Ndege 15 aina ya Tai 'wateka nyumba na kutangaza vita' na mmiliki wake Marekani

A rare and endangered California condor flies through Marble Gorge, east of Grand Canyon National Park, 22 March 2007

Chanzo cha picha, David McNew/Getty Images

Maelezo ya picha, Inaaminika kuwa kuna chini ya tai 500 Marekani na kati yao 160 pekee ndio wamerekodiwa kuwepo California.
Muda wa kusoma: Dakika 2

Kundi la ndege waliopo hatarini kutoweka nchini Marekani aina ya Tai wa California 'limeiteka' nyumba moja katika jimbo la California na "kutangaza vita" na mmiliki wake, familia ya mmiliki huyo imeeeleza.

Takriban tai 15 wakubwa wanaripotiwa kutua na kufanya makazi katika nyumba ya Bi Cinda Mickols katika jiji la Tehachapi toka mwishoni mwa wiki iliyopita.

"Bado hawajaondoka," anaeleza Seana Quintero ambaye ni binti wa mwenye nyumba hiyo, huku akiongeza kupitia mtandao wake wa Twitter kuwa ndege hao "wamechafua kabisa nyumba hiyo kwa kinyesi."

Inaaminika kuwa kuna chini ya ndege wa aina hiyo 500 katika Marekani yote na takribani 160 pekee ndio wamerekodiwa kuwepo California.

Kwa mujibu wa Bi Quintero, ambaye amekuwa akitoa taarifa za mara kwa mara juu ya "uvamizi" huo, ndege hao wamekuwa "wakiambaa ambaa kwenye nyumba hiyo kwa vitisho."

"Mama yangu, mwenye umbo dogo tu alikuwa akiwatazama kundi la ndege wakubwa ambao ni nusu ya umbo lake akiwa umbali wa mita tatu tu," ameandika Bi Quintero na kuongeza, "amejaribu kuwafukuza lakini bado wapo kwenye paa lake ambapo wanaharibu kila kilichopo nje ya nyumba hiyo huku wakitapakaza kinyesi."

Ruka X ujumbe, 1
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 1

Presentational white space

Wanawake hao wawili, mama na binti yake wanasema hawapingani na uwepo wa ndege hao kwenye nyumba yao, lakini tatizo ni uharibifu wanaoufanya kuanzia kwenye makopo ya maua, michoro ya kwenye kuta na vioo vya madirisha na milango.

Ruka X ujumbe, 2
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 2

Presentational white space

Mamlaka ya Uhifadhi wa Samaki na Wanyamapori (USFWS) imejibu baadhi ya ujumbe wa Bi Quintero mtandaoni na kusema kwamba ndege hao wanalindwa kwa mujibu wa sheria na nyumba ya mama yake imejengwa katika eneo la asili la makazi ya ndege hao.

"Kama hali hiyo itatokea tena, namna ya kuwazuia kufanya uharibifu bila kuwadhuru ndege hao ni pamoja na kuwamwagia maji kwa kutumia mpira, kupiga kelele ama kupiga makofi," mamlaka ya USFWS imeeleza.

Ruka X ujumbe, 3
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa X ujumbe, 3

Presentational white space

Bi Quintero anasema mama yake amefanyia kazi ushauri wa mamlaka hiyo na "amewaogesha" mara kadhaa tai hao kwa kutumia mpira. "Sasa kundi zima limerejea na wapo kwenye mti wake. Wakimuangalia. Wakisubiria. Wancheza michezo yai ya kitai," amesema.

Tai wa California, moja ya ndege wakubwa kabisa wawindaji duniani wanalindwa na sheria nchini Marekani kama viumbe vilivyomo hatarini kutoweka toka mwaka 1967 na jimbo la California toka 1971, kwa mujibu idara ya Samaki na Wanyamapori ya California.

Presentational white space
Maelezo ya video, Fahamu jinsi ndege kwa jina tai walivyo katika hatari ya kuangamia Afrika