Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Afghanistan: 'Tumeshinda vita, vilivyoshinda Marekani', wanasema Taliban
Kusafiri katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Taliban haichukui muda mrefu. Karibu dakika 30 kutoka mji wa kaskazini wa Mazar-e-Sharif, kupitia mabaki ya magofu ya nyumba zilizolipuliwa kwa mabomu, tunakutana na mwenyeji wetu: Haji Hekmat, Maya kivuli wa Taliban katika wilaya ya Balkh.
Bw. Hekmat ni mwanachama mkongwe wa kundi hilo, baada ya kuungana nalo mara ya kwanza miaka ya 1990 walipoongoza sehemu kubwa ya nchi.
Taliban wamepanga kutuonesha vikosi vyao. Wanaume waliojihami kwa silaha walipanga foleni pande zote mbili za barabara, mmoj akiwa na kifaa cha kurusha roketi, mwengine akiwa na bunduki aina ya M4 iliyochukuliwa kutoka kwa vikosi vya Marekani.
Balkh wakati mmoja ilikuwa sehemu tulivu zaidi nchini; lakini sasa imegeuka kuwa moja ya sehemu zinazokumbwa na ghasia.
Baryalai, kamanda wa kijeshi wa eneo hilo aliye na sifa ya ukatili, ananyoosha mkono upande wa chini wa barabara na kusema "majeshi ya serikali yamepiga kambi karibu na soko kuu, lakini hawawezi kuthubutu kutoka kambini kwao. Eneo hili inamilikiwa na mujahideen".
Taswira ni hiyo hiyo katika maeneo tofauti nchini Afghanistan: serikali inadhibiri miji mikuu namaeneo yaliyo karibu, lakini Taliban imeanza kuchukua udhibiti wa baadhi ya maeneo.
Wanamgambo hao wanaonyesha uwezo wao kupitia vituo vya ukaguzi kando ya barabara kuu. Wanamgambo wa Taliban wanasimamisha magari na kuwahoji madereva, Aamir Sahib Ajmal, mkuu wa intelijensia wa Taliban katika eneo hilo, aliambia BBC kuwa wanatafuta watu walio na mafungamano na serikali.
"Tutawakamata, na kuwapeleka jela," anasema . "Kisha tuwafikishe mbele ya mahakama zetu kuamua kitakachofuata baadae."
Taliban wanaamini ushindi ni wao. Anasema Haji Hekmat, "Tumeshinda vita ambavyo vimewashinda Wamarekani".
Hatua ya Rais wa Marekani Joe Biden, kuchelewesha hatua ya kuondoa vikosi vyake hadi mwezi Septemba, inamaanisha vikosi hivyo vitasalia nchini humo hadi baada ya muda wa mwisho wa tarehe moja Mei kama ilivyofikiwa mwaka jana, imekosolewa vikali uongozi wa kisiasa wa Taliban. Wanamgambo wa kundi hilo wanaonekana kuwa tayari kutekeleza maagizo yoyote kutoka kwa wakuu wao.
"Tuko tayari kwa lolote," anasema Haji Hekmat. "Tumejiandaa kikamilifu kwa amani, na pia tukotayari kwa jihad." Kamanda wa kijeshi aliyekaa karibu naye, aliongeza: "Jihad ni kitendo cha ibada. Ibada ni kitu ambacho huchoki hata ukafanya mara ngapi ."
Katika miaka iliyopita, kumekuwa na ubishi kuhusu maana ya "jihad'' ya Taliban.
Walikomesha mashambulio dhidi ya vikosi vya kimataifa baada ya kutia saini makubaliano waliofikia na Marekani, lakini wakaendelea kupigana na vikosi vya serikali ya Afghanistan.
Haji Hekmat, hata hivyo anasisitiza hakuna ubishi. "Tunataka serikali ya Kiislamu inayoongozwa kwa misingi ya Sharia. Tutaendelea na jihad yetu hadi waitikie maombi yetu."
Suala la ikiwa Taliban wako tayari kushirikiana na makundi mendine ya kisiasa nchini Afghanistan, Haji Hekmat ameelekeza BBC kwa uongozi wa kisiasa nchini Qatar. "Tutakubaliana na kile Kile watakachoamua," alirudia kusema.
Taliban hawajichukulii kama kundi la waasi, bali ni serikali inayosubiri kuinga madarakani. Wanajiita "Islamic Emirate of Afghanistan," Jjina walilotumia walipokuwa madarakani kuanzia 1996 hadi walipotimuliwa baada ya shambulio 9/11.
Waandishi wa BBC walioneshwa shule ya msingi, iliyokuwa na wasichana na wavulana wakisoma vitabu vilivyotolewa kama msaada na Umoja wa Mataifa.
Walipokuwa madarakani miaka ya 1990, Taliban walipiga marufuku elimu ya watoto wasichana, ijapokuwa awanapinga hilo.
Hata sasa, kuna ripoti ya kwamba wasichana wakubwa hawaruhusiwi kuenda darasani. Lakini katika eneo hili Taliban wanasema wanaunga mkono elimu ya watoto wasichana.
"Bora wavalie hijab, ni muhimu wapate elimu," anasema Mawlawi Salahuddin, kamishena anayesimamia masuala ya elimu katika eneo hilo.
Katika shule za upili, anasema waalimu na wa kike pekee wanaoruhusiwa kufunza, na lazima wajifunike nywele zao. "Wakifuata Sharia ya Kiislamu, hakuna shida."