Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Virusi vya corona: Je unaweza kupata maambukizi mara mbili?
Je unaweza kupata maambukizi ya virusi vya corona kwa mara ya pili? Kwanini wengine wanaugua zaidi kuliko wengine? Je ugonjwa huu utakuwa unarejea kila msimu wa baridi? Chanjo itafanya kazi? Unawezaje kukabiliana na virusi kwa kipindi cha muda mrefu?
Kinga ya mwili ndio msingi wa masuala mengi muhimu yanayohusu virusi vya corona.
Tatizo ni kwamba ufahamu wetu ni mdogo.
Unaweza kuwa na kinga ya mwili ya kubabiliana na virusi vya corona?
Kinga ya mwili ndio muhimu mwilini dhidi ya maambukizi na hilo huwa katika sehemu mbili.
Kwanza huwa iko tayari kupambana na chochote ambacho kinga ya mwili itabaini kinataka kuvamia mwili. Hilo linaweza kutambulika kama kinga ya mwili inayojificha na inajumuisha kutoa kemikali inayosababisha uvimbe na chembe nyeupe za damu ambazo zinaweza kuharibu seli zilizopata maambukizi.
Lakini mfumo huu sio kwamba upo mahsusi kwa virusi vya corona. Hauwezi kujifunza wala kukupa kinga kwasababu ya virusi vya corona.
Badala yake kinga ya mwili inahitajika kuwa ni yenye kubadilika badilika. Hilo linajumuisha seli au chembe chembe zinazozalisha kinga inayoweza kuganda kwenye kirusi ili kusitisha utendakazi wake na chembe za T zenye kutambua virusi ambazo zinaweza kuvamia chembe zilizopata ya kirusi pekee.
Hilo linachukua muda- utafiti unaonesha kwamba inachukua karibu siku 10 kuanza kutengeneza kinga ya mwili ambayo inaweza kuvamia virusi vya corona na kinga ya mwili ya wagonjwa haswa inaanza kutumia nguvu nyingi kupigana na virusi.
Ikiwa kinga ya mwili inayobadilika badilika ina nguvu zaidi, basi inaweza kuacha kumbukumbu ya muda mrefu katika kinga ya mwili iwe ni yenye kutambua mara moja iwapo itakumbana na maambukizi kama hayo siku za usoni.
Bado haijafahamika ikiwa watu wenye dalili za wastani au wasio nazo kabisa miili yao itatengeneza kinga ya mwili imara yenye uwezo wa kubadilika kulingana na mazingira na kupambana na maambukizi.
Je kinga ya mwili inaweza kuwa imara kwa siku ngapi?
Kinga ya mwili ina uwezo wa kutambua maambukizi ya awali lakini pia inatabia ya kusahau maambukizi mengine.
Ugonjwa wa ukambi/surua mara nyingi hukumbukwa - ukitokea mara moja tu, hufanya kinga kuukumbuka kwa kipindi kirefu. Hata hivyo, kuna magonjwa mengine ambayo husahaulika. Mfano, watoto wanaweza kupata maambukizi yanayosababisha matatizo ya kupumua mara nyingi tu msimu mmoja.
Ugonjwa wa virusi vipya ya corona unaojulikana pia kama Sars-CoV-2, ni maambukizi mageni kwahiyo haiwezi kufahamika kinga ya mwili inaweza kupambana kwa kipindi gani lakini kuna virusi vingine 6 vya mwanadamu ambavyo vinaweza kutoa mwelekeo.
Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:
Virusi vinne vinaonesha dalili za mafua na kinga ya mwili ni ya muda mfupi. Utafiti unaonesha baadhi ya wagonjwa wanaweza kuambukizwa tena ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.
Lakini kwa homa, nguvu yake huwa ni ya wastani. Kuna virusi vya corona aina mbili ambavyo ni visumbufu - vile vinavyosababisha matatizo makubwa ya kupumua (Sars) na ugonjwa wa matatizo ya kupumua wa Mashariki ya Kati (Mers) - ambapo kinga ya mwili ilibainika miaka michache baada ya ugonjwa kujulikana.
"Swali sio, vipi unaweza kuwa na kinga, badala yake ni kinga inaweza kuwa imara kwa kipindi gani?," anasema Paul Hunter, profesa katika chuo kikuu cha utabibu Mashariki mwa Anglia.
Aliongeza: "Kuna uwezekano mkubwa haitakuwa ya kudumu milele.
"Kwa kuzingatia kinga ya mwili zilizofanyiwa utafiti katika ugonjwa wa Sars, kuna uwezekano kwamba kinga ya mwili itakuwa imara kwa kipindi cha mwaka mmoja hadi miwili ingawa hili bado halina uhakika."
Lakini hata kama hauna kinga imara kuna uwezekano mkubwa maambukizi ya mara ya pili hayatakuwa makali sana.
Kwanini kinga ya mwili ni muhimu?
Ni muhimu kwasababu ya afya ya mtu binafsi na ikiwa utapata ugojwa wa Covid-mara ngapi.
Kinga ya mwili pia itakuwa na mchango wake kulingana na makali ya kirusi. Ikiwa utakuwa nayo, makali ya ugonjwa yatapungua.
Kuelewa kinga ya mwili kunaweza kusaidia katika kuangazia masharti ya watu kusalia ndani ikiwa itabainika ni nani ambaye hayuko katika hatari ya kupata maambukizi au kusambaza virusi hivyo.
Ikiwa itakuwa vigumu kujenga kinga ya mwili ya muda mreffu, huenda ikawa vigumu kwa kutengeneza chanjo.
Au inaweza kubadilisha vile chanjo inastahili kutumiwa - je itakuwa mara moja kwa maisha ya mwandamu au mara moja kwa mwaka kama ilivyo kwa chanjo ya mafua kwa baadhi ya nchi.
Na muda wa kinga ama iwe kwasababu ya maambukizi au chanjo, itatoa mweleko wa ikiwa itaweza kusitisha virusi hivyo kusambaa.
Haya ndio baadhi ya maswali ambayo bado hayajapata majibu