au kuolewa waliruhusiwa!

Mahali pa kuishi ni wapi?

Maelfu ya watu watawasili makao makoa makuu, ambayo ni matakatifu ya kidini wala sio jiji lililo na miundo mbinu iliyokamilika.

Twasikitika, Olympia kwa sasa ina hoteli moja tu,( the Leonideo), ambayo gharama yake ilikuwa ya juu sana kwa mashabiki wa Olimiki, kwa hivyo ilitengewa wageni wa heshima na maafisa wa michezo.

Mahema ya kukodisha yanaweza kupatikana kwani ni maarufu sana, lakini ni ghali.

Baadhi ya wahudhuriaji hubeba mahema yao, lakini kuna wengine wanaamua kulala chini.

Chakula

Vyakula vya kila aina vinapatikana nje ya uwanja na kando ya sehemu wanariadha wanakimbilia, lakini kuwa mwangalifu wafanyabiashara walaghai huenda wakaltoza bei ya juu kupita kiasi. Na hakikisha una pesa za kutosha.

TJando na hilo jiandae kwa karamu siku ya tatu ya michezo hiyo, wakati ng'ombe 100 kwa kawaida hutolewa kama sadaka kwa mungu wa mbinguni na radi, Zeus.

Siku hiyo,inageuka kuwa mahasusi kwa ajili ya milo maalum.

Ijapokuwa sehemu ya nyama inatengewa Zeus, inayobakia hugawanywa kwa wahudhuriaji 50,000 kwa hivyo hakuna aliyekosa kula.

Cha kujionea

Bila shaka hakuna mtu anayetarajiwa kuhudhuria michezo hiyo na kuwa na hofu yaa kutafuta pa kulala na chakula - kila mmoja yuko hapa kwa ajili ya michezo! Lakini je ni wapi mtu anaweza kujionea tafrija hii maarufu?

Siku ya 1

Siku ya kwanza ni hafla ya sherehe.

Ni wakati ambapo wanariadha hufanya maonyesho yao ya kwanza, haswa kula viapo ambavyo vinawataka kutii sheria, utamaduni ambao umehakikisha kuwa Michezo ni hafla bora ya michezo tofauti katika ulimwengu unaojulikana

Na sio wanariadha pekee ambao huahidi utii kwa uchezaji wa haki - majaji lazima pia wajitolee kuhakikisha Olimpiki iko huru dhidi ya ufisadi.

Baada ya ulaji kiapo kukamilika, wachezaji wanapewa nafasi ya kuamua ni wapiga tarumbeta watapewa heshima ya kutumbuiza.

Kisha inaamuliwa ni akina nani watatangaza majina ya wanariadha watatoa utangulizi kabla ya kila mbio na pigano.

Siku ya 2

Kwenye uwanja wa mbio, michezo ya farasi, ambayo ni maarufu, inaanza shughuli za siku hiyo.

Kuna kila aina ya michezo, ikiwemo mbio za farasi wakubwa wanne wanaovuta mkokoteni kila mmoja na pia ya farasi wadogo

Lakini kumbuka: Hata mwendeshaji farasi awe na ujuzi nama gani, washindi halisi ni wamiliki wa farasi. Baada ya yote, wao ndio hupata nyara.

Nyakati za mchana, mashindano maarufu ya pentathlon inafanyika, kipimo cha mwisho cha hali ya mwili wa mwanariadha na uwezo wa kimichezo.

Ndani ya saa kadhaa, wahusika washiriki michezo mitano tofauti: kurusa sahani(disuss), kuruka, kurusha, mkuki, kukimbia na mieleka.

Yeyote atakayevikwa taji ya ubingwa atasalia nayo kwa kipindi cha miaka minne ijayo .

Siku ya 3

Hii ni siku ya mapunziko na kujivinjari kwa ujumla, bila kuwa na shughuli zozote za michezo.

Kuchinjwa kwa ng'ombe 100 ndio ajenda kuu ya siku.

Siku ya 4

Siku hii mashindano tofauti za mbio zinaanza uwanjani.

Mbio uwanja ni moja ya matukio ya kuvutia sana na kufanya iwe maarufu zaidi.

Mbio zingine maarufu ni za kukimbia ukiwa umejihami pia, ambamo wanariadha hushindana wakiwa wamevaa ngao, helmeti na mabamba.

Baada ya chakula cha mchana, michezo ya mapigano hufanyika.

Hii inajumuisha ndondi, mieleka pamoja na, pankration, ambayoni mchanganyiko wa ndodni na mieleka. Umati wa watu huwa mkubwa kila wakati kwa hafla hizi, kwa hivyo hakikisha unafika mapema.

Fahamu kuwa michezo hii sio ya watu wenye roho ndogo.

Mchezo wa pankration haswa huwa wa kikatili, kwani una mashariti machache ya kupunguza kasi ya washiriki.

Vizuizi pekee ni kwamba wapiganaji hawapaswi kuuma wapinzani wao, kutoboa macho yao, kuingiza vidole puani, au kulenga sehemu zao za siri.

Kando na hayo, mengine yote yanakubaliwa!

Siku ya 5

Siku ya mwisho ya Michezo inawapa wale waliopo fursa ya kuwapongeza mabingwa.

Mshindi wa kila mchezo anapewa taeria (Ribbon nyekundu ya sufi inayoashiria bingwa wa Olimpiki), na anavikwa taji ya sherehe ya majani ya mizeituni.

Siku iliyobaki hutumiwa kusherehekea maonyesho ya juhudi za michezo na utukufu ambao wahudhuriaji wameshuhudia katika siku za hivi karibuni.

Washindi wa Michezo hiyo wanaalikwa kwenye karamu ya kipekee ambayo pia inahudhuriwa na majaji, pamoja na wanasiasa na wageni wa heshima walioalikwa.

Namna ya kuishi

Michezo hiyo hufanyika wakati wa msimu wa joto, ambayo ni hatari. Ndio sababu ni muhimu kunywa maji yakutosha, ijapokuwa kuna uhaba wa maji kutokana na kupungua kwa viwango vya maji katika mto Cládeo.

Inatarajiwa siku zijazo chemi chemi ya maji ya kunywa itajengwa Olimpiki. Kwa sasa kinachopatikana kwa wingi ni mvinyo.

Pia ni muhimu kujua kwamba kutokana na uhaba wa maji kwenye mtu msimu huu wa mwaka, kuna uwezekanomdogo wa kuoga wakati wa sherehe hizo.

Kutokana na hali ya joto jingi na mkusanyiko wa maelfu ya watu waliokaribiana harufu ya Olimpiki bila shaka sio ya kuridhisha.

Kupata kivuli ili kupumzika ni changamoto, kwa hivyo ukipata kivuli chini ya miti ya zeituni jaribu kutulia hapo kwa muda mrefu.

Hata bila ya kuwa na joto kali na kinywaji baridi , kusimama saa 16 kwa siku kufuatilia matukia kunweza kuchokesha.

Kuna viti vichache uwanjani, na vimetengewa wageni mashuhuri na wanasiasa.

Kwa hivyo tumia nafasi unayopata kupumzisha miguu yako.

Onyo: Maeno yaliyo nje ya uwanja yamejaa matapeli kuwa mwangalifu zaidi usije ukapoteza pesa zako

Usikose...

Kitu kingine muhimu, kuna nafasi nzuri ya ktumia michezo hiyo kujiburudisha.

Katika siku hizo chache michezo ya Olimpiki kuna kila aina ya maonyesho ya kupendeza na sehemu tofauti za kujivinjari.

Katika kambi ya malazi kuwa washairi wanaoghani tungo zao, hotuba za wanasiasa , wanafilosofia wanaopeana mafunzo yao, wanahistoria waliyo tayari kuwafahamisha na kuwaelimisha watu.

Adhabu ya kuvunja sheria?

Ijapokuwa majaji hawakuwa na teknolojia ya kisasa kuwaadhibu wanaovunja sheria, walikuwa wakali sana na hawakuwa na huruma katika adhabu walizozitoa.

Adhabu ya kuchapwa viboko ilitolewa hata kwa makosa madogo, kama vile kuanza mbio kabla ya firimbi kupulizwa (na wakati mwingine mwanariadha alishurutishwa kukimbia akiwa uchi).

Hatua kama hizo zilihitajika ili kuzuia udanganyifu, ambao ulijitokeza mara kwa mara.

Kuna, mifano michache ya uvunjifu wa sheria kama vile wanandondi kupokea rushwa na kupoteza pigano lao makusudi.

Kwa makosa makubwa zaidi kulikuwa na faini, fedha zilizochangishwa zilitumiwa kugharamia ujenzi wa safu ya sanamu za shaba za Zeus.