Uchaguzi wa Somaliland:Je kura itafanya nchi hii itambuliwe?

anasema mkurugenzi wa Taasisi ya Bonde la Ufa, Mark Bradbury.

Chanzo cha picha, AFP

Watu huko Somaliland wanatarajia kuwa uchaguzi wa Jumatatu utaongeza nafasi ya jamhuri iliyojitenga kupata kutambuliwa kimataifa kama serikali huru, anaandika mchambuzi wa BBC wa pembe ya Afrika Mary Harper.

"Nina shauku kupiga kura yangu," anasema Yasmin Abdi wa miaka 15. "Ninahisi kama mtu mzima sasa, karibu ninamiliki sehemu ya nchi yangu."

Anastahiki kupiga kura katika jamii ambayo watoto wa miaka 15 wanachukuliwa kuwa wazima, Bi Abdi ni nusu kabisa ya umri wa Somaliland, wa miaka 30 ambayo ilisherehekea siku yake ya kuzaliwa mnamo Mei 18.

Tangu kutangaza uhuru wake kutoka Somalia haijatambuliwa kimataifa lakini inafanya kazi kama taifa - na pasi yake, sarafu, bendera, serikali na jeshi.

"Somaliland inaweza kuishia kama mahali pekee katika Pembe ya Afrika ambayo ina aina yoyote ya uchaguzi wa kidemokrasia wakati wote mwaka huu," anasema mkurugenzi wa Taasisi ya Bonde la Ufa, Mark Bradbury.

Makamu Mwenyekiti wa chama kinachotawala cha Kulmiye, Ahmed Dheere, anaunga mkono maoni ya Bw Bradbury. "Siwezi kukueleza jinsi chaguzi hizi zilivyo na umuhimu," anasema. "Tutakuwa mwangaza wa jua wa Pembe ya Afrika ikiwa tutafanikiwa kupiga kura."

Somaliland inaweza kuwa ya kidemokrasia zaidi kuliko nchi nyingine katika eneo hilo, lakini mfumo wake sio kamili.

Kura ya bunge imechelewa zaidi ya miaka 10. Uchaguzi wa manispaa, ambao utafanyika wakati huo huo, ulipaswa kufanyika miaka minne iliyopita.

somaliland

Chanzo cha picha, AHMED KADLEYE

Mwanachama mwandamizi wa chama cha upinzani cha Waddani, Hersi Ali Haji Hassan, anawalaumu wabunge kwa ucheleweshaji.

"Wabunge wengi wana uchoyo na ubinafsi. Wamekuwa wakinenepa wakati wa miaka 15 bungeni na wanasita sana kuviachia viti vyao. Ninailaumu serikali kwa sababu imefaidika na hali ilivyo sasa."

Waandishi wa habari wanashikiliwa

Kuna shida nyingine pia. Baraza la Wawakilishi la Somaliland halina wajumbe kutoka koo ndogo na kuna mwanamke mmoja tu kati ya wabunge 82, ingawa wanawake wengi zaidi wanawania wakati huu.

Wagombea watano wa upinzani walikamatwa wakati wa kuelekea kupiga kura. Vitendo vya serikali kwa vyombo vya habari vinakuwa vigumu, huku waandishi wa habari wakinyanyaswa na kukamatwa, na ofisi za vyombo vya habari kufungwa.

Jitihada zimefanywa kuzuia vyama vya siasa kuhusishwa kwa karibu sana na koo za kibinafsi, na ni tatu tu zilizoruhusiwa kushindana katika uchaguzi wa wabunge.

Lakini mwenyekiti wa chama cha Justice and Development, Faisal Warabe, anaonya kuwa masuala ya ukabila ni hatari.

somaliland

Chanzo cha picha, OMER-SAYID HASSAN

"Mfumo wetu wa kikabila haiendani na demokrasia. Lazima tuusambaratishe. Vinginevyo Somaliland itaishia kama Yemen, na koo zinazoshindana zilizosambaratisha nchi yao," anasema.

Bwana Warabe anataka kumalizwa kwa nyumba ya Wazee au guurti, ambayo inaundwa na wanachama wakuu wa koo muhimu za Somaliland.

"Watu hao hao wamekuwepo tangu 1993, na mzee mmoja wa ukoo akifa anachukuliwa na mtoto wake. Hii sio demokrasia," anasema.

Ni ngumu kulinganisha hali ya Somaliland na ile ya Somalia.

''Somaliland iko umbali wa maili milioni moja kutoka Somalia, ambayo inaendelea kusisitiza kuwa sisi ni sehemu ya eneo lake lakini bado haiwezi kufanya uchaguzi hata usio wa moja kwa moja," anasema Abdi Ahmed, mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha Hargeisa.

Somaliland na Somalia

somaliland

Chanzo cha picha, AFP

Rais wa sasa wa Somalia, Mohamed Abdullahi Farmajo, aliahidi kufanya uchaguzi wa mtu mmoja kwa kura moja mnamo 2020, lakini haikutokea.

Nchi sasa ina mvutano kuelekea mchakato uliocheleweshwa sana na mgumu unaohusisha wazee wa koo ambao mwishowe unapaswa kusababisha wabunge kuchagua rais mpya.

Bwana Farmajo alipojaribu hivi karibuni, na akashindwa, kuongeza muda wake kwa miaka miwili, vikosi vya usalama viligawanyika, wengine wakimuunga mkono rais, wengine upinzani.

Vikundi tofauti vilichukua sehemu tofauti za mji mkuu, Mogadishu, na kulikuwa na kuibuka kwa wa vurugu.

somaliland

Chanzo cha picha, AFP

Wengine wanaweza kuona ajabu kwamba nchi ambayo haipo rasmi iko karibu kufanya uchaguzi wake wa saba tangu kujitenga na Somalia, nchi ambayo haijafanya uchaguzi wa kidemokrasia kwa zaidi ya miaka 50 - muda mfupi kabla ya Siad Barre kuchukua madaraka kwa mapinduzi mnamo 1969.

Bendera za kigeni zinaruka huko Somaliland

Wakati Somalia ikiwa imesambaratishwa na vita vya ukoo na vurugu za Kiislam kwa miongo mitatu, Somaliland imekuwa na amani kwa kiasi kikubwa.

Imeweza pia kufanya uchaguzi uliopiganwa kwa karibu, kubwa zaidi mnamo 2003 wakati Dahir Riyale Kahin alishinda urais kwa kura chache au karibu 0.01%.

Campaigning has taken place amid the coronavirus pandemic

Kura ya mwisho ya urais ya Somaliland ilifanyika mnamo 2017. Kama marais wanaweza kuhudumu kwa mihula miwili ya miaka mitano, uchaguzi ujao utafanyika mwaka 2022.

Jaribio la miaka 30 la kutaka kutambuliwa Somaliland limeshindwa hadi sasa.

Mataifa ya nje yanasema kwamba hadhi ya Somaliland inapaswa kuamuliwa na Umoja wa Afrika, ambayo inasita kushuhudia majimbo yakivunjika ikiwa itaweka muongozo katika bara ambalo mipaka iliwekwa na mamlaka za kikoloni.

Lakini licha ya ukweli kwamba haipo rasmi kama nchi, Somaliland inavutia maslahi kutoka sehemu tofauti za ulimwengu.

Idadi ya bendera za kigeni zinazopepea katika mji mkuu, Hargeisa, zinaongezeka wakati nchi zaidi zinafungua balozi au ofisi za wawakilishi.

Hizi ni pamoja na Djibouti, Ethiopia, Uturuki, Uingereza, Denmark, Falme za Kiarabu (UAE) na Taiwan, ambayo inajiona kama "kaka" wa Somaliland kwani zote zina hadhi isiyotambulika.

Kenya, ambayo imekuwa ikihusika katika mvutano wa muda mrefu na Somalia, na Misri wanapanga kuzifungua hivi karibuni.

ramani

UAE na makubaliano ya ujenzi wa bandari

Labda machafuko nchini Ethiopia yataifanya Somaliland kuvutia zaidi mamlaka za kigeni.

Mnamo mwaka wa 2016, UAE ilisaini mkataba wa miaka 30 wenye thamani ya karibu $ 500m kukuza na kusimamia bandari ya Berbera, ambayo imeelezewa kama ''mali yenye thamani zaidi katika pembe ya Afrika".

Barabara inajengwa ikiunganisha Berbera na Ethiopia, na kuipatia nchi hiyo isiyokuwa na bandari mbadala wa bandari iliyosongamana huko Djibouti.

somaliland

Somaliland ni tajiri katika mifugo - kondoo wake wa mikia iliyonona wanathaminiwa katika nchi za Ghuba.

Mamilioni ya wanyama husafirishwa kila mwaka, ngamia husafirishwa kwa njia ya anga kwenye meli wakati kondoo na mbuzi husafirishwa kwa njia za chini.

Somaliland ina rasilimali nyingine za asili, pamoja na akiba ya mafuta, makaa ya mawe na vito, bahari iliyojaa samaki.

Wengine labda wana matumaini kidogo juu ya kile uchaguzi huu utafanya kwa Somaliland.

Bwana Dheere wa chama cha Kulmiye anaamini kwamba kura zinaweza kusaidia eneo hilo kufikia lengo lake kuu.

"Ikiwa tutapata haki hii, tunadhani tutatambuliwa," anasema.