Virusi vya Corona: Je wanaume wenye umri wa miaka 50 na zaidi wanaathiriwa kwa kiwango gani?

Wengi miongoni wa watu wenye virusi vya corona huweza kupona katika kipindi cha takriban wiki moja baada ya kupata dalili na huwa hawahitaji uangalizi wa kimatibabu.
Lakini watu wengine watahitaji kutibiwa hospitali- mkiwemo waziri mkuu wa Uingereza.
Boris Johnson, ambaye ana umri wa miaka 55, kwa sasa yuko katika chumba cha matibabu ya dharura (ICU) katika hospitali ya St Thomas mjini baada ya dalili za corona kuwa mbaya sana.
Amekua akiongezewa hewa ya oksijeni,lakini hakuhitaji kusaidiwa na mashine (ventilator) kupumua.
Ni watu gani wanaweza kuugua ?

Chanzo cha picha, Getty Images
Baadhi ya watu wako katika hatari kubwa ya kuugua sana.
Hii inajumuisha watu wenye umri wa zaidi ya miaka 70, iwe wana matatizo mengine ya kiafya au la, pamoja na watu wengine wenye magonjwa ya kudumu kama vile magonjwa ya moyo.
Kuna zaidi ya watu milioni 1.5 nchini Uingereza ambao wako katika hatari kubwa ya kuhitaji matibabu ya hospitali iwapo watapatikana na virusi vua corona
Hii inajumuisha wanaopata matibabu ya saratani ya chemotherapy, na wameombwa wakae nyumbani muda wao wote ili kujikinga na virusi
Kwanini wanaume wazee?
Wanasayansi hawana uhakika
Data za kitengo cha matibabu ya dharura -ICU nchini Uingereza kwa mfano kwa wastani mtu aliyeko mahututi ni mwenye umri wa miaka 60. Wengi wao ni wanaume ambao wamekua na magonjwa ya kudumu ambayo yanawaweka katika hatari zaidi wanapougua corona.

Data kutoka Uchina ambako jangahili lilianzia wanaume walionekana kuwa katika hali ya hatari zaidi kuliko wanaume, ingawa wataalamu wanatahadharisha kuwa kuna sababu zaidi ya jinsia, kama vile uvutaji wa sigara ambao unaweza kuwa ni mojawapo ya sababu.
Wanaume wanauwezekano mkubwa wa kuwa na maradhi ya moyo, kisukari na maradhi ya kudumu ya mapafu kuliko wanawake kulingana na wataalamu wa afya.
Baadhi wamesema kuwa homoni na jeni za jinsia huenda ikawa mojawapo ya sababu pia .
Je wanawake wanakinga ?
Profesa Philip Goulder, mtaalamu wa kinga ya mwili katika Chuo Kikuu cha Oxford, anasema : "Inafahamika sasa sana kwamba kuna utofauti wa wazi wa mfumo wa kinga ya mwili baina ya wanaume na wanawale na hii ina athari kubwa inapokuja katika matokeo ya aina mbali mbali za magonjwa ya maambukizi.
"Ufanisi wa chanjo miongoni mwa wanawake na maambukizi ni bora zaidi miongoni mwa wanawake kuliko wanaume, anasema.

Taarifa zaidi kuhusu virusi vya corona:
Je virusi vya corona husababisha vifo?
Kila mwaka watu wapatao 600,000 hufa nchini Uingereza wenye magonjwa ya kudumu na wazee ndio walio katika hatari kubwa, kama ilivyo kwa ugonjwa wa corona.
Unawezaje kujikinga mwenyewe ?
Fanya mazoezi ya mwili ili uwe thabiti na hakikisha unakua mwenye afya kila uwezavyo kwa kula mlo kamili.
Kama unavuta sigara, sasa ni muda mzuri wa kuacha.
Wanaume wanauwezekano mkubwa kuliko wanawake wa kufanya mambo yafuatayo:
- Kuvuta sigara na vitu vingine kwa siku na vitu wanavyovivuta ni vikali mfano misokoto ya tumbaku
- Kula chumvi kwa kiasi kikubwa
- kula kiwango kikubwa cha nyama nyekundu na nyama za kusindikwa
- hula matunda kidogo na mbboga kidogo
- hunywa pombe na vileo vingine kwa viwango vya juu

Chanzo cha picha, Getty Images
Virusi vya corona husambaa wakati mtu aliyeathiriwa anapokohoa au kupiga chafya na matone ya majimaji hayo- yaliyosheheni virusi kwenda hewani. Matone haya yanaweza kuvutwa ndani ya mwili kwa njia ya kupumua na mtu aliye karibu.
Unaweza pia kupata maambukizi haya pale matone hayo yanapoangukia kwenye kitu fulani na kuyagusa kisha kujigusa kwenye macho, pua au mdomo.
Kwa hivyo basi unapaswa kukohoa, na kupigia chafya kwenye tishu, halafu usiguse uso wako na mikono ambayo haijanawishwa na pia epuka kuwa karibu na mtu aliyeambukia virusi vya corona.
Nikipata dalili za virusi vya corona je?
Iwapo una kikohozi kipya ambacho hakikomi au homa unapaswa kukaa nyumbani na ujitenge kabisa na watu wengine walau kwa siku saba
Kma wewe au mtu fulani unayeishi nae ana dalili, nyumba nzima inahitaji kujitenga walau kwa siku 14 ili kufuatilia kwa karibu dalili za ugonjwa .
Nitafanya nini iwapo dalili zangu hazipungui?
Sababu kuu inayowafanya watu wahitaji matibabu ya hospitali ni ugumu wa kupumua.
Katika nchi yako bila shaka kuna miongozo inayokuelekeza ni nini la kufanya iwapo hali yako inakua mbaya
Kama unashindwa kabisa kupumua kiasi kwamba hauwezi tena kuzungumza maneno machache hivyo utahitaji kupiga namna za dharura zinazotolewa na serikali ya taifa lako za usaidizi wa kufuatia mlipuko wa virusi vya corona.













