Pierre David: Moyo wa meya wa mji wa Ubelgiji wapatikana miaka 137 baada ya kuhifadhiwa

Chanzo cha picha, verviers.be
Jumba moja la kumbukumbu mashariki mwa Ubelgiji limetoa kitu ilichokimiliki kwa zaidi ya karne moja: Moyo wa meya wa kwanza wa mji huo.
Kiungo hicho, kilichohifadhiwa katika chupa kilipatikana wakati wa ukarabati wa maji ya bustani.
Jeneza hilo kwa sasa lipo katika maonesho ya makavazi ya Meya Pierre David alifariki 1839, lakini bustani hiyo ya maji iliotajwa baada yake ilizinduliwa 1883.
Moyo wa Pierre David uliwekwa katika makavazi hayo tarehe 25 mwezi Juni 1883.

Chanzo cha picha, verviers.be
Meya David pierre alifariki baada ya kuanguka akiwa na umri wa miaka 68 akifanya kazi katika jumba la chakula cha mifugo yake 1839.
Mamlaka ya mji huo ilizindua hazina ya kumpatia heshima na baada ya ruhusa kutoka kwa familia yake, daktari wa upasuaji alitoa moyo wake ili kuwekwa katika makavazi hayo.
Mtandao wa Verviers unasema kwamba ilichukua miongo kadhaa kwa mji huo kukusanya fedha za kutosha ili kusimamisha kitu cha kumbukumbu yake.
Wakati huohuo kulikuwa na mjadala kuhusu jinsi ambavyo wakaazi wa eneo hilo watamkumbuka meya wa kwanza wa mji huo kabla ya bustani hiyo ya maji kutengenezwa.

Chanzo cha picha, verviers.be
Je Pierre David alikuwa nani?
Aliishi katika wakati mgumu, wakati ambapo Ubelgiji ilitangazwa kuwa taifa huru 1830.
Kwanza alihudumu kama meya wa Vervier kati ya 1800-1808, wakati ambapo Ubelgiji ilikuwa ikitawaliwa kutoka Ufaransa.
Baadaye uhuru wa Ubelgiji ulitokana na mapinduzi dhidi ya Uholanzi 1830 na mwaka huo Pierre David alichaguliwa kuhudumu kama meya kwa mara nyengine.

Chanzo cha picha, verviers.be
Meya huyo anakumbukwa hususan kwa uvumbuzi wa huduma ya zima moto mjini Vervier 1802, ikiwa ni uvumbuzi usio wa kawaida wakati huo.
Mji wa Vervier uliharibiwa vibaya wakati wa maandamano ya 1830 na Davide Pierre alipatiwa jukumu la kurudisha hali kuwa ya kawaida katika mji huo kutokana na heshima aliokuwa nayo.












