Tetesi za Soka Ulaya Alhamisi 23.07.2020: Aubameyang, Sancho, Sane, Alaba, Gerrard

Pierre-Emerick Aubameyang

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang

Arsenal wanajiandaa kumpatia mkataba mpya mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, unaokadiriwa kuwa £250,000 kwa wiki pamoja na marupurupu mengine katika juhudi za kumshawishi asiondoke klabu hiyo. (Telegraph)

Mkufunzi wa Rangers Steven Gerrard, 40, amekata ofa ya kuwa meneja mpya wa klabu ya Bristol City. (Bristol Post)

Borussia Dortmund wameanza mchakato wa kumsaka winga wa Werder Bremen na Kosovo Milot Rashica, 24, huku wakimtafuta atakayejaza pengo litakaloachwana mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United. (Telegraph)

Jadon Sancho

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Jadon Sancho, 20, amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United

Valencia wanajiandaa kumnunua kipa wa Chelsea na Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, pamoja na mchezaji nyota wa Manchester City Mhispania David Silva, 34. (90min)

Winga wa Bayern Munich Leroy Sane, 24, amemsihi beki wa Austria David Alaba, 28, kusalia katika klabu hiyo badala kurejea tena katika klabu yake ya zamani Manchester City, ama kwenda Real Madrid. (Sport Bild, via Independent)

Leroy Sane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Winga wa Bayern Munich Leroy Sane, 24,

Mlinzi wa Muingereza Japhet Tanganga, 21, anakaribia kusaini mkataba mpya naTottenham. (Evening Standard)

Tottenham wanaamini watafanikiwa kumsaini kiungo wa kati wa Southampton na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, licha ya dau la Everton la £25m kukubaliwa. (Guardian)

Pierre-Emile Hojbjerg

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tottenham wanaamini watafanikiwa kumsaini kiungo wa kati wa Southampton na Denmark Pierre-Emile Hojbjerg

Bayer Leverkusen huenda wakaamua kumsaini kwa mkataba wa mkopo kiungo wa kati wa Real Madrid na Brazil aliye na umri wa chini ya miaka 23 -Reinier, 18, ikiwa mshambuliaji wa Ujerumani Kai Havertz, 21, atahamia Chelsea. (Goal)

Arsenal wanataka kumnunua kiungo wa kati wa Aston Villa Douglas Luiz, 22, lakini Manchester City huenda wakamnunua tena mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil . (90min)

Tetesi za Soka Jumatano

Mshambuliaji wa Aston Villa raia wa Tanzania Mbwana Samatta, 27, huenda akaelekea Fenerbahce baada ya kushindwa kuiridhisha Villa Park tangu alipojiuga nao Januari. (Takvim via Sport Witness)

Samatta

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Aston Villa Mtanzania, Mbwana Samatta

Chelsea imejitayarisha kutoa ofa kwa mlinda lango mwingereza Dean Henderson, 23, ya pauni 170,000 kwa wiki ambaye sasa hivi yuko Sheffield United kwa mkopo , kujaribu kumshawishi kujiunga nao kutoka Manchester United. (Manchester Evening News)

Chelsea pia itajitahidi kusaini mkataba na mlinda lango wa Barcelona na Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 28, na iko tayari kutoa ofa kwa mlinda lango wa kimataifa Kepa Arrizabalaga, 25, kama sehemu ya makubaliano yoyote yale. (Mundo Deportivo, via Mail)

Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika kwamba mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Independent)