Fahamu kwanini mwanamfalme wa Saudia na mwenzake wa UAE wanazozana suala linaloathiri bei ya mafuta duniani

Mianya imeanza kujitoleza katika ya wanawafalme wa Saudia na UAE

Chanzo cha picha, Reuters

Uhasama kati ya UAE na Saudia kuhusu uzalishaji wa mafuta wiki hii ulifanya mazungumzo kati ya wazalishaji hao wawili wa mafuta duniani kufutiliwa mbali na kuwacha masoko ya mafuta katika hali ya kutatanisha hatua iliofanya bidhaa hiyo kupanda bei kwa mara ya sita mwaka huu.

Wanachama wa mataifa 23 yanayozalisha mafuta na kuuza duniani mbali na wazalishaji kama vile Urusi walilazimika kuahirisha mkutano huo ghafla , na kuzua hofu kuhusu udhibiti wa kundi ambalo limesambaza mafuta katika kipindi cha miezi 18 ili kukabiliana na mzozo wa kiuchumi unaosababishwa na virusi vya corona.

Tatizo lilianza wiki iliopita , wakati UAE ilipokataa pendekezo la wanachama wawili wa Opec+ Saudia na Urusi kuongeza usambazaji wa Mafuta kwa kipindi cha miezai minane ijayo.

Mashine ya kuchimbua mafuta kamailivyoochapishwa katika 3D

Chanzo cha picha, Reuters

UAE ilitaka kuanzisha mazungumzo mapya kuhusu nyongeza au punguzo la faida ya mafuta yake - ili kuweza kuipatia uhuru kuzalisha wa mafuta zaidi.

Hatahivyo, Saudia na Urusi walikuwa wanapinga wazo hilo.

Mazungumzo hayo yalichukua mwelekeo tofauti wakati mawaziri wa kawi wa UAE na Saudia ambao ni washirika wa karibu kuamua kutangaza tofauti zao hadharani.

''Uhasama huo umewashangaza wengi, lakini pengine haungeweza kuepukika'' , anasema Ben Cahill, afisa mwandamizi katika kituo cha kimataifa cha mikakati na utafiti mjini Washington.

"Kiwango cha uzalishaji wa mafuta cha Abu Dhabi ni kinyume na kile cha Opec. Imewekeza fedha chungu nzima ili kuongeza kiwango cha Mafuta inachozalisha. Na sasa mahitaji yanaongezeka.

''Na hiyo ndio sababu UAE imekasirishwa katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kushindwa kuongeza kiwango chake cha uzalishaji wa Mafuta'', anaongezea.

Wanawafalme wawili

Kwa miaka kadhaa sasa , ushirikiano kati ya Saudia na UAE umepanga siasa za Arabuni. Ukaribu uliopo kati ya mwanamfalme Mohammed bin Salman na mwanamfalme mwenzake wa Abu Dhabi Mohammed bin Zayed umesaidia katika kuimarisha ushirikiano huo.

Mpigaji anayeungwa mkono na serikali ya Yemen akishika bunduki

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Mpigaji anayeungwa mkono na serikali ya Yemen akishika bunduki

Wote wawili wanaonekana kama viongozi wa maeneo yao na wana maono ya kimaendeleo.

Kwa miaka kadhaa sasa kumekuwa na ushirikiano mkubwa kuhusu masuala ya kimkakati.

Waliunda muungano wa jeshi mwaka 2015 ili kupigana vita dhidi ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen na kuiwekea vikwazo vya kidiplomasia y, kikiashara na kiusafiri Qatar mwaka 2017.

Lakini mianya katika uhusiano huo ilianza kujitokeza miaka miwili iliopita , wakati UAE ilipoondoa wanajeshi wake wengi nchini Yemen , na kuiwacha Saudia ikiwa haina raha.

Mwezi Januari , UAE ilikubali shingo upande kusitisha vikwazo dhidi ya Qatar licha ya kwamba ina wasiwasi kuiamini Doha.

Vilevile Saudia haikupendelea hatua ya UAE kurudisha uhusiano wake na Israel mwaka uliopita.

Waandishi wakitazama kuwasili kwa mjumbe wa Qatar kabla ya kufanyika kwa mkutano wa barazala mataifa ya Ghuba

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Waandishi wakitazama kuwasili kwa mjumbe wa Qatar kabla ya kufanyika kwa mkutano wa barazala mataifa ya Ghuba

Mianya hiyo ilianza kuzidi mwezi februari wakati Saudia ilipotaka makampuni makubwa ya kimataifa kupeleka makao yake makuu katika ufalme huo kufikia 2024 la sivyo zipoteze kandarasi za serikali yake.

Hatua hiyo ilichukuliwa kama shambulio dhidi ya Dubai {UAE} ambayo ndio eneo kuu la kibiashara la eneo la mashariki ya kati.

Baada ya UAE kuzuia makubaliano hayo ya Opec+ , Saudia ilionekana kulipiza kisasi kwa kusitisha ndege kwenda UAE.

Ilidai wasiwasi kuhusu maambukizi ya virusi vya corona . Lakini uamuzi huo ulijiri wakati wa likizo ya Kiislamu ambapo watu wengi huelekea Dubai kupumzika. Saudia pia ilitangaza kwamba haitaruhusu kuingiza nchini humo bidhaa zinazohusishwa na Israel na hivyobasi kuupatia pigo uchumi wa UAE unaotokana na biashara huria.

Mzozo uliopo katika Opec+ unatokana na uhasama wa kiuchumi , huku mataifa yote mawili yakijaribu kuweka uchumi wa mesto kwa kupunguza tegemeo la kuuza nje bidhaa za Hidrokaboni.

Huku Saudia ikiweka mkakati mzuri wa kuimarisha uchumi wake chini ya Mohammed bin Salman hivi sasa wanashindana katika sekta kama vile Utalii, huduma za kifedha na teknolojia.

''Saudi Arabia ndio taifa kubwa katika eneo hilo linaloanza kuamka. Na katika kiwango Fulani hatua hiyo inaitia wasiwasi UAE'' , anasema Neil Quilliam, mshirika katika jumba la Chatham mjini London..

Picha ya mji wa Dubai

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Picha ya mji wa Dubai

"Katika kipindi cha kati ya miaka 15 hadi 20, endapo Saudia itaimarisha uchumi wake kwa kiwango kikubwa basi huenda hatua hyo ikawa tisho kwa uchumi wa UAE."

Haijulikani iwapo Saudia na UAE watakubaliana kuhusu makubaliano mapya ya Opec+

Lakini Ali Shihabi, mchambuzi wa Saudia aliyekaribu na ufalme huo , haamini kwamba uhasama huo utaathiri uhusiano wao katika siku zijazo , hata iwapo wamejaribu kuafikiana bila mafikiano.

''Pande zote mbili zimeshindwa kuafikiana kuhusu masuala tofauti siku za nyuma'', anasema.

Kila uhusiano una misukosuko yake ikiwemo ule kati ya Marekani na Uingereza, lakini misingi ya uhusiano huo haiwezi kuvunja muungano uliopo''.