Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Namibia:Maafisa wa Ujerumani watambua mauaji ya halaiki dhidi ya jamii za Namibia wakati wa ukoloni
Ujerumani imetambua rasmi kwamba ilitekeleza mauaji ya halaiki wakati wa enzi ya ukoloni dhidi ya Namibia na kutangaza kuwa itaisaidia kupitia msaada wa kifedha.
Ujerumani waliokuwa wanatawala chini hiyo wakati wa enzi ya ukoloni walisababisha mauaji ya makumi ya maelfu ya watu wa Herero na Nama mapema karne ya 20.
Waziri wa mambo ya Nje Heiko Maas, Ijumaa alitambua kuwa kulitendeka mauaji ya halaiki.
"Katika historia ya Ujerumani na uwajibakaji wake, tunaiomba Namibia na kizazi cha waathirika msamaha," amesema.
Bwana Maas aliongeza kuwa Ujerumani, katika "hatua ya kutambua madhila yaliyotendewa waathirika", itasaidia maendelea ya nchi hiyo kupitia mpango wenye thamani ya zaidi ya euro bilioni 1.1 (£940m; $1.34bn).
Makubaliano hayo inasemekana kwamba yatakuwa ufadhili wa zaidi ya miaka 30 kupitia ujenzi wa miundo mbinu, afya na makubaliano ya programu za mafunzo kunufaisha jamii zilizoathirika.
Msemaji wa serikali ya Namibia alizungumza na shirika la AFP na kusema hatua ya Ujerumani kutambua yaliyotokea ilikuwa ni "hatua ya kwanza ya kufikia mwelekeo stahiki".
Lakini baadhi ya viongozi wa kimataduni wamekataa kuidhinisha makubaliano hayo na kuyakosoa.
Kipi kilichotokea wakati wa mauaji ya halaiki?
Taarifa iliyotolewa Ijumaa imewadia baada ya miaka mitano ya majadiliano na Namiba - ambayo ilikuwa chini ya Ujerumani kutoka mwaka 1884 hadi 1915.
Wakati huo, kulifanyika unyanyasaji, mateso na madhila ambayo yameelezwa na wanahistoria kama "mauaji yaliyosahaulika" mapema karne ya 20.
Umoja wa mataifa unaelezea matendo kadhaa ikiwemo mauaji yaliyotekelezwa kwa nia ya uharibifu kamili au sehemu, kitaifa, kikabila, ki ubaguzi wa rangi au makundi ya kidini.
Mauaji yalianza mwaka wa 1904 baada ya waasi wa Herero na Nama waliokuwa wanapinga unyakuzi wa ardhi na mifugo uliotekelezwa na Ujerumani.
Kiongozi wa utawala wa kijeshi, Lothar von Trotha, alitoa amri ya kuuawa na watu wa Herero na Nama wakalazimishwa kwenda msituni.
Kila aliyepatikana akijaribu kurejea kwenye ardhi yake ama aliuawa au kuwekwa kwenye kambi za mateso. Idadi ya waliofariki ilikuwa ni ya makumi ya maelfu - ingawa hakuna idadi kamili iliyorekodiwa.
Unyanyasaji na madhila yaliyotokea wakati huo yamekuwa yakiyumbisha uhusiano kati ya Ujerumani na Namibia huku kukiwa na majadaliano ambayo yamefanyika kwa miaka kadhaa kati ya serikali hizo na namna ya kutatua suala la mauaji ya halaiki.
Mwaka 2018, Ujerumani ilikabidhi baadhi ya mabaki ya binadamu ambayo yalikuwa yametumika kama sehemu ya utafiti ulioshutumiwa kuthibitisha umuhimu wa wazungu uliochukuliwa kuwa ubaguzi wa rangi.
Makubaliano ya hivi karibuni yamesemakana kukubaliwa wakati wa majadiliano yaliyofanywa na
Azimio linatarajiwa kitiwa saini na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani huko Namibia mwezi ujao kabla ya kuidhinishwa na bunge, vyombo vya habari vimesema.
Hatua hiyo imechukuliwa vipi?
Serikali ya Namibia imeelezea kukubali kwa Berlin kwamba ilitekeleza mauaji ya halaiki kama hatua ya kwanza muhimu ingawa kuna wale ambao wametofautiana na kauli hiyo.
Vekuii Rukoro, mkuu wa Herero ambaye alijaribu kuishtaki Ujerumani kwa ajili ya fidia katika mahakama za Marekani, amesema makubaliano hayo hayatoshi kufidia "uharibifu ambao hauwezi kurekebishika" dhidi ya walioteseka enzi ya ukoloni.
"Tuna matatizo na aina hii ya makubaliano, ambayo tunahisi kwamba nikusalitiwa upande wa serikali ya Namibia," ameelezea shirika la Reuters.
Bwana Maas alise akuwa majadadiliano yalilenga kutafuta muafaka utakaoleta maridhiano ya kweli katika kumbukumbu za waathirika huku watu wa jamii za Herero na Namazikiwa zimehusishwa kwa karibu katika majadiliano.
Viongozi kadhaa wa utamaduni walioshiriki majadaliano hadi kufikia sasa wamekataa kuidhinisha makubaliano nayo, vyombo vya habari vya Namibia vimesema.