Ugonjwa wa Prosopagnosia: Msanii mchoraji mwenye kiu ya kutambua uso wake

Carlotta

Chanzo cha picha, CORSO Film

Carlotta hajawahi kufanikiwa kutambua uso wake ama au nyuso za wengine. Hali yake, ya upofu wa uso ilikuwa na athari kubwa maishani mwake lakini pia hilo limemfanya kujua kwamba ana kipaji cha kuchora - anaweza kuchora usoa ambao hawezi kuuona kwenye kumbukumbu yake.

Carlotta huketi chini na kuanza kujichora. Chumba chake kina giza pengine awashe mshumaa tu kwasababu haitaji mwanga, hatumii kioo wala picha badala yake anatumia mkono mmoja tu kuchora muonekano wa uso wake huku mkono mwingine ukichora umbo la uso huo kwenye karatasi.

"Huwa inaniacha kinywa wazi ninapoona michoro yangu mchana," anasema.

Nyumba yake ina michoro mingi tu aliyochora mwenyewe - takriban 1,000, anasema.

Na kila mchoro ni tofauti kabisa.

Short presentational grey line

Ikiwa ataweza kujiona kwenye kioo, atafikira kwamba huyu mwanamke anayeniangalia yupo akili kwahiyo, atatambua sura yake na hata nywele zake.

Hali ya Carlotta ilianza kumsababishia matatizo alipokuwa msichana mdogo, miaka ya 1960, ingawa mara ya kwanza hakuna aliyejua kwamba ana tatizo.

"Nilipokuwa ninaenda kufanya manunuzi na mama yangu, au kufanyiwa upasuaji, tungekutana na watu ambao mama yangu anawajua lakini mimi siwatambui," amesema.

"Niliona maajabu kwamba mama yangu anaweza kuwaona. Kwangu nilidhani ana kipaji fulani cha kipekee kutambua watu wengine."

Mara nyingi tu Carlotta angemsubiri mama yake nje ya duka lakini alijikuta akimfuata mtu ambaye siye hadi nyumbani kwake, na kujua tu kwamba sio mama yake baada ya kuona wanashika njia ambayo sio. Lakini hakuwahi kumuarifu mama yake. "Nilifikiria pengine hilo ni tatizo langu tu, lakini sikulitilia maanani."

self-portrait by Carlotta

Chanzo cha picha, Carlotta

Transparent line

Kwahiyo, akaanza kutegemea vinavyomuwezesha kutambua mtu,

"Nilianza kufuatilia nguo walizokuwa wamevaa, wanavyotembea, sauti, je wamevaa miwani na kadhalika. Kila mmoja ana namna yake ya kupumua, kutembea na hiyo ndio njia niliyoitumia kutambua watu."

Lakini hadi pale Carlotta alipokwenda shule ndipo alipojua kwamba kitu alicho nacho sio cha kawaida.

"Ilikuwa vigumu, kwasababu, siri ya kujua wengine kwa kuwaangalia uso kama ilivyo kwa mama na baba yangu, nilianza kufahamu kuwa wanafunzi wengine pia wanakipaji hicho," anasema.

Lakini bado hakuwaarifu wazazi wake, alifikiria kwamba kutambua wengine kwa uso ni ujuzi fulani, kama vile kufunga kamba za viatu na kuwa ipo siku na yeye atajua namna ya kufanya hivyo.

Shuleni hali aliyopitia ilikuwa mbaya. Carlotta aliona watu wote wanafanana. Wakati fulani alitumwa kwenda chumba cha walimu kuchukua kitu kutoka kwa mwalimu mmoja.

"Niligonga mlango wa kuingia chumba cha walimu. Kulikuwa na mwanaume mmoja amesimama na nikasema, 'Nimetumwa kwa mwalimu Schultz.' Nikalazimika kurejelea maneno hayo mara tatu na akawa na hasira sana na mimi. Alisema, 'Mimi ndio mwalimu Schultz!' Kumbe yeye ndio alikuwa mwalimu wangu wa kwanza, lakini sikuweza kumtambua."

Alianza kuandika sifa za walimu wake wote - kama vile wana vaa miwani au kuna mwenye kidevu, viatu walivyovaa - lakini pia aliandika walimu ambao wanaonesha kuwa marafiki na wale ambao ni wakali, na siku moja kuna mwalimu aliyeona alichokuwa ameandika na akakichukua.

Wakati wa chakula cha mchana au mapumziko mafupi, kawaida Carlotta alikuwa anajitenga na watoto wengine.

Tatizo lilikuja pale kengele ilinapolia kaushiria wakati wa kukusanyika lakini baada ya mkutano kitu kingetokea.

"Mara nyingi ningerejea kwenye darasa ambalo sio langu, na nisingeweza kujua hadi ninaingia kwenye darasa hilo. Bila shaka ikiwa huwezi kumtambua mwanafunzi mwenzako atakuwa mjinga."

Walimu walikuwa wanajibu kwa hasira sana.

"Walinilazimisha nisimame mbele ya darasa na kusema 'Huna ulichonacho zaidi ya uchafu katikati ya masikio yako.' Waliiutukana sana: 'Huna akili kama tofali.'"

Watoto walimnyanyasa. Matokeo yake, aliamua kuwa peke yake tu. "Nisingesema chochote kwa sauti. Hakuna nilichofanya zaidi ya kuandika tu."

Carlotta drawing her face using touch

Chanzo cha picha, CORSO Film

Maelezo ya picha, Carlotta akishika uso wake na kuuchora

Shule ilifikiria kwamba Carlotta ana ulemavu fulani wa kutoweza kusoma na ikaandika barua kwa wazazi wake kupendekeza kwamba apelekwe kwa shule ya watu wenye mahitaji maalum.

Lakini wazazi walijua kwamba hakuna haja ya kufanya hivyo na wakaamua kupuuza wito huo.

Mwisho wa siku ya shule, Carlotta angekimbia nyumbani moja kwa moja na akifika tu achukua vitabu vyake.

Angesoma kila kitu alichoweza, hasa kuhusu uhalisia na kwenda sehemu nyingine mbali kabisa na nyumbani yaani alitaka tu kuwa peke yake.

"Nilikuwa nikijiwa na fikra kwamba ninaweza kwenda msitu wa mbali na kujitengenezea pango langu," anasema.

"Nilifikira kwamba kungekuwa na pango jikoni, pamoja jingine la vitabu - kubwa. Nilichokuwa natamani ni kuingia kwenye mapango hayo ndani kabisa kwenye giza totoro.

"Kutangamana na watu wengine ilikuwa changamoto kwangu. Nilipenda sana kuwa karibu na uhalisia na kujitegemea."

Alipoondoka shule akiwa na miaka umri wa 17 aliomba kazi ambayo kwa kiasi kikubwa haikuhitaji kutangama na mwanadamu.

Akiwa katika miaka ya 20 alitimiza azimio lake la kutotaka kuwa karibu na watu. Alinunua boti na kutembelea pwani ya Australia kwa mwaka mzima kazi yake ikiwa ni kusoma na kula akiwa baharini.

Carlotta holds a photograph of her climbing the mast of her sailing boat

Chanzo cha picha, Corso Film

Maelezo ya picha, Carlotta akipanda mlingoti wa boti lake

"Hicho kilikuwa kipindi muhimu sana kwangu, kwasababu niliutua mzigo niliokuwa nimeubeba kwa muda mrefu. Ni ugonjwa wa kurithishwa na hakuna ninachoweza kufanya."

Mtu mwenye ugonjwa wa prosopagnosia kama unavyofahamika kwa kiingereza, huenda asitake kutangamana na watu.

Pia wanaweza kuwa na wakati mgumu kuwa na mahusiano au kuwa na matatizo katika taaluma yake.

Hisia za kuwa na sonona pia ni jambo la kawaida kwa menye ugonjwa huo.

Utafiti unaonesha kwamba mtu mmoja kati ya 50 huenda akapata ugonjwa huo sawa na watu milioni 1.5 kote Uingereza kulingana na wizara ya afya Uingereza.

Lakini mara ya kwanza alikuwa na hasira sana.

"Nilikuwa na hasira kwasababu hakuna wa karibu yangu aliyejua kwamba nina tatizo na pia hakuna aliyeniambia kwamba ni ugonjwa wa kurithi.

"Nafikiri walimu wa siku hizi ni waelewa zaidi kwa wanafunzi wao, na mara nyingi shuleni huwa kuna wanasaikolojia ambao huenda wakabaini tatizo, lakini mimi nazungumzia kipindi nikiwa shuleni miaka 50 iliyopita, na walimu hawakujua kabisa kile kilichokuwa kinaendelea.

"Ikiwa kuna mtu ambaye angetambua kwamba nina tatizo, basi dunia ingekutofauti kwangu nikilinganisha na niliokutana nayo."

self-portrait by Carlotta

Chanzo cha picha, Carlotta

Transparent line

Wakati huo, wazazi wa Carlotta, ambao walikuwa wamemuasili walikuwa wamekufa.

"Ningependa sana kuwashirikisha nilichokifahamu na changamoto nilizopitia shuleni zingeelezeka," anasema.

Hata hivyo alifanikiwa kuzunguma na mama yake mzazi mwanamke ambaye wameachana kwa miaka 15 pekee na awali alikuwa akifahamishwa kwamba mwanamke huyo ni shangazi lake.

Jinsi alivyofahamu ukweli huo ni simulizi ya siku nyengine.

Akiwa na umri wa miaka sita, Carlotta alipelekwa hospitali kufanyiwa upasuaji.

Alisikia madaktari wakizungumza juu yake kama mwenye uvimbe wa ajabu.

Lakini miaka 12 baadae, Carlotta akiwa anatimiza miaka 18 aliona cheti chake cha kuzaliwa na hapo ndipo alipogundua kwamba anayemuita shangazi ni mama yake, 'Susanne'.

Na alipomuelezea Susanne kuhusu hali yake na ugumu wa kutambua watu kwa sura, akabaini kwamba pia Susanne ana tatizo hilo hilo.

Short presentational grey line

Carlotta anasema kuchora uso haijakuwa kazi rahisi kwake.

"Uso upo kama kilima ninaugusa kwa vidole vyangu na kuuchora kwenye karatasi. Sio rahisi, kwasababu sioni kile ninachofanya," anasema.

self-portrait by Carlotta

Chanzo cha picha, Carlotta

"Sanaa ya uchoroji bila shaka ni baraka kwangu - bila kipaji hiki nisingekuwa nilipo leo hii," anasema.

"Nimeweza kukabiliana na hisia nyingi sana kupitia mchoro na changamoto nyingi wakati nikiwa mtoto, lakini sasa hivi hayo ni ya kale.

"Sasa hivi naweza kutazama yaliyonitokea nyuma kwa mtazamo tofauti, nikiwa na uelewa zaidi wa walimu wangu na wazazi wangu. Najua kwamba hawakufahamu chochote kuhusu ninachopitia."

Michoro ya Carlotta inapatikana sehemu nyingi tu nchni Ujerumani na pia iliangaziwa na Valentin Riedl, mwansayansi wa ubongo aliyeamua kufanya filamu inayomhusu.

Carlotta at home

Chanzo cha picha, CORSO Film

Maelezo ya picha, Carlotta na Valentin

Ugonjwa alionao Carlotta hauna tiba - neva au mishipa husika haina uunganisho stahiki wa kuwasiliana na hakuna kianchoweza kufanyika.

Ingawa ugonjwa huo unaelezwa kama upofu, hauna uhusiano wowote na nguvu ya kuona, lakini ni mapungufu ya uwezo wa uso kutambua kinachoendelea.

Yaani sehemu ya ndani ya uso haiwezi kuwasilisha taarifa.

"Anaona mengine yote kwa kina, lakini anaposongea tu anasahau kila kitu," Valentin anaelezea.

"Ni kama vile kukumbuka ndani ya bakuli kulikuwa na chakula gani: unajua kabisa kwamba kulikuwa na ndizi lakini huwezi kusema kama bakuli lilikuwa juu au chini na ikiwa mtu atakuonesha bakuli jingine, unaweza hata kusema 'Naam, ni hii.'"

"Siwezi kutambua nyuso za watu kwasababu siwezi kuwakumbuka," Carlotta anasema. "Najijua mimi ni Carlotta, lakini sijui uso wangu."

Carlotta having an MRI scan

Chanzo cha picha, CORSO Film

Maelezo ya picha, Valentin Riedl akimfanyia matibabu Carlotta

Hata hivyo hali yake haimzuii kujua mwingine anavyohi

"Naweza kujua hisia za mtu na kuona ishara za uso wake, na hapo ndipo ninapoishia katika kuwakumbuka - hisia zao na vile mtu alivyo kijumla," anasema.

Na sasa hivi kwasababu amekuwa na mtazamo mwingine ana maono tofauti.

Alistaafu mapema kwasababu ya ugonjwa wa yabisi-kavu na anatumia muda mwingi kuchora uso wake akitafuta njia ya kutosheleza kiu chake cha kutaka kujua uso wake uko vipi.

"Sanaa yangu ni kitu muhimu sana ndani yangu," anasema. "Ninachohisi kufanya kila wakati ni kujichoratu kwenye karatasi na kuendelea kutafuta kujua usoa wangu uko vipi, kitu ambacho kitaondoka kwenye kumbukumbu zangu sekunde inayofuata.

"Nauona lakini siwezi kuukumbuka, naufikia lakini sekunde inayofuata unapotea akilini - ni mchakato unaoendelea ambao hauna mwisho"