Walilazimishwa kufanyiwa vipimo vya sehemu zao za siri wakati wa ukoloni India

Indian women, 1870

Chanzo cha picha, Heritage Images

Maelezo ya picha, Wanawake nchini India mwaka 1870 - utafiti mpya wa Profesa wa Harvard unaelezea ujinsia wakati wa utawala wa ukoloni wa Kiingereza

Mwaka 1868, polisi katika utawala wa Uingereza uliotawala mji wa india wa Calcutta (sasa ukifahamika kama Kolkata) waliwapeleka wanawake walioitwa Sukhimonee Raur gerezani kufanyiwa vipimo vya sehemu zao za siri ambavyo vilikuwa vya lazima kwa makahaba "waliosajiliwa".

Chini ya sheria ya ukoloni wa Muingereza kuhusu magonjwa hatari, iliyoandaliwa kwa ajili ya ya kudhibiti kusambaa kwa magonjwa ya zinaa, makahaba walitakiwa "kujisajiri' katika vituo vya polisi, kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na kuweza kuchunguzwa".

Raur alipambana - akaishitaki mahakama, akitaka aachiliwe huru

"Sikuhudhuria upimwaji mara mbili kwamwezikwasababu sikuwa kahaba ," alisema. Alisema kuwa polisi walimsajiri kimakosa na kwamba ahajawahi kuwa mfanyabiashara wa ngono.

Mwezi Machi 1869, mahakama ya ngazi ya juu zaidi ya Calcutta ilimuachilia huru.

majaji walisema kuwa Raur hakuwa "kahaba wa umma aliyesajiriwa" na zaidi ya hayo, usajiri wa aina hiyo wa wanawake utakuwa ni wa kujitolea. Kwa maneno mengine , wanawake hawapaswi kulazimishwa kujisajiri.

Katika kuchambua makavazi ya enzi ya ukoloni, Durba Mitra, profesa wa wanawake , jinsia na ujinsia katika Chuo Kikuu cha Havard, alibaini kuwa maelfu ya wanawake walikuwa wakikamatwa na polisi wa kikoloni kwa kushindwa kuheshimu sheria za kusajiliwa kwa ajili ya kufanyiwa vipimo vya uke kwa mujibu wa sheria.

Utafiti mpya wa Mitra Indian -Sex Life, uliochapishwa na makala ya Princeton University, ni utafiti mkubwa wa jinsi mamlaka za wasomi wa Uingereza na India "walivyoanzisha wazo kuhusu namna ujinsia wa kike ulivyotumika kudhibiti jamii nchini India". Njia moja ya kudhibiti ujinsia kwa kuweka katika makundi, kuwasajiri na kuwafanyia uchunguzi wa kimatibabu wanawake walioonekana kama makahama, alisema.

Foot with Silver Ankle Bracelets and Toe Ring

Chanzo cha picha, Michael Maslan

Maelezo ya picha, Walioitwa wacheza densi wanawake walitambuliwa kama "makahaba"

Wanawake wa waliandamana dhidi ya "mchakato wa upimaji wa chuki ambao kwa maneno mengine kuoneshwa vibaya ". Waliandika kwamba wale wanaokamatwa na polisi ''walilazimishwa kujionesha utupu wao kwake na kwa wasaidizi wake … Hatuhisi kuheshimiwa mioyoni mwetu kama wanawake ".

Mamlaka zilipinga haraka malalamiko yao.

Maafisa waliokuwa na mamlaka makuu katika mji walisema "makahaba'' waliokwepa usajiri walikuwa tisho kwa sheria. Kuadhibiti makahaba katika Bengal ilikuwa ni kazi ambayo haikuwezekana alidai Dkt Robert Payne, mkuu wa hospitali muhimu katika Calcutta. Anasema wanawake wanapaswa kusajiriwa kwa lazima.

Kati ya mwaka 1870 na 1888, anasema Profesa Mitra, wanawake 12 walikuwa wanakamatwa kila sikukwa kukiuka sheria katika Calcutta pekee. Mamlaka zilitambua kwamba wanawake wengi ,waligundua kuwa walikuwa wanafuatiliwa kwa hiyo wakawa wanaukimbia mji huo.

Serikali ya shirikisho ilijadili juu ya ikiwa polisi katika Bengal wanaweza kuwafanya kisheria vipimo vya uke dhidi ya wanawake "ambao walishutumiwa kutoa mimba na kuwauwa watoto".

Jaji mmoja alihisi kwamba "kesi za uongo kuhusu ubakaji na usaidizi wa kutoa mimba vitaongezeka bila uchunguzi wa lazima wa uke dhidi ya wanawake ". Mwingine alidai kuwa kupata idhini kutoka kwa wanawake kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi kunaweza kusababisha "haki ya kiutawala ".

Katika barua kwa waziri anayehusika na masuala ya Bengal , Kamishina wa polisi wa mji huo alisema kuwa , Stuart Hogg, alisema wanawake waliendelea kuwaambukiza wanaume magonjwa ya zinaa kwasababu ya mapungufu ya sheria.

Lakini kutokana na kuongezeka kwa upinzani dhidi ya sheria katika India na Uingereza, sheria ya uchunguzi dhidi ya magonjwa ya zinaa kwa wanawake ilirekebishwa mwaka.

Mwanahistoria na mwandishi wa vitabu vya Jinsia na hali za kijinsia Jessica Hinchy wakati wa enzi ya Ukoloni ya India, alisema kuwa, haikuwa ukahaba unaoshukiwa peke yake ambao uliwafanya wanawake wa India wafanyiwe uchunguzi wa sehemu zao za siri.

Alisema kuwa watu ambao Uingereza "iliwaweka katika daraja la watu wachafu , hususan wenye jinsia mbili -Hijras" walilazimishwa kufanyiwa uchunguzi wa sehemu zao za sirichini ya sheria tata ya mwaka 1871 ambayo iliyalenga makundi ya watu waliotambuliwa kama 'waliorithi uhalifu'.

"Lengo la sheria hii lilikuwa ni kusabanisha 'kutengwa taratibu ' kwa Hijras - kimwili na kiutamaduni -kwa njia ya kuwasajiri wa polisi.

Sheria ya magonjwa ya zinaa pia inaangaliwa kama enzi ya aibu katika historia ya ukoloni nchini India

Secretary Mackenzie’s summary of district commissioner

Chanzo cha picha, courtesy: durba mitra

Maelezo ya picha, Ushahidi rasmi wa Uingereza wa makahaba nchini India

Maafisa walisambaza vijikaratasi vya maswali kwa mahakimu, polisi na madaktari juu ya namna ya kuuelezea ukahaba .

Pia , katika maeneo kama Bengal, ambako alifanya utafiti, Wanaume ilibainika kuwa wanaume pia "walidhibiti ujinsia wa wanawake kwa maono yao ya jamii ya India ".

Mzizi wa yote haya ilikuwa ni imani ''potofu'' kwamba uanauke ulikuwa ni tatizo ambalo haliwezi kutatuliwa kwa urahisi . Matokeo yake, anasema profesa Mitra, wanawake ''walielezewa'' kama watu wa kujaribiwa, kuchunguzwa kwa maoni ya umma, kufungwa, kupimwa kinyume na matakwa yao ". Na mengi zaidi kuhusu historia hii, yanafanana na kile ambacho bado kinafanyikwa kwa wanawake.

A pavement under construction in Calcutta, circa 1880.

Chanzo cha picha, Hulton Archive

Maelezo ya picha, Picha ya mji wa Calcutta (kwa sasa ukifahamika kama Kolkata) mwaka 1870

Bankim Chandra Chatterjee, wakati huo awakiwa watu wenye itikadi za urasimu kwa kiwango kidogo katika Bengal ambao hatimae walikuwa ni waandishi mashuhuri wa vitabu vya tamthilia na waandishi wawimbo wa taifa wa India, walielezea kwa kina "masaibu mbalimbali ya wanawake waliofanya biashara ya siri ya ukahaba ".

Katika India ya ukoloni , kwa mujibu wa Prodesa Mitra, karibu wanawake wote nje ya ndoa ya mke mmoja ya Wahindu walitambuliwa kama makahaba.

Walikuwa ni pamoja na wale waliojulikana kama wacheza densi wasichana, wajane, Wahindu na Waislamu walioolewa na mume mwenye wanawake zaidi ya mmoja , ombaomba, badhi ya wanawake wanaofanya kazi viwandani na vijakazi . Mwaka 1881 sensa ya Bengal iliwatambua wanawake wote ambao hawajaolewa wenye zaidi ya miaka 15 kama makahaba.

Sensa ya kwanza ya mji wa Calcutta na miji mingine jirani iliwahesabu makahaba 12,228 wanaofahamika kati ya wanawake 145,000 . Kufikia mwaka 1891, idadi ilikuwa imepanda hadi zaidi ya makahaba 20,000.

"Kuanzishwa kwa sheria hiyo kulisababisha janga ambapo , kulikuwa na umuhimu wa mabadiliko kwani vitendo vya ngono vilikuwa ndio picha ya taita uliyokuwa nayo ukoloni wa Muingereza ," anasema Profesa Mitra.

Indian ayah with her European charges, c 1870.

Chanzo cha picha, Royal Photographic Society

Maelezo ya picha, Kijakazi Muhindi katika kazi ya kuwatunza watoto wa mkoloni mwaka 1870

Lakini vitendo vya ngono vya wanaume vilisalia kutotambuliwa na taifa rasmi. Profesa Mitra anasema "udhibiti wa na kumaliza ujinsia wa wanawake lilikuwa ni jambo muhimu kwa ukoloni wa taifa la uingereza kwa namna ulivyoingilia maisha ya kila siku ".

Pia , katika maeneo kama Bengal, ambako alifanya utafiti, Wanaume Wahindi "pia walidhibiti ujinsia wa wanawake kwa mitizamo ya jamii ya Kihindi kwa kujingatia ndoa ya mke mmoja na kuwatenga Waislamu na jamii nyingine