Vifahamu vyuo vikuu bora duniani 2021

Chanzo cha picha, Getty Images
Kwa mwaka wa tisa mfululizo, Chuo kikuu cha Teknolojia mjini Massachusetts MIT kimeongoza orodha ya vyuo vikuu bora duniani ilioandaliwa na kampuni ya Uingereza ya Quacquareli Symonds QS.
Chuo hicho cha elimu ya juu kinafuatiwa na vingine vitatu kutoka Marekani: Stanford, Harvard na Taasisi ya teknolojia katika jimbo la California huku nafasi ya tano ikichukuliwa na chuo kikuu cha Uingereza Oxford University.
Vyuo 10 bora duniani
1.Massachusetts Institute of Technology, USA
2.Stanford University, USA
3.Harvard University, USA
4.California Institute of Technology, USA
5.Oxford University, UK
6.Federal Polytechnic School of Zurich, Switzerland
7.Cambridge University, UK
8.Imperial College London, UK
9.University of Chicago, USA
10.University College London, UK
Orodha hiyo iliotolewa siku ya Jumatano na huchapishwa kila mwaka, inaandaliwa kupitia utafiti wa wasomi, wafanyakazi huku utafiti huo ukitokana na dondoo katika machapisho ya masomo na zile zinazohusishwa na utafiti huo mbali na idadi ya wanafunzi wa kimataifa na walimu miongoni mwa vigezo vingine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Ni matokeo yanayoashiria utendaji wa kitaalamu wa vyuo hivyo kulingana na walimu na wanafunzi.
Vyuo hivyo kumi duniani vinashirikisha chuo cha ETH Zurich kilichopo Switzeland,[6], Chuo kikuu cha Cambridge Uingereza [7] chuo cha British Imperial College kilichopo nambari nane na American University kilichopo Chicago.
Cha kushangaza ni kwamba kati ya vyuo 1002 vilivyoorodheshwa kote duniani hakuna hata chuo kimoja kinachotoka Afrika katika orodha ya vyuo 100 bora.
Vilevile katika orodha ya 10 bora kutoka Afrika , vyuo vitano vinatoka Afrika Kusini vikiongozwa na chuo kikuu cha Capetown ambacho ndio chuo bora Afrika na chuo nambari 220 kwa ubora duniani.

Chanzo cha picha, Getty Images
Vyuo vingine vilivyotawala orodha ya 10 bora Afrika ni vile vya Misri vinavyoongozwa na Ame
rican University iliopo mjini Cairo.
Hakuna hata chuo kimoja cha Afrika mashariki kilichoorodheshwa kati ya vyuo hivyo 1002 duniani.
Vyuo 10 bora Afrika
1. University of Capetown - Afrika Kusini
2.University of Witwatersrand - Afrika Kusini
3.American University Cairo - Misri
4.University of Johannesburg - Afrika Kusini
5. Stellenbosch University -Afrika Kusini
6. Cairo University - Misri
7. University of Pretoria - Afrika Kusini
8. Ain Shams university - Misri
9. Alexander University - Misri
10. Rhodes University Afrika kusini












