Mzozo wa Israel na Palestina: Ni nani aliyeibuka mshindi baada ya kusitishwa kwa vita?

Chanzo cha picha, ANADOLU AGENCY VIA GETTY IMAGES
Baada ya kusitishwa kwa mapigano, raia wa Palestina huko Gaza ambao wamekuwa wakijificha kila wakati wakihofia kuuawa, walitoka nje na kwenda kuangalia kile kilichofanywa na jirani yake Israeli.
Watu walikuwa wanaangalia vifusi vya jengo la ghorofa ambalo lilikuwa limepigwa bomu na Israeli. Baadhi ya barabara zilikuwa zimefungwa kwa vifusi huku waokoaji wakiwa wanajitahidi kwa kila namna kuondoa vifusi hivyo.
Lakini hakuna kile kilchokuwa kinashangaza raia wa Palestina, kwasababu kila kitu ambacho kilikuwa kinatokea kimekuwa kikioneshwa katika runinga tena kwa kina. Lakini baadhi ya watu walipenda kuona kile ambacho kimetokea kwa macho yao wenyewe.
Katika mji wa Gaza wa Khan Yunis, kulikuwa na mazishi ya wapiganaji 9 waliouawa kufuatia kuanguka kwa sehemu ya handaki lililolengwa na Israeli.

Chanzo cha picha, Reuters
Wanasiasa wa Israel na viongozi wao walisema wamesababisha hasara kubwa kwa kile walichokiita ''miundo mbinu ya magaidi'' iliyokuwa inaendeshwa na kundi la Hamas.
Uharibu wa mejengo ulikuwa umedhihirika wazi na mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea ni kuwa kundi la Hamas lilishutushwa na uwezo wa Israel wa kuua wapiganaji wake wakati ambao walidhani kwamba wako salama chini ya ardhi.
Eneo la Khan Yunis lilikuwa linaendeleza sala ya maiti. Maelfu ya wanaume walikuwa katika uwanja wa michezo wakibeba maiti zilizofunikwa kwa kutumia bendera za Palestina, walikuwa wanakwenda makaburini huku wakipaza sauti kwa kusema maneno yanayoashiria kuunga mkono upande wao hadi walipofika makaburini.
Kila moja adai kuwa mshindi
Israel na Hamas wote walidai kupata ushindi katika vita hivi vya karibuni vilivyodumu kwa siku 11.
Viongozi wa Israel walitanagaza orodha ya majengo waliyoharibu na kutaja majina ya viongozi wa Hamas na wapiganaji waliokuwa wanawalengwa na kuwaua.

Chanzo cha picha, AFP VIA GETTY IMAGES
Kwa upande mwingine, Hamas ilichukulia kuwa kumudu vita hivyo ni ushindi kwao. Kamanda wake wa Gaza, Yahya Sinwar, alionekana kuwa bingwa mitaani baada kujitokeza kutoka kwenye makazi aliyokuwa amejificha baada ya vita kusitishwa. Kundi la Hamas linachukulia ushindi wa wanasiasa wake kuwa kitu kikubwa sana.
Misemo ya kundi la Hamas ilisikika katika msikiti wa Al-Aqsa huko Jerusalem baada ya sala, kilomita 96 kutoka mji wa Gaza. Hamas ikatuma ujumbe kwa Wapalestina kuwa iko tayari kupigana huko Jerusalem wakati ambapo Israel inasisitiza kuwa Jerusalem ni mji wake wa kudumu kimoja kati ya vinavyozozaniwa na pande hizo mbili.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas anatambulika kimataifa kama mwakilishi wa watu wa Palestina kupitia chama cha Palestine Liberation Organization na Mamlaka ya Palestina ambayo ina miliki sehemu ya eneo hilo kulingana na makubaliano ya Oslo miaka ya 1990.
Lakini raia wa Palestina hawajafurahishwa na kazi ya rais huyo kwasababu alifuta uchaguzi ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika Mei baada ya kuoneka kushindwa. Raia wa Palestina hawajapiga kura katika uchaguzi wa urais au uchaguzi wowote ule wa ubunge tangu mwaka 2006.
Kwa upande mwingine, ujumbe kutoka kwa Hamas wa utayari wao kupigana hadi kufa kupigania eneo la Jerusalem uliungwa mkono na raia wengi wa Palestina.
Israeli nako, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahau atarejea katika vita kwa misingi ya kisiasa hali ambayo alikuwa bado anaiweka katika mizani kabla ya vita na Hamas.
Netanyahau anakabiliwa na madai ya ufisadi ambayo huenda yakamsababishia kufungwa gerezani kama ilivyokuwa kwa mtangulizi wake, Ehud Olmert.
Mei 10, siku ambayo kundi la Hamas lilichochea vita kwa kurusha roketi upande wa Jerusalem, Waziri Mkuu alikuwa katika hatari ya kupoteza nafasi yake.
Siasa za Israel
Katika uchaguzi uliofanyika Israeli, Netanyahau alishindwa kuunda serikali ya muungano ambapo alihitajika kupata asilimia 61 ya kura ili kumuwezesha kuwa na wingi wa kura bungeni.
Pia, Israeli ina kibarua kigumu cha kukabiliana na kutoelewa ambako kumekuwepo kati ya Wayahudi walio wengi na raia wa Palestina walio wachache, ambao ni takriban asilimia 20 ya idadi yote ya watu. Lakini mgogoro wao umeongezeka zaidi kipindi cha Netanyahu.

Chanzo cha picha, Reuters
Makubaliano ya kusitisha vita ya sasa hivi yamewahi kutokea nyakati za nyuma kati ya Israeli na Hamas. Mgogoro wao bado haujatatuliwa. Na lolote linaweza kutokea pengine kurushwa kwa bomu kutoka upande wa Gaza au vurugu zaidi kutoka kwa polisi wa Israeli kuelekea upande wa Palestina huko Jerusalem.
Baada au pengine mtihani huo utarejea kwa mfumo wa kesi iliyowasilishwa na kundi la wakazi wa Israeli wanaotaka kuwafurusha Wapalestina kutoka kwenye makazi yao katika eneo jirani la Jerusalem Mashariki lililokaliwa.
Jaribio la kufurusha familia za Wapalestina kutoka kwenye kaya zao na kuwapeleka katika makazi ya Wayahudi ndio iliokuwa sababu ya kuanza kwa vita huko Jerusalem.
Uamuzi wa kesi hiyo uliahirishwa kama hatua moja ya kutuliza hali. Lakini, bedo kes hiyo inaendelea na uamuzi katika kesi hiyo utatolewa aa hivi karibuni au siku za baadaye.
Ingawa, mipango ya Israeli huenda ikawa ndio changamoto kubwa katika usitishaji wa vita sasa hivi.













