Vurusi vya corona: Mikakati iliyowekwa na serikali za Afrika kuhakikisha raia wanaendelea kupata chakula.

Richard Kabanda

Tumekwama nyumbani kwasababu ya amri ya kutotoka nje, Richard Kabanda raia wa Uganda mwenye umri wa miaka 25, ana wasiwasi kuhusu chakula cha familia yake

Dereva wa pikipiki, anayepata karibu $2 (£1.60) kwa siku, hajafanyakazi tangu serikali ilipopiga marufuku usafiri wa umma mwezi uliopita kama sehemu ya hatua ya kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

"Tutakufa kwasababu hakuna tunachoweza kufanya," amezungumza na BBC akiwa nyumbani kwake, katika eneo moja la mabanda karibu na ziwa Victoria.

"Tutakufa ndani ya nyumba zetu kwasababu chakula tulichonacho kitaisha na ilihali tumeambiwa hakuna ruhusa ya kutoka nje."

Uwiano kati ya mapato na maisha ya kila siku

Chakula alichonacho kilipoisha, alikuwa na matumaini ya kufaidika na chakula cha msaada kilichoahidiwa na serikali kwa raia milioni 1.5 kwa wenye uhitaji zaidi.

Anachopitia ni sawa na kile wanachopitia watu 4 kati ya 5 wafanyakazi wa Afrika wanaoishi wakitegemea sekta isiyorasmi na hawana uwezo wa kupata usaidizi wa serikali.

Wenye vibanda vya biashara katika mji mkuu wa Uganda Kampala waliambiwa walalana bidhaa zao wakati wa amri ya kukaa nyumbani kuwazuwia wasizunguke

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Wenye vibanda vya biashara katika mji mkuu wa Uganda Kampala waliambiwa walalana bidhaa zao wakati wa amri ya kukaa nyumbani kuwazuwia wasizunguke

Serikali za Afrika ikiwemo Uganda kwasasa wanakumbana na janga la corona na zimeweka hatua kadhaa kukabiliana na ugonjwa wa Covid-19.

Kuna nchi kidogo kutoka Afrika zenye mifumo na miradi ya ustawi wa jamii ya kusaidia raia wasiokuwa na kazi.

Mazingira hatari wanayofanyakazi watu hao na idadi kubwa ya watu inayowategemea kuna maanisha kwamba kusitishwa kwa shughuli za uchumi huenda kukawa na athari kubwa kwao.

Sasa je serikali za Afrika zinafanya nini kuelezea raia wao athari za ukosefu wa ajira?

Watu wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi ni asilimia 80% ya nguvukazi kote barani Afrika

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Watu wanaoishi katika makazi yasiyo rasmi ni asilimia 80% ya nguvukazi kote barani Afrika

Ukiangalia eneo la jangwa la Sahara kwa ujumla, Benki ya Dunia imetabiri kwamba huenda eneo hilo likajipata katika mkwamo wa uchumu mwaka 2020 kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 25 kama moja ya athari za virusi vya corona.

Nigeria, Afrika Kusini na Angola kuna uwezekano mkubwa zikaathirika zaidi lakini nchi zote barani humo kwa ujumla zitashuhudia kiwango kidogo cha ukuaji wa uchumi.

Jane Barrett, mfanyakazi wa kampuni ya South Africa for Wiego, shirika linalosaidia wanawake waliojiajiri kwenye sekta zisizo rasmi, anasema uhalisia ni kwamba kwa sasa hali sio nzuri.

Watu wanategemea chakula cha msaada kinachogawanywa na mashirika yasio ya kiserikali lakini kila wakati tunakumbana na simulizi za kusikitisha kuwa watu wa vijijini hawafikiwi", ameongeza.

Takriban dola bilioni 2.6 zinazotumiwa na serikali zitatolewa kama pesa taslim kwa wanaohitaji.

Watu ambao tayari wanapokea msaada kutoka kwa serikali wa dola 23 kwa mwezi kwa sababu ya watoto, wataongezwa pesa hizo hadi dola16 kwa kila mtoto mwezi ujao na pengine hata huenda wakapokea pesa zaidi baada ya hapo.

Nchini Afrika Kusini, mashirika ya misaada yamekua yakigawa chakula kwa wale wanahitaji zaidi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Nchini Afrika Kusini, mashirika ya misaada yamekua yakigawa chakula kwa wale wanahitaji zaidi

Hili linastahili kusaidia watu milioni 18 raia wa Afrika Kusini idadi hiyo ikiwa ni chini tu ya theluthi moja ya idadi yote ya watu nchini humo.

Malipo ya uzeeni yanayotolewa na serikali pia yataongezwa na wale ambao sio miongoni mwa makundi hayo, yaani wasiokuwa na ajira wanaweza kuwa miongoni mwa watakaoanza kulipwa dola 18 kila mwezi kwa kipindi cha miezi sita ijayo.

Ingawa si sawa na kukosa kabisa, Bi. Barrett amesema, "lakini sina uhakika kama kiasi hiki kitatosha kukabiliana na tatizo la njaa tunalolishuhudia".

Baadhi ya pesa za kuchechemua uchumi hazitatoka kwenye kodi wala mikopo lakini itakuwa ni baada ya kuangalia tena matumizi ya serikali na yaliyopewa kipaumbele na kuongeza pesa za ziada katika mfuko kwa wasiokuwa na ajira.

Lakini Afrika Kusini bado itahitaji kukopa zaidi ili iweze kutekeleza ahadi zake.

Wakati ambapo wafadhili wametangaza kusimamisha malipo ya madeni waliokuwa wanadai kwa sasa, hili halitaendelea milele.

Sasa Je ni mkakati gani unaotekelezwa Uganda?

Mfumo wa pesa unaondelea Kenya inaonekana bado haujaigwa na jirani zao.

Kwa mfano Rwanda na Uganda kwasasa zinategemea kutoa chakula kwa wasiojiweza.

Baadhi ya watu wanaweza kuendelea na kazi licha ya hatua zilizochukuliwa kuzuwia kusambaa kwa virusi

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Baadhi ya watu wanaweza kuendelea na kazi licha ya hatua zilizochukuliwa kuzuwia kusambaa kwa virusi

Lakini kwa Uganda, huenda usimfikie kila mmoja mwenye njaa.

Dereva wa pikipiki wa Uganda, Bwana Kabanda, anasema kwamba yeye bado hajapokea chakula wiki mbili baada ya kutangazwa kwa mpango huo.

Waziri wa Kupambana na Majanga Musa Ecweru ameiambia BBC kwamba hadi kufikia sasa mradi huo umefikia watu nusu milioni ambao hawakuwa na ajira.

Aliongeza kwamba imekuwa vigumu kutafuta waathirika kwasababu ya hatua zilizochukuliwa kama vile kutokaribiana hiyo ikimaanisha kwamba serikali inaweza tu kuwasilisha misaada hiyo nyumba hadi nyumba kwa maeneo ya vitongoji duni ambayo si rahisi kufikika.

Coronavirus

Taarifa zaidi kuhusu corona:

virusi vya corona

Vipi kuhusu Nigeria?

Nigeria, moja ya nchi za Afrika yenye idadi kubwa ya watu karibia milioni 200, imetoa masharti ya kusalia ndani katika mji wa kibiashara wa Lagos, jimbo jirani la Ogun na mji mkuu wa Abuja.

Mfanyakazi anayeuza vipuri vya magari huko Lagos katika soko la Ladipo ambalo linasemekana ndio kubwa zaidi katika mauzo ya vipuri eneo hilo, ameiambia BBC kwamba anataabika.

"Baadhi yetu hatujafungua maduka kwa wiki tatu sasa na hapo ndipo tunapopata pesa za kununua chakula," amesema.

Wasanii wa Kenya wamechora michoro kwenye kuta katika moja ya eneo la jiji la Nairobi , kuwakumbusha watu kuhusu njia za kuwa salama

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wasanii wa Kenya wamechora michoro kwenye kuta katika moja ya eneo la jiji la Nairobi, kuwakumbusha watu kuhusu njia za kuwa salama

Serikali imeanzisha hatua za kupunguza kodi na vichocheo vyengine kwa wafanyakazi. Lakini kwasababu asilimia 90 ya raia wapo kwenye sekta isiyo rasmi, kulingana na Shirika la Wafanyakazi Ulimwenguni la Umoja wa Mataifa (ILO), sera hizo zitafikia wachache.

Rais Muahammadu Buhari ametangaza mfululizo wa kile alichokiita hatua stahiki miongo mwayo ni kuongeza idadi ya wanaopokea pesa kutoka kwa serikali katika mradi uliotengewa milioni 2.6 hadi milioni 3.6.

Hiyo itamaanisha kwamba watu karibia asilimi 10 watapokea dola 13 kwa mwezi. Yaani kwa maskini hasa lakini je kipi kitakachotokea kwa idadi nyengine iliyosalia.