Uvamizi wa Jumba la Capitol Hill Marekani : Bunge lamuidhinisha Joe Biden kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais Marekani

Bunge la Congres limemuidhinisha Joe Biden na Kamala Hariss kama rais mtarajiwa na makamu wake wa Marekani.
Bunge hilo liliwaidhinisha wawili hao kwa kura 282 huku wabunge 138 wakipiga kura ya kupinga matokeo ya jimbo la Pennsylvania.
Bunge la seneti lilikataa pingamizi kama hiyo.
Kura za wajumbe zilithibtishwa baada ya mabunge yote mawili lile la uwakilishi na lile la seneti kukataa pingamizi kuhusu kura zilizopigwa katika vituo vya jimbo la Pennsylvania na Arizona.
Shughuli za bunge zilikatizwa siku ya Jumatano wakati wafuasi wa rais Trump walipovamia jumba la Capitol Hill.
Shughuli baadaye zilirejea na kuendelea usiku kucha baada ya waandamanji hao kutolewa.

Chanzo cha picha, Reuters
Bunge la uwakilishi pamoja na lile la Seneti litaendelea kuhesabu kura za wajumbe zilizosalia ili kumuidhinisha Joe Biden kuwa rais mtarajiwa wa Marekani.
Makamu wa rais Mike Pence alitoa tangazo hilo pamoja na Spika wa bunge la uwakilishi Nancy Pelosi, katika mkutano wa pamoja wa mabunge yote.
Wakati huohuo Rais Donald Trump ametoa taarifa akikubali kukabidhi madaraka kwa njia ya amani tarehe 20 mwezi Januari huku akirudia madai yake ya awali kwamba uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu.
''Licha ya kwamba sikubali na matokeo ya uchaguzi na ukweli upo, kutakuwa na shughuli ya amnai ya kukabidhi mamlaka ifikiapo tarehe 20 januari'' , alisema katika chapisho lililochapishwa katika akunti ya twitter ya msemaji wake.
Twitter imefunga kwa muda akaunti ya rais huyo anayeondoka madarakani.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 1
''Nimekuwa nikisema mara kwa mara kwamba ni kura halali pekee zinahesabiwa. Huku hatua hiyo ikiwakilisha mwisho wa kuifanya Marekani kuwa bora zaidi katika historia ya muhula wa rais ni mwanzo wa vita vya kuhakikisha tutaiboresha Marekani zaidi'', aliongezea.
Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue
Mwisho wa X ujumbe, 2












