Afghan: Msichana aliyechukua bunduki na kutetea familia yake

Chanzo cha picha, Ghor district government
Nyumba yao ilipovamiwa mwezi uliopita, Nooria mwenye umri wa miaka 15, alichukua bunduki ya AK-47, na kuua wanaume wawili na kumjeruhi wa tatu.
Alisifiwa kwa kuwa shujaa. Lakini kinachokanganya zaidi ni kile kilichotokea usiku huo.
Je Nooria alipiga risasi washambuliaji wa Taliban, au mume wake? ama wote?
Majina yote yamebadilishwa kwa sababu za kiusalama.
Wanaume hao waliingia kijijini humo usiku wa manane kukiwa na giza totoro.
Kulingana na Nooria, ilikuwa ni karibu saa saba usiku walipoingia kupitia mlango wa mbele nyumbani kwa wazazi wake.
Akiwa kwenye chumba chake, kijana huyo aliyeamshwa na kelele zilizokuwa zinaendelea, alikaa kimya na mkakamavu. Alifikiria kaka yake wa miaka 12 ambaye yuko kwenye chumba chake.
Kisha akasikia wanaume hao wakiwachukua wazazi wake na kuwatoa nje kuliko na nyumba ndogo eneo la milimani. Anaelezea tukio hilo katika mahojiano na BBC.
Kitu kilichofuata, akasikia milio ya risasi, anasema.
"Waliwaua."
Noori amekulia eneo la kijijini huko Afghanistan.
Alikuwa msichana mwenye haya na mkimya, lakini alijua kutumia bunduki na kufyatua risasi sahihi - jambo lililokuwa kama ulinzi wake baada ya kupewa mafunzo hayo na baba yake akiwa na umri mdogo.
Usiku huo, badala ya kujificha, Nooria alichukua bunduki ya baba yake - aina ya AK-47 - kisha akafyatulia risasi wanaume hao waliokuwa nje ya nyumba yao. Alipiga risasi hadi akakaribia kuzimaliza zote, anasema.
Hatimae, karibia saa moja tangu walipowasili, wanaume hao walisalimu amri, anasema.
Nje ya nyumba yao kulikuwa na miili ya wanaume watano: ule wa mama yake na baba yake, mwili wa jirani yao mzee ambaye alikuwa jamaa wake na miili ya washambuliaji wawili.
"Hali ilikuwa inatisha," amesema. "Walikuwa wakatili. Baba yangu alikuwa mlemavu. Mama yangu hakuwa amefanya lolote. Na wakawaua tu bila sababu."

Chanzo cha picha, Getty Images
Kukulia Afghanistan, watoto vijana kama Nooria hawajui kingine chochote zaidi ya vita.
Mgogoro unaoendelea kati ya vikosi vinavyopendelea serikali na Taliban, wanamgambo wenye msimamo mkali umekuwepo kwa zaidi ya miaka 25.
Vikosi vinavyopendelea serikali vinadhibiti miji mikubwa huku kundi la Taliban likitwaa maeneo ya vijijini. Vijiji kama vya Nooria mara nyingi hujikuta vimetumbukia kwenye mgogoro huo.
Nooria na kaka yake mkubwa wa kambo, afisa wa jeshi wanasema baba yao alilengwa na wanamgambo kwasababu alikuwa mzee wa kijiji na kiongozi wa jamii anayependelea serikali.
Kulingana na walioshuhudia tukio waliozungumza na BBC, mmoja wa wanaume waliokuwa na silaha usiku ule alikuwa mume wa Nooria na simulizi ya msichana huyo mdogo shujaa aliyeua wanamgambo wa Taliban kulisababisha gumzo katika familia nyingi.
Kile kinachozua gumzo zaidi kilichotokea usiku ule ni kuhusu wanaume waliovamia nyumba ya kina Nooria, na kwanini walikwenda huko. Pande zote zilikubaliana kitu kimoja: kwamba kulikuwa na shambulizi kijijini humo saa za alfajiri siku hiyo.
Kulingana na Nooria, wanaume hao walijitambulisha kama "mujahideen" yaani wapiganaji - neno linalotumiwa na kundi la Taliban - na pia walikuwa wamemfuata baba yake.
Kundi la Taliban limekanusha kuhusika katika shambulizi na msichana huyo, lakini likathibitisha kuwa kulikuwa na shambulio katika kijiji hicho hicho usiku ule, na kusema kituo cha ukaguzi wa polisi kililengwa na kusababisha wanamgambo wawili wa Taliban kupata majeraha lakini hakuna aliyepoteza maisha.
Wakati huohuo, maafisa wa eneo na serikali ya Afghanistan wamemtangaza Nooria kama shujaa dhidi ya washumbuliaji wa Taliban.
Sio jambo la kawaida nchini Afghanistan kwa raia kusifiwa na rais kwa kushinda washambuliaji wa Taliban. Lakini pale Rais Ashraf Ghani alipomwalika Nooria katika mji mkuu wa Kabul, kulikuwa na hisia mchanganyiko.

Chanzo cha picha, Local Afghan authorities
Siku iliyofuata katika eneo la tukio, polisi wa eneo walibaini vitambulisho katika miili ya wanaume wawili waliouawa. Wote walikuwa wanafahamika kuunga mkono Taliban, maafisa wameiambia BBC.
Mwanaume wa tatu alijeruhiwa lakini akatoroka alikuwa kamanda wa Taliban wa ngazi ya juu, kwa mujibu wa polisi.
BBC ilifanikiwa kutambua wanaume wawili waliouawa waliokuwa katika umri wa miaka ya 20, na nguo zao zilikuwa zimelowa damu.
And sources close to the Taliban said the commander named by police and alleged to have fled was indeed currently injured, but the sources would not confirm when or where he was hurt.
Na vyanzo karibu na Taliban vimesema kamanda aliyetajwa na polisi na kusemekana kutoroka alikuwa amejeruhiwa lakini vyanzo havikuthibitisha alijeruhiwa wapi na lipi?
Vyanzo vya eneo vya Taliban pia vimethibitisha kwamba mmoja wa wanaume hao awali alikuwa na uhusiano na mtandao wa huko Helmand, kusini mwa Afghanistan, miaka kadhaa iliyopita.

Wiki moja baada ya shambulio, taarifa kikaanza kusambaa kwamba mmoja kati ya washambuliaji waliouawa hakuwa tu mshambuliaji asiyejulikana kama ilivyo kawaida, bali mume wa Nooria.
Ingawa watu wa familia na vyanzo vya eneo viliambia BBC kwamba mume wa Nooria, Rahim, alikuwa ameenda kijijini humo akidhamiria kumchukua mchumba wake baada ya mgogoro wa kifamilia ulisababisha baba yake kumchukua binti yake na kurejea nae nyumbani kwake.
Vyanzo vyasema kuwa mume wake, Rahim, alikuwa amejiunga na kundi la Taliban na alikwenda nyumbani kwa kina Nooria akiwa ameandamana na wanamgambo wa kundi hilo.
Mume wa Nooria alitambuliwa kuwa miongoni mwa waliouawa usiku ule.
Hata hivyo, Nooria amekanusha kwamba aliwahi kuolewa.

Polisi wa eneo eneo la Nooria pamoja na viongozi wengine kijijini na mamlaka ya Afghanistan wanasisitiza kwamba Rahim na Nooria hawakuwa wameoana na uvamizi uliotokea nyumbani kwao ulikuwa ni kama mashambulizi mengine ya kawaida yanayotekelezwa na kundi la Taliban, huku baba yake akiwa mlengwa mkuu.
Ni watu wachache sana wanaojua nini hasa kilichotokea usiku ule. Nooria, kaka yake mdogo na mshambuliaji aliyenusurika kifo. Na huenda hakuna mwingine yeyote atakayejua ukweli wa kile kilichotokea.
Asubuhi baada ya kutokea kwa shambulio hilo, Nooria na majirani zao walizika wazazi wake kwa awamu katika makuburi ya karibu na nyumbani kwao.














