Jaribio la kombora jipya lawaua kimakosa wanajeshi 19 wa Iran Ghuba ya Oman

Kisa hicho kilitokea karibu na eneo la kimkakati la Hormuz

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Jeshi la Iran lilichapisha picha likionysha uharibifu uliofanyiwa meli ya Konarak
Muda wa kusoma: Dakika 2

Wanamaji 19 wameuawa na wengine 15 wakajeruhiwa katika tukio la ajali lililohusisha meli za kijeshi za Iran katika Ghuba ya Oman , jeshi la Iran limesema.

Vyombo vya habari vya Iran vimesema kwamba meli hiyo kwa jina Konarak ilishambuliwa na kombora jipya lililokuwa likijaribiwa na meli ya kijeshi ya Frigate Jamaran wakati wa zoezi la kijeshi siku ya Jumapili.

The Konarak ilishambuliwa na kombpora jipya Jumapili mchana wakati wa zoezi la kijeshi katika maji ya Bandar-e Jask kusini mwa pwani kulingana na runinga ya taifa katika tovuti yake.

Wanamaji hao walisema kwamba meli hiyo ilivutwa hadi ufukweni na kwamba uchunguzi umeanza.

Ruka YouTube ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: Imetoka kwingine na inaweza kuwa na matangazo

Mwisho wa YouTube ujumbe

Kisa hicho kilitokea karibu na mkondo wa bahari ya hormuz , eneo muhimu la kimkakati ambapo kiwango kikubwa cha mafuta duniani hupitia.

Presentational grey line

Uchanganuzi wa mwanadishi wa BBC Jonathan Marcus

Sio mara ya kwanza kwa jeshi la Iran kufanya makosa hayo.

Mwezi Januari , kitengo cha ulinzi wa angani kilirusha kumbora kutoka ardhini kikilenga kitu kisichojulikana, hatua ilioangusha ndege ya kampuni ya Ukrain na kuwaua wote waliokuwa wakiabiri ndege hiyo.

Makosa hayo yalifanyika wakati wa hali ya wasiwasi huku Iran ikisubiri kombora la kulipiza kisasi kutoka kwa Marekani.

Lakini tukio hilo la siku ya Jumapili lilifanyika katika hali tofauti - wakati wa zoezi la wanamaji - na linaibua maswali mengi kuhusu uongozi na udhibiti na utaalam wa jeshi la wanamaji wa Iran.

Iran inataka kupanua operesheni zake na kuimarisha silaha katika meli zake, Frigate Jamaran ambayo ni miongoni mwa vyombo vilivyoundwa nchini humo ikitarajiwa kuweka rekodi mpya.

Lakini ni jeshi lisililotiliwa maanani . Ni jeshi la wanamaji wa Revolutionary Guard lenye boti zinazopiga doria katika eneo hilo ambalo linahusika mara kwa mara katika kuhangaisha na kuchunguza meli za Marekani na nyenginezo katika Ghuba hilo.

Presentational grey line

"Siku ya Jumapili jioni...wakati wa zoezi la wanamaji ambalo lilihusisha vyombo kadhaa vya wanamaji katika maji ya Jask and Chabahar , tukio moja lilifanyika likihusisha meli ya Konarak , na kuwaua baadhi ya wanajeshi jasiri wa jeshi hilo, wanamaji hao walisema katika taarifa siku ya Jumatatu.

Meli ya Frigate Jamaran ikionekana wezi Disemba - iliripotiwa kushambuliwa meli ya kivita ya Konarak

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Meli ya Frigate Jamaran ikionekana wezi Disemba - iliripotiwa kushambuliwa meli ya kivita ya Konarak

Taarifa hiyo iliongezea kwamba meli hiyo ya Konarak ilikuwa imepelekwa katika bara moja kwa uchunguzi wa kiufundi, lakini haikutaja tukio la ajali hiyo.

Vyombo vya habari vya Iran awali vilikuwa vimeripoti kwamba meli ya Konarak ilishambuliwa kwa bahati mbaya na kombora moja lililifyatuliwa kutoka katika meli.

Meli hiyo ilishambuliwa baada ya kupita katika eneo ambalo kombora hilo lilikuwa likirushwa baada ya kushindwa kupita mbali, runinga ya serikali ilisema katika tovuti yake.

Chombo cha habari cha Tasnim kilituma ujumbe wa twitter kwa kiingereza kwamba Konarak ilizamishwa katika tukio hilo.

Kiliripoti kwamba meli hiyo iliharibiwa vibaya. Haijulikani kulikuwa na wanamaji wangapi ndani yake wakati huo.

Meli ya kivita ya Konarak ina urefu wa mita 47 na ilitenegenezwa nchini Uholanzi na kununuliwa na Iran kabla ya mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979.

Ramani ya mkondo wa hormuz
Presentational white space