Virusi vya corona: Waliobadilisha jinsia 'wana hatari kubwa' wakati huu

Chanzo cha picha, Huw Evans picture agency
Makundi ya kimataifa ya kutetea haki za watu waliobadili jinsia wanaonya kuwa amri za kukaa nyumbani zilizowekwa na mataifa mbali mbali kote duniani zimewafanya watu waliobadili jinsia zao kunyimwa huduma za afya.
Wengi upasuaji wa kubadili jinsia umecheleweshwa, na baadhi wanahangaika kupata tiba ya homoni na huduma za ushauri nasaha.
Upasuaji wa kurekebisha jinsia umekuwa ukicheleweshwa kote duniani kutokana na virusi vya corona-huku upasuaji wa awali ukisitishwa ili kupanua zaidi uwezo wa vitengo vya dharura kwasababu ya janga la corona.
Ingawa matibabu ya homoni bado yapo kwa wanaobadili jinsia zaokatika nchi nyingi za magharibi, makundi ya watu wanaobadili jinsia katika nchi za Afrika Mashariki yanaonya kuwa hali ni tofauti kwa wanaobadili jinsia zao nkatika mabara mengine.
"Watu wanaobadili jinsia tayari ni miongoni mwa makundi yenye hatari kubwa," anasema Barbra Wangare, Mkurugenzi mkuu wa Mtandao wa Masuala ya Afya ya Watu wanaobadili jinsia na kutetea maslahi yao Afrika Mashariki (EATHAN), " na usaidizi kwa watu hao kihistoria haujawahi kupewa kipaumbele - hata miongoni mwa watu waliobadili jinsia na wapenzi wa jinsia moja. Virusi vya corona vitaimarisha zaidi hatari hizi.
" Tunasikia kutoka kwa watu wanaosema wanaogopa kuwa wanashindwa kufikia mabadiliko yao ya jinsia kutokana na ukosefu wa huduma za matibabu. Hii inawaweka katika hali mbaya sana ya kihisia ."
Watu wanaobadili jinsia wana uwezekano wa kujiua takriban mara mbili zaidi ya wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja , kwa mujibu wa utafiti wa mwaka 2017 uliofanywa na Chuo kikuu cha Lancaster nchini Uingereza unaofahamika kama 'Suicide in Trans Populations'.
BBC imezungumza na wanaume wawili wanaobadili jinsia zao nchini Kenya na Marekani kufahamu amri za kukaa nyumbani zimekua na maana gani kwao.
Mauricio Ochieng, mwenye umri wa miaka 30, kutoka kaunti ya Kisumu , Kenya
Mauricio husafiri saa saba kwa basi hadi Nairobi kuchukua sindano zake za homoni za kiume. Ni safari ambayo amekua akiifanya kwa zaidi ya mwaka. Na anasema imekua ni safari ya mafanikio.
"Kwa sindano ninazopigwa mwili wangu umeanza kubadilika. Sasa muonekano wangu si wa ''kike kama ulivyokua'' , sauti yangu ni nzito na ndevu zinaota," anasema. "Nilikua nimefikia hatimae katika hatua ya kuwa mimi. Mimi ni mwanaume. Sijawahi kuwa mwanamke."
Mauricio ambaye alikulia katika eneo la kijijini nchini Kenya, yapata kilomita 350 kutoka mji mkuu Nairobi, alifahamu kuwa alikua tofauti. Ana mabinamu zaidi ya 150 na hakujiona anafafanana na yeyote miongoni mwao.
"Nilikua kondoo mweusi wa familia."

Chanzo cha picha, Somsara Rielly/BBC
Alifahamu fika kuwa hakua msichana, licha ya mwili wake kuonekana ni wa kike. Wazazi wake waliamini kuwa alikua msagaji. Hili lilikua ni jambo baya la kutosha , walisema, lakini ni kitu ambacho walikielewa. Wakati alipowaambia kuwa yeye ni mwanaume ndani ya mwili wa mwanamke, walimfukuza nyumbani.
Mauricio alikuwa hana makazi akiwa na umri wa miaka 16. Alinyanyaswa kijinsia mara kadhaa. Baada ya mwaka mmoja baadae alipata ujauzito kutoka kwa mmoja wa watu waliombaka. Watu walimuita "chkora", jina wanaloitwa watoto ombaomba wa mitaani nchini Kenya.
Alikwenda nyumbani kwa mama yake na kusema: "Tafadhari usinifanye nizalie mtoto mtaani kama mbwa".
Akamruhusu aingie nyumbani..
Binti yake Mauricio alizaliwa mwaka 2007. Alifanya kazi katika soko la Kisumu, akinunua na kuuza viatu.
Mwaka 2018 aliamua kuanza kubadili jinsia yake. Sindano za kuingizwa homoni zinagarimu taktriban shilini 1,200 kwa dozi moja ( £9) - ambalo ndilo pato lake la siku.
Safari ya saa 14 ya kila mwezi ya kuchukua dawa zake ilimfanya ajihisi mwenye mafanikio makubwa. Mauricio alikua anaweka pesa ya akiba kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji wa hali ya juu : ambao ungemuwezesha kuondoa matiti yake.
Halafu virusi vya corona vikafika Kenya, na baada ya muda mfupi masharti ya kutotembea yakafuatia.
Mauricio hana dawa za muda ujao za homoni za kubadili jinsia.
"Ninashindwa kupata usingizi, msongo wa mawazo," anasema. "Ni nini kitatokea kama sitaweza kupata matibabu yangu? Maumivu haya yote yanafaida gani?
"Ninabadilika kuwa mwanaume katika nchi inayowanyanyapaa wanaobadili jinsia. Kama sitapata dawa ni nini kitakachotokea kwa mwili wangu - tayari umeanza kubadilika. Niataonekana mtu asiye wa kawaida? Ni nani atatupigania tusikike katika kipindi hiki cha mkanganyiko?"


Liam T Papworth, mwenye miaka 30 huko mjini Chicago, Marekani ni mwanaume aliyefanya mabadiliko ya jinsia na kuingia katika kazi ya jeshi
2020 ulikuwa mwaka ambao Liam alikuwa anatarajia kumaliza upasuaji wake wa kubadili mwili wake kuwa mwili wa mwanaume unaofahamika kwa jina la kigeni kama phalloplasty.
"Upasuaji huu ufanyika kwa mwanamke ambaye ana jinsia mbili anataka kuondoa uume wake, baada ya miaka mingi ya mahangaiko."
Mlipuko wa virusi vya corona umechelewesha zoezi la upasuaji wa Liam mpaka mwishoni mwa mwaka 2021, hajaona kama ana uhitaji wa huduma ya kiafya ambao unapaswa kupewa kipaumbele.
"Ni pigo kubwa kwangu kwa sababu nilikuwa ninasubiri upasuaji huu katika maisha yangu yote.
"Nilikuwa napaswa kurudi shuleni na niliamua kutofanya hivyo mpaka baada ya upasuaji wangu."
Upasuaji ndio hatua ya mwisho kwa Liam kupata suluhu ya tatizo lake tangu alivyoanza jitihada ya tiba tangu akiwa na miaka 19.

Chanzo cha picha, Somsara Rielly/BBC
Akiwa mtoto, Liam hakuhisi kuwa yeye ni msichana.Anakumbuka jinsi alivyokuwa akibishana na shangazi yake katika msiba wa baba yake, alipokuwa anamkataza kutovaa mavazi ya kiume.
Baada ya kupata ushauri wa wanasaikolojia alipokuwa na miaka 19, Liam alianza kuchomwa sindano zifahamikazo kama 'testosterone'. Muda ulipoisha alianza kujihisi kukubali mwili wake.
Lakini ni hatua ambayo ilichukua muda mrefu , msongo wa mawazo na urasimu mwingi, alisema.
Ubadilishaji wa jinsia huwa unatofautiana katika kila jimbo nchini Marekani.
Madaktari wanawakatalia wagonjwa kutokana na hali ya bima zao binafsi.
Mwaka 2016, akiwa na umri wa miaka 25, Liam alifanyiwa upasuaji wa kuondolewa matiti yake yote uliochukua muda wa saa 12.
Maisha yamebadilika. Liam sasa anaweza kwenda kuogelea, kutembea kifua wazi bila shati .Aliweza kushiriki mashindano yam bio za mita 15.Yani ni mapinduzi makubwa ya maisha yake.
Licha ya kwamba sera ya Marekani ,ilikataza mwaka 2017, kuwa watu wanaobadili jinsia zao wasijiunge jeshini,baadhi ya mahakama walipunguza ukali wa sheria hiyo na na hivyo Liam akawa mtu wa kwanza ambaye amebadili jinsia zao kujiunga jeshi la Marekani 23.2.2018 na kuweka wazi hali yake.
"Huduma ya afya kwa watu kubadili jinsia haijawahi kupewa kipaumbele duniani kote.
"Ndio virusi vya corona ni janga la dunia nzima lakini afya ya akili kwa jamii hiyo ni muhimu pia.
"Ninaelewa kuwa wahudumu wa afya wanapaswa kufanya maamuzi magumu katika kipindi hiki, lakini itakuwa vyema kama na sisi tutakuwa kipaumbele pia hata mara moja."












